Dar es Salaam, 28.01.2018 

KONGAMANO lililoitishwa na Shirikisho la taasisi za kifedha nchini TAMFI limesema kwamba  vikwazo vinavyokabili sekta hiyo vikiondolewa vitawezesha huduma  za kifedha kusambaa kila mahali.

Pamoja na kutoa kauli hiyo washiriki wa kongamano walielezea kuridhishwa kwoa na mafanikio yaliyopatikana katika sekta hiyo kwa mwaka jana, 2017 kuhusu utengenezaji wa sera ya kitaifa ya taasisi za fedha. 
“Ni hatua njema kuelekea upande sahihi na kama wadau tunatumaini kwamba utekelezaji wake utawezesha kuongezeka kwa matumizi ya huduma ya mifumo rasmi ya kifedha, ambayo kwa sasa ni kidogo,” alisema mtendaji wa TAMFI, Bi Winnie Terry.    

Hata hivyo alisema changanoto zilizopo katika sekta hiyo kunatoa fursa kwa wadau kufanyakazi na serikali kuboresha mazingira ya biashara nchini na hivyo kuwasaidia watanzania wengi kuwa na nafasi ya kuopata huduma za fedha hasa maeneo ya vijijini.

Ili kuwezesha matumizi zaidi ya huduma ya fedha nchini ni muhimu  kwa changamoto zinazokabili taasisi za kifedha kwa ajili ya watu wa ngazi ya chini na kati (MFIs) kutatuliwa ili kubioresha mazingira ya biashara. 

Kwa msaada wa BEST Dialogue, TAMFI walifanikiwa kufanya utafiti  wa kutambua changamoto zinazokabili mchakato wa kupatikana kwa leseni na pia kipindi cha kuhuisha.

Utafiti huo ulifanywa na mtaalamu huru katika sekta ya fedha na kilimo, Bi  Specioza Mashauri,.

Katika utafiti wake alishauri kuwepo na njia rahisi ya upatikanaji wa leseni kwa taasisi za kifedha kwa ajili ya wafanyabiashara wa kati na chini na uhuishaji wake.

Matokeo ya awali ya utafiti huo aliwakilisha katika kongamano hilo. 

Alisema katika utafitiw ake huo kwamba mchakato wa kusajili taasisi ya kifedha una gharama kubwa hasa kwa wale ambao wapo nje ya Dar es Salaam . Hii inatokana na ukweli kuwa mamlaka ya utoaji leseni ipo katika mji huo pekee. 

Utafiti huo umeshauri kwamba suala la usajili linatakiw akugatuliwa  ili isiwepo lazima ya kuja Dar es salaam kwa ajili ya kupata leseni au kuhuisha.

Watoaji leseni hao ni Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji na kwa maoni ya wadau, gharama hizo zipo juu na haziangalii ukubwa wa MFIs.   

Kwa sasa taasisi zote zinalipa gharama ya sh 600,000 bila kujali ukubwa.

Utafiti huo unataka kuwepo na kategori kwa taasisi hizo kulingana na  mtaji na kiwango cha uwekezaji na uwekaji wa akiba hasa kwa zile ambazo haziweki akiba.

“Gharama za wizara ya viwanda,biashara na uwekezaji kwa taasisi ni ghali kwa taasisi yenye mtaji wa kama milioni hasa ikizinmgatiwa kwamba wizara haina gharama yoyote kwa kuwa sio inaowashauri,”  alisema Bi Mashauri. 

Bw Prosper Mzee,  Mtendaji Mkuu wa Planet Microfinance Fund  alishauri serikali kufikiria kuwa na kituo kimoja cha kupata leseni na pia kulipia tozo mbalimbali ikiwamo kodi. 

“Inachukua muda mrefu sana kukamilisha taratibu za kusajili taasisi za kifedha kutoka kwa mtoaji huduma mmoja hadi mwingine,” alisema na kuongeza kwamba inachukua muda mrefu kutekeleza taratibu hizo. 

Bw Julius Mcharo, Ofisa Mtendaji mkuu wa Victoria Finance   kufikiria uitoaji leseni kwa njia ya mtandao ili kupunguza gharama na muda.

Pia alisema wakatik wa kuhuisha leseni hakuna haja ya kufikisha nyaraka zote kama mtu anaomba kwanza leseni. 

Bw Gustav A. Kway, Meneja mikopo wa Zane Microcredit   alisema kwake yeye anaamini ni laizma kuwepo na bodi yenye uwezo kushughulikia utoaji wa leseni na uendeshaji wa taasisi hizo ili sekta MFIs iweze kukua.
mwisho


Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO