WATOTO WANAOELELEWA VITUONI WAASWA KUJITAMBUA

WATOTO wanaolelelewa katika vituo vya kulea watoto yatima na wale wanaoishi katika mazingira hatarishi wametakiwa kujitambua na kujikubali i...

WATOTO wanaolelelewa katika vituo vya kulea watoto yatima na wale wanaoishi katika mazingira hatarishi wametakiwa kujitambua na kujikubali ili kutekeleza wajibu wao wa kupokea malezi mema. Aidha imeelezwa kuwa watoto wanathaminika sana ndio maana wapo watu wameamua kujitolea kuhakikisha wanaishi maisha ya kawaida na kuwa watu muhimu katika jamii. Kauli hiyo imetolewa na Mchungaji msaidizi, Faith Tetemeko wa Kanisa la Ukombozi tawi la Dar es Salaam, wakati akizungumza na watoto wa wa kituo cha Watoto Wetu Tanzania kilichopo Mbezi Luis hivi karibuni. [caption id="attachment_3467" align="aligncenter" width="1404"] akimkabidhi Mama mlezi wa kituo cha yatima cha Watoto Wetu Tanzania kilichopo Mbezi Luis, wilaya ya Ubungo mkoani Dar es salaam, Getrude Nyalubamba (kushoto) akiwa ameongozana na Mwenyekiti kamati ya Msamaria mwema ya kanisa la Ukombozi, Leonard Masano (kulia) walipowasili kituoni hapo kwa ajili ya kukabidhi misaada mbalimbali.[/caption] Mchungaji huyo na kundi la wanawake na wanaume wa kanisa hilo walifika kituoni hapo kutembelea watoto hao na kuwapa zawadi mbalimbali. Alisema katika hafla hiyo kwamba watoto hao wanapojiamini, kujikubali na kujithamini wataona manufaa yake hasa kwa kukubali malezi na kutambua uwepo wa walezi ambao wanajali maslahi yao. Aidha alisema kwamba ni wajibu wa jamii na kanisa kwa ujumla kutekeleza kwa vitendo kujali yatima wajane na wale wanaoishi katika mazingira hatarishi kwa kuwa kitendo hicho kina Baraka kubwa. [caption id="attachment_3468" align="aligncenter" width="1404"] Mchungaji msaidizi, Faith Tetemeko (kulia) wa Kanisa la Ukombozi, akibeba gunia la unga kuingiza katika eneo la kituo cha yatima cha Watoto Wetu Tanzania kilichopo Mbezi Luis, wilaya ya Ubungo mkoani Dar es salaam hivi karibuni. Anayemsaidia ni mmoja wa wakazi wa kituo hicho Elizabeth Samweli anayesoma shule ya sekondari ya Pomerini, Iringa. Wanawake na wababa wa kanisa la Ukombozi walifika kituoni hapo wakiongozwa na mchungaji huyo kwa ajili ya kutoa misaada mbalimbali.[/caption] Alisema kwamba amefurahishwa kufika katika kituo hicho na kutekeleza wajibu wa kukaa pamoja na watoto hao na kumpongeza mama mlezi kwa kazi yake kubwa anayoifanya katika kuwahudumia watoto takribani 31 wanaoishi hapo. Aliwataka watanzania kuwa na tabia ya kujali watoto hao kwa kuhakikisha wanapata mahitaji yao kila siku na sio siku ya sikukuu tu. Kituo cha Watoto Wetu Tanzania kilihamishwa kutoka Stop Over kwenda Mbezi Luishi ili kupisha matakwa ya sheria ya barabara ya Morogoro. [caption id="attachment_3469" align="aligncenter" width="1404"] Mchungaji msaidizi, Faith Tetemeko wa Kanisa la Ukombozi katika picha ya pamoja na baadhi ya watoto wanaolelewa kwenye kituo cha yatima cha Watoto Wetu Tanzania kilichopo Mbezi Luis, wilaya ya Ubungo mkoani Dar es salaam wakisaidia kubeba zawadi mbalimbali zilizotolewa na kanisa hilo hivi karibuni.[/caption] Naye mmoja wa watoto 130 waliopita katika mikono ya kituo hicho tangu kianzishwe 1998, Oscar Gabone mwanafunzi Chuo Kikuu Mzumbe aliwataka wananchi kufika kuwatembelea watoto hao na kuzungumza nao kuonesha upendo hata kama hawana kitu cha kuwapeleka. Alisema kituo hicho kina changamoto nyingi hasa zinazotokana na kubomolewa kwa makazi yao Stop Over na kwamba juhudi za kujenga maboma ya wanawake na wavulana yanaendelea sio kwa kasi inayoridhisha. Alitaka wananchi kuchangia ustawi wa watoto wa kituo hicho ambao wengi wamefikishwa wakiwa wadogo na wengine wakubwa kwa lengo la kuwapatia elimu na matunzo. [caption id="attachment_3470" align="aligncenter" width="1404"] Mchungaji msaidizi, Faith Tetemeko wa Kanisa la Ukombozi akizungumza na watoto yatima wa kituo cha Watoto Wetu Tanzania kilichopo Mbezi Luis, wilaya ya Ubungo mkoani Dar es salaam alipotembelea kituo hicho hivi karibuni na kutoa misaada mbalimbali. Kushoto ni Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa kanisa la Ukombozi tawi la Dar es Salaam, Esther Pilila[/caption] Alisema kwamba sasa wana changamoto kubwa ya kuhamisha makao yao na hawana fedha na pia wanahitaji kujenga ghala la chakula. Gabone alishawishi wananchi kuendelea kufika kituoni kuongea na watoto wa kituo hicho ili wawe na thamani ya upendo, si lazima wabebe kitu. Mama Mlezi wa kituo hicho, Mama Getrude Nyalubamba alisema amefurahishwa na ziara hiyo ya kanisa, kwa kuwafikia na kuwapatia vitu mbalimbali kama nguo na vyakula katika kituo hicho na wakazi wake. [caption id="attachment_3471" align="aligncenter" width="1404"] Mmoja kati ya watoto 130 waliopita katika mikono ya kituo hicho tangu kianzishwe 1998, Oscar Gabone mwanafunzi Chuo Kikuu Mzumbe akifafanua jambo wakati walipotembelewa na waumini waliombatana na Mchungaji msaidizi Faith Tetemeko wa Kanisa la Ukombozi (hawapo pichani) hivi karibuni kituoni hapo.[/caption] Alisema kwamba anaamini Mungu anawapenda sana ndio maana watu wanafika kwao kuwaangalia. Mmoja wa mabinti hao Rose Lemenga ambaye anasoma kidato cha 5 mkondo wa HKL shule ya sekondari Pomelin ameitaka jamii kuendelea kuwasaidia kutokana na wao kukabiliwa na changamoto nyingi za darasani na makuzi. Kituo hicho kina watoto ambao wako shule ya msingi, sekondari na hata chuo kikuu. [caption id="attachment_3472" align="aligncenter" width="1404"] Mama mlezi wa kituo cha yatima cha Watoto Wetu Tanzania kilichopo Mbezi Luis, wilaya ya Ubungo mkoani Dar es salaam, Getrude Nyalubamba akiwa amembeba mtoto Grace Tegete (1.5) aliyefika kituoni hapo baada ya mzazi wake kumtelekeza kwenye basi la abiria.[/caption] [caption id="attachment_3473" align="aligncenter" width="1404"] Baadhi ya wasichana wanaolelewa kwenye kituo hicho wakimsikiliza Mchungaji msaidizi wa kanisa la Ukombozi tawi la Dar es Salaam, Faith Tetemeko (hayupo pichani) wakati alipotembelea kituo hicho kukabidhi misaada mbalimbali.[/caption] [caption id="attachment_3474" align="aligncenter" width="1404"] Baadhi ya wanaukombozi na wageni wengine waliofika kituoni hapo kukabidhi misaada mbalimbali.[/caption] [caption id="attachment_3475" align="aligncenter" width="1404"] Mwalimu Scolla (kushoto) wa Kanisa la Ukombozi tawi la Dar es Salaam akibadilishana mawazo na baadhi ya wasichana wanaolelewa kwenye kituo cha yatima cha Watoto Wetu Tanzania kilichopo Mbezi Luis, wilaya ya Ubungo jijini hapa.[/caption] [caption id="attachment_3476" align="aligncenter" width="1404"] Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa kanisa la Ukombozi tawi la Dar es Salaam, Esther Pilila na Mwenyekiti kamati ya Msamaria mwema ya kanisa hilo, Leonard Masano wakisaidiana kupanga misaada mbalimbali zikiwemo nguo na vyakula walivyokabidhi kituoni hapo hivi karibuni.[/caption] [caption id="attachment_3477" align="aligncenter" width="1404"] Mchungaji msaidizi, Faith Tetemeko wa Kanisa la Ukombozi, akimkabidhi Mama mlezi wa kituo cha yatima cha Watoto Wetu Tanzania kilichopo Mbezi Luis, wilaya ya Ubungo mkoani Dar es salaam, Getrude Nyalubamba moja ya bidhaa zilizowasilishwa hapo kwa ajili ya matumizi ya watoto wa kituo hicho. Anayeshuhudia ni Mwenyekiti kamati ya Msamaria mwema ya kanisa la Ukombozi, Leonard Masano.[/caption] [caption id="attachment_3479" align="aligncenter" width="1404"] Mchungaji msaidizi, Faith Tetemeko wa Kanisa la Ukombozi akigawa zawadi ya juisi kwa mtoto Godfrey Steven anayeishi kituoni hapo wakati wa kukabidhi mahitaji mbalimbali kwa kituo hicho.[/caption] [caption id="attachment_3480" align="aligncenter" width="1404"] Mchungaji msaidizi, Faith Tetemeko wa Kanisa la Ukombozi akiendelea na zoezi la ugawaji zawadi mbalimbali kwa kituo cha yatima cha Watoto Wetu Tanzania kilichopo Mbezi Luis, wilaya ya Ubungo mkoani Dar es salaam.[/caption] [caption id="attachment_3481" align="aligncenter" width="1404"] Watoto wa kituo cha Watoto Wetu Tanzania kilichopo Mbezi Luisi, Ubungo Dar es salaam wakiwa katika picha ya pamoja na Mchungaji, Faith Tetemeko wa Kanisa la Ukombozi akiwa ameambatana na Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa kanisa la Ukombozi tawi la Dar es Salaam, Esther Pilila katika hafla ya kukabidhiwa misaada mbalimbali iliyofanyika hivi karibuni kusherehekea mwaka mpya. Misaada hiyo ikiwamo chakula na mahitaji ya shule ilikabidhiwa kwa kituo hicho na kanisa la Ukombozi.[/caption] [caption id="attachment_3484" align="aligncenter" width="1404"] Mtoto Grace Tegete (1.5) anayelelewa kwenye kituo cha yatima cha Watoto Wetu Tanzania kilichopo Mbezi Luis, wilaya ya Ubungo mkoani Dar es salaam akifurahia ndani ya gari la mmoja wa wanaukombozi waliofika kituoni hapo.[/caption]

COMMENTS

Name

Anga,11,Arusha,27,Burudani,302,burundani,1,come rain,1,come sun,1,Crazy in Love kama wimbo kama wao wenyewe,1,dahh sijui kweli mbona shida,1,Dar utakuja je tumejiandaa,1,daraja sahau nini,1,demokrasia ya upanga,1,Dodoma,77,Dole tupu vijana wa zamani,1,Duhh bibie endeleza libeneke,1,Duhh kaisikie Walibana,1,duhh kwa mbagala mama lazima awe supa,1,Fedha za maiti haziliwi bure,1,Fedha za watu kwa maendeleo ya watu,1,Fikira,14,filamu,238,Filamu ndio kielelezo cha ukuzi wa taifa,1,flamu,7,Gandamiza Kibara baba ake,1,Habari,4810,habari. dodoma,24,hadithi,19,hakika tumeweka historia,1,hakuna noma jongwe,1,hapa kwetu inakuwaje vile,1,hasira hasara,1,hata maji,1,hataki masikhara na maisha yake,1,hatubonyezi kizenji,1,haya ndiyo mambo ya Ulaya,1,haya si yangu ni ya mdau mwenye hasira,1,haya wabongo na mambo kutoka nje,1,He he he wananikumbusha upishi wa shaba,1,Headline,1,Hii hurejesha uhai,1,Hii iko sawa kweli?,1,Hii imekaa vizuri,1,Hii inakaaje vile,1,Hii kweli noma,1,Hii maana yake Moro kuna uhaba wa chakula,1,Hii mexico,1,Hii mihasira mingine bwana,1,Hii ndio moro sio mpaka dar,1,hii ni hatari,1,Hii ni kiboko anayetaka kubisha ajibishie tu,1,Hii ni moja ya staili za kunyoa nywele,1,Hii si lukwangule,1,hii staili mpya,1,hili ni jengo pacha la malaysia ghorofa 88,1,Hivi ni ngoma tu,1,hivi nini siri za serikali,1,hivi sisi tunajua kama kuna vitu vya aina hii,1,hivi vitu bwana,1,Hiyo ndiyo gharama ya demokrasia,1,Hizi imani nyingine ni hatari,1,Hizi takwimu hizi mhh,1,Hongera bibie,1,Hongera dada etu kwa kutuletea kaka etu (shemeji) kwani mwenye dada hakosi shemeji,1,Hongera sana,1,huhitaji mifedha kuwa msafi,1,Huko Ulaya,1,Huu ndio ustaarabu,1,huu ujiko utakuwa mkubwa,1,imetosha,1,Inahitaji nidhamu fulani,1,inakuuma au...,1,Inakuwaje kama filamu yenyewe itahitaji busu la nguvu,1,Inaonekana watanzania hatukuwepo,1,Ipo kazi Maximo,1,Iringa,22,Isiwe mijineno tu manake mihela hubadili watu kweli,1,Itakuwa laki moja ya halali,1,jamani huu kama si ushamba kumbe nini,1,Jamani mbona Mungu anatupigania,1,Jamani watoto wanatakiwa kupendwa,1,jamani.. jamani ukiikosa Diamond usijutie,1,Je nyumbani hakuna vitu vya aina hii?Tuambie,1,je walikuwepo watu wa huduma ya kwanza,1,Je watanzania wanalipa kodi,1,jela kwa raha,1,Jolie,1,juhudi za lazima kuinua filamu,1,kama si kiwanda cha chumvi nani atawajua hawa,1,Kama kweli ndio kweli basi kila heri,1,Kama Mkristo naamini hilo hiyo si sahihi,1,kama unajua kuyarudi nenda Malta,1,kama wao wanaweza sisi je,1,Kamua baba waache wakanyagane,1,karibu nyumbani dada yote maisha tu,1,karibu Tatiii,1,KARIBUNI,1,Katavi,5,kaza buti hakuna kukata tamaa inalipa,1,kazi kwako mheshimiwa waziri wa madini,1,kazi na burudani,1,keep it up bloggers,1,kero ya usafiri sasa kwisha,1,Kila chenye roho na mwili kitaonja umauti,1,kila kitu kina vitu,1,Kila la Heri jamila,1,kila la heri kwani ni changamoto,1,Kipya,51,Kiuno bila mfupa,1,Kolelo mzimu ambao bado hai,1,KUBWA,1,Kudumisha urafiki wa dunia,1,Kuna dalili za wasomi kukubali Uafrika,1,kuna makala humu humu ndani ya blogu sijui mnasemaje,1,Kuu,113,kwa mara nyingine tena Tigo imewezesha,1,Kwa mchanganyiko huu muungano lazima udumu,1,Kwa mihasira hajambo,1,kweli,1,Kweli ina mkono mrefu tuone,1,Kweli duniani tunatofautiana,1,la maana ni kuwa na jiko au vipi,1,labda halitabadilika tena,1,lakini mwafaka lazima,1,lengo ni kutafakari,1,leteni vitu tuvione,1,lets us,1,Lucy wanakuelewa hawa...,1,Lukwangule nyumbani kwetu,2,M ungu bariki mikono ya madaktari wafanikiwe,1,MAARUFU,1,maendeleo ya soka siku zote yanahitaji fedha ili yapatikane,1,maisha ni vyema kuyaangalia,1,MAJIBU,1,makala,51,mama ni mama tu anapendeza,1,mambo mengine we angalia tu,1,mambo msimamo,1,mambo sasa mchanganyiko,1,Mara nyingine huona tunakotoka kwa kuona wenzetu,1,Mashabiki wa rhumba mpooooooooo,1,Masitaa,12,Maskani,1,MASOKO,3,Masupa staa mnaoinukia mpoo,1,Matamasha,6,mavazi ya kuogelea yanaposhindaniwa,1,Mbeya,11,Mchakamchaka anti Asmah,1,Mchanganyiko,81,MCHANYATO,1,mchezo,5,mengi wanayoyaita siri ni public information,1,mfumuko wa bei mpaka noma,1,Mhh sijui watu wa Sua ambao wako huko wanasemaje,1,Mhh ugua pole dada watu wanataka burudani,1,Michezo,501,Michezo maalum inatakiwa kupigiwa debe,1,miguu,1,miguu babu,1,Mikataba mingine ama hakika tuiangalie hata wakopeshaji nao wanatugeuza sakala,1,MIMI NI KISURA NAJITAMBUA,1,Mimi sijajua hasa kumetokea nini kwani ninavyojua hawa huwa na ungalizi wa hali ya juu,1,Mimi simo,1,mimi sisemi,1,mkiwa chumvi basi mkoze,1,Mkiwa taa mulikeni,1,Mnaonaje je hii imekaa vyema,1,Mnaweza wakwetu hapa,1,Morogoro,51,mrithi wa mwanadada Whitney Houston,1,Mtwara,4,Mungu aiweke mahali pema roho yake,4,Mungu amrehemu,1,Mungu amweke pema peponi,1,Mungu awabariki sana,1,Mungu awe nao,1,Mungu ibariki Tanzania,1,Mungu tuepushe na imani hizi za kishirikina,1,mungu tufanye tuwe na upendo,1,Mungu twaomba utuhurumie,1,Muziki,350,muziki na fasheni,5,Mwanahabari,33,Mwanza,6,Mwendo mdundo dada,1,Mwenge huo utakimbizwa duniani kwa siku 130,1,Mwenge wa olimpiki ni ishara ya urafiki,1,Mzee wa Farasi nakupa saluti,1,Mzimbabwe huyu kutoka kwa mama mkali,1,N i dar mpaka Moro au bao tatu bila,1,Na sisi je,1,Naam kama haiwezekani hapa,1,Nairobi waanzisha tena utalii,1,namna bora ya kusaidia jamii,1,nani abebe hukumu na lawama,1,nani asiyejua utamu wa pipi,1,Nani kama baba,1,naona inafaa kuchangia mimi sitoi hoja,1,ndoa za mastaa huwa na mgogoro,1,nenda mwaya nenda,1,New Zanzibar Modern Taarab na wapenzi big up,1,news,5,Ni bikini kwa kwenda mbele,1,Ni Dar mpaka Moro au.. tatu bila,1,ni furaha za muungano,1,Ni kazi ngumu yenye kuhifadhi utamaduni,1,Ni kuchakarika kuonyesha urafiki na biashara pia,1,ni mfumuko wa bei au mfumuko wa nchi,1,Ni muhimu kutazama afya yako,1,ni muziki kwa kwenda mbele,1,Ni muziki mpaka China,1,Ni raha tupu,1,Ni Serengeti Premium Lager,1,Ni Tigo na mawasiliano ya kisasa,1,Ni wakati wa kuujadili utamaduni,1,Ni zaidi ya jazz,1,Nitasubiri and welcome home,1,nje je?,1,NUKUU YA LEO,1,nyie mnasemaje kuhusu hili,1,Ona Kolelo na sindikizwa na Wazee wa Gwasuma,1,ona vya dunia,1,One step ahead,1,patna mwingine mjamzito,1,Pengine anamuogopa Jada Pinkett manake kwa wivu..,1,picha,494,Pole Jamila hayo ndiyo mashindano,1,poleni sana,1,poleni sana wanyalukolo,1,Powa sana,1,Profesa jamaa wanakumaindi,1,Roho za marehemu zipate pumziko la milele,1,Ruvuma,9,sakata dansi mpaka kwenye kilele cha dunia,1,sasa kumebakia ugonjwa mmoja polisi kuendesha mashtaka,1,sasa mifedha kila mahali hongereni,1,Sasa ni mavuno,1,Sasa ni wakati wa kutafuta upenyo ndani ya IDOLS,1,SAYANSI,1,SAYANSI ANGA,1,See Uluguru Montains,1,serikali inataka kujihami kwanini,1,Show of support Big Up Madame,1,Si kitu kidogo hata kidogo,1,si unajua tena namie naimwaga hivyo hivyo,1,Siasa,346,siasa habari,2,Sijui kama City wanajua Mbagala noma,1,Sijui tunaishi karne gani yailahi,1,Sinema,9,sio advencha....kaaa ...niko kibaruani,1,Sisi ndio tunaanza vitongoji,1,Sisi yetu macho na masikio,1,Slow slow jamani,1,sto,1,tabasamu kali la mwenge wa olimpiki,1,Tabora,1,Tazama Waziri Mkuu Pinda wasije wakapindisha maamuzi yako,1,TEKNOLOJIA,1,Thats big man game,1,This is crazy Africa,1,This is Mgeta,1,Tibet wamegeuza Olimpiki jukwaa la siasa,1,Titbits collection,1,Tubadili tamaduni,1,Tuchangie mambo yaive,1,tuendeleze sanaa,1,tuienzi na sisi mbona wizara haituambii,1,Tuipeleke kaskazini,1,Tuisaidie serikali shida ya Mererani,1,tujue namna ya kupumzika,1,Tulienda kustarehe au kufanya fujo,1,Tumsaidie mtototo huyu kurejea katika hali ya kawaida,1,tunahitaji haya,1,Tunajifunza kweli kutoka kwao,1,Tunapandisha chati tu,1,Tunasubiri,1,tunazidi kuhesabu siku,1,TUNAZISUBIRI ZA VINARA ADAR,1,Tuombe nafuu kwa wagonjwa,1,Tuombe rehema kwa mungu,1,Tuone yatufae,1,Tusingoje wengine watusemee,1,tutampa tafu kubwa Prof,1,tuuenzi utamaduni au vipi,1,Tuukuze na kuulinda,1,tuvipende,1,tuwalinde maalbino,1,Tuwe kweli wakweli,1,ubunifu siku zote hulipa,1,uchumi huzunguka kwa kuwawezesha wasukaji,1,udumu muungano,1,Ugonjwa huu wa sasa ni kitendawili,1,Ukiiona kolelo utaipenda,1,Ukirejea salama kila mtu anafurahi,1,Umelenga Mkuchika utamaduni unakufa,1,unaposaka uwakilishi wa dunia,1,urafiki,1,Usisahau wazee wa Ngwasuma,1,UTAMADUNI,1,Video,2,Vionjo vipya ndani ya Gwasuma,1,Vita dhidi ya ufisadi,1,vitongoji Miss Tanzania navyo vimeanza,1,Vitu vikali vyazidi kuingia Dar,1,Vituko,77,Vituo vya polisi Tanga vyatelekezwa,1,VIVALO,1,Wacha tujifue,2,Wadau ilitolewa kiingereza,1,wakali wa ubunifu,1,wala usibabaike mwakwetu hii noma,1,wanadamu wanapotaka kujua zaidi,1,wanasema mpaka kieleweke,1,Wanataka kujua mali za JK na wengine,1,Wanawake wenye mvuto: Monroe,1,Wapo mabinti wa matawi ya juu,1,watu wanapofanya weli kwenye sanaa,1,waweza kurejea enzi ya Moro jazz na Cuban malimba,1,Wazee tupo kusindikiza,1,waziri,1,welcome dar baby,1,Wenzetu wameona sisi tunangoja nini kuangalia,1,wewe unasemaje,1,wigo mpana wa utamaduni,1,wilaya ya 'Mbagala' mlie tu,1,Yaaani sijui itawezekana,1,Yaani wakati mwingine hata huelewi prioty over priority,1,yeye mbele sisi nyuma,1,Yote maisha dada,1,ZA MOTOMOTO,1,Zanzibar,79,zawadi zinatakiwa ziende shule,1,ZILIZOTIA FORA,1,zitachangia kupunguza makali ya bei za umeme,1,
ltr
item
Lukwangule Entertainment: WATOTO WANAOELELEWA VITUONI WAASWA KUJITAMBUA
WATOTO WANAOELELEWA VITUONI WAASWA KUJITAMBUA
http://www.thebeauty.co.tz/wp-content/uploads/2018/01/IMG_4986.jpg
Lukwangule Entertainment
http://lukwangule.blogspot.com/2018/01/watoto-wanaoelelewa-vituoni-waaswa.html
http://lukwangule.blogspot.com/
http://lukwangule.blogspot.com/
http://lukwangule.blogspot.com/2018/01/watoto-wanaoelelewa-vituoni-waaswa.html
true
934549962738256429
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy