Zuma alisema anajiuzulu mara moja japokuwa hakubaliani na uamuzi wa chama cha ANC cha kumtaka ajiuzulu.Chama cha ANC kilikuwa kimemuambia aondoke madarakani au akabiliwe na kura ya kutokuwa na imani naye bungeni.

Zuma mwenye umri wa miaka 75 ambaye amekuwa madarakani tangu mwaka 2009, amekuwa akituhumiwa matumizi mabaya ya madaraka, ufisadi na rushwa.
Zuma katika hotuba yake ya kujiuzulu alianza hotuba kwa kucheka na kufanya mzaha na waandishi wa hahari.
Baada ya kuwashukuru wale ambao amefanya kazi nao kwa miaka kadhaa, Zuma alisema ameamua kujiuzulu kuepusha nyufa zaidi katika chama chake cha ANC.
Alisema hataki kuona ANC inapotea au kumeguka kwa sababu yake na hivyo anaamua kujiuzulu.
"Licha ya kutokubaliana na uamuzi wa chama changu, siku zote nimekuwa mwanachama mwenye nidhamu wa ANC.
"Ninapoondoka, nitaendelea kuwatumikia watu wa Afrika Kusini sawa na ANC, chama ambacho nimekitumikia maisha yangu yote."

Wasifu wake
Jacob Zuma ni Rais wa aina yake na mwenye utata kuwahi kutokea Afrika Kusini baada ya utawala wa weupe mwaka 1994. Amekuwa ni mwanasiasa mwenye maisha tisa akiponea chupuchup kashfa kadhaaa ambazo zineweza kuangamiza kabisa nafasi na historia ya kisiasa ya mtu mwingine yeyote.
Lakini Zuma aliyezaliwa katika familia masikini na baadae kuishi uhamishoni sababu ya kupinga ubaguzi wa rangi kabla ya kupanda ngazi na kushika hatamu kama rais wa watu, hawezi kunusurika kashfa hizi kila mara.
Licha ya kukana mara zote tuhuma za rushwa dhidi yake tuhuma hizo zimekuwa zikijirudia kila mara.
Zuma mwaka 2009 kuelekea uchaguzi mkuu tayari alikuwa akikabiliwa na tuhuma za rushwa na ubakaji.
Alituhumiwa kumbaka rafiki wa familia yake ambaye anaishi na virusi vya ukimwi mwaka 2006, na wakati wa shauri mahakamani Zuma alisema mahakamani kuwa alioga ili kujikinga na virusi vya ukimwi.
Alikumbwa pia na tuhuma za utakatishaji wa fedha na kupanga mpango katika mkataba tata wa silaha wa mwaka 1999. Mwaka 2017 iliamua tuhuma 18 za rushwa dhidi yake  ziangaliwe upya.
Mara zote Zuma amekanusha tuhuma hizo na kuapa kuachia ngazi ikithibitika kama ni kweli amehusika.
'Raisi wa Watu'
Ulikuwa ni utu wake ndio ulimpeleka Zuma madarakani mwaka 2009 wafuasi wake waliona namna alivyokuwa akikubalika na wengi na kushika hisia zao na kuwa mbadala wa Rais Thabo Mbeki ambaye alionekana kuwa mbali na watu.
Ukaribu wa bwana Zuma katika usimamizi na utetezi wa mila na desturi katika familia ni miongoni mwa sababu zilizosababisha kujizolea wafuasi hasa kwa raia masikini wa nchi hiyo wengi wao wakiwa ni wakazi wa vijijini.
Zuma mwenye miaka 75 anajivunia ndoa za mitala kama ilivyo ilivyo desturi ya wazulu. Zuma kwa sasa ana wake wa nne ameoa mara sita ana watoto 21 na mmoja wa wake zake raia wa Msumbiji ,Kate Mantsho alijiua mwaka 2000.
Kadhalika anasifa ya kutokuwa mwaminifu katika ndoa zake na analea mtoto wa nje ya ndoa na mwanamke mwingine.
Imani hii ya raia kwa Zuma kama rais wa watu haikudumu kwa muda mrefu ,mapema mwaka 2013 moshi ulianza kufuka baada ya Zuma kuboresha makazi yake ya kijijini kwao Nkandla kaskazini mwa KwaZulu-Natal akitumia hela za serikali.
Wakati wa ibada ya mazishi ya Rais wa kwanza mweusi wa Taifa hilo Nelson Mandela wafuasi wa ANC walikuwa wakimkosoa wazi wazi mbele ya wageni mbali mbali wa kimataifa akiwemo aliyekuwa Rais wa Marekani wakati huo Barrack Obama.
''Anakula wakati tuna njaa'' mmoja wa waandamanaji alisema na kuamsha hasira kwa waandamanaji juu wa maboresho Zuma aliyofanya kwenye makazi yake huko Nkandla ikiwa na eneo la kufugia ng'ombe, ukumbi wa Sanaa , bwawa la kuogelea ,sehemu ya wageni na banda la kuku.
Bw Zuma alifanikiwa kulipa hela za ziada alizotumia.
Visa vya kisheria vinavyomuandama Zuma
§  2005: Alituhumiwa kwa rushwa ya mabilioni ya dola kwenye mkataba wa silaha wa mwaka 1999 madai ambayo yalitupiliwa mbali kabla hajawa rais mwaka 2009
§  2016: Mahakama iliamuru ashitakiwe kwa makosa 18 ya rushwa dhiya yam kata wa silaha ambao alikatia rufaa
§  2005: Aishitakiwa kwa kumb'aka rafiki wa familia na kufutiwa mashitaka2006
§  2016: Mahakama iliamuru kuwa amekiuka kiapo chake kama raisi na kutumia fedha za serikali kuboresha makazi yake binafsi fedha ambazo alizilipa baadae
§  2017: Wakili wa serikali alisema ateu jaji kiongozio wa kamati ya kuchunguza iwapo ana uhusiano na familia tajiri ya Gupta madai ambayo ameyakanusha
§  2018: Zuma alikubali maombi hayo


Miaka mitatu Mahakama kuu nchi Afika kusini iliamua kwamba amekiuka katiba kwa kushindwa kulipa pesa za serikali alizo tumia kuboresha makazi yake binafsi
Rasi Zuma aliwaomba radhi raia wa nchi hiyo kwa tuhuma hizo na kulipa fedha hizo.
Lakini tuhuma hizi za makazi zilitarajiwa kufunikwa na tuhuma kubwa zaidi za namna alivyoingia madarakani.
Baada ya muda kidogo mahusiano ya Zuma na familia tajiri ya India Gupta yakaanza kumulikwa tuhuma zikiwa ni kwamba walishinikiza uteuzi wa baraza la mawaziri ili waweze kupata mikataba yenye fedha nyingi ya serikali.
Tuhuma hizi zimepingwa vikali na Zuma mwenyewe na hata familia ya Gupta.
Akiwa na miaka 17 Zuma alijiunga na ANC na kuwa mwanacha hodari katika tawi lake la Jeshini Umkhonto We Sizwe, mwaka1962.

Wake zake Zuma

§  Gertrude Sizakele Khumalo alimuoa mwaka 1973
§  Nompumelelo Ntuli (2008)
§  Thobeka Madiba (2010)
§  Gloria Bongi Ngema (2012)
Wake aliotalikiana nao
§  Nkosazana Dlamini-Zuma (alimuoa mwaka 1972; na kuachana naye 1998)
§  Kate Mantsho (alimuoa 1976; alifariki 2000)
Alihukumiwa kwa kula njama za kutaka kupindua serikali ya kibaguzi ya makaburu na kufungwa miaka 10 katika gereza la kisiwa cha Robben pamoja na Nelson Mandela.

Inaelezwa Zuma alikuwa akichochea morali ya wapigania uhuru hawa kwa nyimbo na tungo za kizalendo na wengi wana amini hiki ndo kilimfanya kuwa maarufu miongoni mwa Raia hata wale wa vijini kabla ya kuupata uraisi

Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO