Serikali imetoa pole kwa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni
Bagamoyo kwa kumpoteza Mwalimu mahiri John Mponda aliyekuwa balozi wa tasnia ya Sanaa nchini.
Kauli hiyo imetolewa leo na Naibu
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza katika ibada ya
kumuaga marehemu huyo iliyofanyika katika Chuo cha TaSUBa Wilayani Bagamoyo kwa
ajili ya kumuaga kwani anatarajiwa kuzikwa kijiji cha Mbalizi Mkoani Mbeya.
“Tunatambua mchango wa Mwalimu
John Mponda katika tansia ya sanaa nchini na kupitia wanafunzi waliyopita katika
mikono yake pamoja na vikundi vya vijana alivyovianzisha ambavyo amekuwa
akivifundisha kazi za sanaa, hakika tumempoteza mtu makini,”alisema Mhe.Shonza.
Akiendelea
kuzungumza katika msiba huo Mheshimiwa Shonza
aliwasihi wasanii waliyopata mafunzo kutoka
kwa mwalimu huyo kuwa mabalozi kwa
wasanii wenzao na kuwashauri misingi iliyobora katika katika kukuza na
kuendeleza kazi za sanaa.
Kwa
upande wa Mkuu wa Chuo cha TaSUBa Dkt.Herbert Makoye alisema kuwa marehemu
mwalimu Mponda ameondoka katika kipindi walichokuwa wanamuhitaji sana kwani
kwasasa taasisi hiyo ipo katika maandalizi ya Tamasha la Utamaduni la Bagamoyo
ambalo nilakimataifa na hufanyika kila mwaka na yeye alikuwa mratibu na mpaka mauti yanamfika
alikuwa akiwa shughulikia maandalizi hayo.
“Kwa
hakika msiba huu ni pigo kwa taasisi yetu na mwalimu huyu alikuwa kiungo
miongoni mwetu na alifanya kazi yake kwa weledi na kujituma alikuwa ni mtu
aliyeipenda kazi yake ,’’alisema Dkt.Makoye.
Pamoja
na hayo nae Mwenyekiti wa Umoja wa Wanafunzi waliyosoma TaSUBa Deosonga
Njelekela alisema kuwa mwalimu huyo kwao hakuwa tu kama mwalimu bali alikuwa baba na mlezi kwani na alikuwa
mstari wa mbele kutoa nasaha zake kwa lengo la kutaka wanafunzi wake waweze
kufanikiwa zaidi.
Hata
hivyo nae mtoto wa Marehemu Bi. Mery Mponda aliwashukuru watu wote
waliyojitokeza kuungana nao katika msiba huo kwa imekuwa ni faraja kubwa kuona
watu wakiomboleza pamoja nao baada ya kumpoteza baba yao mzazi ambaye alikuwa
mlezi na nguzo ya familia.
Source:Anitha Jonas – WHUSM
Post a Comment
Post a Comment