Mbwa mmoja atatekelezewa adhabu ya kifo baada ya kubainika kuwaua watu wanaommiliki.
Imethibitishwa kwamba mbwa huyo aliwararua wamiliki wake ambao ni wagonjwa.
Tukio hilo lililotokea mji jirani na Hanover, na kumhusu mbwa aliyeitwa Chico.
Mbwa huyo aina ya  Staffordshire Terrier  mchanganyiko aliwaua mmliki wake mwenye umri wa miaka 52 na mtoto wake wa miaka 27 kwa kuwararua.
Majibu ya uchunguzi wa maiti za watu hao wawili  yalitolewa Aprili 6,  na yalionesha kufa kutokana na mashambulio ya mbwa huyo.
Kikosi cha zimamoto kilifanikiwa kumnasa mbwa huyo wakati walipopewa taarifa ya kuwapo na tatizo kwenye ghrofa.
Binti wa mama huyo alipiga simu baada ya  kushindwa kupata majibu wakati alipopiga simu nyumbani.

Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO