Wakulima katika kijiji cha Dakawa  kata ya Bwakila chini Mkoani Morogoro huenda wakakabiliwa na uhaba wa chakula kutokana na mashamba yao kuvamiwa na panya na panzi waharibifu.
Wakulima hao wameieleza Lukwangule blog kuwa wamepanda mahindi  na mpunga zaidi ya mara mbili lakini panya wamekuwa wakifukua mbegu na kula.
Hatahivyo afisa kilimo wa halmashauri ya Morogoro vijijini hakuweza kupatikana kuweza kutoa ufafanuzi wa ukubwa wa tatizo na hatua zinazokukuliwa na serikali za kuweza kutatua tatizo hilo.
Mmoja wa wakulima hao Khadija Legeza wa kijiji cha Dakawa  amesema kuwa  hasara wanayoipata hawajui ni lini itaisha kutokana na wadudu kuendelea kuwepo.
Alisema kuwa ni vyema serikali ikawasaidia dawa za kuwaua wadudu hao kabla msimu wa kilimo haujaisha.
Alisema kuwa walishajalibu mara kadhaa kumwagia dawa lakinj wadudu hao hawaishi hivyo wanazidi kupata hasara na kuishiwa hakiba yao ya vyakula kwa kutumia kwa mbegu bila kuona mafanikio.
Alisema hofu yao kubwa ni pale msimu unapozidi kusogea na wadudu bado wanasumbua hivyo ni wazi km tatizo halitashughulikiwa mapema wakazi wengi watakosa chakula msimu huu kutokana na uharibifu unaoendelea kufanywa na wadudu hao.
"msimu ndio huo unasogea hatujui kama tutafanikiwa wadudu ni wengi tunapanda mahindi yanafukuliwa shimo hadi shimo mpunga nao hivyo hivyo unaobaki unakatwa na panzi ni wazi hatujui cha kufanya,"alisema.
Naye  mkulima Habiba Mawaga amesema kuwa hasara kubwa wanayoendelea kuipata  hawajui itaisha lini kutokana na wadudu kuendelea kuwepo

Alisema kuwa wadudu wamekua ni tatizo kutokana na wakulima kupoteza kiasi kikubwa cha pesa bila kuwa na matumainj na wanachokilima
Alisema kuwa wakati wengi wa vijiji vya kisaki, Bwakila Juu  chamgoi wanaishi kwa kutumia kilimo hivyo mpaka sasa vyakula ndani vinaisha kwa ajili ya kuuza kwa kuendeshea lakini kilimo kinaonyesha kuwaangusha kutokana na wadudu wa haribifu kuvamia mashamba yao.
"heka tunalima shilingi elfu hamsini nimelima  Heka mbili  kwa shilingi laki moja nimeweka vibarua ahilingi 40000 nisharudia mara mbili hii ya tatu, vyakula ndani vinaisha msimu unapita hivi unadhani tutaishije sie na tunafamilia kubwa,"alisema mwisho


Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO