KATIKA kitabu cha Masimulizi ya Sheikh Thabiti  Kombo Jecha kuna eneo ambalo , amejadili kw aurefu matukio ya usaliti nchini Zanzibar baada ya mapinduzi ya mwaka 1964.
… Wapinga mapinduzi hawa walishidnwsa kukubali ukweli wa mapinduzi ya Afro Shirazi na kuwa sultani kweli ndio kaondolewa; wakajaribu mwaka ule ule wa 1964 kututikisa. Mwishoni mwa mwaka ule wa 1964 tukashtushwa na jaribio la mtu mmoja Amour Zahor wa kajificheni Unguja na wenzake wanne wenye itikadi ya Hizbu, kutaka kuiangusha serikali ya ASP kwa matumaini ya kurudisha umwinyi Visiwani humu Tulijua kuwa mpango huo ulibuniwa na wafuasi wa ZNP, kwa sababu ya chuki ya kupinduliwa serikali yao. Kikundi chao kiliitwa kwa jina la Peiople’s Fighters Union.
Hizbu walijaribu tena mwaka 1967; mwaka huo wa 1967 ulikuwa wa balaa kubwa kwetu, yalikuwapo majaribio matatu. Kwanza mafisadi watatu wakiongozwa na Suleiman Hamad Suleiman wa Msingine Pemba, mwarabu wa kabila la El-Kindy, walipojaribu kuiangusha serikali ya mapinduzi. Baadaye tena watu wengine wawili waliokuwa na nguvu kubwa ya fedha kutoka nje, nao wakafanya jaribio lao. Hao walijiita Freedom Fighters, kiongozi wao Saleh Ali Nassor wa Mchambawima Unguja, Mwarabu wa kabila la Barwan. Hawa walitegemea zaidi fedha, ambazo hazikuwafaa kitu..
Mwaka huo huo tena kikazuka kikundi kingine cha watu watatu kilichoongozwa na Salim Mohamed Abdallah wa Madungu, Pemba. Hawa walijiita Jitihada. Wao walikuwa wanataka kuiangusha serikali ya ASP ili kwanza wavunje muungano; na si hivyo tu,walitaka wakifanikisha kuigawa, pemba iwe nchi mbali na Unguja nchi mbali!
..Usaliti uliotisha sana ulitoka kwa viongozi wenznetu ndani ya ASP na ndani ya serikali ya Mapinduzi, wakati zilipopangwa njama kuviza makusudi siasa ya chama, ili chama kifarakane na wananchi. Visa hivyo vilikuwa vikubwa sana, na ukielekezwa vyote wala huwezi kuamini.
Katika njama hizo alikuwako Abdullah Kasim JHanga, saleh Saadallah Akida na Abdul-aziz Twalha, wote wakati huo  mawaziri wa serikali hiyo hiyo waliyokuwa wanataka kuiangusha. Wengine maarufu serikalini, kama Aboud Nadhif na Mdungi Ussim, wote makatibu wakuu. Baadaye tena akajitokeza Othman Shariff Mussa, Waziri wa Elimu na  na wenzake watatu, waliokuwa na mawazo kuwa wakifuzu kuiangusha serikali hii watarejesha kwa wenyewe mashamba yaliyotaifishwa, maana wao waliamini kuwa ASP ilifanya dhuluma kubwa kutaifisha mashamba baada ya mapinduzi.
Msukosuko mkubwa zaidi nilioushuhudia na ambao nusura uniondolee maisha yangu ni ule wa 1972, uliosababisha kuuawa kwa Rais wa Kwanza wa ASP, Sheikh Abeid Amani Karume. Mafgisadi walidhani kuwa akiuawa Karume basi Afro-Shirazi hakuna tena, na mapinduzi yatakoma. Karume kweli akafa, akazikwa; lakini ASP ikabaki palepale na mapinduzi yakabaki palepale.
Kama kawaida, siku ya Aprili 7 mimi nilifika hapo makao makuu ya ASP kiasi cha saa 10 jioni, nikamkuta Maalim Shaban Kombo kesha fika, yuko ndani ya ofisi yake sehemu ya hapo chini. Mara akaingia mheshimiwa Ibrahim Saadallah, na punde akafuatia Mzee Mtoro Rehani. Halafu akafika Sheikh Muhiddin Ali Omar, na kiasi cha saa 11 hivi akafika mheshimiwa Sheikh Karume. Wakati nilipofika mimi na mpaka hapo mheshimiwa Rais alipofika, askari walinzi wa FFU walikuwa bado hawajaja kulinda makao makuu ya Chama, kwa kawaida wao hufika kiasi cha saa 12 jioni. Mwenyewe Rais alipoingia alikuwa na walinzi wake wa kawaida kutoka Idara ya Usalama, na alipoingia ndani wao aliwaacha nje wakichukua nafasi zao za ulinzi.
Mheshimiwa Sheikh Karume alipofika alitukuta tumekaa kuzungukia meza kama kawaida yetu; mpango wa meza hiyo ulikuwa sisi sote tunaupa ubavu mlango mkuu.
 Nitaendelea kesho

Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO