Kiongozi wa Msafara wa wachezaji waliyokwenda katika Mashindano ya Jumuiya ya Madola nchini Australia ambaye Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo kutoka Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bw.Yusuph Singo akizungumza na kwa waandishi wa habari kuhusu hali ya mashindano pamoja na suala la mchezaji mmoja kutoroka kambini.  

Bondia Selemani Kidunda (wa kwanza) akiwasilini leo jijini Dar es Salaam katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere akitokea nchini Australia ambapo alikwenda kwa ajili ya Mashindano ya Jumuiya ya Madola  nyuma yake ni Bondia mwenzie Haruna Swanga

Mwanariadha wa kike Bi.Sara Ramadhani akiwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam baada ya kuwasili akitokea nchini Australia ambapo alikwenda katika Mashindano ya Jumuiya ya Madola na ameshika nafasi ya tisa katika mbio za Kilometa 42

Kapteni wa Timu ya wachezaji waliyokwenda nchini Australia katika Mashindano ya Jumuiya ya Madola Bw.Masoud Mtalaso (kulia) akirejesha bendera aliyokabidhiwa wakati wanakwenda katika mashindano kwa Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bw.Alex Nkenyenge (kushoto) mara baada ya kurejea nchini leo jijini Dar es Salaam.
Source:  Anitha Jonas – WHUSM

Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO