MTALAKA  wa Rais wa Kwanza mweusi nchini Afrika Kusini, Nelson Mandela, bibie Winnie Madikizela Mandela amefariki dunia leo akiwa na umri wa miaka 81.
Mwanaharakati huyo ambaye walipiga picha ya kukumbukw ana dunia wakati mume wake akitoka gerezani baada ya miaka 27 ya kazi ngumu katika magereza ya makaburu, alizaliwa Bizana ,  katika iliyokuwa Transkei sasa ikijulikana kama Eastern Cape mwaka 1936 na kupewa jina la Nomzamo Winifred Madikizela.

 Alipewa talaka na Mandela na kupewa ruhusa ya kuendelea kutumia jina hilo mwaka 1996.
Msemaji wa familia, Victor Dlamini  amesema kwamba amefariki baada ya kuugua kwa muda mrefu.
Aidha alisema amefariki akiwa amezungukwa na familia yake.Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO