Mkuu wa Mkoa wa Rukwa mh. Joachim Wangabo amemwagiza Katibu Tawala wa Mkoa huo kuanzisha mchakato wa kinidhamu na uchunguzi mara moja dhidi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo kutokana na utendaji kazi wake usioriddhisha..
Amesema kuwa mkurugenzi huyo amekuwa akichelewesha juhudi za serikali baada ya kushindwa kumaliza ujenzi wa upanuzi wa kituo cha afya cha Mwimbi kwa wakati na kuchelewa kuanza ujenzi wa kituo kipya cha afya cha Legeza mwendo hata baada ya kupatiwa Shilingi Bilioni 1.1 na serikali kwa ajili ya vituo vyote viwili vilivyopo katika halmashauri hiyo.
“Huyu mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo utendaji wake siridhishwi nao hata kidogo katika mazingira ya sekta ya afya kwa ujumla wake, ujenzi na ukarabati wa miundombinu katika kituo cha afya cha Mwimbi ulianza mwezi wa nane mwaka 2017 mpaka leo naongea hapa mwezi wa tano mwaka 2018 kituo cha afya kile bado hakijakamilika,” alisema
Ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na wauguzi katika siku yao ya wauguzi duniani iliyoadhimishwa kimkoa katika kata ya Laela, Wilaya ya Sumbawanga.

IMETOLEWA NA 
OFISI YA MKUU WA MKOA WA RUKWA 
E-mail:       ras@rukwa.go.tz
                   ras.rukwa@tamisemi.go.tz
                   rukwareview@gmail.com
Website:    www.rukwa.go.tz


Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO