UCHOKOZI YAKINIFU KWA SANAA NCHINI

Na  Martin Mhando Nasikitika kuwa sitoweza kuwa na ndugu zangu wasanii na wadau katika sanaa na utamaduni katika majadiliano haya muhi...

Na Martin Mhando

Nasikitika kuwa sitoweza kuwa na ndugu zangu wasanii na wadau katika sanaa na utamaduni katika majadiliano haya muhimu kuhusu impact ya bajeti ya serikali kwa sanaa nchini. Haya ni majadiliano ambayo yalikuwa yafanyike miezi sita kabla ya bajeti, ambapo hayakufanyika,  na pia wiki moja baada ya bajeti- kama hivi itakavyofanyika Jumanne hii tarehe 23 Juni.

Lakini kukosekana kwangu kusitupe shida maana dunia imebadilika na tusipotumia fursa zilizopo hatutakuwa na haki ya kulalamika. Hivyo hata kwa kutoweza kuwepo kwangu kushiriki kizoom au kigoogle-meeting ni alama ya uzembe wangu na labda uzembe wako wewe mdau wa sanaa mwenzangu pia.

Tuliache hilo ingawa kimsingi tatizo letu linaanzia hapo.

Maana kukosa ubunifu ni tatizo kubwa katika nchi zinazoendelea, na hilo halitokei kwa sababu wananchi hawana huo ubunifu, la hasha. Kama kuna kitu ambacho wanadamu tumepewa kwa magunia na sio kwa kijiko, ni ubunifu. Lakini tunapotaka kuweka miongozo mikalimikali (hiyo ninayoiita miundombinu) ili kuwezesha ubunifu ndipo tunapokosea na kujikuta tunaua ubunifu.

Ubunifu ni uwezo muhimu ambao huwezesha watu au hata taasisi kushughulikia na kusimamia mabadiliko, ambayo kimsingi ndio nia ya mipango. Mara nyingi, ubunifu hujumuisha pia kuona vitu kutoka kwa mtazamo mpya na kuacha fikra za jadi ambazo zinaweza kuwa zimepitwa na wakati.

Ubunifu hauna mpango na wala hausubiri mpango, na saa nyingine huchukia hasa mipangilio. Ubunifu hutaka wenyewe kujitengenezea mpango na kuuendeleza hadi hapo unapoweza kubuni mpango mwingine. Hilo mara kwa mara linakuwa gumu kueleweka ingawa, japo siye sote sio wanafilosofia, mtakubaliana nami kuwa ili kubuni kitu mtu unaanzia pale unapopaweza. Aghalabu unaweza kubuni kitu kizuri zaidi mara unapoweza kujenga uwezo mkubwa zaidi kuliko ule ulionao wakati ule. Haijalishi ni kwa njia gani utapata ule uwezo mkubwa zaidi, lakini huo uwezo unahitajika ili uweze kuvuka pale. Shurti uwezo huo upatikane, na kwa njia yeyote ile. (By all means necessary)

Sasa sisi tunapoangalia wenzetu katika tasnia za sanaa duniani, na tukaona jinsi walivyojijengea taasisi zinazofanyakazi vizuri tunadhani kuwa hizo taasisi ndio misingi ya maendeleo yao. La hasha, misingi ni zile fujo walizokuwa wanafanya na walizotaka kufanya hata ikabidi au wakaweza kujijengea miundombinu ya kujiongoza ili kuwezesha mfumo fulani wa ufanyaji kazi kibunifu, uwepo na ukuwe.

Kwa mfano hiyo Hollywood tunayoisifia ilitokana na majaribio mengi yanayofanana na jinsi Nollywood na Bongo movies walivyojitengenezea miundombinu iliyoweza kujenga taasisi kama kimasiharamasihara vile.
Hapa kwetu Bongo movies ililalia katika vitu vitatu:
Lugha ya Kiswahili- ili kupata soko kubwa (social access)
Kutengeneza kitu kwa bei nafuu ili kupata faida- (production formula)
Kupambana kiharamia katika soko - ili kujenga soko (piracy)

Ukiangalia vyote vitatu vilikuwa vinakwenda pamoja na japo vilikuwa na mapungufu mengi hayo mapungufu hayakuzuia kukua kwa biashara na papo hapo kujenga miundombinu inayokidhi haja za wakati ule.

Sasa sisi kwa kutaka kutengeneza miundombinu kamili tukaanza kwa kuona makosa tu. Hatukuangalia nini kinafanya kazi na kuweza kuisaidia tasnia kutokea ndani. Sisi tulikuja na mipango kamambe ya kusahihisha makosa. Kumbe kusahihisha kukawa  ndio kisa na mkasa wa kuua tasnia.

Ni wazi kabisa kuwa kina Steps, GMC na Pilipili walikuja na mifumo yao ya kiajabu na hata ya kutisha.  Na wote wakaanza kujenga miundombinu yao ili kujikuza katika soko. Haikuwa rahisi, na walipambana hata baina yao, lakini taratibu waliweza kukua. Shida ikawa mtazamo wetu wa kijamii ulioona kuwa huo ni wizi tu, na haukuona kuwa humo pia mlikuwa na fursa nyingi zaidi. Kwa kweli kuachia mapambano ya ndani kwa ndani katika tasnia kati ya majogoo wale kuliwezesha pia tasnia kukua. Kilichokuwa kinatokea ni kuuweka huru ubunifu.

Je huo ulikuwa mfumo usio waa (perfect)? Hapana, ulikuwa unahitaji kubadilika lakini si kwa kuungalia kutoka kwenye ubaya wake tu, bali pia katoka uzuri wake. Nadhani sisi tulikosea na mpaka sasa tunakosea kwa kuangalia makosa yanayotokea katika taratibu za kibiashara badala ya kuona fursa zilizopo na zinazoendelea kuwepo kwa sababu ya uhuru uliokuwepo. Taasisi zile zilikuwa zinamenyana lakini pia ziliachia wengine kujiunga na kumenyama katika tasnia.

Ninachosema hapa ni kuwa katika tasnia nyingi za utamaduni kitu kinachohitajika kwanza ni kukubali kuwa uhuru wa kufikiri na kufanya makosa ndicho kinachohitajika zaidi kuliko kitu kingine chochote. Unapozuia uhuru huo basi ujuwe chochote kile utachofanya kitapunguza kasi ya kukua kwa tasnia yeyote ya sanaa. Saa nyingine inabidi tufumbe macho kwa kusema mabadiliko fulani ni ya lazima. Kwa mfano Mwalimu Nyerere alipoona mini sketi zimeingia nchini na Waziri wake Rashid Kawawa akasimama na kukamata wasichana mitaani, yeye alisema, “jamani hii ni fasheni tu na kama ni fasheni basi itapita, tusijiudhi”. Ingezewezekana kabisa kuwa tungevuka msimu ule wa minisketi kwa kuwalazimisha wasichana wavae nguo ndefu lakini nina uhakika tusingejua ni kitu gani ambacho tumekikosa kwa kuzuia vile.

Serikali lazima iwe na mtazamo tofauti kwa tasnia za sanaa. Mtuvumilie kwa sababu msingi wa tasnia yetu ni utafouti wa mtazamo na kile kinachoendelea- kwa wakati wowote ule, ili tuweze kuendelea. Ikibidi basi tujenge mifumo ambayo itaruhusu huo uhuru kwa kiwango kikubwa cha kufumbia macho ili tusizuie matokeo makubwa zaidi toka tasnia hii muhimu.

Umuhimu wake unatoka wapi? Unatoka katika kuipa jamii nzima nguvu ya kujikuza haraka zaidi. Kujikuza kwa kuongeza ubunifu katika kila nyanja.

Unajua tunapenda kusahau kuwa, katika miaka ya 1980 wakati  serikali ya China ilipoona kuwa haina fedha ya kuzipa taasisi zao za maendeleo ilisema “sisi hatuwapi fedha bali tunawapa nafasi ya kutengeneza fedha kwa njia yeyote ile ili nyie mkuze uchumi ambao utatuletea fedha katika serikali kuu. Miaka mingi baadaye, baada ya serikali ya China kupata fedha, ndipo ilipoaanza kujenga miundombinu ya serikali kuu kusaidia na kuongoza taasisi za sanaa mitaani.

Mimi nasema nini sasa? Naiomba serikali ianze kwa kuingalia sanaa kama chombo wanachokihitaji sana ili kuweza kujikwamua hapa tulipo. Serikali inaweza kutumia fedha nyingi sana kujenga miundombinu ya kuisadia tasnia lakini fedha hiyo ikaishia mikononi mwa maofisa na tusione mabadiliko katika tasnia kwa sababu mtazamo huo haujengi ubunifu. Tutoe nafasi za wasani kujitathmini wenyewe, kwa kufanya makosa na kuigana na kujikosoa zaidi bila kuingiliwa na utaona jinsi tasnia hii itakavyopanuka. Mfano upo. Bongo movies.

Miaka michache huko nyuma tasnia ilikuwa inakua kwa mapana lakini baada ya serikali kuanza kuiingilia, ili kuondoa uharamia, tasnia imezidi kudidimia.
Wako wasanii watakaosema mawazo haya yataturudisha nyuma maana tunataka mirabaha, lakini ukweli utabakia kuwa mirabaha haikuzi ubunifu. Kuwa na fursa nyingi zaidi za kubuni ndiko kutakakotuinua na kuleta na kukuza mirabaha.

Najua kuna wale watakaoona mtazamo huu hauna mpango na hautatupa njia ya kujipima. Hapana. Kwanza kama nilivyoanza kusema, mpango umo ndani ya kutokuwepo mpango. Maana, kukua kwa mtoto wa Binaadamu kungechekwa sana na mtoto wa Twiga maana mtoto wa binaadamu anachukuwa muda mrefu mno kukua na watoto wote wangeliwa na Simba kama wangelizaliwa porini.

Sisi aghalabu tungeweza kuwabeza Twiga kwamba japo watoto wao wanainuka haraka na kuwakimbia Simba lakini risasi wanazopigwa nazo na mitego wanayowekewa na majangili vinazidi kuwanasa kwa uzuri zaidi kuliko hata Simba anavyoweza kuwala.

Tuwe na ujasiri wa kukubali kuwa tasnia ya ubunifu inahitaji uhuru wa kubuni zaidi kuliko mipango.

Siku zote nawaambia wanafunzi wangu kuwa kama tungekuwa na uwezo wa kujua filamu gani itakuwa bora sokoni basi tusingekuwa na filamu nyingi kama hizi zinazotengenezwa na wala tusingekuwa na biashara ya filamu, hata hii yenye tija hafifu. Lakini kule kutokuwa na tija tegemezi ndiko kunakoikuza tasnia hii, na hilo ni jambo jema. Kwa watazamaji au walaji wa filamu duniani kutuamini watengeneza filamu kuwa tutawapa kitu kizuri waendapo kuangalia filamu ndio msingi bora wa mahusiano kati ya tasnia na jamii. Imani.

Mtoto wa Binaadamu hapimwi kwa viwango vya mtoto wa Twiga.
Asalaam Aleykum!
Martin Mhando
Zanzibar

COMMENTS

Name

Anga,11,Arusha,27,Burudani,302,burundani,1,come rain,1,come sun,1,Crazy in Love kama wimbo kama wao wenyewe,1,dahh sijui kweli mbona shida,1,Dar utakuja je tumejiandaa,1,daraja sahau nini,1,demokrasia ya upanga,1,Dodoma,77,Dole tupu vijana wa zamani,1,Duhh bibie endeleza libeneke,1,Duhh kaisikie Walibana,1,duhh kwa mbagala mama lazima awe supa,1,Fedha za maiti haziliwi bure,1,Fedha za watu kwa maendeleo ya watu,1,Fikira,14,filamu,238,Filamu ndio kielelezo cha ukuzi wa taifa,1,flamu,7,Gandamiza Kibara baba ake,1,Habari,4810,habari. dodoma,24,hadithi,19,hakika tumeweka historia,1,hakuna noma jongwe,1,hapa kwetu inakuwaje vile,1,hasira hasara,1,hata maji,1,hataki masikhara na maisha yake,1,hatubonyezi kizenji,1,haya ndiyo mambo ya Ulaya,1,haya si yangu ni ya mdau mwenye hasira,1,haya wabongo na mambo kutoka nje,1,He he he wananikumbusha upishi wa shaba,1,Headline,1,Hii hurejesha uhai,1,Hii iko sawa kweli?,1,Hii imekaa vizuri,1,Hii inakaaje vile,1,Hii kweli noma,1,Hii maana yake Moro kuna uhaba wa chakula,1,Hii mexico,1,Hii mihasira mingine bwana,1,Hii ndio moro sio mpaka dar,1,hii ni hatari,1,Hii ni kiboko anayetaka kubisha ajibishie tu,1,Hii ni moja ya staili za kunyoa nywele,1,Hii si lukwangule,1,hii staili mpya,1,hili ni jengo pacha la malaysia ghorofa 88,1,Hivi ni ngoma tu,1,hivi nini siri za serikali,1,hivi sisi tunajua kama kuna vitu vya aina hii,1,hivi vitu bwana,1,Hiyo ndiyo gharama ya demokrasia,1,Hizi imani nyingine ni hatari,1,Hizi takwimu hizi mhh,1,Hongera bibie,1,Hongera dada etu kwa kutuletea kaka etu (shemeji) kwani mwenye dada hakosi shemeji,1,Hongera sana,1,huhitaji mifedha kuwa msafi,1,Huko Ulaya,1,Huu ndio ustaarabu,1,huu ujiko utakuwa mkubwa,1,imetosha,1,Inahitaji nidhamu fulani,1,inakuuma au...,1,Inakuwaje kama filamu yenyewe itahitaji busu la nguvu,1,Inaonekana watanzania hatukuwepo,1,Ipo kazi Maximo,1,Iringa,22,Isiwe mijineno tu manake mihela hubadili watu kweli,1,Itakuwa laki moja ya halali,1,jamani huu kama si ushamba kumbe nini,1,Jamani mbona Mungu anatupigania,1,Jamani watoto wanatakiwa kupendwa,1,jamani.. jamani ukiikosa Diamond usijutie,1,Je nyumbani hakuna vitu vya aina hii?Tuambie,1,je walikuwepo watu wa huduma ya kwanza,1,Je watanzania wanalipa kodi,1,jela kwa raha,1,Jolie,1,juhudi za lazima kuinua filamu,1,kama si kiwanda cha chumvi nani atawajua hawa,1,Kama kweli ndio kweli basi kila heri,1,Kama Mkristo naamini hilo hiyo si sahihi,1,kama unajua kuyarudi nenda Malta,1,kama wao wanaweza sisi je,1,Kamua baba waache wakanyagane,1,karibu nyumbani dada yote maisha tu,1,karibu Tatiii,1,KARIBUNI,1,Katavi,5,kaza buti hakuna kukata tamaa inalipa,1,kazi kwako mheshimiwa waziri wa madini,1,kazi na burudani,1,keep it up bloggers,1,kero ya usafiri sasa kwisha,1,Kila chenye roho na mwili kitaonja umauti,1,kila kitu kina vitu,1,Kila la Heri jamila,1,kila la heri kwani ni changamoto,1,Kipya,51,Kiuno bila mfupa,1,Kolelo mzimu ambao bado hai,1,KUBWA,1,Kudumisha urafiki wa dunia,1,Kuna dalili za wasomi kukubali Uafrika,1,kuna makala humu humu ndani ya blogu sijui mnasemaje,1,Kuu,113,kwa mara nyingine tena Tigo imewezesha,1,Kwa mchanganyiko huu muungano lazima udumu,1,Kwa mihasira hajambo,1,kweli,1,Kweli ina mkono mrefu tuone,1,Kweli duniani tunatofautiana,1,la maana ni kuwa na jiko au vipi,1,labda halitabadilika tena,1,lakini mwafaka lazima,1,lengo ni kutafakari,1,leteni vitu tuvione,1,lets us,1,Lucy wanakuelewa hawa...,1,Lukwangule nyumbani kwetu,2,M ungu bariki mikono ya madaktari wafanikiwe,1,MAARUFU,1,maendeleo ya soka siku zote yanahitaji fedha ili yapatikane,1,maisha ni vyema kuyaangalia,1,MAJIBU,1,makala,51,mama ni mama tu anapendeza,1,mambo mengine we angalia tu,1,mambo msimamo,1,mambo sasa mchanganyiko,1,Mara nyingine huona tunakotoka kwa kuona wenzetu,1,Mashabiki wa rhumba mpooooooooo,1,Masitaa,12,Maskani,1,MASOKO,3,Masupa staa mnaoinukia mpoo,1,Matamasha,6,mavazi ya kuogelea yanaposhindaniwa,1,Mbeya,11,Mchakamchaka anti Asmah,1,Mchanganyiko,81,MCHANYATO,1,mchezo,5,mengi wanayoyaita siri ni public information,1,mfumuko wa bei mpaka noma,1,Mhh sijui watu wa Sua ambao wako huko wanasemaje,1,Mhh ugua pole dada watu wanataka burudani,1,Michezo,501,Michezo maalum inatakiwa kupigiwa debe,1,miguu,1,miguu babu,1,Mikataba mingine ama hakika tuiangalie hata wakopeshaji nao wanatugeuza sakala,1,MIMI NI KISURA NAJITAMBUA,1,Mimi sijajua hasa kumetokea nini kwani ninavyojua hawa huwa na ungalizi wa hali ya juu,1,Mimi simo,1,mimi sisemi,1,mkiwa chumvi basi mkoze,1,Mkiwa taa mulikeni,1,Mnaonaje je hii imekaa vyema,1,Mnaweza wakwetu hapa,1,Morogoro,51,mrithi wa mwanadada Whitney Houston,1,Mtwara,4,Mungu aiweke mahali pema roho yake,4,Mungu amrehemu,1,Mungu amweke pema peponi,1,Mungu awabariki sana,1,Mungu awe nao,1,Mungu ibariki Tanzania,1,Mungu tuepushe na imani hizi za kishirikina,1,mungu tufanye tuwe na upendo,1,Mungu twaomba utuhurumie,1,Muziki,350,muziki na fasheni,5,Mwanahabari,33,Mwanza,6,Mwendo mdundo dada,1,Mwenge huo utakimbizwa duniani kwa siku 130,1,Mwenge wa olimpiki ni ishara ya urafiki,1,Mzee wa Farasi nakupa saluti,1,Mzimbabwe huyu kutoka kwa mama mkali,1,N i dar mpaka Moro au bao tatu bila,1,Na sisi je,1,Naam kama haiwezekani hapa,1,Nairobi waanzisha tena utalii,1,namna bora ya kusaidia jamii,1,nani abebe hukumu na lawama,1,nani asiyejua utamu wa pipi,1,Nani kama baba,1,naona inafaa kuchangia mimi sitoi hoja,1,ndoa za mastaa huwa na mgogoro,1,nenda mwaya nenda,1,New Zanzibar Modern Taarab na wapenzi big up,1,news,5,Ni bikini kwa kwenda mbele,1,Ni Dar mpaka Moro au.. tatu bila,1,ni furaha za muungano,1,Ni kazi ngumu yenye kuhifadhi utamaduni,1,Ni kuchakarika kuonyesha urafiki na biashara pia,1,ni mfumuko wa bei au mfumuko wa nchi,1,Ni muhimu kutazama afya yako,1,ni muziki kwa kwenda mbele,1,Ni muziki mpaka China,1,Ni raha tupu,1,Ni Serengeti Premium Lager,1,Ni Tigo na mawasiliano ya kisasa,1,Ni wakati wa kuujadili utamaduni,1,Ni zaidi ya jazz,1,Nitasubiri and welcome home,1,nje je?,1,NUKUU YA LEO,1,nyie mnasemaje kuhusu hili,1,Ona Kolelo na sindikizwa na Wazee wa Gwasuma,1,ona vya dunia,1,One step ahead,1,patna mwingine mjamzito,1,Pengine anamuogopa Jada Pinkett manake kwa wivu..,1,picha,494,Pole Jamila hayo ndiyo mashindano,1,poleni sana,1,poleni sana wanyalukolo,1,Powa sana,1,Profesa jamaa wanakumaindi,1,Roho za marehemu zipate pumziko la milele,1,Ruvuma,9,sakata dansi mpaka kwenye kilele cha dunia,1,sasa kumebakia ugonjwa mmoja polisi kuendesha mashtaka,1,sasa mifedha kila mahali hongereni,1,Sasa ni mavuno,1,Sasa ni wakati wa kutafuta upenyo ndani ya IDOLS,1,SAYANSI,1,SAYANSI ANGA,1,See Uluguru Montains,1,serikali inataka kujihami kwanini,1,Show of support Big Up Madame,1,Si kitu kidogo hata kidogo,1,si unajua tena namie naimwaga hivyo hivyo,1,Siasa,346,siasa habari,2,Sijui kama City wanajua Mbagala noma,1,Sijui tunaishi karne gani yailahi,1,Sinema,9,sio advencha....kaaa ...niko kibaruani,1,Sisi ndio tunaanza vitongoji,1,Sisi yetu macho na masikio,1,Slow slow jamani,1,sto,1,tabasamu kali la mwenge wa olimpiki,1,Tabora,1,Tazama Waziri Mkuu Pinda wasije wakapindisha maamuzi yako,1,TEKNOLOJIA,1,Thats big man game,1,This is crazy Africa,1,This is Mgeta,1,Tibet wamegeuza Olimpiki jukwaa la siasa,1,Titbits collection,1,Tubadili tamaduni,1,Tuchangie mambo yaive,1,tuendeleze sanaa,1,tuienzi na sisi mbona wizara haituambii,1,Tuipeleke kaskazini,1,Tuisaidie serikali shida ya Mererani,1,tujue namna ya kupumzika,1,Tulienda kustarehe au kufanya fujo,1,Tumsaidie mtototo huyu kurejea katika hali ya kawaida,1,tunahitaji haya,1,Tunajifunza kweli kutoka kwao,1,Tunapandisha chati tu,1,Tunasubiri,1,tunazidi kuhesabu siku,1,TUNAZISUBIRI ZA VINARA ADAR,1,Tuombe nafuu kwa wagonjwa,1,Tuombe rehema kwa mungu,1,Tuone yatufae,1,Tusingoje wengine watusemee,1,tutampa tafu kubwa Prof,1,tuuenzi utamaduni au vipi,1,Tuukuze na kuulinda,1,tuvipende,1,tuwalinde maalbino,1,Tuwe kweli wakweli,1,ubunifu siku zote hulipa,1,uchumi huzunguka kwa kuwawezesha wasukaji,1,udumu muungano,1,Ugonjwa huu wa sasa ni kitendawili,1,Ukiiona kolelo utaipenda,1,Ukirejea salama kila mtu anafurahi,1,Umelenga Mkuchika utamaduni unakufa,1,unaposaka uwakilishi wa dunia,1,urafiki,1,Usisahau wazee wa Ngwasuma,1,UTAMADUNI,1,Video,2,Vionjo vipya ndani ya Gwasuma,1,Vita dhidi ya ufisadi,1,vitongoji Miss Tanzania navyo vimeanza,1,Vitu vikali vyazidi kuingia Dar,1,Vituko,77,Vituo vya polisi Tanga vyatelekezwa,1,VIVALO,1,Wacha tujifue,2,Wadau ilitolewa kiingereza,1,wakali wa ubunifu,1,wala usibabaike mwakwetu hii noma,1,wanadamu wanapotaka kujua zaidi,1,wanasema mpaka kieleweke,1,Wanataka kujua mali za JK na wengine,1,Wanawake wenye mvuto: Monroe,1,Wapo mabinti wa matawi ya juu,1,watu wanapofanya weli kwenye sanaa,1,waweza kurejea enzi ya Moro jazz na Cuban malimba,1,Wazee tupo kusindikiza,1,waziri,1,welcome dar baby,1,Wenzetu wameona sisi tunangoja nini kuangalia,1,wewe unasemaje,1,wigo mpana wa utamaduni,1,wilaya ya 'Mbagala' mlie tu,1,Yaaani sijui itawezekana,1,Yaani wakati mwingine hata huelewi prioty over priority,1,yeye mbele sisi nyuma,1,Yote maisha dada,1,ZA MOTOMOTO,1,Zanzibar,79,zawadi zinatakiwa ziende shule,1,ZILIZOTIA FORA,1,zitachangia kupunguza makali ya bei za umeme,1,
ltr
item
Lukwangule Entertainment: UCHOKOZI YAKINIFU KWA SANAA NCHINI
UCHOKOZI YAKINIFU KWA SANAA NCHINI
Lukwangule Entertainment
http://lukwangule.blogspot.com/2020/06/uchokozi-yakinifu-kwa-sanaa-nchini.html
http://lukwangule.blogspot.com/
http://lukwangule.blogspot.com/
http://lukwangule.blogspot.com/2020/06/uchokozi-yakinifu-kwa-sanaa-nchini.html
true
934549962738256429
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy