Kazi ya Mussa Banzi yenye simulizi za asili
Na Beda Msimbe
TUPO kwenye wakati ambapo simulizi nyingi za mapenzi lakini
kila simulizi unaweza kuliona raha yake kubwa ni kuonesha mitikisiko ya kupenda
na kufumaniana au kuachana.
Simulizi hizi siku zote zimelenga kuywapata vijana ambao ndio
waangalizi wa sinema.
Mussa Banzi naye hayuko nyuma katika hilo, lakini kwa mara
nyingine tena mapenzi ameyaunga katika simulizi la zamani, simulizi ambalo
chanzo chake ni kitu kidogo,kisasili cha ndege Gawa.
Kwa wakazi wa Mkuyuni ndege Gawa wamempachika jina la mpasua
sanda kutokana na ukweli kuwa anapolia au unapomuona usiku ujuwe hapo kwenye
nyumba yako kuna mushkeri utakuandamana, kifo.
Lakini unapofika mwishoni mwa hadithi hii unagundua kwamba
ndege huyu anapoonekana mchana hasa jioni huwa anatoa taarifa nzuri ya
mabadiliko ya maisha yako kutoka kule unakotoka.
Gawa ndiye anayejenga simulizi ambalo upande mkubwa lina chuki
na husuda na migogoro ya kifamilia ambayo ilikuwa inatishia ustawi wa maeneo na mapenzi.
Naam madairekta wawili Mussa Banzi na Mgeni khamisi walifanya
kazi ya kutosha kutafuta watu
wanaofanana na mazingira na mazingira yanayofanana na hadithi hii, hadithi
ambayo ina aina ya raha yake kwa kuzingatia kwamba imetwaliwa kutoka katika
imani za kiasili.
Simulizi lake ,limejijenga katika imani za wananchi kwamba
ndege huyo gawa anapokutokea unajawa na mikosi au misiba. Lakini jinsi banzi
alivyotwisti simulizi ndege huyo anakuja na taswira nyingine, ya bahati na
mabadiliko ya maisha ya watu.
Binti ambaye alikuwa anangoja kukutana na mchumba wake mtoni
anakuta akimshangilia ndege gawa kwa rangi zake, lakini mwenzake anamuona
kwamba, ndege huyo ni mikosi.
Baada ya kupewa maelezo hayo
Avana , nafasi iliyochezwa Husna Chobis, anaondoka mtoni pale na kuelekea
kwa mganga Nyambi nafasi iliyochezwa na Nyambi kuitaka tafsiri ya kuonwa na
ndege huyo jioni ile.
Maelezo ya fundi (mganga) yanamchanganya Avana ambaye alisema
kwamba ana mchumba wake Diko, mtu ambaye alikuwa anajua kusoma.
Fundi anasema kwamba Avanna hataolewa na mchumba wake wa sasa
lakini ataolewa na mchumba ambaye hajui kusoma na anaishi maisha ya kawaida
kijiji kwao.
Utabiri huu wa Nyambi ndio unakuja kutokea lakini si kwa namna
ambayo wewe unaweza kuing’amua kwa haraka.
Anaporejea kutoka kwa Fundi, Avana anampasulia wazi mpenzi
wake Diko kwamba ndiyo imetoka hawawezi kufunga ndoa.
Ukiangalia simulizi hili lipo wakatik wakoloni wanaingia na
wananchi wanapewa maarifa ya dini ya wazungu lakini wakati huo huo watu
waliopata nafasi ya kusoma wakila njama kuwapora wengine mali zao.
Pili majeshi aliyecheza nafasi ya mama yake Avanna alionekana
kuwa kweli mama mchimvi ambaye alikuwa
anakula njama za kumpora Chega eneo lake la mto mbezi , eneo alilorithi kutoka
kwa baba yake.
Chega ambaye kitaalamu ni fundi (mganga) bado kijana lakini
akiishi na dada yake Otesa nafasi iliyochezwa na Sada Ubeo.
Katika mazingira yaliyolelewa na simulizi hili uadui
unaibuliwa tangu mapema, uadui ambao unafanya familia ya Chega na akina Avanna kutolewana.
Familia hizi zenye uadui wa muda mwingi na njama za wazi za
kutaka kumiliki mali za wengine zinasababisha vifo vya watu wasiokuwa na hatia,
lakini mwishoni sumu iliyooenea inakuja
kutanzuliwa na haja ya matibabu kwa Avanna kitu kilichotokea bila hata
kutarajiwa.
Baada ya njama za kutwaa ardhi kirahisi kutofanikiwa
zinaandaliwa njama za kumuua Chega lakini kwa bahati mbaya anauawa mtu mwingine
na Chega analipuka kwa hasira.
Anafika kwa akina Avanna na kuanzisha varangati kubwa ambalo
kesho Avanna mwenyewe anashiriki lakini kwa namna ya pekee ugomvi unamalizika na mama Avanna
anaendeleza njama zake kwa kumfikisha Chega kwa mamlaka.
Chega anashinda shauri lile na kuwashutumu sana familia ile
kama muuaji.
Lakini siku moja Avanna akiw amtoni anaanguka na mtu
aliyemuohjna alimkimbiza kw amatibabu nyumbani wka fundi Chega ambaye awali
anakataa lakini baada ya kuraiwa na dada yake anamtibia na anapoamka anagombana
naye kwanini anamshikashika.
Naam, ni simulizi la aina yake ambalo baadaye linaokoa na
kubadili kabisa tabia ya Avanna,anatokea kumpenda Chega na kukubali kuolewa
naye, mtihani mkubwa ukiwa inakuaje watoto wa maadui wanapokutana na kuanzisha
mapenzi.
Kuonesha kwamba kweli anampenda Chega, Avanna aliiba hati
halisi ya eneo la mto mbezi aliyoibiwa Chega na rafiki yake Funga na kumrejeshea
mwenyewe.
Lakini katika kumpoteza Chega mama wa Avanna aliagiza wabaya
wake kufanyakazi ya kumuua Chega ambaye alipondeka vibaya lakinbi alipona na
baadaye yeye na Avanna kufanya mazungumzo na mama yake Avanna.
Simulizi hili linamalizika wka amani zaidi na kuonekana kwamba
kumbe mapenzi yanaweza kuondoa chuki.
Gawa yule ambaye
mtabiri Nyambi alisema kuonekana kwake kutabaduili mfumo wa Avanna,
kweli alipeleka salamu sahihi kwani kutoka mtoto wa kike jeuri asiyejali, mpaka
mpenzi mwenye kujali na hata kuwa fimbo ya kujishikiza Chega.
Moja ya vitu vya kifolosophia ambavyo unaweza kuona katika
picha ni maji yakiwa yanatiririka na katika simulizi za watu wa Morogoro, maji
ni uhai na unaondoa fitina zote na kusafisha dhambi.
Maji huunganisha na maji
hutumika kutambika. Kwa wanaojua maana ya maji ,banzi alifanya vyema kuanza na
kumalizia katika maji ambako ndiko kwenye uhai.
Hadithi nimeipenda kwa kuwa ilikuwa imejaa nakshi
zinazotakiwa, simulizi za kienyeji katika mazingira ya kienyeji, majira ya kati
ambayo hayaumizi sana.
Kiukweli simulizi la gawa ambalo pengine ni simulizi la nne
lenye mwelekeo wa asili kutoka kw a Mussa Banzi kunaonesha bado haja kubwa ya
watuj kuendelea kutumia masimulizi ya zamani ambayo yapo tele kutengeneza vitu
vyenye asili ya kikweli kweli.
Banzi ndiye aliyemwezesha Jennifer Kyaka kutokelezea katika
dunia ya uigizaji katika filamu ya Odama,
moja ya filamu zenye kusaka mazingira ya zamani buila kutumia
kompyuta.Filamu nyingine ni Beyonce na Adima.
Simulizi zote hizo huwa zimelenga kusema kwamba mapenzi ndio
hasa mwisho wa migogoro na matatizo ya mali na maisha ya binadamu.
Aidha namna ya watu wanavyozungumza katika filamu hizi inakupa mazingira bora zaidi za namna
nyingine ya kuigiza huku ukiwa hupati vionjo kinyume na vile ambavyo vinaharibu
na kuchafua hali ya hewa.
Simulizi hili bado unaweza kuliona na watu wengine wakubwa kwa
kuwa mapenzi si ya kuchusha na wala mauaji hayatishi kihivyo. Usiku wake
umechukuliwa katika hali bora zaidi, bila kutegemea kompyuta.
Katika simulizi za kawaida hii nimeipenda kwa kuwa ukimtazama
banzi unajua unaangalia sihnema zenye mwelekeo wa kuonesha maisha ya kati
kwenye mabadiliko ya ukoloni na uhuru. Je una hoja katika hilo? Usijali mimi
nipo katika msimbebeda@gmail.com au
SMS 0713176669
mwisho
DOA LA NDOA
Sijamwelewa Mtitu
KUSEMA ukweli, haki ya nani vile sikuweza kumwelewa dairekta wangu William Mtitu katika sinema yake ya Doa la Ndoa. Kwenye sinema hii kinyume na fikira na huwa inanoga ikiwa hivyo, watu wawili wanauawa. Dairekta anamuua mtu kwa risasi na mwingine anamuua kwa zidisho la dawa katika mwili wake.
Niliona si sawasawa, lakini nikasema huyu dairekta anayependa kuua watu katika simulizi zake za kuomba msamaha ana akili gani hasa? Sitaki hata kujibu kwani nilikuwa nadhani simulizi kama Doa la ndoa, filamu ambayo inafanana kijina na filamu fulani ya marehemu Kanumba, inayohusu wanandoa ilistahili kuonesha matunda ya kuomba msamaha na kupatikana.
Kwa sinema ya Kanumba tatizo lilikuwa hilohilo kunyimwa nafasi ya kufanya mapenzi, hali iliyomfanya atafute kwingine, ila katika sinema ya mtitu pamoja na kunyimwa nafasi hiyo jamaa aligangamala, akatulia kumsubiri wake ajirudi.
Mimi nafikiri hatujafikia ubazazi wa Hollywood wa kuua bila sababu na katika simulizi hili la mapenzi mauaji yaliyofanyika yana walakini hasa kutokana na staili ya masimulizi na mantiki ambayo mimi naweza kusema yanastahili kuwa na uhai, hasa ukizingatia kwamba mauaji hayo hayakutatua tatizo bali kisirani.
Nasema kisirani kutokana na ukweli kuwa mwandishi wa skripti alijitahidi sana kuonesha mapenzi ni sehemu ya maisha kukoseana na kusameheana na kuwa mkweli katika roho. Hapa wawili walikuwa si wa kweli katika roho, lakini akamwacha mmoja akiwa huru kama vile yeye si chanjo cha upuuzi ulikokuwa unafanyika miongoni mwa wanandoa wawili Mussa Kompaund kama Alex na Irene Uwoya kama Winnie.
Mariam Ismail kama Irene ndiye hasa mpuuzi, kwani alikuwa kwa namna fulani anajua anachokifanya Winnie na jamaa yake Irene, Nashon nafasi iliyochezwa na Ibrahim Mputa.
Ndani ya sinema hii aliye na moyo wa mapenzi ya kwelikweli ni Alex ambaye pamoja na kushughulikiwa na mkewe mara mbili na kumfumania mara moja bado alidiriki kumrejesha nyumbani na kumwandalia Hepibesidei bila kujua kwamba mkewe amelamba kiasi kikubwa cha dawa zilizomuua na pale hakuwa amepumzika bali amekwenda moja kwa moja.
Kilikuwa kilio kwa Alex kilio ambacho mimi nasema si cha lazima sana kufanyika kwani bado filamu ingelipenda kwa kumuua mtu mmoja au kutomuua kabisa, lakini jamaa wakaendelea kuishi. Doa la Ndoa ya Mtitu iliweka twisti ndogo sana ambayo haikupi muonjo wa moja kwa moja, lakini mastaa ni wale waliokuwa na bifu la leo na kesho na jana Wolper kwa Kanumba na Uwoya kwa Mtyitu.
5 effects wanaweza kuwa na sababu za kutafuta fedha za chapuchapu, lakini wanaua ukuaji wa filamu kwa kuwa na mawazo ya skripti yanayofana na mno ila mwisho tofauti.
Masuala ya mapenzi humu ndani na hasa mazungumzo yake pamoja na Uwoya kutumia sana lugha ya kujishaua (ndio fikira zangu) na Kompaund kuonekana kutulia, mtu anayejua anachokifanya, sinema hii huwezi kuwa karibu na jamaa unayemheshimu kidogo lugha imekuwa kama tundu la maji mabovu, asali inaonekana kutiririka muda wote na hata maleba hasa ya bibie Uwoya yalikuwa yanatoa motisha mwingine.
Usibishe ukadhani nadanganya kuna maneno hapa yanaweza kukutia wazimu... mapenzi alisema Irene, si gari si nini bali namna unavyojisikia ukiwa pembeni mwa mtu ... ah hapo anamwambia mchuchu wake na si mume wake katika hoteli ya kifahari waliokokuwa wakifanya vurugu zao.
Simulizi la Mtitu kama Dairekta linaanza pale ambapo watu hawaelewani kisha tu naingia katika sababu na sababu yenyewe ni ujauzito uliotoka. Lakini ukiangalia utaona shida hasa pale ambapo Nashon rafiki mkubwa wa Alex anamtwaa mke wa jamaa huku akimwambia jamaa yake anachotaka mkewe ampe kwani ipo siku mambo yatakuwa poa kumbe yeye alikuwa akuimla kisogo jamaa.
Unaweza kusema kwamba ni urafiki wa mashaka na lazima mtu uwe na mashaka lakini katika simulizi hili, unaweza kusema wazi kwamba kuna kuchapia kwingi katika maisha, lakini wapiga picha walienda vyema huku mhariri akitumia zaidi mtindo wa kufyuzi badala ya kukata huku akifunga na kufungua matukio dalili ya kukua kwa utaalamu wa kuhariri filamu.
Mimi nimekuwa na hamu ya kumuuliza Mtitu hivi inakuwaje anaua kama ametumia maneno matatu kama yale ya mapenzi, ya kuombana msamaha na angalau Alex na Winnie walikuwa wameanza gari lao upya.
Niliyemuona kuwa staa hasa wa sinema hii Kompaund wengine waliuza sura na maumbile yao ingawa mdada Mariam akipata picha bora zaidi hasa ya aksheni anaonekana kutulia vyema katika skrini.
Je, niseme nini hasa kuhusu filamu hii ya kuona majumbani?Kama vile hujui maneno ya kuliwazana baada ya ukakasi mkubwa unaokumbana nao huku ukiambiwa baada ya kazi..'baby your are the best' , ukiangalia bila kutumia akili unaweza kumshushia kipondo cha wazimu dairekta wa sinema hii kwani amekuletea gogoro ambalo linafunua mtima wako.
Katika maana halisi ya doa, filamu hii haina doa ina mtafaruku, kwani doa hufutwa na nguo kuvaliwa huyu Mtitu hakutaka kuvaa aliwaua wahusika wake kama mshahara wa dhambi ni mauti, hii si sawasawa.

FUNGATE
Kwanini Dairekta Claud 112 amuua Niza bila sababu?
WIKI hii nilipata nafasi ya kuangalia sinema ya Fungate ambayo imetengenezwa na Issa Mussa maarufu kama Claud 112.
Katika sinema hii pamoja na kuridhika na staili ya uhariri nilisikitishwa na kitendo cha dairekta kumuua Niza (nafasi iliyochezwa na mdada Yobnesh Yussuph) bila sababu yoyote ile ya msingi. Nilikasirika kwa sababu nyingi sana na moja ya sababu hizo Niza alipata shida ambazo si zake na kumpelekea kujiua si sawa sawa.
Wakati naandika makala haya mafupi nilimtwangia Claud 112 kwa ufafanuzi kama Dairekta kwanini alimuua binti yule akacheka sana kisha akasema:" kiongozi hadithi ile imelenga kutufunza wanaume tusisababishe umauti kwa wanawake kwa kuwaahidi tusichowapa"
Alisema katika mazungumzo yetu kwamba mara zote wanaume tumekuwa tukijidai kwamba ndio wenye maamuzi , hali ambayo baadae inawaathiri wenzetu hasa wale wenye maamuzi ya haraka na mara zote tunasababisha kifo kama Niza alivyofanya baada ya kufikiri hawezi kupata penzi la Tobi (nafasi iliyochezwa na Issa Mussa).
Simulizi la kadhia hii ni jema sana hasa staili iliyotumika ambayo ilikuw ainafanya twisti ndani ya simulizi na kuona mwishoni kabisa mkasa na kisa ni kitu gani.
Ndani ya filamu hii makosa yamepachiwa sehemu mbili yaani kila upande unaonekana kufanya vurugu fulani. Wakati Tobi (Issa Mussa-Cloud 112) anamvuruga Niza na kumuahidi kumuoa kisha anaenda kumuoa Luwi (nafasi iliyochezwa na Manka Maina), Luwi yeye alikuwa ametelekeza penzi la Kila (nafasi iliyochezwa na Liberty Msuya).
Kimsingi filamu hii ina rangi ya kupendeza kwa maana ya kwamba matukio mengi yapo kikubwa zaidi na japokuwa inakubalika kwa daraja la 16 kipo kipande kidogo kinaleta kiza (katika mapenzi ya kubakana) kisha katika mauaji. Cut katika sehemu zote mbili zilikuwa za kiungwana, uhakika na bila kupoteza ladha unakuja kujua nini kimetokea.
Naam, ni Fungate na Tobi anaondoka na Luwi kwenda kukamilisha ndoa yake, nje kidogo na kwao mahali bomba ambako walitarajia kutulia, lakini njiani wanafuatwa na mdada mmoja ambapo tangu unaanza simulizi mpaka eneo fulani huweiz kujua kulikoni.
Huku kulikoni ndio kunafanya simulizi hili uendelee kuwa nalo mpaka mwisho huku vipande fulani, vikiashiria imani ya Dairekta kwamba akili ya binadmau huiona matukio kabla ya kutokea labda uinachoshindwa ni kutafsiri tu. Tobi anafuatwa na mwanamke ambaye alikuwa amemuahidi kumuoa na mbaya zaidi hakuwa amemwambia mwenzake ambaye naye huko alikotoka alikuwa amemtelekeza mwenzake kwa kukosa fedha na kazi.
Wakiwa ndani ya gari safi la kispoti Tobi na mkewe wanafika katika hoteli ambayo Niza naye anafika. Unaweza kusema ni bahati tu lakini baadaye unalazimika kuunga kwamba simulizi la hadithi hii linaenda mbele na nyuma na unapoanzia ni katikati.
Niza alipata taarifa ya wapi anapoenda Tobi na akamfuatilia na alikuwa na nia njema kwani kulikuwa na ahadi na pia kulikuwa na penzi na hata wafanyakazi wa ofisini kwake Tobi walikuwa wanalitambua hilo wakashangazwa na bosi wao kumuoa Luwi badala ya Niza.
Seleka la hotelini mpaka kifo ndilo ambalo unatakiwa kuliangalia.
Kimsingi Issa anapanda katika kutengeneza sinema zake na unaweza kuliona hilo hasa katika lugha, watu wanaofanya kasti,wanaotengeneza sinema na hata katika ufuatiliaji wa mambo.
Anayefurahisha sana katika sinema hii si Cloud 112 ni Yobnesh Yussuph, mwanamke aliyecheza kama Niza,aliyependa kisha akaona penzi lake linavyoyeyuka mithili ya barafu, tena kwa muda mfupi tu akashangaa amemkosea nini Tobi.
Unaiona hisia ile kwenye macho, kwenye mwili na kwenye kila kiungo chake na watu kama hawa ndio wanaoipa chati sinema, plani zake, lakini pasi shaka dairekta akiwa pia muigizaji nayo imeipa ladha fulani kwani mwenyewe alijinyima sana laini za kuzungumza akawapa akina manka na Yobnesh.
Mimi ningelisema kwamba watunzi wanakomaa, wpaiga picha wanakomaa na wahariri wanaanza kuelewa kwamba hawatengenezi michezo ya kuigiza bali wanatengeneza filamu.
Ukiangalia sana picha hii si mikasa ya ndoa, ni maamuzi mabovu yasiyozingatia hisia za watu, uzushi wa wanaume na mapenzi yanavyopofusha maisha na kutufanya tuwe na kauli zinazosababisha karaha kwa wengine.
Kutapata na ukweli anaoujua baada ya kukumbushwa kunaleta hisia kali kwamba wanaume wanatakiw akuwa waangalifu sana katika maisha na hasa kwenye ahadi zao.
laini ambayo nitaikumbuka ni ile ya kwenye ndoto, wewe sizungumzi na mbwa nazungumza na mwenye mbwa.. alisema Niza katika ndoto ya Tobi.. ishara mbaya kabisa.
Mwisho
Megan Denise Fox :Mwanamwali aliyefanya vyema ndani ya
Transformers: Revenge of the Fallen
NI mwanamitindo muigizaji ambaye kila anapoigiza anakuacha hoi. Ni mwigizaji aliyezaliwa Mei 16, 1986 wa Marekani aliyeanza shughuli zake za kuigiza 2001.
Alipata nafasi ya kujulikana kw aupana mwaka 2004, alipoigiza Confessions of a Teenage Drama Queen. Mwaka 2007, aliigiza Mikaela Banes, kama mapenzi wa Shia LaBeouf kwenye filamu ya Transformers. Fox alicheza tena katika mititiriko wa filamu hiyo wa mwaka 2009: Transformers: Revenge of the Fallen. ndio filamu niliyoipenda nitakusimulia kama nitapata muda na mwaka 2009 aliigiza filamu nyingine ya Jennifer's Body.
Fox pamoja na kuwa muigizaji mzuri ni mrembo wa haja ambaye alitokea katika majalida kadhaa ya urembo.
Mwanamwali huyu aliyezaliwa Oak Ridge, Tennessee, Marekani aliolewa mwaka 2010 na Brian Austin Green na wana mtoto mmoja ni binti wa Gloria Darlene (née Cisson) na Franklin Thomas Fox. Wazazi wa Fox waliachana wakati yeye akiwa na miaka 12.
Akiwa na miaka 16 aliigiza filamu ya Holiday in the Sun, (2001) baadaye aliigiza What I Like About You na Two and a Half Men, Bad Boys II (2003). Mwaka 2004, aliigiza Confessions of a Teenage Drama Queen akiwa na Lindsay Lohan,akicheza kama Carla Santini, mpinzani wa Lola (Lohan).
Fox pia aliigiza katika televisheni ya ABC ya Hope & Faith, akicheza kama Sydney Shanowski na Jennifer's Body mwaka 2009.
Fox in October, 2007 with two of her tattoos visible
Fox ambaye amekuwa akilinganishwa mara kwa mara na Angelina Jolie na vyombo vya habari vya Ulaya Magharibi kutokana na michoro katika mwili, na nywele na urembo wao kwa sasa anafabnyakazi ya ziada kuondoa michoro hiyo.
Pamoja na urembo wake Transformers ndiyo iliyomfanya ajulikane zaidi katika dunia ya sinema , alimudu nafasi hiyo.
Fox alijuana na muigizaji Brian Austin Green kuanzia mwaka 2004, walipokutana katika usukaji wa Hope & Faith akiwa na miaka 18 na jamaa akiwa na miaka 30. Mwaka 2006, walichumbiana lakini wakiachana 2009 na kutangaza kurudiana tena Juni 2010 na Juni 24, 2010, wawili hao walioana kwa faragha katika hoteli ya Four Seasons Resort katika kisiwa cha Hawaii.
Fox na Green wana mtoto mmoja kwa jina la Noah Shannon Green, ambaye alizaliwa Septemba 27, 2012.
Fox ni mama mdogo kwa mtoto wa Green anayejulikana kwa jina na Kassius (Aliyezaliwa 30, 2002), ambaye alitokana na uhusiano wake na muigizaji Vanessa Marcil Giovinazzo.
Filamu ya Transformers: Revenge of the Fallen 2009 aliyocheza kama Mikaela Banes akiwa na akina Shia LaBeouf, Megan Fox, Josh Duhamel, Tyrese Gibson, na John Turturro, huku Rainn Wilson akiwa kama profesa anayejua kuchekeshainaanzia pale ambapo filamu ya kwanza imeishia.
Huku adui katika sinema hiyo Megatron akiwa amezikwa chini kabisa ya bahari, Optimus Prime na rafiki yake Autobot wakiwa pamoja na askari wanadamu wanaangalia mabaki yaliyotawanyika duniani kote ya Decepticons .
Wakati mambo hayo yote yafanyika Sam Witwicky, ambaye ndiye shujaa wa filamu ya kwanza ya mwaka 2007, yuko bize akijiandaa kwa mwaka wake wa kwanza chuoni, rafiki yake wa kike, Mikaela Barnes, alikuwa katika gereji ya baba yake akiendelea na kazi bila kung'amua kwamba Cybertron ambaye ni miongoni mwa wazee wa Decepticon akijulikana kama “The Fallen” anatengeneza mpango wa kuivamia dunia.
Alikuwa anahitaji kufika katika chanzo cha energon, damu inayowaendeshaTransformers wote. Na kama akifanikiwa maana yake ni balaa kubwa na maangamizi kwa binadamu. Huku dunia ikikabiliwa na majanga makubwa Sam na Mikaela lazima waungane kwa mara nyingine tena na Optimus na Autobots kumkabili adui mpya mwovu na mwenye nguvu kubwa.
The Angel
FILAMU iliyotengenezwa nchini Norway imepelekwa kwa ajili ya tuzo za Oscar lakini uhakiki wa filamu hiyo uliofanywa na baadhi ya wahakiki inafanya ionekane kushindwa hata kabla ya wakati wenyewe.
Katika uhakiki wao wafuatiliaji wamesema kwamba unahitaji kuwa na moyo wa chuma ili kuweza kuipenda sinema hiyo ya uteja
ambayo inaonekana taratibu inaimeza dunia.
Filamu hiyo "The Angel," imetengenezwa
katika mazingira ya kudhani kwamba hakuna filamu nyingine ya aina hiyo
iliyokwisha tengenezwa.
Hali hiyo inatokana na kujirudia kwa
maeneo kadha yale yale yaliyozoeleka na hata katika sinema yenyewe maeneo hayo
yanaendele akujitokeza hapa na pale.
Mwandishi na mtengeneza sinema hiyo Margreth Olin anadai kuwa filamu hiyo
inamwakilisha rafiki yake , yaani simulizi ni la rafiki yake na ama hakika unaweza
kuona jinsi jamaa anavyoteseka naye katika njia nzma.
Mateja katika filamu hii ni
wengi wa umri tofauti lakini wanaishia
kwa Maria Bonnevie ambaye kw anamna Fulani analeta uhai kwa kuwa yeye
angalau anafanya vitu ambavyo ni sawasawa.
Hilo hasa ni kutokana na kumwangalia
motto wake katika masuala ya usafi vinginevyo filamu hiyo ni mbaya
huku ikiwa inaunyanyasaji wa kijinsia, pombe, ukahaba, na hakuna kitu
chochote kile kinachofanyika kuhakikisha kwamba hali hiyo inakemewa na
kurekebishwa. Inaonekana kama kitu kinachofaa.
Ukiiangalia kwa makini unaona kwamba
labda fuilamu hii haizungumzii uteja inazungumzia matatizo ya kifamilia kizazi
kwa kizazi. Kinachofurahisha ni kuwa amewatumia vyema wanawake kuelezea
tatizo lakini swali linalokuja ni kwa
namna gani anatengeneza filamu kama vile hakuna kilichowahi kuzunguzmwa kuhusu
uteja hasa ikizingatiwa kwamba kunasinema nyingi zimezungumzia shauri hilo.
Ni
shauri la familia kujikuta katika matatizo kutokana na uteja na hata
wazazi wanapokuwa wateja na watoto wanashindwa kule ainakuwaje hasa.
hilo nis hauri la pekee lakini mwendesheji Olin alipaswa kufahamu kwamba
ameishiwa na sinema nyingi za aina hii zimeshatengenezwa.
COMMENTS