TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI Sekretarieti ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) inaendelea na maandalizi ya Mkutano...
TAARIFA KWA VYOMBO VYA
HABARI
Sekretarieti ya
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) inaendelea na
maandalizi ya Mkutano
Mkuu wa Uchaguzi utakaofanyika Oktoba 26 na 27 mwaka
huu jijini Dar es Salaam.
Awali mkutano wa uchaguzi
ulikuwa ufanyike Februari 23 na 24 mwaka huu
lakini tukauahirisha
kusubiri maelekezo ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira
wa Miguu (FIFA), hivyo
tayari wajumbe wana taarifa rasmi kuhusu mkutano huo.
Orodha ya wajumbe
iliyotumwa awali kwa ajili ya Mkutano tunayo, isipokuwa
kama kuna wanachama wetu
wana mabadiliko ya majina ya wajumbe
watakaohudhuria
wanatakiwa kutuma majina hayo kabla ya Septemba 30 mwaka
huu.
Wanachama wa TFF ni vyama
vya mpira wa miguu vya mikoa, vyama shiriki na
klabu 14 za Ligi Kuu ya
Vodacom.
WAWILI WAPINGWA UCHAGUZI
WA TFF*
Wanamichezo wawili
walioomba kuwania uongozi kwenye uchaguzi wa Shirikisho
la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF) utakaofanyika Oktoba 27 mwaka huu
wamewekewa pingamizi.
Waliopingwa ni Wallace
John Karia anayeomba kupitishwa kuwania urais na
Vedastus Kalwizira Lufano
anayewania ujumbe wa Kamati ya Utendaji kupitia
Kanda Namba Mbili ambayo
ni mikoa ya Mara na Mwanza. Anyempinga Karia ni
Shamsi Rashid Kazumari wa
Dar es Salaam wakati Lufano anapingwa wa Samwel
Nyalla wa Mwanza.
Pamoja na mambo mengine,
Kazumari anampinga Karia kwa madai kuwa akiwa
Mwenyekiti wa Kamati ya
Ligi, aliwashawishi wajumbe wenzake kuingia mkataba
na Azam Tv wakati akijua
kamati hiyo ni ya muda, hivyo haina nguvu za
kisheria kusaini mkataba
huo.
Naye Nyalla ambaye pia ni
mmoja wa wanamichezo waliojitokeza kuwania ujumbe
kupitia Kanda hiyo
anampinga Lufano kwa madai hana uzoefu wa miaka mitano
katika uongozi wa mpira
wa miguu.
Kamati ya Uchaguzi ya TFF
chini ya Mwenyekiti wake Hamidu Mbezeleni
itakutana kesho (Agosti
28 mwaka huu) saa 4 kamili asubuhi kusikiliza
pingamizi hizo ambapo
wawekaji pingamizi na waliopingwa wanatakiwa kufika
wenyewe ndani ya muda kwa
vile uwakilishi hautakiwi.
* *
*YANGA, COASTAL UNION
KUUMANA VPL*
Ligi Kuu ya Vodacom (VPL)
inaingia raundi ya pili kesho (Agosti 24 mwaka
huu) kwa timu zote 14
kuwa viwanjani huku macho na masikio ya washabiki
wengi yakielekezwa kwenye
mechi kati ya Yanga na Coastal Union.
Mechi hiyo itachezwa
Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 10.30 jioni
kwa kiingilio cha sh.
5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000. Mwamuzi
Martin Saanya wa Morogoro
ndiye atakayepuliza filimbi wakati Kamishna
atakuwa Omari Walii
kutoka Arusha.
Mtibwa Sugar
itaikaribisha Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Manungu ulioko
Turiani mkoani Morogoro
wakati Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora
utakuwa mwenyeji wa
pambano kati ya wenyeji Rhino Rangers na Azam.
Vumbi lingine litatimka
kwenye Uwanja wa Mabatini ulioko Mlandizi mkoani
Pwani wakati maafande wa
JKT Ruvu watakapokwaruzana na wenzao wa Tanzania
Prisons kutoka Mbeya.
Mbeya City na Ruvu Shooting zitacheza kwenye Uwanja
wa Kumbukumbu ya Sokoine
jijini Mbeya.
Jiji la Tanga litakuwa
mwenyeji wa mechi kati ya Mgambo Shooting na Ashanti
United itakayochezwa
kwenye Uwanja wa Mkwakwani. Oljoro JKT itakuwa
mwenyeji wa Simba kwenye
Uwanja wa Kumbukumbu ya Sheikh Kaluta Amri Abeid
jijini Arusha.
*RATIBA COPA U15 KUPANGWA
ALHAMISI*
Ratiba ya michuano ya U15
Copa Coca-Cola ngazi ya kanda mwaka huu itapangwa
keshokutwa (Agosti 29
mwaka huu) saa 5 asubuhi kwenye ofisi za Shirikisho
la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF).
Michuano hiyo ya kanda
itaanza Septemba Mosi mwaka huu wakati mikoa
inakumbushwa kuwa
inatakiwa iwe imewasilisha usajili wa wachezaji wao
kufikia Agosti 28 mwaka
huu kupitia email ya TFF ambayo ni
tanfootball@tff.or.tz na nakala kwa madadi_salum@
yahoo.com
Pia mikoa inakumbushwa
kutowajumuisha wanafunzi wa darasa la saba katika
timu zao katika ngazi ya
kanda na fainali itakayochezwa Dar es Salaam
kuanzia Septemba 7 mwaka
huu kwa vile watakuwa katika mitihani ya kumaliza
elimu ya msingi. Timu
zinatakiwa kufika vituoni Agosti 30 mwaka huu.
Kanda hizo ni Mwanza
itakayokuwa na timu za mikoa ya Geita, Kagera, Kigoma,
Mara, Mwanza, Shinyanga,
Simiyu na Tabora. Mikoa ya Arusha, Kilimanjaro,
Manyara na Singida
inaunda Kanda ya Arusha.
Zanzibar itakuwa na
Kaskazini Pemba, Kusini Pemba na mikoa miwili ya Unguja
wakati Kanda ya Dar es
Salaam ina Ilala, Kinondoni, Lindi, Mtwara, Temeke
na mkoa mmoja wa Unguja.
Kanda ya Mbeya inaundwa
na Iringa, Katavi, Mbeya, Njombe, Rukwa na Ruvuma
wakati Dodoma, Morogoro,
Pwani na Tanga zinaunda Kanda ya Morogoro.
Mwanza itatoa timu nne
kucheza hatua ya fainali wakati kanda nyingine za
Arusha timu mbili,
Zanzibar (2), Mbeya (3) na Kanda ya Morogoro itaingiza
timu mbili.
*Boniface Wambura*
*Ofisa Habari*
*Shirikisho la Mpira wa
Miguu Tanzania (TFF)*
COMMENTS