ZIFF BUANA!: LAKE MTU HALIMTAPISHI

KWA mara ya kwanza katika historia ya kuanzishwa kwake miaka 25 iliyopita, Tamasha la Kimataifa la Filamu la Zanzibar (ZIFF) limepata mawasi...


KWA mara ya kwanza katika historia ya kuanzishwa kwake miaka 25 iliyopita, Tamasha la Kimataifa la Filamu la Zanzibar (ZIFF) limepata mawasilisho 3,498 ya filamu kwa ajili ya tamasha litakalofanyika Juni mwaka huu.

ZIFF ambayo ilibuniwa kwa malengo kadhaa lakini likiwa na mtazamo wa muda mrefu ulikuwa ni kuanzisha tamasha la filamu litakalodumu, la kuaminika na muhimu katika ulimwengu wa sinema, sanaa na utamaduni , mawakilisho ya mwaka huu yametia fora. 

Hiyo inatokana na ukweli kuwa katika miaka 25, urithi wa ZIFF umekuwa kielelezo chema kwa watu binafsi, mashirika, taifa na ulimwengu wa filamu na sanaa.

Aidha kama shirika lisilo la kiserikali ZIFF linalenga kuongeza uwezo wa ubunifu na mapato ya wanajumuia wa tasnia ya ubunifu kupitia kuboresha mifumo ya soko na ubora wa huduma za kiufundi na miundombinu.

Kuanzia mwaka wa 1998 lengo lake ni kuchangia ukuaji wa kijamii na kitamaduni na wa kikanda na tamaduni za kimataifa za uvumilivu. Hii inafanywa kwa kutoa nafasi kwaa matukio ambayo filamu, muziki, maonyesho na aina nyingine za sanaa hushirikishwa katika kukuza, kuendeleza, kufanya maonyesho, kuchunguza, na kuutambulisha utamaduni wa kikanda. 

Ikiwa inakwenda na mabadiliko ya kiteknolojia na sayansi kwa kuwa na matumizi makubwa ya tehama, njia mpya ya mawasilisho ya filamu katika ushiriki wa tamasha kwa kutumia majukwaa ya mtandaoni ya Filmfreeway na Festhome yanayomilikiwa na tamasha hilo, yameleta maingizo hayo. 

Mkurugenzi wa Tamasha, Profesa Martin Mhando anasema kutokana na uwingi wa filamu walilazimika kualika idadi kubwa ya wateuzi wa awali wapatao 40 klusaidia kazi za uchambuzi kupata zinazoweza kushiriki katika mashindano zipatazo 85.

Kwa kutumia Jukwaa la Filmfreeway wamepokea filamu fupi 2124, filamu za makala 415 na  filamu za dokumentari 766 na  filamu za wanafunzi 424.

Aidha alisema taifa lililoongoza kwa kupeleka mawasilisho mengi ni Iran iliyoingiza filamu 668 ikifuatiwa na India filamu 268 na Ufaransa 160.

Nchi zingine zilizowasilisha filamu ni Brazil (160), Marekani (155),Italia (115), Hispania (112),Tanzania (77),Ujerumani (76),Uganda (71),Kenya (54),Uingereza (53), Mexico (53),China (46), Nigeria (46), Rwanda (38), Afrika Kusini (35),Korea (34), Ukraine (23), Ghana (17),Ubelgiji (16),Tunisia (16), Iraq (15),Congo(15), Uswis (13),Lebanon (13),Senegal (10),Zambia (7),Pakistan( 5)Nepal (5) Sudan (4) Ethiopia (4) na  Japan (4).

 Kwa maingizo ya mwaka huu inadhirisha kuwa kulikuwa na maana kubwa kuanzishwa kwa shirika hili miaka 25 iliyopita, wakati tasnia ya sinema ilipotetereka.

“ ZIFF ilizaliwa kwa ahadi ya kuzaliwa upya kwa tasnia hio, ambayo tunajivunia. Kusema kweli Afrika Mashariki ina tasnia ya filamu iliyochangamka, inayochochewa na lugha ya  Kiswahili” anasema Profesa Mhando.

ZIFF likiwa ni tamasha la kitamaduni linaloipa Tanzania na Afrika Mashariki muda wa kuisanifu tasnia ya filamu kwa  kupitia mitazamo kadhaa, mwaka huu imeingiza sinema 14 za Kitanzania katika mashindano pamoja na usaili wa sinema 77.

 Profesa Mhando katika mazungumzo amezitaja filamu hizo za kitanzania kuwa  ni Janga  ya Ben Royal, Mvamizi ya Phillipo Ngonyani, Mpiganaji ya Daniel Manege,Mgeni ya Juma Saada,Obambo ya Fred Feruzi, Vuta N'Kuvute ya Amil Shivji, Uncle ya Hatibu Madudu na Nuru ya Maisha iliyotengenezwa na Juma Saada.

Pia kuna filamu fupi za Binti Jasiri ya Juma Saada, Binti Maringo ya Mohamed Hamis, Kazija ya  Mohamed Suleiman  (Muddy Sule, Black live Matter, Chumba 61 ya Edwin Kazoka na Urithi wa Mila ya Mohamed Suleiman (Muddy Sule).

Anasema kutokana na mabadiliko makubwa yaliyofanyika katika sinema za Kitanzania anatarajia zitatoa ushindani wa kimataifa hasa ukizingatia moja ya filamu ilishafanyiwa uzinduzi wa kimataifa mjini Toronto Canada

Filamu hiyo Vutan ikuvute  ndiyo itafungua pazia la ZIFF miaka 25 pale Ngome Kongwe mjini Unguja.

Pamoja na kuonesha filamu tamasha la Mwaka huu pia litajumuisha warsha kuu 6 zitakazotolewa na wakufunzi wanaotambulika zikiangazia jukumu la tamasha kwa taaluma ya filamu barani Afrika.

 Profesa Mhando anazitaja warsha hizo kuwa ni pamoja na: On Documentary (Docubox- Kenya); uandishi wa vipindi vya TV (Pilipili Entertainment, Tanzania); Wanawake na Filamu (EU); Maabara ya filamu fupi (Kenya/Wales); Utengenezaji filamu wa majaribio (Hispania na Ajabu-Ajabu); Uhariri wa filamu (Off-courts-Ufaransa).

 Warsha nyingine ni ya Wanawake na Filamu ambayo itawasilisha maoni ya waongozaji wa filamu wanawake jinsi wanavyoendeleza wahusika wao wanawake, na vile vile wanavyotamani watazamaji wawatambue.

 Pia kutakuwa na mipango kadhaa ya kikanda ya filamu itayozinduliwa wakati wa ZIFF ikiwa ni pamoja na kikao cha kwanza cha The East Africa Screen Collective (EASC), ambao ni muungano wa makampuni na mashirika yanayotetea uhuru wa simulizi katika sekta ya sanaa katika Afrika Mashariki.

Kama kawaida, tamasha litawasilisha programu zake ikiwa ni pamoja na Panorama za Wanawake, Watoto na Vijiji ambapo kunaangaziwa filamu na shughuli zinazozunguka vikundi vitatu vya jamii. 

Kazi hiyo inafanywa kwa kuungwa mkono na Umoja wa Ulaya (EU) na mwaka huu kutafanya shughuli za filamu na utamaduni Pemba baada ya kushindwa kufanya hivyo mwaka jana. Kutakuwa na maonyesho ya filamu juu ya mada ya wanawake na ujasiriamali, na vikundi vya uzalishaji vya wanawake vitafadhiliwa kuzalisha sanaa za mwonekano wa ZIFF na bidhaa nyinginezo.

Jambo kuu la tamasha hili mwaka huu ni utayarishaji wa Kitabu cha ZIFF@25. Kwa msaada wa EU na GIZ (Deutsche Gesellschaft für Internationale Zusammenarbeit).

“Tutachapisha kitabu cha ukumbusho katika safari ya kusherehekea historia ya miaka 25 ya ZIFF na kuweka kumbukumbu ya uungaji mkono wa wafadhili wetu kwa hafla hii muhimu ya kitamaduni nchini Tanzania.

Pamoja na kuwapo kwa mambo mengi yanayogusa filamu na uandazi wake mwaka huu kunaanzisha jukwaa la kudumu la ZIFF kwenye YouTube kwa filamu zilizopata kuoneshwa katika tamasha hilo. Mrejeo huo utajumuisha filamu ambazo zimeshinda au kuvutia katika ZIFF. 

“Tunakusudia jukwaa letu la Youtube liwe kituo cha kuangalizia na cha majadiliano ya ambapo watengenezaji filamu wanaweza kufikia hadhira muhimu na kufanya mazungumzo nao,” anasema Profesa Mhando. 

Kwa miaka 25 ZIFF imejitambulisha kama miongoni mwa matamasha matatu bora ya filamu barani na kwa kujiamini Profesa Martin anasema: “ZIFF sio tu imedumu pale ambapo wengine wameshindwa bali pia imejitengenezea misingi imara wa kuendelea. Udhaifu wowote ambao ZIFF inaweza kuonyesha, tutabaki kujivunia hivyo, ndio maana tunasema Lake Mtu Halimtapishi! Kama ilivyo katika bango litalaotumika mwaka huu kuwasilisha msimu wa 25 wa maonesho ya ZIFF.

mwisho


COMMENTS

Name

Anga,11,Arusha,27,Burudani,302,burundani,1,come rain,1,come sun,1,Crazy in Love kama wimbo kama wao wenyewe,1,dahh sijui kweli mbona shida,1,Dar utakuja je tumejiandaa,1,daraja sahau nini,1,demokrasia ya upanga,1,Dodoma,77,Dole tupu vijana wa zamani,1,Duhh bibie endeleza libeneke,1,Duhh kaisikie Walibana,1,duhh kwa mbagala mama lazima awe supa,1,Fedha za maiti haziliwi bure,1,Fedha za watu kwa maendeleo ya watu,1,Fikira,14,filamu,238,Filamu ndio kielelezo cha ukuzi wa taifa,1,flamu,7,Gandamiza Kibara baba ake,1,Habari,4810,habari. dodoma,24,hadithi,19,hakika tumeweka historia,1,hakuna noma jongwe,1,hapa kwetu inakuwaje vile,1,hasira hasara,1,hata maji,1,hataki masikhara na maisha yake,1,hatubonyezi kizenji,1,haya ndiyo mambo ya Ulaya,1,haya si yangu ni ya mdau mwenye hasira,1,haya wabongo na mambo kutoka nje,1,He he he wananikumbusha upishi wa shaba,1,Headline,1,Hii hurejesha uhai,1,Hii iko sawa kweli?,1,Hii imekaa vizuri,1,Hii inakaaje vile,1,Hii kweli noma,1,Hii maana yake Moro kuna uhaba wa chakula,1,Hii mexico,1,Hii mihasira mingine bwana,1,Hii ndio moro sio mpaka dar,1,hii ni hatari,1,Hii ni kiboko anayetaka kubisha ajibishie tu,1,Hii ni moja ya staili za kunyoa nywele,1,Hii si lukwangule,1,hii staili mpya,1,hili ni jengo pacha la malaysia ghorofa 88,1,Hivi ni ngoma tu,1,hivi nini siri za serikali,1,hivi sisi tunajua kama kuna vitu vya aina hii,1,hivi vitu bwana,1,Hiyo ndiyo gharama ya demokrasia,1,Hizi imani nyingine ni hatari,1,Hizi takwimu hizi mhh,1,Hongera bibie,1,Hongera dada etu kwa kutuletea kaka etu (shemeji) kwani mwenye dada hakosi shemeji,1,Hongera sana,1,huhitaji mifedha kuwa msafi,1,Huko Ulaya,1,Huu ndio ustaarabu,1,huu ujiko utakuwa mkubwa,1,imetosha,1,Inahitaji nidhamu fulani,1,inakuuma au...,1,Inakuwaje kama filamu yenyewe itahitaji busu la nguvu,1,Inaonekana watanzania hatukuwepo,1,Ipo kazi Maximo,1,Iringa,22,Isiwe mijineno tu manake mihela hubadili watu kweli,1,Itakuwa laki moja ya halali,1,jamani huu kama si ushamba kumbe nini,1,Jamani mbona Mungu anatupigania,1,Jamani watoto wanatakiwa kupendwa,1,jamani.. jamani ukiikosa Diamond usijutie,1,Je nyumbani hakuna vitu vya aina hii?Tuambie,1,je walikuwepo watu wa huduma ya kwanza,1,Je watanzania wanalipa kodi,1,jela kwa raha,1,Jolie,1,juhudi za lazima kuinua filamu,1,kama si kiwanda cha chumvi nani atawajua hawa,1,Kama kweli ndio kweli basi kila heri,1,Kama Mkristo naamini hilo hiyo si sahihi,1,kama unajua kuyarudi nenda Malta,1,kama wao wanaweza sisi je,1,Kamua baba waache wakanyagane,1,karibu nyumbani dada yote maisha tu,1,karibu Tatiii,1,KARIBUNI,1,Katavi,5,kaza buti hakuna kukata tamaa inalipa,1,kazi kwako mheshimiwa waziri wa madini,1,kazi na burudani,1,keep it up bloggers,1,kero ya usafiri sasa kwisha,1,Kila chenye roho na mwili kitaonja umauti,1,kila kitu kina vitu,1,Kila la Heri jamila,1,kila la heri kwani ni changamoto,1,Kipya,51,Kiuno bila mfupa,1,Kolelo mzimu ambao bado hai,1,KUBWA,1,Kudumisha urafiki wa dunia,1,Kuna dalili za wasomi kukubali Uafrika,1,kuna makala humu humu ndani ya blogu sijui mnasemaje,1,Kuu,113,kwa mara nyingine tena Tigo imewezesha,1,Kwa mchanganyiko huu muungano lazima udumu,1,Kwa mihasira hajambo,1,kweli,1,Kweli ina mkono mrefu tuone,1,Kweli duniani tunatofautiana,1,la maana ni kuwa na jiko au vipi,1,labda halitabadilika tena,1,lakini mwafaka lazima,1,lengo ni kutafakari,1,leteni vitu tuvione,1,lets us,1,Lucy wanakuelewa hawa...,1,Lukwangule nyumbani kwetu,2,M ungu bariki mikono ya madaktari wafanikiwe,1,MAARUFU,1,maendeleo ya soka siku zote yanahitaji fedha ili yapatikane,1,maisha ni vyema kuyaangalia,1,MAJIBU,1,makala,51,mama ni mama tu anapendeza,1,mambo mengine we angalia tu,1,mambo msimamo,1,mambo sasa mchanganyiko,1,Mara nyingine huona tunakotoka kwa kuona wenzetu,1,Mashabiki wa rhumba mpooooooooo,1,Masitaa,12,Maskani,1,MASOKO,3,Masupa staa mnaoinukia mpoo,1,Matamasha,6,mavazi ya kuogelea yanaposhindaniwa,1,Mbeya,11,Mchakamchaka anti Asmah,1,Mchanganyiko,81,MCHANYATO,1,mchezo,5,mengi wanayoyaita siri ni public information,1,mfumuko wa bei mpaka noma,1,Mhh sijui watu wa Sua ambao wako huko wanasemaje,1,Mhh ugua pole dada watu wanataka burudani,1,Michezo,501,Michezo maalum inatakiwa kupigiwa debe,1,miguu,1,miguu babu,1,Mikataba mingine ama hakika tuiangalie hata wakopeshaji nao wanatugeuza sakala,1,MIMI NI KISURA NAJITAMBUA,1,Mimi sijajua hasa kumetokea nini kwani ninavyojua hawa huwa na ungalizi wa hali ya juu,1,Mimi simo,1,mimi sisemi,1,mkiwa chumvi basi mkoze,1,Mkiwa taa mulikeni,1,Mnaonaje je hii imekaa vyema,1,Mnaweza wakwetu hapa,1,Morogoro,51,mrithi wa mwanadada Whitney Houston,1,Mtwara,4,Mungu aiweke mahali pema roho yake,4,Mungu amrehemu,1,Mungu amweke pema peponi,1,Mungu awabariki sana,1,Mungu awe nao,1,Mungu ibariki Tanzania,1,Mungu tuepushe na imani hizi za kishirikina,1,mungu tufanye tuwe na upendo,1,Mungu twaomba utuhurumie,1,Muziki,350,muziki na fasheni,5,Mwanahabari,33,Mwanza,6,Mwendo mdundo dada,1,Mwenge huo utakimbizwa duniani kwa siku 130,1,Mwenge wa olimpiki ni ishara ya urafiki,1,Mzee wa Farasi nakupa saluti,1,Mzimbabwe huyu kutoka kwa mama mkali,1,N i dar mpaka Moro au bao tatu bila,1,Na sisi je,1,Naam kama haiwezekani hapa,1,Nairobi waanzisha tena utalii,1,namna bora ya kusaidia jamii,1,nani abebe hukumu na lawama,1,nani asiyejua utamu wa pipi,1,Nani kama baba,1,naona inafaa kuchangia mimi sitoi hoja,1,ndoa za mastaa huwa na mgogoro,1,nenda mwaya nenda,1,New Zanzibar Modern Taarab na wapenzi big up,1,news,5,Ni bikini kwa kwenda mbele,1,Ni Dar mpaka Moro au.. tatu bila,1,ni furaha za muungano,1,Ni kazi ngumu yenye kuhifadhi utamaduni,1,Ni kuchakarika kuonyesha urafiki na biashara pia,1,ni mfumuko wa bei au mfumuko wa nchi,1,Ni muhimu kutazama afya yako,1,ni muziki kwa kwenda mbele,1,Ni muziki mpaka China,1,Ni raha tupu,1,Ni Serengeti Premium Lager,1,Ni Tigo na mawasiliano ya kisasa,1,Ni wakati wa kuujadili utamaduni,1,Ni zaidi ya jazz,1,Nitasubiri and welcome home,1,nje je?,1,NUKUU YA LEO,1,nyie mnasemaje kuhusu hili,1,Ona Kolelo na sindikizwa na Wazee wa Gwasuma,1,ona vya dunia,1,One step ahead,1,patna mwingine mjamzito,1,Pengine anamuogopa Jada Pinkett manake kwa wivu..,1,picha,494,Pole Jamila hayo ndiyo mashindano,1,poleni sana,1,poleni sana wanyalukolo,1,Powa sana,1,Profesa jamaa wanakumaindi,1,Roho za marehemu zipate pumziko la milele,1,Ruvuma,9,sakata dansi mpaka kwenye kilele cha dunia,1,sasa kumebakia ugonjwa mmoja polisi kuendesha mashtaka,1,sasa mifedha kila mahali hongereni,1,Sasa ni mavuno,1,Sasa ni wakati wa kutafuta upenyo ndani ya IDOLS,1,SAYANSI,1,SAYANSI ANGA,1,See Uluguru Montains,1,serikali inataka kujihami kwanini,1,Show of support Big Up Madame,1,Si kitu kidogo hata kidogo,1,si unajua tena namie naimwaga hivyo hivyo,1,Siasa,346,siasa habari,2,Sijui kama City wanajua Mbagala noma,1,Sijui tunaishi karne gani yailahi,1,Sinema,9,sio advencha....kaaa ...niko kibaruani,1,Sisi ndio tunaanza vitongoji,1,Sisi yetu macho na masikio,1,Slow slow jamani,1,sto,1,tabasamu kali la mwenge wa olimpiki,1,Tabora,1,Tazama Waziri Mkuu Pinda wasije wakapindisha maamuzi yako,1,TEKNOLOJIA,1,Thats big man game,1,This is crazy Africa,1,This is Mgeta,1,Tibet wamegeuza Olimpiki jukwaa la siasa,1,Titbits collection,1,Tubadili tamaduni,1,Tuchangie mambo yaive,1,tuendeleze sanaa,1,tuienzi na sisi mbona wizara haituambii,1,Tuipeleke kaskazini,1,Tuisaidie serikali shida ya Mererani,1,tujue namna ya kupumzika,1,Tulienda kustarehe au kufanya fujo,1,Tumsaidie mtototo huyu kurejea katika hali ya kawaida,1,tunahitaji haya,1,Tunajifunza kweli kutoka kwao,1,Tunapandisha chati tu,1,Tunasubiri,1,tunazidi kuhesabu siku,1,TUNAZISUBIRI ZA VINARA ADAR,1,Tuombe nafuu kwa wagonjwa,1,Tuombe rehema kwa mungu,1,Tuone yatufae,1,Tusingoje wengine watusemee,1,tutampa tafu kubwa Prof,1,tuuenzi utamaduni au vipi,1,Tuukuze na kuulinda,1,tuvipende,1,tuwalinde maalbino,1,Tuwe kweli wakweli,1,ubunifu siku zote hulipa,1,uchumi huzunguka kwa kuwawezesha wasukaji,1,udumu muungano,1,Ugonjwa huu wa sasa ni kitendawili,1,Ukiiona kolelo utaipenda,1,Ukirejea salama kila mtu anafurahi,1,Umelenga Mkuchika utamaduni unakufa,1,unaposaka uwakilishi wa dunia,1,urafiki,1,Usisahau wazee wa Ngwasuma,1,UTAMADUNI,1,Video,2,Vionjo vipya ndani ya Gwasuma,1,Vita dhidi ya ufisadi,1,vitongoji Miss Tanzania navyo vimeanza,1,Vitu vikali vyazidi kuingia Dar,1,Vituko,77,Vituo vya polisi Tanga vyatelekezwa,1,VIVALO,1,Wacha tujifue,2,Wadau ilitolewa kiingereza,1,wakali wa ubunifu,1,wala usibabaike mwakwetu hii noma,1,wanadamu wanapotaka kujua zaidi,1,wanasema mpaka kieleweke,1,Wanataka kujua mali za JK na wengine,1,Wanawake wenye mvuto: Monroe,1,Wapo mabinti wa matawi ya juu,1,watu wanapofanya weli kwenye sanaa,1,waweza kurejea enzi ya Moro jazz na Cuban malimba,1,Wazee tupo kusindikiza,1,waziri,1,welcome dar baby,1,Wenzetu wameona sisi tunangoja nini kuangalia,1,wewe unasemaje,1,wigo mpana wa utamaduni,1,wilaya ya 'Mbagala' mlie tu,1,Yaaani sijui itawezekana,1,Yaani wakati mwingine hata huelewi prioty over priority,1,yeye mbele sisi nyuma,1,Yote maisha dada,1,ZA MOTOMOTO,1,Zanzibar,79,zawadi zinatakiwa ziende shule,1,ZILIZOTIA FORA,1,zitachangia kupunguza makali ya bei za umeme,1,
ltr
item
Lukwangule Entertainment: ZIFF BUANA!: LAKE MTU HALIMTAPISHI
ZIFF BUANA!: LAKE MTU HALIMTAPISHI
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgUGUSFRQMf5u9zInfSJYn_myx8A-yqNDD5P_1xxIkcTkAq8h07sRobWWmj9thsJ8ND6k-STV7Nqix8ojeUC5n7hD8iwqbSHlq6sf2OT_cZG8q8EddurfFKHxGzpkajhtAQKOoqxIZGXs68g0zStVLPRAoQu-XB_vt14BKnHV15T5PUsokbM1fsjb5qeg/s320/ziff.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgUGUSFRQMf5u9zInfSJYn_myx8A-yqNDD5P_1xxIkcTkAq8h07sRobWWmj9thsJ8ND6k-STV7Nqix8ojeUC5n7hD8iwqbSHlq6sf2OT_cZG8q8EddurfFKHxGzpkajhtAQKOoqxIZGXs68g0zStVLPRAoQu-XB_vt14BKnHV15T5PUsokbM1fsjb5qeg/s72-c/ziff.jpg
Lukwangule Entertainment
https://lukwangule.blogspot.com/2022/05/ziff-buana-lake-mtu-halimtapishi.html
https://lukwangule.blogspot.com/
http://lukwangule.blogspot.com/
http://lukwangule.blogspot.com/2022/05/ziff-buana-lake-mtu-halimtapishi.html
true
934549962738256429
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy