TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI Benki ya ABC imesaini mkataba wa miaka mitatu na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kudhami...
TAARIFA KWA VYOMBO VYA
HABARI
Benki ya ABC imesaini
mkataba wa miaka mitatu na Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF) kudhamini
michuano ya BancABC Super 8 inayoshirikisha timu nane, nne
kutoka Tanzania Bara na
nyingine nne kutoka Zanzibar.
Hafla ya utiaji saini
imefanyika leo (Julai 26 mwaka huu) kwenye ofisi za TFF, Dar
es Salaam ambapo Katibu
Mkuu Angetile Osiah amesaini kwa niaba ya shirikisho wakati
kwa upande wa ABC, saini
yake iliwekwa na Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo kwa
Tanzania, Boniface Nyoni.
Mashindano hayo yataanza
Agosti 4-18 mwaka huu yakichezwa katika miji ya Dar es
Salaam, Arusha, Mwanza na
Zanzibar ambapo timu zote shiriki zitacheza katika vituo
hivyo.
Uzinduzi rasmi wa
mashindano hayo utafanywa Agosti 2 mwaka huu na Ofisa Mtendaji
Mkuu (CEO) wa benki ya
ABC yenye makao yake makuu nchini Botswana, na ina matawi
katika nchi za Msumbiji,
Zambia, Tanzania, Zimbabwe.
Katika uzinduzi huo, CEO
ataelezea thamani ya mkataba huo ambapo utahusisha gharama
za malazi, usafiri, vifaa
na uendeshaji wa mashindano hayo.
Akizungumza baada ya
kutia saini, Osiah amesema hatua hiyo ni sehemu ya mikakati ya
TFF kuwa na mashindano
mengi yatakayosaidia kuziandaa timu kabla ya kuanza Ligi Kuu.
Naye Nyoni amesema ABC
imekubali kuingia kudhamini mpira wa miguu ikiwa ni lengo la
kuchangia ustawi wa
mchezo huo na kutoa sehemu ya faida wanayopata kwa kupitia
michezo.
Timu zitakazoshiriki
mashindano hayo ni zile zilizoshika nafasi tatu za juu katika
Ligi Kuu ya Tanzania Bara
na Ligi Kuu ya Zanzibar. Nyingine ni timu iliyoshika
nafasi ya kwanza kwenye
Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara na Ligi Daraja la Kwanza
ya Zanzibar ambazo nazo
kwa kushika nafasi hizo zimeshaingia katika Ligi Kuu.
RAMBIRAMBI MSIBA WA MCHEZAJI ISSA KIHANGE
Shrikisho la Mpira wa
Miguu Tanzania (TFF) limepokea kwa masikitiko kifo cha
mchezaji wa zamani wa
timu ya Simba, Issa Kihange kilichotokea juzi (Julai 24 mwaka
huu) jijini Dar es
Salaam.
Msiba huo ni mkubwa kwa
wadau wa mpira wa miguu kwani kwa nyakati tofauti akiwa
mchezaji Kihange alitoa
mchango mkubwa kwa timu mbalimbali alizochezeaz ikiwemo
Simba na CDA ya Dodoma,
hivyo mchango wake tutaukumbuka daima.
TFF inatoa pole kwa
familia ya marehemu Kihange, klabu za Simba na CDA na na
kuwataka kuwa na subira
na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha msiba huo mzito.
Mungu aiweke roho ya
marehemu Kihange mahali pema peponi. Amina
HATIMAYE FLYING EAGLES YATUA KUIVAA NGORONGORO HEROES
Hatimaye timu ya Taifa ya
vijana wenye umri chini ya miaka 20 ya Nigeria (Flying
Eagles) imewasili nchini
leo mchana (Julai 26 mwaka huu) kwa ndege ya RwandAir ikiwa
na msafara wa watu 32
wakiwemo wachezaji 18.
Awali timu hiyo ilikuwa
iwasili jana jioni (Julai 25 mwaka huu) ikitokea Kigali,
Rwanda lakini ikashindwa
baada ya kuchelewa ndege. Flying Eagles itapambana na
Ngorongoro Heroes katika
mechi ya kwanza ya raundi ya pili itakayofanyika Jumapili
(Julai 29 mwaka huu)
Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 10 kamili jioni.
Mechi hiyo ya kuwania
tiketi ya kucheza fainali za 18 za Afrika kwa vijana wenye
umri chini ya miaka 20
zitakazochezwa mwakani nchini Algeria itachezeshwa na waamuzi
kutoka Kenya wakati
Kamishna ni Charles Masembe kutoka Uganda.
Flying Eagles ambayo iko
chini ya kocha John Obuh, Julai 24 mwaka huu ilicheza mechi
ya kirafiki na Rwanda
(Young Amavubi) kwenye Uwanja wa Amahoro jijini Kigali na
kufungwa bao 1-0.
Msafara wa timu hiyo
unaongozwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Ufundi ya Shirikisho la
Mpira wa Miguu Nigeria
(NFF), Chris Green umefikia hoteli ya Rungwe iliyoko Mtaa wa
Livingstone, maeneo ya
Kariakoo.
Baadhi ya wachezaji
walioko katika kikosi cha Flying Eagles ni Chidi Osuchukwu,
Alhaji Gero, Shehu
Abdullahi, Aminu Umar, Aliyu Mohamed, Uche Agbo, Jonah Usman,
Harrison Egbune, Hassan
Abubakar na Yahya Adamu.
Makocha wote, Jakob Michelsen
wa Ngorongoro Heroes na Obuh wa Flying Eagles wakiwa
na manahodha wao,
Jumamosi (Julai 28 mwaka huu) saa 4 asubuhi watazungumza na
waandishi wa habari juu
ya walivyoviandaa vikosi vyao kwa ajili ya mechi hiyo.
Mkutano huo utafanyika
ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
Viingilio katika mechi
hiyo vitakuwa sh. 3,000 kwa viti vya rangi ya chungwa, bluu
na kijani wakati VIP B na
C itakuwa sh. 5,000. Kiingilio kwa VIP A itakuwa sh.
10,000.
Source:Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa
Miguu Tanzania (TFF)
COMMENTS