Tuesday, July 14, 2009

Mkuu wa Majeshi Afrika Kusini akaribishwa WhiteHouse Dar




Mkuu wa Majeshi ya Afrika Kusini amewasili nchini na kuishukuru tanzania kwa kusaidia kuleta Uhruu Kusini mwa Afrika.Kauli hiyo aliitoa alipokutana na Rais Jakaya Mrisho Kikwete ikulu leo asubuhi.


Mkuu wa Majeshi ya Afrika ya kusini Jenerali Godfrey Ngwenya alikaribishwa kama pichani inavyoonekana na rais Mwenyewe Ikulu akauzngumza naye kisha walipata nafasi ya kupiga picha na wakuu wa majeshi ya tanzania na Afrika kusini na maofisa waandamizi kama picha inaovyoonyesha.


Picha ya kwanza rais akimkaribisha mgeni Ikulu na Nyingine Rais Jakaya Mrisho Kikwete(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa majeshi ya Afrika ya kusini Jenerali Godfrey Ngwenya(kushoto), Mkuu wa Majeshi ya Tanzania Jenerali Davis Mwamunyange(kulia) pamoja na maafisa waandamizi wa majeshi ya Afrika ya kusini na Tanzania ikulu jijini Dar es Salaam leo asubuhi(picha na Freddy Maro)

Monday, July 13, 2009

Mahakama ya kadhi, mambo hadharani, mchakato waanza

Mufti wa Tanzania, Sheikh Mkuu Issa bin Shaaban Simba ameunda kamati maalumu ya Masheikh 25 ambao watakaa na wataalamu wa serikali kuandaa mfumo wa uendeshaji wa mahakama ya Kadhi nchini.
Uteuzi huo ni utekelezaji wa makubaliano ya kikao kilichofanyika wiki iliyopita kati ya waislamu wa madhehebu yote nchini walioongozwa na Mufti Simba na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kwa niaba ya serikali.
Kaimu Katibu Mkuu wa Baraza Kuu la Waislamu(Bakwata) Suleiman Lolila, katika taarifa yake leo, alisema kamati hiyo ambayo iko chini ya uenyekiti wa Mufti Simba, ina wanasheria wa kiislamu, mawakili wa kujitegemea na wataalamu wa fani za jamii.

Maiti za Yemenia ufukwe wa Tanzania zafikia 25







JUMLA ya maiti 25 zinazokisiwa kuwa za abiria wa wa ndege ya Shirika la Ndege la Yemen, Yemenia, iliyoanguka katika bahari ya Hindi jirani na kisiwa cha Comoro hivi karibuni zimepatikana katika pwani ya tanzania , kisiwani Mafia.
Maiti hizo zilikokotwa na mkondo mkali wa bahari ya Hindi.
Ubalozi wa Ufaransa nchini umetoa taarifa ifuatayo kwa Kiingereza kuelezea kilichojiri na msaada wake kwa tanzania baada ya serikali kuomba kusaidiwa. Kwa wanaounyaka umombo kazi kwenu.
PRESS RELEASE

TANZANIA AND FRANCE COOPERATE TO RETRIEVE DEAD BODIES FROM THE ILL-FATED YEMENIA FLIGHT 626 SANAA-MORONI, ALONG TANZANIAN COASTAL AREAS.

A French Navy ship and a French medical forensic team are currently in Tanzania, at the request of the Tanzanian government, to assist in an emergency operation to retrieve and identify dead bodies believed to have come from the plane which crashed at sea off Comoros on June 30, 2009
The plane, carrying more than 153 people; plunged into the sea near Moroni (Comoro), killing all but a 14 year-old girl who was found alive in the sea. 66 French nationals are believed to have been aboard the ill-fated plane, which they boarded in Sanaa on their way to Moroni.
Since July 7th, about 25 bodies have been retrieved, mainly off-Mafia Islands. They are presumed to be the some of the victims of the Flight 626 crash, and to have been brought to the Tanzanian coastal line by powerful Indian Ocean streams.
A Tanzanian Task Force, with two components (search and medical) has been created to follow the situation.
- The search and medical component of the Tanzanian Task Force is assisted since July 9th by French Navy Frigate ''FLOREAL''. This Frigate was re-routed in emergency to Tanzania, after participating for a few days in a search and rescue operation on Comorian territorial waters, at the request of the Comorian government. Before the air crash, the French frigate was navigating extreme North in the Indian Ocean, within the framework of anti-piracy operations.
The French Frigate “Floreal¨, which carries a helicopter, has participated in operations decided by the Tanzanian Task Force, to search for bodies along the Tanzanian coast, and to retrieve bodies caught in the reefs and mangrove areas.
The medical component of the Tanzanian Task Force is composed of seven French forensic doctors from the French Disaster Victim Identification (DVI) team. They have joined the Tanzanian Task Force and are collaborating in identification work of dead bodies, jointly being carried at the Muhimbili Medical Centre from July 13, 2009.
The identification procedure follows the Tanzanian law ; identifying dead bodies according to legal protocols is crucial, for Police and Justice ; as an essential part for compensation of the families or close relatives of people who lost their lives in the plane accident.
As no more new dead bodies are foreseen along the Tanzanian Coastal line, the French Navy Ship FLOREAL is expecting to leave soon from Tanzania. The forensic experts will stay longer in Tanzania, to help finalizing identification work.
Jacques de LABRIOLLE
Ambassadeur de France en Tanzanie
Ligne directe : +255 22 219 8883
Télécopie : +255 22 219 8815
Pichani: Ndege kama hiyo iliyoanguka, Meli ya Kifaransa iliyovinjari pwani ya Tanzania na wananchi wenye msiba huko comoro.

ERIC and the MAPINDUZI BAND live this and every Thursday at ClubAfrique


hi people,
if you haven't laughed in a really long time here's one reson youshould be at club afrique this week. we laugh!!! im telling you therejust is no end to the suprises Eric will pull at his shows each week.come have a really really good laugh. also we say Good bye to theGerman Ambassador. Walter Lindner. He has in many ways supported thearts in Kenya and this is a fantastic way to say thank you andKwaheri.
send this off to some friends. if you haven't been in a whilecome and bring a friend.
look foward to seeing you.
Hi,
He just gets better every week. With energy at its peak and the words andbeats that keep us wanting more…ERIC and the MAPINDUZI BAND live this and every Thursday at ClubAfrique!
this week we have an Afro band that’s young and fresh, AZIZA to startus off , then KENYA'S PHATTEST keyboard player,Aaron and the AaronRimbui Trio, He just relaesed his second album- Alfajiri, definately amust watch.
Where: Club Afrique, Museum Hill
When: Thur, 16th July 8.00 to 11.00 pm.
Your input? 400/= only.

Sunday, July 12, 2009

maiti zaidi za Yemenia zapatikana

Shughuli ya kutafuta maiti ambazo zinahusishwa na ajali ya ndege ya Shirika la Ndege la Yemen, Yemenia iliyoanguka katika bahari ya Hindi jirani na kisiwa cha Comoro hivi karibuni, bado zinaendelea ambapo mpaka sasa wamepatikana maiti 18.
Pamoja na hayo bado maiti mbili ambazo hazijathibitishwa kuhusishwa na ajali lakini zinadhaniwa kuwa zinahusiana, utaratibu wa kuzifukua unaendelea katika wilaya ya Kilwa.

Mchongo wa watengeneza sinema

SCREENPLAY DEVELOPMENT FUND - AMIENS INTERNATIONAL FILM FESTIVAL
Hujambo,
we are happy to inform you that Amiens International Film Festival in Francehas just launched its 14th screenplay development fund. Feel free to log onto its website and get in touch with the festival.
Best regardsMathilde and Antoine
Antoine Yvernault
Attaché Audiovisuel Régional Afrique de l'est
Regional Audiovisual Attache for Eastern Africa
Ambassade de France. Nairobi
LD 254 20 277 87 30
Fx 254 20 277 87 80

Saturday, July 11, 2009

karume azungumzia uimarishaji miundombinu bandari ya Zenj


RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Amani Abeid Karume amesema kuwa juhudi zinazofanywa za kuimarisha miundombinu ya bandari ya Zanzibar zina lengo la kuwasaidia wananchi kupata ajira pamoja na kuinua uchumi wa nchi yao.
Rais Karume aliyasema hayo leo huko katika Bandari ya Malindi mjini Zanzibar mara baada ya kuzindua vifaa vya shughuli za bandari ikiwemo tagi pamoja na vifaa vya kuchukulia na kunyanyulia makontena bandarini.
Katika maelezo yake Rais Karume alisema kuwa hatua iliyofikiwa hivi sasa bandarini hapo ni nzuri na itasaidia kwa kiasi kikubwa katika kuimarisha shughuli za bandari na kazi kubwa iliyobaki hivi sasa kwa Shirika la Bandari ni kutafuta wateja.
Alisema kuwa mbali ya kuimarika kwa huduma za bandari pia suala la ajira nalo litachukua nafasi yake kwa kuongezeka na kuwasaidia wananchi kwa kiasi kikubwa.
“Sasa bandari tunayo na vifaa tunavyo, lililopo hivi sasa ni kwa Shirika la Bandari kutafuta wateja kwa ajili ya kuimarisha shughuli za bandari”,alisema Rais Karume.
Rais Karume pia alisisitiza utunzaji wa vifaa hivyo na vile vya zamani ili viweze kuchukua muda mrefu na kuweza kusaidia shughuli za bandari.
Pamoja na hayo, Rais Karume aliutaka uongozi wa Shirika la Bandari kuandaa programu maalumu kwa ajili ya mafundi wa vifaa vya bandarini hapo kwa lengo la kupata mafunzo ya ndani na nje ya nchi ili wapate kuwa na ujuzi zaidi wa kufanya kazi zao.
Katika maelezo yake kwenye uzinduzi huo, Rais Karume alisema kuwa ujenzi wa bandari sanjari na vifaa vilivyopo hivi sasa kutawasaidia wafanyabiashara kuleta mizigo yao moja kwa moja hapa Zanzibar badala ya kupitia bandari nyengine.
Rais Karume alieleza kuwa pia alitoa changamoto kwa wale wote waliokuwa na imani ndogo ya kuona kuwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar haitakuwa na uwezo wa kujenga bandari sanjari na kununua vifaa kwa ajili ya kuendeshea shughuli za bandarini.
Kutokana na hali hiyo, Rais Karume alisisitiza haja ya kuwa na subira na kueleza kuwa juhudi za makusudi zimekuwa zikichukuliwa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar katika kuimarisha huduma za maendeleo.
Sambamba na hayo, Rais Karume alitoa pongezi kwa Shirika la Bandari kwa kujenga na kuiimarisha bandari hiyo siku hadi siku.
Mapema Waziri wa Nchi Afisi ya Rais Mawasiliano na Uchukuzi Mhe. Machano Othman alieleza kuwa hatua za utendaji bandarini hapo zimeimarika ambapo hivi sasa shughuli za uteremshaji makontena bandarini hapo hazichukui zaidi ya siku tatu.
Pia, Waziri Machano alimuhakikishia Rais Karume kuwa vifaa hivyo vitatunzwa ili vidumu na kuweza kufanyiwa kazi kwa muda mrefu.
Alieleza kuwa kuimarika kwa huduma bandarini hapo kumepelekea meli nyingi kuja moja kwa moja badala ya kupitia katika bandari ya Dar-es-Salaam na Mombasa.
Waziri Machano pia aliwataka wafanyabiashara wanaoshusha makontena yao bandarini hapo kutoyaacha kwa muda mrefu na kuifanya bandari kuwa ghala la kuhifadhia mizigo na badala yake waweze kuchukua juhudi ya kuitoa mapema mizigo yao.
Waziri Machano alieleza kuwa vifaa hivyo vimenunuliwa na Shirika la Bandari kupitia mkopo wa Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ).Vifaa vyote kwa pamoja vina thamani ya zaidi ya Shilingi za Tanzania Bilioni 3.7.
Utengenezaji wa Mradi wa ujenzi wa Gati ya Malindi ulianza Julai, 2005 na kukamilika Novemba 2008 chini ya Ufadhili wa Jumuiya ya Ulaya.
Katika hafla hiyo viongozi mbali mbali wa chama na serikali walihudhiria ambapo Rais Karume alianza uzinduzi kwa kuizindua Tagi mpya iliyotengenezwa na Kampuni ya Damen Shipyards ya Uholanzi na baadae alizindua vifaa vya kuchukulia na kunyanyulia makontena ambavyo vimetengenezwa na Kampuni ya Kalmar ya Sweden.

Pichani Rais wa Zanzibar Amani Abeid Karume,akizungumza na Balozi Mpya wa Indonesia Nchini Yudhistiranto Sungadi,aliyekuja kwa ajili ya kujitambulisha Ikulu Mjini Zanzibar jana.(Picha na Ramadhan Othman).stori ni ya Ikulu Zenj