Mlimbwende Iluminata James kutoka mkoani Mwanza juzi usiku alitwaa taji la Miss Universe Tanzania kwa mwaka 2009 na kujikatia tiketi ya kuli...

Mlimbwende Iluminata James kutoka mkoani Mwanza juzi usiku alitwaa taji la Miss Universe Tanzania kwa mwaka 2009 na kujikatia tiketi ya kuliwakilisha taifa katika michuano ya dunia itakayofanyika baadaye mwaka huu katika visiwa vya Bahamas.
Iluminata ambaye anampokea taji hiyo mwanadada nyota katika fani ya mitindo nchini Miriam Odemba alifanikiwa kutwaa taji hilo baada ya kuwashinda walimbwende wenzake 19 ambao nao walikuwa wakichuana vikali kuwania taji hilo.
Shindano hilo lililofanyika katika ukumbi wa Mlimani city jijini Dar es Salaam , mbali ya mashabiki wa masuala ya ulimbwende kupata burudani ya kuonyeshwa mavazi na miondoko ya ‘catwalk’ kutoka kwa washiriki 20 pia walikongwa nyoyo zao na burudani safi ya muziki kutoka kwa msanii nyota wa Bongofleva , Ambwene Yesaya ‘Mzee wa Comercial’ , mwanadada Wahu kutoka Kenya anayetamba na wimbo wa ‘Sweet love’.
K abla ya bendi ya Diamond Musica chini ya Allaine Mulumba kuja na wimbo wao maarufu wa ‘Mapenzi kitu gani’ na kufuatiwa na sebene la uhakika na burudani hiyo ilihitimishwa na ngoma za utamaduni kutoka kikundi cha Albino Revolution Cultural Troope.
Mbali na Iluminata washindi wengine katika fainali hizo za Miss Universe Tanzania ambazo zilihusisha warembo kutoka mikoa mitano ya Tanzania , Arusha , Mwanza , Dodoma , Morogoro na Dar es Salaam walikuwa ni Evelyne Almasi mabywe alichukua nafasi ya pili na hivyo kujipatia nafasi ya kushiriki kwenye shindano la Miss Earth.
Wakati mwanadada Hidaya Maeda ambaye alishinda nafasi ya tatu katika kinyang’anyiro hicho, yeye ataliwakilisha taifa katika shindano la Miss International baadaye mwaka huu, na nafasi ya nne ilikwenda kwenye Zeinab Kianda na Gisela Tarimo alinyakua nafasi ya tano.
Miss Universe Tanzania 2009 mbali ya kujipatia tiketi ya kushiriki kwenye shindano la dunia pia alizawadiwa Sh milioni tatu , nafasi ya kusoma kozi ya lugha ya kifaransa kwa mwaka mmoja katika kituo cha Alliance Francaise pamoja na kupatiwa vipodozi vyenye thamani ya Sh 500,000 na duka la Shear Illusion .
Majaji wa shindano hilo walikuwa ni pamoja na Mbunge wa Viti Maalum CCM, Al Sharyamaa Kwegyabir , mwanamuziki John Kitime,Masoud Kipanya , Mbunifu wa mavazi Ally Rhemtullah, Maria Sarungi Tsehai , Amit Patel kutoka kwa wadhamini wa shindano hilo kampuni ya Samsung ambao waliongozwa na jaji mkuu Rosie Motene kutoka Afrika Kusini ambaye ni Muigizaji nyota na Mtangazaji wa kituo cha Studio 53.

COMMENTS