YALIKUWA majira ya saa mbili jioni,Ijumaa wakati nilipopita katika mtaa wa Majengo maarufu kama Kingspalace. Nilikuwa nimechoka lakini...
YALIKUWA majira ya
saa mbili jioni,Ijumaa wakati nilipopita katika mtaa wa Majengo maarufu kama Kingspalace. Nilikuwa
nimechoka lakini pia nilikuwa na hamu ya kujua usiku Mpanda ikoje na eneo
ambalo niliambiwa linaweza kunipa
taswira ya mpanda usiku ni eneo la Majengo.
Mtu aliyenielekeza
hakuwa na muda wa kunipa hadhari, aliniona ni mtu wa makamo na ipo haja ya
kukutanishwa na watu wa aina yangu katika maeneo ambayo ni wenye hulka fulani tu wanakuwa na uwezo wa
kufika na kuvinjari.
Nilinyoosha miguu
yangu kutoka Kenyatta, taratibu kama vile nina muda wote duniani, nikiangalia
watu na miondoko yao hapa na pale na katika safari yangu kutoka mtaa wa
Kenyatta nasikia harufu ya bangi hapa na pale,lakini ahh nilifikiri huenda si
bangi ni majani yanachomwa moto.
Kwa siku ya leo
Mpanda imeoneka usiku wake huwa mtulivu ukiachia muziki wa hapa na pale; maduka
mengi ya bidhaa za kawaida hufungwa mapema zaidi , lakini maduka yenye bidhaa
zinazofanana na maisha ya usiku hubaki wazi mpaka saa nne usiku na mengine
kuendelea.
Katika muda huu
nanyoosha miguu wamachinga wa mtaa wa Kenyatta walikuwa bado wanaendelea na
shughuli zao japo wengijne walikuwa wakifunga mafurushi lakini maduka ya pombe yalikuwa bado wazi na ya
muziki pia.
Katika mji ambao
hadithi zake zinamaingiliano makubwa na watu kutoka nje ya Tanzania na yenye
uchumi unaonekana kukua kwa sasa, maisha haya ya usiku yasiyo na fujo yanaonekana kuwa ndio bora zaidi.
Dakika zilizidi
kuyoyoma na kasi ya mwendo ilizidi kupungua kwa jinsi ninavyokaribia mtaa wa
Majengo ambao wakazi wa hapa wameupatia jina la Uwanja wa Fisi.
Nilitaka kukuficha
ukweli, ukweli kwanini niliamua kufika Mtaa wa majengo, maarufu kama uwanja wa
Fisi. Nilipata tetesi kuwa upo ukahaba wa haja katika eneo hili na washiriki
wake ni kutoka mikoa ya Singida,Mbeya,Tabora na kidogo Kigoma.
Nikaambiwa tena
kwamba wapo wanafunzi walioacha sekondari wakaenda katika kituo kile kikubwa
kufanya ukahaba kwani unalipa. Swala kwamba unalipa ni gumu kidogo lakini
ukifika eneo unaweza kujua unalipa kwa
kiasi gani.
Naam nilifika eneo
lile majira ya saa tatu na nusu kutokana na kutembea kuzembe kwangu, mambo
yalikuwa ndio kwanza yanaanza kuchangamka lakini nilichotaka sikukikiona
kirahisi vile.
Niliamua kuketi
mahala kupata supu, kwa wale tuliozoea kuandika upuuzi kama huu, unapokosa dira
supu au pombe husaidia kuvuta muda kuona kuna kitu gani eneo lile.
Katika supu maneno
yalikuwa zaidi kuhusu madili makubwa, mambo ya machimbo.Watu wanazungumzia
madini wanazungumzia utafutaji wa fedha wanazungumzia masoko na mawakala
wanaowadhulumu.Lakini katika mazungumzo haya
unaambulia kujua kwamba vijana wa eneo hili ambao ni mchanganyiko kutoka mikoa na nchi mbalimbali wana fedha za
kukutandikia usoni kwa kukosa nidhamu
wanayoitaka wao.
Wanachozungumza ni
kuishi leo kama vile hakuna kesho, wakati unamaliza supu, wanaokunywa pombe
sasa wanaanza kubadilika na hata wewe unaanza kuona kuna mabadiliko, mabinti
ambao ulikuwa unawaona wana ustaarabu wanaanza kuvaa nguo zinazoshiria kuwapo
kwa biashara.
"Hapa pana
mambo" nilisema nikitega njia ya maneno ili niweze kuambulia kitu. Kijana
mwenye umri kati ya miaka 25 na 30 alinitazama kicha akatabasamu."U mgeni
wewe" aliniuliza na mimi nikawambia ndio.
Hapo ndipo
alipoanza kutiririka kwani alisema ni eneo zuri hilo kw abiashara mbalimbali,
wagumu wanaokaa migodini ndipo huja kuambulia asusa za maisha baada ya kuumia.
Pana pilikapilika
sana hapa na kuwapo kwa madalali wa vyumba kuliniashiria kwamba kuna uwezekano mabinti
hawa wanaofanya biashara wanamalizia mashauri hayo ya mapatano palepale, kumbe
haikuwa hivyo.
Ukimuita binti
pale, anataka muende naye ulikopanga, lakini si kutafuta pale ambapo pana
madalali wa vyumba vya kupanga na madini,na bei yao waliwazaji hao kwa
kukuangalia usoni ni nzuri lakini kimsingi
shilingi 5000 inatosha kwa uliwazaji wa fasta.
Uwanja wa Fisi ni
uwanja wa Fisi kweli kama tabia za fisi zinavyojulikana kuna kila kitu
kinachotakiwa kama ilivyokuwa katika
uwanja wa Fisi wa dar es salaam, tatizo ni moja tu hakuna magodoro ya fasta
eneo hilo, hakuna uwazi katika mipira japo baadhi ya gesti zina mipira.
Nilipata nafasi ya
kuongea na Agness (si jina lake la kweli) ambaye ni mwenyeji wa Mbeya.
Aliniambia kwamba amefika hapo kutafuta fedha kwa kuwa mji umeshaanza kuwa na
watu ambaow anahitaji pia burudani.
Alisema kuwepo kwa
wageni wengi hasa wanaofanya mambo mbalimbali kuanzia usakaji wa
madini,biashara za madini na vyakula wakiwa vijana wanafanya watu kama wao kuwa
na sehemu ya kujipatia fedha.
Wanalipa vizuri
watu hawa ambao alisema wengi wao ni vijana wa Kisukuma na hivyo na wao
wanakuwa na uwezo wa kujisaidia na kusaidia wengine katika familia zao.
Agness katika
miaka yake ya 20 anapendeza kwa umbile lake lilijoaa sihiri pamoja na kwamba bei
yake yeye ni nafuu ya shilingi 5000 tu bado hakuwa na uwezo wa kutengeneza fedha nyingi kama
wenzake wengine, lakini amesema hakuna siku anayolala na njaa, wateja wapo.
Kwa watafuta
huduma ya kuliwazwa,wanatumia fedha kwa kuwa kesho itatapatikana fedha nyingine,
machimbo yalikuwa poa sana, yalikuwa yanatema na biashara ya mahindi ni nzuri
pia, fedha zipo Mpanda na mzunguko katika
shughuli za aina hii upo kwa sana.
Ofisa maendeleo wa
Mpanda , Grace nilipomuuliza kuhusu vijana kesho yake na matatizo wanayokabiliana
nayo, alizungumzia mahitaji ya fedha kiurahisi kunachochea mambo mengi ambayo
si mazuri ukiwemo ukahaba.
Anasema kwamba upo
ubishi wa wazi na kutojituma miongoni mwa vijana, ingawa anajua biashara ya
ukahaba inayofanyika Mpanda washiriki wengi si wakazi wa Mpanda bali wageni
waliokuja kutafuta fedha. Wapo wanaotafuta madini, wapo wanachimba madini na
wapo waliokuja kufuata fedha za watafuta na wachimbaji madini.
Mpaka sasa hakuna
mvutano wa wazi kati ya Polisi na makahaba hawa ambao kuanzia saa 12 jioni
hutega mingo zao uwanja wa Fisi wakitarajia biashara hadi usiku wa manane.
“Unaweza kuja hata
saa nane hapa na kukuta loose “ alisema Jovin (si jina lake) ambaye kazi yake
ni dalali wa madini ya shaba.
Kwa wanafunzi
wanaofanya ukahaba, labda ipo haja kwa taasisi za kiraia kutofumbia macho
matatizo yanayoamnza kuchipuka Mpanda kwani jinsi spidi ya madini inavyozidi
kuongezeka ni dhahiri biashara ya ukahaba itashamiri na maambukizi ya magonjwa
mbalimbali ya ngono yataanza kushika kasi na serikali mwishoni italazimika
kutibia watu wake kwa fedha nyingi kutokana na ukweli kuwa mchezo wao ni mauti
yetu.
ILITOKA AWALI HABARILEO
COMMENTS