KWA tulio wengi mahindi yanalimwa kwa ajili ya chakula. Lakini kiukweli mahindi ni mali ghafi ya kutengenezea bidhaa zaidi ya 12 bidh...
KWA tulio wengi mahindi yanalimwa
kwa ajili ya chakula. Lakini kiukweli mahindi ni mali ghafi ya kutengenezea
bidhaa zaidi ya 12 bidhaa ambazo zingelitengenezwa hata soko la mahindi
lingekuwa kubwa sana hapa nchini.
Uwapo wa teknolojia wa kutengeneza
bidhaa hizo kunafanya zao la mahindi lisiwe la chakula tu bali, la biashara
kusaidia uwapo wa viwanda vingine.
Unapokuwa unajua hilo hoja ya Naibu
katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Chakula na ushirika Raphael Daluti la kuwataka wafanyabiashara wa mahindi nchini
kuachana na uchuuzi na kusaidia wakulima kupata kipato zaidi kwa kuanzisha
viwanda vya kutengeneza bidhaa zinazotokana na mahindi ni muhimu sana.
Kauli hiyo ambayo ilitolewa katika
mahojiano na gazeti hili hivi karibuni inataka
kueleza ukweli kuwa mavuno mengi yaliyopatikana msimu uliopita,na hoja za
wananchi serikali kutafuta masoko zaidi, hazina maana kama wafanyabiashara wa
Tanzania wangeachana na tabia za kichuuzi na kuanza kuwekeza nguvu katika
kutengeneza bidhaa zinazotokana na mahindi.
Kuyumba kwa soko la mahindi
kunatokana na wakulima kutegemea uuzaji wa mahindi yao kwa wasagishaji sembe,
chakula kinachokuw amaarufu sana nchini Tanzania kwa sasa.
Bidhaa ambazo zinaweza kusindikwa
kutokana na mahindi ni pamoja na chakula cha wanyama kutokana na mabaki ya
kukandamizwa kwa mahindi ili kutoa mafuta ya kula, mafuta ya kuendeshea mitambo
na kutengeneza bidhaa muhimu kwa ajili ya utengenezaji wa siagi .
Kwa taifa lililotengeneza ziada ya
tani milioni moja na zaidi ya mahindi, ziada ya hiyo ingelimezwa kirahisi kabisa na
viwanda vya kusindika bidhaa mbalimbali.
Kwa kuangalia mwenendo wa soko na maisha hakika wakati umefika kwa wafanyabiashara
wetu kubadilika na si kusubiri serikali ili kuweka mambo sawa na kulifanya
taifa hili kutegemea bidhaa za viwandani katika kutengeneza fedha za kigeni
badala ya kilimo.
Jasi tunazotumia kutengeneza dari
(gypsum board) katika majumba yetu kuna kiasi cha wanga maalumu unatokana na
mahindi . Kitu hiki kinaitwa kitaalamu kama fabrilose maalumu.Hii fabrilose pia
hutumika kiwandani kwa ajili ya mashine za spidi kali za kutoa vipimo vya
nyuzi.
Wanga huu maalumu kwa maneno mengine unatumika katika viwanda
vya nyuzu na jasi za dari.
Aidha katika mahindi kuna vimeng’enya
ambavyo hutumika pia kutengeneza sirapu inayosaidia kuzuia kuharibika kwa
bidhaa na pia kuwezesha shughuli za uokaji kuwa sahihi.
Ndio
kusema hizi ashkrimu, uokaji mikate na bidhaa nyingine huongezwa sirapu hii ili
kuweza kuwa bora zaidi.
Aidha mahindi hutoa kemikali aina ya sorbitol hutumika katika kutengeneza dawa ya kifua, dawa ya meno na
vifaa vingine vya usafi, pia vipodozi, rangi na sigara.
Ndio
kusema kemikali hii inatumika katika telnoknolojia ya viwanda.
Imeelezwa
kuwa kemikali hiyo inauwezoa wa kuchangamana na kemikali nyingine kutengeneza kitu kinachotakiwa kwa ajili ya kukabili pia
bacteria kuliko sukari.
Aidha majimaji kutoka katika mahindi
kitaalamu yanajulikana kama CSL husaidia uzalishaji wa antibayotiki mbalimbali
ikiwamo penicillin na pia kutumika katika chakula cha wanyama.
Mahindi pia hutumika kutengeneza Anhydrous Dextrose
IP/BP/USP ambayo husaidia sana kwa
wagonjwa wa kuharisha na wale walipigwa
na joto.
Ndio kusema kilimo cha mahindi ni
muhimu kwa kuangalia namna ambavyo mahindi yanatoa bidhaa mbalimbali za msingi
zaidi ya sembe tunayotumia kula.
Na maana yake siku dunia ikiacha
kuzalisha mahindi kuna tatizo linaweza kuzuka katika viwanda vyua madawa na
hata wale wanaotumia teknolojia ya mahindi kupata mchanganuo mbalimbali wa
bidhaa.
Vyakula vingi katika mahoteli wakati
mwingine husawazishwa na mahindi katika mfumo mwingine.
Mahindi pia hutengenezwa shampuu na hutumika
kutengeneza daipa za watoto ili kuwaweka wakavu.
Ndio kusema kama tanzania , wawekezaji
wakapewa elimu hii ya bidhaa mbalimbali zinazotokana na mahindi, tegemeo la
mahindi katika bidhaa moja tu ya chakula kitaisha kwani pia mahindi yanaweza
kutoa mafuta ya kuendeshea mitambo.
Tunastahili kujifunza mambo mengi ili
kupata mwanga wa kutambua kwamba tunahitajika kubadilika katika uwekezaji na
kutumia mali ghafi za kilimo kuzalisha bidhaa za viwandani zenye kipato kikubwa
hali itakayofanya maisha ya wakulima,pia yabadilike.
Kwa Tanzania ambako kariobu mikoa
yote inamalia mahindi ni dhahiri kwamba soko la mahindi ni tatizo lakini kama
viwanda vitaanzishwa kutengeneza mahindi kwa maana ya matumizi mbalimbali
uzalishaji utazidi kuongezeka na wakulima kufaidika.
Mahindi ambalo ni zao la 5 la
kutegemewa nchini Tanzania kwa thamani yake kwa mwaka 2005 hadi 2010 hutoa
asilimia 25 ya nishati inayotakiwa katika maisha ya watanzania walio wengi.
Pamoja na kwamba ni zao
linalotumika kutengeneza usalama wa chakula ambapo wakala wa taifa wa hifadhi
ya Chakula (NFRA) huyanunua na kuyahifadhio kilio cha soko bado ni kubwa kwa
kuwa NFRA haikutengenezwa kimuundo kununua mahindi kwa sababu za kibiashara.
Kutokana na ukweli huo, zao la
mahindi halionekani kumtoa mkulima kwa sababu hakuna mnunuzi baada ya NFRA na
mahindi yanatumika zaidi kwa ajili ya
kuzalisha sembe.
COMMENTS