WAKRISTO WA ITALIA WAWEZESHA ZAHANATI YA KISASA VIKAWE

Mkuu wa Masista Waabuduo Damu ya Kristo, Euprasia Julius akimtambulisha mgeni rasmi na meza kuu kwa wageni waalikwa na wanakijiji wa Vikawe...

IMG_0282

Mkuu wa Masista Waabuduo Damu ya Kristo, Euprasia Julius akimtambulisha mgeni rasmi na meza kuu kwa wageni waalikwa na wanakijiji wa Vikawe (hawapo pichani) katika hafla ya ufunguzi wa Zahanati ya Da.Ma Africa Maria De Mathias (MDM) Vikawe, Kibaha.

Na Mwandishi wetu, Kibaha

MGANGA Mkuu wa halmashauri ya Mji Kibaha, Dk. Happniness Ndosi amepongeza shirika la masisita wa Waabuduo Damu ya Kristo kwa kufanikisha ujenzi wa zahanati ya kisasa katika kijiji cha Vikawe wilayani Kibaha mkoani Pwani.

Mganga huyo ambaye alikuwa mgeni rasmi katika hafla ya uzinduzi wa zahanati hiyo,pamoja na kuwapongeza amesema serikali itaendelea kushirikiana na mashirika yote kwa lengo la kuwezesha kila kijiji kiwe na zahanati na kila kata kituo na kila wilaya kuwa na hospitali.

Aliwapongeza masista hao kwa kuonesha upendo na huruma kama Biblia inavyomsimulia msamaria mwema ambaye alikuta mtu aliyepigwa na majambazi na kumsaidia.

Aliahidi ushirikiano wa serikali katika kufanikisha usajili wa zahanati hiyo na kuendelea kuisaidia hatua kwa hatua hadi inakuwa kituo mpaka watakapofanikisha safari yao ya kuwa hospitali kubwa ya kisasa.

Mganga huyo pamoja na kutoa ahadi hiyo aliwataka wananchi wa Vikawe kutumia huduma hiyo na kwamba zahanati hiyo itakapohitaji msaada wa gari la kubebea wagonjwa (Ambulance) wataletewa kuchukua mgonjwa na kumfikisha panapohusika.

Zahanati hiyo ya DA.MA Africa imejengwa kwa ufadhili wa wakristo wa Italia chini ya usimamizi wa Muitalia, Germano Frioni.

Akitoa salamu zake Muitalia huyo amesema kwamba anawashukuru wakazi wa Vikawe kwa kumpa nguvu ya kusonga mbele hasa kwa kutambua kwamba yeye na marafiki zake wamefanyakazi usiku na mchana kutafuta fedha kwa ajili ya kusaidia marafiki wa Afrika.

Alisema atajitahidi kufanya kila linalowezekana kuhakikisha changamoto za zahanati hiyo zinafanyiwa kazi.

Aliwaomba wananchi wa Tanzania kuendelea kumuombea yeye na wenzake kama Papa Francis anavyoagiza ili malengo ya safari ya kuwapo duniani yafanikiwe.

Alisema kwamba watoto wake Daniel na Marco (kwa sasa wote ni marehemu) ambao ndio kifupi cha zahanati hiyo DA.MA wamemfanya kujitambua na kusaidia wengine katika kuonesha upendo.

Aidha alisema kwamba ataendelea kukumbuka Vikawe kwani alifika mara ya kwanza mwaka 2005 na kuona hali ilivyokuwa ambapo sasa lipo jengo la zahanati hiyo likiwa limekamilika.

Wazo la ujenzi wa zahanati hiyo , lilitolewa na wananchi wa Vikawe kwa Masisita Waabuduo Damu ya Kristo mwaka 2004 wakati wakiwa katika eneo hilo baada ya kununua ekari 40 kwa ajili ya kilimo mwaka 1994.

Alisema pamoja na maombi hayo na wao wenyewe kutambua kwamba kuna mahitaji makubwa ya huduma ya afya japokuwa kuna zahanati ya serikali, hawakuweza kutekeleza maombi ya wanavijiji hadi mwaka 2011 walipofanikiwa kupata ufadhili kutoka Italia na kuanza ujenzi mwaka 2013.

Katika risala yao walisema kwa ushirikiano kati yao na wafadhili hao wamefanikiwa kuwapo kwa zahanati hiyo yenye mahitaji yote ya msingi kwa mujibu wa taratibu za serikali na kuzidi.

Msoma risala alisema kwamba wataendelea kupanua miundombinu mpaka zahanati hiyo ifikie ngazi ya cha afya na baadae hospitali.

Pamoja na ujenzi wa zahanati hiyo ya kisasa masisita hao wameanzisha shule ya awali kuwaandaa wanafunzi wa darasa la kwanza.

Wamesema kwamba wanaamini kwamba wataendelea kushirikiana na wananchi na wadau wengine wa afya katika kuimarisha huduma za hospitali hiyo.

Zahanati hiyo pamoja na vifaa tiba pia ina raslimali ya visima vya maji ya mvua ujazo zenye ujazo wa lita laki moja na kingine lita 49 elfu, wanatumia umeme wa sola na jenereta .

Walisema kwamba wanachangamoto ya kukosa umeme wa Tanesco, barabara nzuri na nyumba za wafanyakazi.

IMG_0289

Mwenyekiti wa kijiji cha Vikawe, Kibaha, Shabaan Mgini akiwasalimia wageni waalikwa wakati wa utambulisho.

IMG_0301

Sr. Theresia Rogatus akisoma risala katika hafla ya ufunguzi wa Zahanati ya Da.Ma Africa DMD iliyopo Vikawe, Kibaha.

IMG_0323

Mganga Mkuu wa Halmashauri ya wilaya ya Kibaha, Dr. Happiness Ndosi akizungumza kwenye hafla ya ufunguzi wa Zahanati ya Da.Ma Africa -DMD kijiji cha Vikawe, Kibaha. Kutoka kushoto ni Mdau wa Zahanati hiyo, Dr. Zuberi Mzige wa Hospitali ya Mwananyamala,

IMG_0335

Mganga Mkuu wa Halmashauri ya wilaya ya Kibaha, Dr. Happiness Ndosi akimpa mkono wa shukrani Mfadhili aliyejitolea kujenga Zahanati hiyo Raia wa Italia, Germano Frioni kwa ujenzi wa Zahanati hiyo itakayohudumia wakazi wa kijiji cha Vikawe, Kibaha.

IMG_0341

Masista Waabuduo Damu ya Kristo wakielekea meza kuu kwa mwendo wa madaha huku wakiwa wamebeba zawadi kwa ajili ya kumkabidhi mgeni rasmi na wafadhili waliojitolea kujenga Zahanati hiyo.

IMG_0348

Mganga Mkuu wa Halmashauri ya wilaya ya Kibaha, Dr. Happiness Ndosi (kulia) akimkabidhi zawadi Mfadhili aliyejitolea kujenga Zahanati hiyo Raia wa Italia, Germano Frioni. Anaye shuhudia tukio hilo ni Baba Paroko wa Parokia ya Bikira Maria wa Mlima Kalmeri Bunju...

IMG_0351

Mganga Mkuu wa Halmashauri ya wilaya ya Kibaha, Dr. Happiness Ndosi akikabidhi zawadi kwa wadau waliombatana na Mfadhili aliyejitolea kujenga Zahanati hiyo Muitalia, Germano Frioni.

IMG_0354

IMG_0194

Mganga Mkuu wa halmashauri ya Mji wa Kibaha, Dr. Happniness Ndosi (wa pili kulia) pamoja na Mfadhili wa ujenzi wa Zahanati ya Da.Ma Africa ya kijiji cha Vikawe, Kibaha, Muitalia, Germano Frioni wakikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Zahanati hiyo inayosimamiwa na Masista Waabuduo Damu ya Kristo nchini.

IMG_0230

Muonekano wa ndani ya Zahanati ya Da. Ma Africa-DMD iliyop Vikawe, Kibaha mkoa wa Pwani.

IMG_0211

Mganga Mkuu wa halmashauri ya Mji wa Kibaha, Dr. Happniness Ndosi akiangalia chumba cha dawa katika Zahanati hiyo mara baada ya kuzinduliwa.

IMG_0235

Wageni waalikwa wakijadiliana jambo mara baada ya kufungiliwa rasmi Zahanati hiyo nje ya moja ya chumba cha upasuaji mdogo.

IMG_0128

Baba Paroko wa Parokia ya Bikira Maria wa Mlima Kalmeri Bunju akiendesha ibada takatifu ya misa maalum kabla ya ufunguzi rasmi wa Zahanati hiyo.

IMG_9973

IMG_0089

Wanakijiji wa Vikawe wakishiriki ibada maalum wakati wa uzinduzi wa Zahanati ya Da. Ma Africa.

IMG_0126

IMG_0086

IMG_0265

Kwaya ikitoa burudani.

IMG_0017

Wageni waalikwa na wanakijiji wakishiriki kuimba pamoja na kwaya.

IMG_0102

Pichani juu na chini ni baadhi ya wanakijiji na wageni waalikwa waliohudhuria uzinduzi huo.

IMG_0140

Umati wa wageni waalikwa na wanakijiji wa Vikawe.

IMG_0361

Mgeni rasmi Mganga Mkuu wa Halmashauri ya wilaya ya Kibaha, Dr. Happiness Ndosi katika picha ya pamoja na wadau pamoja na wafadhili waliojenga Zahanati hiyo.

IMG_9898

Masista Waabuduo Damu ya Kristo wakifurahia taswira za picha za mnato kutoka kwenye kamera.

IMG_0224

Jenereta la Zahanati ya Da.Ma Africa linalotumika kutoa umeme katika Zahanati hiyo.

IMG_9881

Muonekano wa nje wa jengo la Zahanati ya Da.Ma Africa kabla ya kuzinduliwa rasmi.

IMG_0247

Wanakijiji wa Vikawe na wageni waalikwa wakiingia kukagua Zahanati hiyo mara baada ya kuzinduliwa.

COMMENTS

Name

Anga,11,Arusha,27,Burudani,308,burundani,1,come rain,1,come sun,1,Crazy in Love kama wimbo kama wao wenyewe,1,dahh sijui kweli mbona shida,1,Dar utakuja je tumejiandaa,1,daraja sahau nini,1,demokrasia ya upanga,1,Dodoma,78,Dole tupu vijana wa zamani,1,Duhh bibie endeleza libeneke,1,Duhh kaisikie Walibana,1,duhh kwa mbagala mama lazima awe supa,1,Fedha za maiti haziliwi bure,1,Fedha za watu kwa maendeleo ya watu,1,Fikira,14,filamu,243,Filamu ndio kielelezo cha ukuzi wa taifa,1,flamu,7,Gandamiza Kibara baba ake,1,Habari,4976,habari dodoma,19,habari. dodoma,31,hadithi,19,hakika tumeweka historia,1,hakuna noma jongwe,1,hapa kwetu inakuwaje vile,1,hasira hasara,1,hata maji,1,hataki masikhara na maisha yake,1,hatubonyezi kizenji,1,haya ndiyo mambo ya Ulaya,1,haya si yangu ni ya mdau mwenye hasira,1,haya wabongo na mambo kutoka nje,1,He he he wananikumbusha upishi wa shaba,1,Headline,1,Hii hurejesha uhai,1,Hii iko sawa kweli?,1,Hii imekaa vizuri,1,Hii inakaaje vile,1,Hii kweli noma,1,Hii maana yake Moro kuna uhaba wa chakula,1,Hii mexico,1,Hii mihasira mingine bwana,1,Hii ndio moro sio mpaka dar,1,hii ni hatari,1,Hii ni kiboko anayetaka kubisha ajibishie tu,1,Hii ni moja ya staili za kunyoa nywele,1,Hii si lukwangule,1,hii staili mpya,1,hili ni jengo pacha la malaysia ghorofa 88,1,Hivi ni ngoma tu,1,hivi nini siri za serikali,1,hivi sisi tunajua kama kuna vitu vya aina hii,1,hivi vitu bwana,1,Hiyo ndiyo gharama ya demokrasia,1,Hizi imani nyingine ni hatari,1,Hizi takwimu hizi mhh,1,Hongera bibie,1,Hongera dada etu kwa kutuletea kaka etu (shemeji) kwani mwenye dada hakosi shemeji,1,Hongera sana,1,huhitaji mifedha kuwa msafi,1,Huko Ulaya,1,Huu ndio ustaarabu,1,huu ujiko utakuwa mkubwa,1,imetosha,1,Inahitaji nidhamu fulani,1,inakuuma au...,1,Inakuwaje kama filamu yenyewe itahitaji busu la nguvu,1,Inaonekana watanzania hatukuwepo,1,Ipo kazi Maximo,1,Iringa,22,Isiwe mijineno tu manake mihela hubadili watu kweli,1,Itakuwa laki moja ya halali,1,jamani huu kama si ushamba kumbe nini,1,Jamani mbona Mungu anatupigania,1,Jamani watoto wanatakiwa kupendwa,1,jamani.. jamani ukiikosa Diamond usijutie,1,Je nyumbani hakuna vitu vya aina hii?Tuambie,1,je walikuwepo watu wa huduma ya kwanza,1,Je watanzania wanalipa kodi,1,jela kwa raha,1,Jolie,1,juhudi za lazima kuinua filamu,1,kama si kiwanda cha chumvi nani atawajua hawa,1,Kama kweli ndio kweli basi kila heri,1,Kama Mkristo naamini hilo hiyo si sahihi,1,kama unajua kuyarudi nenda Malta,1,kama wao wanaweza sisi je,1,Kamua baba waache wakanyagane,1,karibu nyumbani dada yote maisha tu,1,karibu Tatiii,1,KARIBUNI,1,Katavi,5,kaza buti hakuna kukata tamaa inalipa,1,kazi kwako mheshimiwa waziri wa madini,1,kazi na burudani,1,keep it up bloggers,1,kero ya usafiri sasa kwisha,1,Kila chenye roho na mwili kitaonja umauti,1,kila kitu kina vitu,1,Kila la Heri jamila,1,kila la heri kwani ni changamoto,1,Kipya,51,Kiuno bila mfupa,1,Kolelo mzimu ambao bado hai,1,KUBWA,1,Kudumisha urafiki wa dunia,1,Kuna dalili za wasomi kukubali Uafrika,1,kuna makala humu humu ndani ya blogu sijui mnasemaje,1,Kuu,113,kwa mara nyingine tena Tigo imewezesha,1,Kwa mchanganyiko huu muungano lazima udumu,1,Kwa mihasira hajambo,1,kweli,1,Kweli ina mkono mrefu tuone,1,Kweli duniani tunatofautiana,1,la maana ni kuwa na jiko au vipi,1,labda halitabadilika tena,1,lakini mwafaka lazima,1,lengo ni kutafakari,1,leteni vitu tuvione,1,lets us,1,Lucy wanakuelewa hawa...,1,Lukwangule nyumbani kwetu,2,M ungu bariki mikono ya madaktari wafanikiwe,1,MAARUFU,1,maendeleo ya soka siku zote yanahitaji fedha ili yapatikane,1,maisha ni vyema kuyaangalia,1,MAJIBU,1,makala,52,mama ni mama tu anapendeza,1,mambo mengine we angalia tu,1,mambo msimamo,1,mambo sasa mchanganyiko,1,Mara nyingine huona tunakotoka kwa kuona wenzetu,1,Mashabiki wa rhumba mpooooooooo,1,Masitaa,12,Maskani,1,MASOKO,3,Masupa staa mnaoinukia mpoo,1,Matamasha,6,mavazi ya kuogelea yanaposhindaniwa,1,Mbeya,11,Mchakamchaka anti Asmah,1,Mchanganyiko,81,MCHANYATO,1,mchezo,5,mengi wanayoyaita siri ni public information,1,mfumuko wa bei mpaka noma,1,Mhh sijui watu wa Sua ambao wako huko wanasemaje,1,Mhh ugua pole dada watu wanataka burudani,1,Michezo,510,Michezo maalum inatakiwa kupigiwa debe,1,miguu,1,miguu babu,1,Mikataba mingine ama hakika tuiangalie hata wakopeshaji nao wanatugeuza sakala,1,MIMI NI KISURA NAJITAMBUA,1,Mimi sijajua hasa kumetokea nini kwani ninavyojua hawa huwa na ungalizi wa hali ya juu,1,Mimi simo,1,mimi sisemi,1,mkiwa chumvi basi mkoze,1,Mkiwa taa mulikeni,1,Mnaonaje je hii imekaa vyema,1,Mnaweza wakwetu hapa,1,Morogoro,51,mrithi wa mwanadada Whitney Houston,1,Mtwara,4,Mungu aiweke mahali pema roho yake,4,Mungu amrehemu,1,Mungu amweke pema peponi,1,Mungu awabariki sana,1,Mungu awe nao,1,Mungu ibariki Tanzania,1,Mungu tuepushe na imani hizi za kishirikina,1,mungu tufanye tuwe na upendo,1,Mungu twaomba utuhurumie,1,Muziki,351,muziki na fasheni,6,Mwanahabari,33,Mwanza,6,Mwendo mdundo dada,1,Mwenge huo utakimbizwa duniani kwa siku 130,1,Mwenge wa olimpiki ni ishara ya urafiki,1,Mzee wa Farasi nakupa saluti,1,Mzimbabwe huyu kutoka kwa mama mkali,1,N i dar mpaka Moro au bao tatu bila,1,Na sisi je,1,Naam kama haiwezekani hapa,1,Nairobi waanzisha tena utalii,1,namna bora ya kusaidia jamii,1,nani abebe hukumu na lawama,1,nani asiyejua utamu wa pipi,1,Nani kama baba,1,naona inafaa kuchangia mimi sitoi hoja,1,ndoa za mastaa huwa na mgogoro,1,nenda mwaya nenda,1,New Zanzibar Modern Taarab na wapenzi big up,1,news,5,Ni bikini kwa kwenda mbele,1,Ni Dar mpaka Moro au.. tatu bila,1,ni furaha za muungano,1,Ni kazi ngumu yenye kuhifadhi utamaduni,1,Ni kuchakarika kuonyesha urafiki na biashara pia,1,ni mfumuko wa bei au mfumuko wa nchi,1,Ni muhimu kutazama afya yako,1,ni muziki kwa kwenda mbele,1,Ni muziki mpaka China,1,Ni raha tupu,1,Ni Serengeti Premium Lager,1,Ni Tigo na mawasiliano ya kisasa,1,Ni wakati wa kuujadili utamaduni,1,Ni zaidi ya jazz,1,Nitasubiri and welcome home,1,nje je?,1,NUKUU YA LEO,1,nyie mnasemaje kuhusu hili,1,Ona Kolelo na sindikizwa na Wazee wa Gwasuma,1,ona vya dunia,1,One step ahead,1,patna mwingine mjamzito,1,Pengine anamuogopa Jada Pinkett manake kwa wivu..,1,picha,494,Pole Jamila hayo ndiyo mashindano,1,poleni sana,1,poleni sana wanyalukolo,1,Powa sana,1,Profesa jamaa wanakumaindi,1,Roho za marehemu zipate pumziko la milele,1,Ruvuma,9,sakata dansi mpaka kwenye kilele cha dunia,1,sasa kumebakia ugonjwa mmoja polisi kuendesha mashtaka,1,sasa mifedha kila mahali hongereni,1,Sasa ni mavuno,1,Sasa ni wakati wa kutafuta upenyo ndani ya IDOLS,1,SAYANSI,1,SAYANSI ANGA,2,See Uluguru Montains,1,serikali inataka kujihami kwanini,1,Show of support Big Up Madame,1,Si kitu kidogo hata kidogo,1,si unajua tena namie naimwaga hivyo hivyo,1,Siasa,346,siasa habari,2,Sijui kama City wanajua Mbagala noma,1,Sijui tunaishi karne gani yailahi,1,Sinema,9,sio advencha....kaaa ...niko kibaruani,1,Sisi ndio tunaanza vitongoji,1,Sisi yetu macho na masikio,1,Slow slow jamani,1,sto,1,tabasamu kali la mwenge wa olimpiki,1,Tabora,1,Tazama Waziri Mkuu Pinda wasije wakapindisha maamuzi yako,1,TEKNOLOJIA,1,Thats big man game,1,This is crazy Africa,1,This is Mgeta,1,Tibet wamegeuza Olimpiki jukwaa la siasa,1,Titbits collection,1,Tubadili tamaduni,1,Tuchangie mambo yaive,1,tuendeleze sanaa,1,tuienzi na sisi mbona wizara haituambii,1,Tuipeleke kaskazini,1,Tuisaidie serikali shida ya Mererani,1,tujue namna ya kupumzika,1,Tulienda kustarehe au kufanya fujo,1,Tumsaidie mtototo huyu kurejea katika hali ya kawaida,1,tunahitaji haya,1,Tunajifunza kweli kutoka kwao,1,Tunapandisha chati tu,1,Tunasubiri,1,tunazidi kuhesabu siku,1,TUNAZISUBIRI ZA VINARA ADAR,1,Tuombe nafuu kwa wagonjwa,1,Tuombe rehema kwa mungu,1,Tuone yatufae,1,Tusingoje wengine watusemee,1,tutampa tafu kubwa Prof,1,tuuenzi utamaduni au vipi,1,Tuukuze na kuulinda,1,tuvipende,1,tuwalinde maalbino,1,Tuwe kweli wakweli,1,ubunifu siku zote hulipa,1,uchumi huzunguka kwa kuwawezesha wasukaji,1,udumu muungano,1,Ugonjwa huu wa sasa ni kitendawili,1,Ukiiona kolelo utaipenda,1,Ukirejea salama kila mtu anafurahi,1,Umelenga Mkuchika utamaduni unakufa,1,unaposaka uwakilishi wa dunia,1,urafiki,1,Usisahau wazee wa Ngwasuma,1,UTAMADUNI,1,Video,2,Vionjo vipya ndani ya Gwasuma,1,Vita dhidi ya ufisadi,1,vitongoji Miss Tanzania navyo vimeanza,1,Vitu vikali vyazidi kuingia Dar,1,Vituko,77,Vituo vya polisi Tanga vyatelekezwa,1,VIVALO,1,Wacha tujifue,2,Wadau ilitolewa kiingereza,1,wakali wa ubunifu,1,wala usibabaike mwakwetu hii noma,1,wanadamu wanapotaka kujua zaidi,1,wanasema mpaka kieleweke,1,Wanataka kujua mali za JK na wengine,1,Wanawake wenye mvuto: Monroe,1,Wapo mabinti wa matawi ya juu,1,watu wanapofanya weli kwenye sanaa,1,waweza kurejea enzi ya Moro jazz na Cuban malimba,1,Wazee tupo kusindikiza,1,waziri,1,welcome dar baby,1,Wenzetu wameona sisi tunangoja nini kuangalia,1,wewe unasemaje,1,wigo mpana wa utamaduni,1,wilaya ya 'Mbagala' mlie tu,1,Yaaani sijui itawezekana,1,Yaani wakati mwingine hata huelewi prioty over priority,1,yeye mbele sisi nyuma,1,Yote maisha dada,1,ZA MOTOMOTO,1,Zanzibar,79,zawadi zinatakiwa ziende shule,1,ZILIZOTIA FORA,1,zitachangia kupunguza makali ya bei za umeme,1,
ltr
item
Lukwangule Entertainment: WAKRISTO WA ITALIA WAWEZESHA ZAHANATI YA KISASA VIKAWE
WAKRISTO WA ITALIA WAWEZESHA ZAHANATI YA KISASA VIKAWE
http://dewjiblog.com/wp-content/uploads/2015/07/IMG_0282.jpg
Lukwangule Entertainment
https://lukwangule.blogspot.com/2015/08/wakristo-wa-italia-wawezesha-zahanati.html
https://lukwangule.blogspot.com/
http://lukwangule.blogspot.com/
http://lukwangule.blogspot.com/2015/08/wakristo-wa-italia-wawezesha-zahanati.html
true
934549962738256429
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy