Mhasdhamu Isuja akiwa na rais Mstaafu wakati wa sherehe za miaka 40 ya uaskofu ASKOFU wa kwanza Mzalendo na wa tatu kwa jimbo kato...
![]() |
Mhasdhamu Isuja akiwa na rais Mstaafu wakati wa sherehe za miaka 40 ya uaskofu |
ASKOFU wa kwanza Mzalendo na
wa tatu kwa jimbo katoliki Dodoma, Mhashamu Mathias Isuja Joseph (
86) amefariki dunia akitibiwa katika hospitali ya misheni ya Mtakatifu
Gaspar, Singida.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka
kwa Uongozi wa Jimbo Kuu Katoliki Dodoma,Mhashamu Isuja ambaye alistaafu kazi
hiyo ya uaskofu mwaka 2005 atazikwa kanisa kuu la Jimbo katoliki Dodoma la
Paulo wa Msalaba Jumatano ijayo.
Mhashamu Isuja aliteuliwa kuwa
askofu wa Dodoma Juni 26 1972 akichukua nafasi ya Askofu Anthony Jeremiah
Pesce ambaye alifariki Desemba 20 1971. Kabla ya askofu Pesce ambaye aliteuliwa
Mei 10,1951 alikuwapo askofu Stanislas dell’Addolorata ambaye aliteuliwa
Juni16 1937 na kufariki 1941.
Jimbo Katoliki Dodoma lilianzishwa
mwaka Januari 28,1935.
Jimbo hilo kwa sasa
linaongozwa na Askofu Mkuu Beatus kinyaiya aliyeteuliwa Novemba 6,2014
kuchukua nafasi ya Askofu Gervas John Mwasikwabhila Nyaisonga ambaye alikwenda
kuwa Askofu wa Mpanda. Askofu Nyasionga alichukua nafasi ya Askofu Jude Thadeus
Ruwa’ichi ambaye 2010 alichaguliwa kuwa askofu wa Mwanza.
Askofu Isuja, ambaye wengi
walizoea kumwita “Babu”, amefariki dunia akiwa ametumikia utumishi wa Mungu kwa
miaka 55 ya huduma ya Upadre na miaka 43 ya Uaskofu huku akibahatika kuona
Jimbo Katoliki Dodoma likizaa Jimbo Katoliki la Kondoa na hatimaye, kupandishwa
hadhi kuwa Jimbo kuu la Dodoma.
Katika uhai wake Askofu Isuja
tangu akiwa Padre hadi Askofu alikuwa chachu kubwa katika masuala ya elimu
Jimboni Dodoma,kupambana na umasikini lakini pia alisistiza wakazi wa mikoa ya
kanda ya kati kukabili umaskini kwa kujikita katika kilimo cha zabibu.
Askofu Isuja alikuwa pia
kipenzi cha watoto wa Shirika la Utoto Mtakatifu Kipapa ambapo mara nyingi
alikuwa akiwasisitiza kupeleka neno kwa watoto wenzao huku akiimba sisi ni
Christopher.
Askofu Isuja alizaliwa Agosti
14,1929 katika kijiji cha Haubi Kondoa,alipata daraja takatifu la Upadre
Desemba 24,1960 Parokiani Kondoa na Septemba 17,1972 alipata daraja takatifu la
Uaskofu Jimboni Dodoma.
Aidha mwaka 2005 Askofu Isuja alikabidhi
utawala wa kichungaji kwa Ruwaichi kwa mujibu wa sheria za Kanisa pamoja na
kwamba aling’atuka.
Askofu Isuja
ni mtoto wa Mzee Joseph Chundu na mama Odilia Mbula alizaliwa Agosti 14, 1929
katika kijiji cha Haubi Wilayani Kondoa.
Alisoma
shule ya msingi Kondoa na Bihawana kuanzia mwaka 1942 hadi 1948, mnamo mwaka
1949 hadi 1953 alichaguliwa kujiunga na elimu ya Sekondari katika
Seminari ya Bihawana.
Mwaka
1953 hadi 1955 alijiunga na seminari ya Tosamaganga kwa elimu ya falsafa na
mwaka 1956 hadi mwaka 1960 alijiunga na seminari ya Kibosho kwa elimu ya
theology.
Mnamo
mwaka 1960 alitunukiwa daraja la upadri katika parokia ya Kondoa mara baada ya
kupewa daraja la upadri alitumwa parokia ya Kibakwe kuwa paroko mwaka 1961 hadi
1963 na mwaka 1963 hadi mwaka 1969 aliteuliwa kuwa katibu wa elimu na ilipofika
mwaka 1966 hadi mwaka 1971 aliteuliwa kuwa makamu wa askofu huku
akiendele na nafasi yake ya katibu wa elimu na mwaka 1971 hadi mwaka 1972
aliteuliwa kuwa msimamizi wa kitume wa jimbo la Dodoma.Aliwekwa wakfu na Kardinali Laurean
Rugambwa mwaka 1972.
Pia
katika uongozi wake taasisi mbalimbali zilianzishwa ikiwemo Bihawana seminari,
nyumba ya malezi ya waseminari wa jimbo Miyuji, chuo cha ufundi
Mpwapwa-magogo,Chuo cha ufundi veyula, chuo cha Ufundi cha John Bosco, Seminari
na chuo cha walimu cha wasalesiani, sekondari ya wasichana ya masista wa
Huruma, kituo cha watoto walemavu Mlali, kituo cha watoto wenye mtindio wa
akili (Cheshire Home Miyuji).
Vile
vile vyuo vya kilimo Ipala na Chikopelo, Holy cross centre, hospitali ya
masista wa Mtakatifu Gemma Galgani Miyuji, Kituo cha Hija Mbwanga, hosteli ya
mapadri Kondoa, nyumba ya watoto yatima Kondoa, nyumba mpya ya Askofu na Ofisi
ya Jimbo.
Askofu Isuja
atakumbukwa pia kwa ushauri alioutoa Julai mwaka 2014 kwamba watanzania
wanapaswa kuheshimu hadhi na mamlaka aliyonayo Rais wa Jamhuri ya Muunganao wa
Tanzania Dk Jakaya Mrisho Kikwete, kwa kuthamini na kuzingatia mwongozo na
ushauri mbalimbali anaoutoa kwa wananchi kwani mamlaka hayo yanatoka kwa Mungu.
Kauli hiyo ambayo aliitoa katika mahubiri yake maalum wakati wa ibada ya misa ya jumapili katika Parokia ya Makole, Jimbo Katoliki la Dodoma, iliyokuwa na lengo la kuchangia ujenzi wa kanisa la kiaskofu Jimbo la Kondoa, alisisitiza Watanzania waombe Mungu ajalie busara na hekima katika kutenda na kuamua mambo mbalimbali yahusuyo nchi yakiwemo malumbano yaliyokuwa yakifanyika nchini kote kuhusu mchakato wa kupata Katiba Mpya.
Askofu huyo alisema hafurahishwi na jinsi makundi mbalimbali ya Watanzania yalivyokuwa yanalumbana na kubeza hata miongozo inayotolewa na Rais Kikwete.
Kauli hiyo ambayo aliitoa katika mahubiri yake maalum wakati wa ibada ya misa ya jumapili katika Parokia ya Makole, Jimbo Katoliki la Dodoma, iliyokuwa na lengo la kuchangia ujenzi wa kanisa la kiaskofu Jimbo la Kondoa, alisisitiza Watanzania waombe Mungu ajalie busara na hekima katika kutenda na kuamua mambo mbalimbali yahusuyo nchi yakiwemo malumbano yaliyokuwa yakifanyika nchini kote kuhusu mchakato wa kupata Katiba Mpya.
Askofu huyo alisema hafurahishwi na jinsi makundi mbalimbali ya Watanzania yalivyokuwa yanalumbana na kubeza hata miongozo inayotolewa na Rais Kikwete.
Wakati
wa wakati wa sherehe ya miaka 40 ya Uaskofu wa Mhashamu baba Askofu Mathias Isuja, Septemba 18 ,2012, Rais
wa awamu ya tatu Benjamini William Mkapa aliwataka kuachwa kwa mtazamo wa
mbaya wa kuwabeza viongozi wastaafu ambao wameitumikia nchi.
“Kustaafu si kuchoka, sio uwe legelege lakini
kwa imani unatakiwa kutoa mchango wako kwa kutumiza wajibu wako katika jamii”
alisema
Alisema
kuwa tatizo kubwa lililo katika jamii ni kutotaka kuheshimu mamlaka kwani kila
mtu anajifanya kuwa mjuaji maishani, haambiliki.
Aidha
Rais mstaafu Mkapa alishawahi kusikika akisema kwamba anamheshimu Askofu huyo kutokana na kutosikia
malumbano ya dini.
Alisema
kuwa,Katika kipindi alichokuwa waziri wa mambo ya nje na hata alipokuwa rais
hakuwahi kusikia malumbano yoyote ya kidini mkoani Dodoma na hilo ni jambo la
kujifunza katika umoja na mshikamano wa madhehebu ya dini ya kikristo na
kiislam.
“Tutamuenzi
Askofu Isuja kwa kuzingatia kauli mbiu yake na ngao yake ya mapendo, haki na
amani.” Alisema.
Naye
Askofu Mkuu Jimbo Kuu la Dar es Salaam Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo
alisema kuwa askofu Isuja atakumbukwa kwa mchango wake kwa kuboresha huduma za
afya na ujenzi wa shule na zahanati.
Source: Sifa Lubasi, Habarileo Dodoma
COMMENTS