MBEGU BORA ZA MIGOMBA, VIAZI LISHE NA MIHOGO KUWAKOMBOA WAKULIMA MKOANI KAGERA

Kaimu Ofisa Kilimo Wilaya ya Muleba,  Kokushubila Pesha akipanda mbegu ya muhogo katika shamba darasa la kikundi cha Ujamaa  lililopo Kata...

Kaimu Ofisa Kilimo Wilaya ya Muleba,  Kokushubila Pesha akipanda mbegu ya muhogo katika shamba darasa la kikundi cha Ujamaa  lililopo Kata ya Magata Karutanga wilayani humo. 


Ofisa Mtendaji wa kata ya Magata Karutanga Joyce Rassia akizungumza na wakulima wakati wa uzinduzi wa upandaji wa shamba darasa la kikundi hicho.










Mjumbe wa kikundi cha Ujamaa,  Liberatha Lespicius akisoma risala wakati wa uzinduzi huo mbele ya mgeni rasmi.


Mtafiti wa mazao ya mizizi kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo Maruku,  Jojianas Kibula akitoa maelekezo kwa wakulima jinsi ya kupanda mbegu hizo bora za mihogo kwa wakulima wa kata ya Magata Karutanga wilayani Muleba.


Baadhi ya wana kikundi cha Ujamaa wakishirikiana kwenye kupanda mbegu hizo bora baada ya uzinduzi rasmi wa shamba darasa hilo.


Kaimu afisa ugani wa wilaya ya Muleba  Kokushubila Pesha akizungumza na wakulima wakati akizungua shamba darasa hilo kwa niaba ya Mkurugenzi mtendaji wa wilaya hiyo.


Afisa mtendaji wa kijiji cha Omurunazi Edga Rumanyika akitoa neno kwa wageni na wanakikundi cha Mendeleo wakati wa uzindizi wa shamba darasa la Migomba.


Muwakilishi wa mk urugenzi mtendaji wa wilaya ya Muleba Kokushubila Pesha akitoa neno kwa wageni na wanakikundi cha Mendeleo wakati wa uzindizi wa shamba darasa la Migomba.


Wanakikundi cha Maendeleo kwenye kijiji cha Omurunazi wilayani Muleba  wakisikiliza maelekezo na maneno ya viongozi na wataalamu kabla ya kuzindua upandaji wa shamba darasa lao la Migomba kijijini hapo.


Afisa kilimo Mkoa wa Kagera Luois Baraka akizungumza na wakulima wa kijiji cha Omurunazi na kutoa salama za ofisi ya mkuu wa mkoa kwa wakulima hao.


Picha ikionyesha shamba darasa lililoandaliwa na wanakikundi cha Omurunazi kikundi cha Maendeleo kwaajili ya kupanda mbegu safi za migomba iliyozalishwa kwa njia ya chupa.


Mtafiti kutoka COSTECH,  Bestina Daniel akizungumza na wakulima na kuwapa salamu za mkurugenzi mkuu wa COSTECH.


Msaidizi wa katibu wa kikundi cha Maendeleo Sekunda Peter akisoma Risala ya kikundi chao


Mtafiti kutoka COSTECH Beatrice Lyimo akizungumza na wakulima wa kikundi cha maendeleo na kuwaeleza malengo na faida za mbegu hizo wilayani humo.






Muwakilishi wa Mkurugenzi mtendaji wa wilaya ya Muleba Kokushubila Pesha akizungua shamba la kikundi cha Maendeleo kwa kupanda mche wa kwanza wa Mgomba kwenye shamba darasa hilo.
Na Dotto Mwaibale, Muleba, Kagera

Imeelezwa kuwa Usambazaji wa mbegu za mazao ya mizizi na Migomba kwa vikundi vya wakulima kwenye Mkoa wa Kagera utasaidia kuwahakikishia wananchi wa mkoa huo usalama wa chakula na mazao mbadala baada ya zao lao kuu la chakula la mgomba kuathiriwa na ugonjwa wa  mnyauko.

Kauli hiyo imetolewa na Afisa Kilimo Mkoa wa Kagera,  Louis  Baraka wakati akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukamilika kwa zoezi la ugawaji wa mbegu bora za mazao hayo kwenye wilaya tano za mkoa huo ambazo ni Missenyi, Karagwe, Kyerwa, Biharamulo na Muleba.

Alisema kuwa wakazi wa mkoa huo wamekuwa na njaa kali kwa misimu miwili iliyopita  kutokana na zao lao kuu la chakula la migomba kushambuliwa na ugonjwa hatari wa mnyauko na hivyo kuwafanya wananchi kuhangaika kutafuta chakula na kuomba chakula cha msaada kutoka Serikalini.

Baraka alisema kuwa upatikanaji wa mbegu bora za migomba safi iliyozalishwa kwa njia ya chupa itafufua zao hilo ambalo wakulima wengi walishalitelekeza kabisa baada ya kuona zao hilo likikauka na kushindwa kuwapatia chakula walichokizoea kwa miaka mingi.

Aidha Baraka  ameishukuru  Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) na Jukwaa la Bioteknolojia kwa Maendeleo ya Kilimo OFAB kwa kuwapelekea pia mbegu bora za Mihogo aina ya Mkombozi na Mbegu bora za viazi lishe ili kuwapatia wananchi wa mkoa huo mazao mbadala baada ya kutegemea zao la mgomba pekee.

Alisema kuwa kwenye wilaya zote tano za mkoa wa Kagera COSTECH imeweza kuwapatia mbegu za marando ya viazi lishe  30,000, Mihogo mbegu 27,000 na Migomba 1,000, ingawa wameongea na wafadhili hao na kuwaahidi kuwaongeza mingine zaidi ya 500.

Kwa upande wake Mtafiti kutoka COSTECH, Bestina Daniel alisema kuwa mpango huo ni mkakati wa utekelezaji wa majukumu ya tume ya kufikisha matunda ya tafiti mbalimbali zinazofanywa hapa nchini kwa walengwa ili ziweze kuzaa matunda yaliyokusudiwa.

Alisema kuwa baada ya watafiti kumaliza kufanya tafiti zao huziacha kwenye vituo vyao vya utafiti lakini COSTECH inasaidia kuhakikisha tafiti hizo zinatoka kwenye vituo hivyo na kwenda kwa wakulima kama ambavyo wameamua kufanya kwenye zao la 
Muhogo,Migomba na viazi lishe ambavyo vinasaidia kuongeza lishe,usalama wa chakula na kipato.

Bestina pia alibainisha kuwa ili kufikia uchumi wa viwanda ni lazima maandalizi ya upatikanaji wa malighafi kwaajili ya viwanda hivyo yafanyike ili wawekezaji wanapokuja wakute tayari malighafi zipo na hivyo kumhakikishia upatikanaji wa 
malighafi hizo zitokananzo na mazao ya kilimo.

Mtafiti huyo kutoka COSTECH alisema mara viwanda vinapoanzishwa vitasaidia wakulima wengi wa mazao hayo kupata soko la uhakika na kuongeza chachu ya uzalishaji kwakuwa wakulima wengi nchini kilio chao kikubwa ni soko la mazao yao.

Hata hivyo amewataka kuendelea kuzalisha mazao hayo kwa wingi hususani mihogo na viazi lishe kwakuwa soko la kwanza ni wao wenyewe na hata sasa mahitaji ya mazao 

kama vile viazi lishe ni makubwa kwenye kaya na maeneo mengi nchini hivyo wasiwe na shaka na soko kwa sasa.

Akizungumzaia umeuhimu wa vikundi,mashamba darasa hayo ya mbegu Mtafiti kutoka  COSTECH Dkt. Beatrice Lyimo alisema kuwa COSTECH haiwezi kuwafikia wakulima wote kwenye mkoa mzima na kuwagawia mbegu hizo bora lakini kupitia vikundi wakulima  wanaweza kuzizalisha na kasha kugawana kwenda kwenye mashamba yao na baadae kuwapatia na wakulima wengine nje ya vikundi hivyo.

Aliwataka kuzitunza na kuhakikisha zinalindwa maana ni lulu na zimenunuliwa kwa gharama kubwa na endapo watazitunza vizuri baadae wataweza kuwauzia wakulima wengine kwenye maeneo mbalimbali na hivyo kuzifanya zienee kwenye maeneo yote ya 
mkoa huo.

Mtafiti wa Mazao ya Miziz kutoka Kituo cha Utafiti wa kilimo ARI-Maruku cha mkoani Kagera Jojianas Kabula aliwaambia wakulima kuwa hekta moja ya muhogo tani 25 hadi 
32 wakati viazi tani 7 hadi 9 kwa Hekta moja.

Alisema kuwa endapo watafuata kanuni bora za kilimo cha mazao hayo kwa kuzingatia nafasi kati ya mche na mche na mstari kwa mstari na matumizi ya mbolea wataweza kuongeza uzalishaji zaidi tofauti na sasa ambapo kwenye hekta moja ya muhogo tani
nane hadi kumi wakati kwenye viazi wanapata tani moja hadi 3.

Mtafiti huyo alisisitiza kuwa mbegu hiyo ya Muhogo ya Mkombozi imefanyiwa utafiti  na kuonekana kustahimili magonjwa hatari ya mihogo ya batobato kali na michirizi ya kahawia ambayo imekuwa ikiwapatia hasara kubwa wakulima wengini kwa kupoteza hadi asilimia 90 za mazao.

Akizungumzia zao la Migomba Mtafiti wa zao hilo kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo Maruku,  Jasmeck Kirangi alisema mbegu hizo zilizozalishwa kwa njia ya chupa ni safi na hazina magonjwa kabisa na endapo wakulima watazipanda kwenye maeneo safi wataweza kupata mavuno bora kulimo matumizi ya mbegu hizo zao za kawaida.

Aliwaondoa hofu kuwa mbegu hizo walizowaletea ni zilezile za asili zinazopendwa na wakulima wengi kama vile Nshakala hivyo wasiwe na shaka kuwa mbegu hizo zilizozalishwa kwa njia ya chupa sio zile walizozizoea.

Kilangi amesema kuwa mbegu hiyo aina ya Nshakala kama mkulima ataipanda vizuri na kuweka mbolea na kwa kuzingatia nafasi zinazoelekezwa na wataalamu mkulima anaweza 
kupata tani kumi na mbili hadi  ishirini na nne kwa ekari mavuno ambayo kwa sasa wakulima wengi hawafikii.

(Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com simu namba 0712727062)



COMMENTS

Name

Anga,11,Arusha,27,Burudani,312,burundani,1,come rain,1,come sun,1,Crazy in Love kama wimbo kama wao wenyewe,1,dahh sijui kweli mbona shida,1,Dar utakuja je tumejiandaa,1,daraja sahau nini,1,demokrasia ya upanga,1,Dodoma,78,Dole tupu vijana wa zamani,1,Duhh bibie endeleza libeneke,1,Duhh kaisikie Walibana,1,duhh kwa mbagala mama lazima awe supa,1,Fedha za maiti haziliwi bure,1,Fedha za watu kwa maendeleo ya watu,1,Fikira,14,filamu,244,Filamu ndio kielelezo cha ukuzi wa taifa,1,flamu,7,Gandamiza Kibara baba ake,1,haba,1,Habari,4984,habari dodoma,19,habari. dodoma,31,hadithi,19,hakika tumeweka historia,1,hakuna noma jongwe,1,hapa kwetu inakuwaje vile,1,hasira hasara,1,hata maji,1,hataki masikhara na maisha yake,1,hatubonyezi kizenji,1,haya ndiyo mambo ya Ulaya,1,haya si yangu ni ya mdau mwenye hasira,1,haya wabongo na mambo kutoka nje,1,He he he wananikumbusha upishi wa shaba,1,Headline,1,Hii hurejesha uhai,1,Hii iko sawa kweli?,1,Hii imekaa vizuri,1,Hii inakaaje vile,1,Hii kweli noma,1,Hii maana yake Moro kuna uhaba wa chakula,1,Hii mexico,1,Hii mihasira mingine bwana,1,Hii ndio moro sio mpaka dar,1,hii ni hatari,1,Hii ni kiboko anayetaka kubisha ajibishie tu,1,Hii ni moja ya staili za kunyoa nywele,1,Hii si lukwangule,1,hii staili mpya,1,hili ni jengo pacha la malaysia ghorofa 88,1,Hivi ni ngoma tu,1,hivi nini siri za serikali,1,hivi sisi tunajua kama kuna vitu vya aina hii,1,hivi vitu bwana,1,Hiyo ndiyo gharama ya demokrasia,1,Hizi imani nyingine ni hatari,1,Hizi takwimu hizi mhh,1,Hongera bibie,1,Hongera dada etu kwa kutuletea kaka etu (shemeji) kwani mwenye dada hakosi shemeji,1,Hongera sana,1,huhitaji mifedha kuwa msafi,1,Huko Ulaya,1,Huu ndio ustaarabu,1,huu ujiko utakuwa mkubwa,1,imetosha,1,Inahitaji nidhamu fulani,1,inakuuma au...,1,Inakuwaje kama filamu yenyewe itahitaji busu la nguvu,1,Inaonekana watanzania hatukuwepo,1,Ipo kazi Maximo,1,Iringa,22,Isiwe mijineno tu manake mihela hubadili watu kweli,1,Itakuwa laki moja ya halali,1,jamani huu kama si ushamba kumbe nini,1,Jamani mbona Mungu anatupigania,1,Jamani watoto wanatakiwa kupendwa,1,jamani.. jamani ukiikosa Diamond usijutie,1,Je nyumbani hakuna vitu vya aina hii?Tuambie,1,je walikuwepo watu wa huduma ya kwanza,1,Je watanzania wanalipa kodi,1,jela kwa raha,1,Jolie,1,juhudi za lazima kuinua filamu,1,kama si kiwanda cha chumvi nani atawajua hawa,1,Kama kweli ndio kweli basi kila heri,1,Kama Mkristo naamini hilo hiyo si sahihi,1,kama unajua kuyarudi nenda Malta,1,kama wao wanaweza sisi je,1,Kamua baba waache wakanyagane,1,karibu nyumbani dada yote maisha tu,1,karibu Tatiii,1,KARIBUNI,1,Katavi,5,kaza buti hakuna kukata tamaa inalipa,1,kazi kwako mheshimiwa waziri wa madini,1,kazi na burudani,1,keep it up bloggers,1,kero ya usafiri sasa kwisha,1,Kila chenye roho na mwili kitaonja umauti,1,kila kitu kina vitu,1,Kila la Heri jamila,1,kila la heri kwani ni changamoto,1,Kipya,51,Kiuno bila mfupa,1,Kolelo mzimu ambao bado hai,1,KUBWA,1,Kudumisha urafiki wa dunia,1,Kuna dalili za wasomi kukubali Uafrika,1,kuna makala humu humu ndani ya blogu sijui mnasemaje,1,Kuu,113,kwa mara nyingine tena Tigo imewezesha,1,Kwa mchanganyiko huu muungano lazima udumu,1,Kwa mihasira hajambo,1,kweli,1,Kweli ina mkono mrefu tuone,1,Kweli duniani tunatofautiana,1,la maana ni kuwa na jiko au vipi,1,labda halitabadilika tena,1,lakini mwafaka lazima,1,lengo ni kutafakari,1,leteni vitu tuvione,1,lets us,1,Lucy wanakuelewa hawa...,1,Lukwangule nyumbani kwetu,2,M ungu bariki mikono ya madaktari wafanikiwe,1,MAARUFU,1,maendeleo ya soka siku zote yanahitaji fedha ili yapatikane,1,maisha ni vyema kuyaangalia,1,MAJIBU,1,makala,52,mama ni mama tu anapendeza,1,mambo mengine we angalia tu,1,mambo msimamo,1,mambo sasa mchanganyiko,1,Mara nyingine huona tunakotoka kwa kuona wenzetu,1,Mashabiki wa rhumba mpooooooooo,1,Masitaa,12,Maskani,1,MASOKO,3,Masupa staa mnaoinukia mpoo,1,Matamasha,6,mavazi ya kuogelea yanaposhindaniwa,1,Mbeya,11,Mchakamchaka anti Asmah,1,Mchanganyiko,81,MCHANYATO,1,mchezo,5,mengi wanayoyaita siri ni public information,1,mfumuko wa bei mpaka noma,1,Mhh sijui watu wa Sua ambao wako huko wanasemaje,1,Mhh ugua pole dada watu wanataka burudani,1,Michezo,511,Michezo maalum inatakiwa kupigiwa debe,1,miguu,1,miguu babu,1,Mikataba mingine ama hakika tuiangalie hata wakopeshaji nao wanatugeuza sakala,1,MIMI NI KISURA NAJITAMBUA,1,Mimi sijajua hasa kumetokea nini kwani ninavyojua hawa huwa na ungalizi wa hali ya juu,1,Mimi simo,1,mimi sisemi,1,mkiwa chumvi basi mkoze,1,Mkiwa taa mulikeni,1,Mnaonaje je hii imekaa vyema,1,Mnaweza wakwetu hapa,1,Morogoro,51,mrithi wa mwanadada Whitney Houston,1,Mtwara,4,Mungu aiweke mahali pema roho yake,4,Mungu amrehemu,1,Mungu amweke pema peponi,1,Mungu awabariki sana,1,Mungu awe nao,1,Mungu ibariki Tanzania,1,Mungu tuepushe na imani hizi za kishirikina,1,mungu tufanye tuwe na upendo,1,Mungu twaomba utuhurumie,1,Muziki,351,muziki na fasheni,6,Mwanahabari,33,Mwanza,6,Mwendo mdundo dada,1,Mwenge huo utakimbizwa duniani kwa siku 130,1,Mwenge wa olimpiki ni ishara ya urafiki,1,Mzee wa Farasi nakupa saluti,1,Mzimbabwe huyu kutoka kwa mama mkali,1,N i dar mpaka Moro au bao tatu bila,1,Na sisi je,1,Naam kama haiwezekani hapa,1,Nairobi waanzisha tena utalii,1,namna bora ya kusaidia jamii,1,nani abebe hukumu na lawama,1,nani asiyejua utamu wa pipi,1,Nani kama baba,1,naona inafaa kuchangia mimi sitoi hoja,1,ndoa za mastaa huwa na mgogoro,1,nenda mwaya nenda,1,New Zanzibar Modern Taarab na wapenzi big up,1,news,5,Ni bikini kwa kwenda mbele,1,Ni Dar mpaka Moro au.. tatu bila,1,ni furaha za muungano,1,Ni kazi ngumu yenye kuhifadhi utamaduni,1,Ni kuchakarika kuonyesha urafiki na biashara pia,1,ni mfumuko wa bei au mfumuko wa nchi,1,Ni muhimu kutazama afya yako,1,ni muziki kwa kwenda mbele,1,Ni muziki mpaka China,1,Ni raha tupu,1,Ni Serengeti Premium Lager,1,Ni Tigo na mawasiliano ya kisasa,1,Ni wakati wa kuujadili utamaduni,1,Ni zaidi ya jazz,1,Nitasubiri and welcome home,1,nje je?,1,NUKUU YA LEO,1,nyie mnasemaje kuhusu hili,1,Ona Kolelo na sindikizwa na Wazee wa Gwasuma,1,ona vya dunia,1,One step ahead,1,patna mwingine mjamzito,1,Pengine anamuogopa Jada Pinkett manake kwa wivu..,1,picha,494,Pole Jamila hayo ndiyo mashindano,1,poleni sana,1,poleni sana wanyalukolo,1,Powa sana,1,Profesa jamaa wanakumaindi,1,Roho za marehemu zipate pumziko la milele,1,Ruvuma,9,sakata dansi mpaka kwenye kilele cha dunia,1,sasa kumebakia ugonjwa mmoja polisi kuendesha mashtaka,1,sasa mifedha kila mahali hongereni,1,Sasa ni mavuno,1,Sasa ni wakati wa kutafuta upenyo ndani ya IDOLS,1,SAYANSI,1,SAYANSI ANGA,2,See Uluguru Montains,1,serikali inataka kujihami kwanini,1,Show of support Big Up Madame,1,Si kitu kidogo hata kidogo,1,si unajua tena namie naimwaga hivyo hivyo,1,Siasa,346,siasa habari,2,Sijui kama City wanajua Mbagala noma,1,Sijui tunaishi karne gani yailahi,1,Sinema,9,sio advencha....kaaa ...niko kibaruani,1,Sisi ndio tunaanza vitongoji,1,Sisi yetu macho na masikio,1,Slow slow jamani,1,sto,1,tabasamu kali la mwenge wa olimpiki,1,Tabora,1,Tazama Waziri Mkuu Pinda wasije wakapindisha maamuzi yako,1,TEKNOLOJIA,1,Thats big man game,1,This is crazy Africa,1,This is Mgeta,1,Tibet wamegeuza Olimpiki jukwaa la siasa,1,Titbits collection,1,Tubadili tamaduni,1,Tuchangie mambo yaive,1,tuendeleze sanaa,1,tuienzi na sisi mbona wizara haituambii,1,Tuipeleke kaskazini,1,Tuisaidie serikali shida ya Mererani,1,tujue namna ya kupumzika,1,Tulienda kustarehe au kufanya fujo,1,Tumsaidie mtototo huyu kurejea katika hali ya kawaida,1,tunahitaji haya,1,Tunajifunza kweli kutoka kwao,1,Tunapandisha chati tu,1,Tunasubiri,1,tunazidi kuhesabu siku,1,TUNAZISUBIRI ZA VINARA ADAR,1,Tuombe nafuu kwa wagonjwa,1,Tuombe rehema kwa mungu,1,Tuone yatufae,1,Tusingoje wengine watusemee,1,tutampa tafu kubwa Prof,1,tuuenzi utamaduni au vipi,1,Tuukuze na kuulinda,1,tuvipende,1,tuwalinde maalbino,1,Tuwe kweli wakweli,1,ubunifu siku zote hulipa,1,uchumi huzunguka kwa kuwawezesha wasukaji,1,udumu muungano,1,Ugonjwa huu wa sasa ni kitendawili,1,Ukiiona kolelo utaipenda,1,Ukirejea salama kila mtu anafurahi,1,Umelenga Mkuchika utamaduni unakufa,1,unaposaka uwakilishi wa dunia,1,urafiki,1,Usisahau wazee wa Ngwasuma,1,UTAMADUNI,1,Video,2,Vionjo vipya ndani ya Gwasuma,1,Vita dhidi ya ufisadi,1,vitongoji Miss Tanzania navyo vimeanza,1,Vitu vikali vyazidi kuingia Dar,1,Vituko,77,Vituo vya polisi Tanga vyatelekezwa,1,VIVALO,1,Wacha tujifue,2,Wadau ilitolewa kiingereza,1,wakali wa ubunifu,1,wala usibabaike mwakwetu hii noma,1,wanadamu wanapotaka kujua zaidi,1,wanasema mpaka kieleweke,1,Wanataka kujua mali za JK na wengine,1,Wanawake wenye mvuto: Monroe,1,Wapo mabinti wa matawi ya juu,1,watu wanapofanya weli kwenye sanaa,1,waweza kurejea enzi ya Moro jazz na Cuban malimba,1,Wazee tupo kusindikiza,1,waziri,1,welcome dar baby,1,Wenzetu wameona sisi tunangoja nini kuangalia,1,wewe unasemaje,1,wigo mpana wa utamaduni,1,wilaya ya 'Mbagala' mlie tu,1,Yaaani sijui itawezekana,1,Yaani wakati mwingine hata huelewi prioty over priority,1,yeye mbele sisi nyuma,1,Yote maisha dada,1,ZA MOTOMOTO,1,Zanzibar,79,zawadi zinatakiwa ziende shule,1,ZILIZOTIA FORA,1,zitachangia kupunguza makali ya bei za umeme,1,
ltr
item
Lukwangule Entertainment: MBEGU BORA ZA MIGOMBA, VIAZI LISHE NA MIHOGO KUWAKOMBOA WAKULIMA MKOANI KAGERA
MBEGU BORA ZA MIGOMBA, VIAZI LISHE NA MIHOGO KUWAKOMBOA WAKULIMA MKOANI KAGERA
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEj3ocY7d9f9Kpw5_NwJonTSP-iJNDqLoL7FY69TFmlQkL_xaM2pk45v1Pbw7TJZ8ffGmeCAPSSH_HQ8fkkTjxFE9K5HWuFS51O5u167zI27y1me_kFS_7AcgoYTpCbcCa13EQqR6xL8ErkZ/s640/1.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEj3ocY7d9f9Kpw5_NwJonTSP-iJNDqLoL7FY69TFmlQkL_xaM2pk45v1Pbw7TJZ8ffGmeCAPSSH_HQ8fkkTjxFE9K5HWuFS51O5u167zI27y1me_kFS_7AcgoYTpCbcCa13EQqR6xL8ErkZ/s72-c/1.JPG
Lukwangule Entertainment
https://lukwangule.blogspot.com/2017/10/mbegu-bora-za-migomba-viazi-lishe-na.html
https://lukwangule.blogspot.com/
http://lukwangule.blogspot.com/
http://lukwangule.blogspot.com/2017/10/mbegu-bora-za-migomba-viazi-lishe-na.html
true
934549962738256429
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy