TITAN: Sabmarini iliyoua mabilionea watano

  TITAN Sabmarini iliyoua mabilionea watano .Muundo wake wahisiwa kuwa chanzo cha kufumuka, hakikufuata mfumo .Inaelezwa kilishindwa k...

 

TITAN

Sabmarini iliyoua mabilionea watano

.Muundo wake wahisiwa kuwa chanzo cha kufumuka, hakikufuata mfumo

.Inaelezwa kilishindwa kuhimili mgandamizo bahari ya Atlantiki

.Walikuwa wanaenda kuzuru TITANIC walipofia matajiri wengine 1912

 


Na Rahel Pallangyo

ILIKUWA ni safari ya kwenda kwenye mabaki ya meli iliyozama kwa kasi mwaka 1912, safari iliyotarajiwa kutumia kutumia saa 10 ndani ya sabmarini  (nyambizi) Titan, iliyotengenezwa mahususi kwa ajili ya mbizi za kina kirefu.

Titan (iliyojulikana kama Cyclops 2 hadi 2018)  ni chombo cha pili cha kupiga mbizi kilichoundwa na  OceanGate,  kinachomilikiwa na kampuni binafsi na kikiwa na uwezo uliokusudiwa wa kufika mita 4,000 (futi 13,000).

Kikiwa ni chombo cha kwanza cha chini cha maji kilichokamilishwa kikiwa kimejengwa na titanium na nyenzo zenye mchanganyiko wa nyuzinyuzi za kaboni zikipitishiwa metali zote muhimu kwa ajili ya kuhifadhi maisha ya binadamu.

Lakini pamoja na  tajiri yake kuamini kwamba kazi ya kihandishi imefanyika vyema, wapo wataalamu waliowahi kutumia chombo hicho wanasema kilikuwa na shida na hawakushangazwa na  kufumuka kwake kulikotokana na kubanwa na uzito mkubwa wa maji.

Ni kazi kubwa kuamini na itachukua muda watu kupata majwabu sahihi nini kilitokea katika nyambizi hiyo, lakini kauli za watu zinaonesha kwamba kulikuwa na ukiukwaji wa taratibu za kiuhandisi.

"Unakumbukwa kwa sheria unazovunja," anasema mmiliki na mmoja wa watu waliokufa,  Stockton Rush akimnukuu Jenerali wa Marekani Douglas MacArthur kuhusu nini amekifanya kuwa na Titan.

"Nimevunja sheria kadhaa," anasema kuhusu Titan. "Nadhani nimezivunja kwa mantiki lakini kuna uhandisi mzuri nyuma yangu uliowezesha chombo kujengwa na kuwa salama." anasema Rush akizungumza na waandishi wa habari mwaka 2017 lakini Juni 18, 2023, OceanGate ilipoteza mawasiliano na Titan wakati wa kupiga mbizi kwa mara ya kwanza mwaka huo kuelekea  kwenye meli ya Titanic.

Stockton Rush III  alizaliwa California mwaka 1962 katika familia ambayo ilitengeneza utajiri wake kutokana na mafuta na meli anapenda sana kuvumbua na katika pilikapilika hizo amekufa.

Kwa kuwa Titan ilikuwa inapoteza mawasiliano mara nyingi wakati wa majaribio ya awali wa upigaji mbizi wa kitalii, OceanGate haikutahadharisha mamlaka kuhusu kadhia hiyo hadi saa nyingi zilipopita bila chombo hicho kuibuka.

 Juni 22, 2023 jeshi la Marekani linaloshughulika na ulinzi wa pwani ya taifa hilo walipotoa taarifa kuhusu kishindo cha kufumuka kwa chombo chini ya bahari  nabaadaye kupata baki la chombo hicho kikiwa katika omo la meli ya Titanic ambayo ndiyo ilikuwa inatembelewa.

Titanic iliyozama mwaka 1912 imeteka fikira za umma, kwani idadi ya abiria na aina zao ambao wengi walikuwa ni matajiri wa Ulaya waliotaka kuinjoi baharini na kufika Marekani walikufa.

Kipindi hicho Titanic ilikuwa moja ya meli kubwa na tajiri zaidi ulimwenguni. kama waliokufa wakati huo ni amatajiri pia waliokufa safari hii ndani ya Titan nao walikuwa matajiri akiwemo aliyebuni na  kutengeneza chombo chenyewe.

Titanic ilijengwa kwa kuhakikisha kwamba haiwezi kuzama, kutokana na mfululizo kihandisi ulioweka umadhubuti kiasi cha kufanywa kama upinde unaovutika.

Pamoja na umahiri kwa kihandisi siku nne baada ya kuondoka bandarini 1912 meli hiyo ilikwaa jabali la barafu ikakatika na kuza katika kipindi cha saa tatu tu, hapakuwepo na muda wa kutosha kuokoa watu katika majira ambapo bahari ilikuwa baridi zaidi.

Ni moja ya misiba mikubwa ya dunia ya sasa. Ilizama muda huo lakini mabaki yake yalikuja kuonekana mwaka wa 1985 ikiwa imeachana kivipande kwa umbali wa kutosha.

Ikiwa inapatikana 41°43′57′′ Kaskazini  na 49°56′49′′ magharibi hapa ndipo Titan yenye watu watano wote matajiri walipokuwa wamepanga kuzuru kiasi cha futi 13,000 sawa na mita 2000 kutoka usawa wa bahari, kiasi cha takriban maili 400 za baharini (kilomita 740) kutoka Newfoundland, Canada.

Tunaambiwa vipande hivi viwili kuu omo  na tezi  yaani gubeti na shetri kwa maneno mengine na  hawa watalii sehemu ya mabaki ya sabmarin yalionekana katika omo.

Katika historia tunaambiwa kwamba omo la Titanic lilijikita katika usawawa sakafu ya bahari saa nane na dakika 29 usiku. Lakini shetri inaelezwa ilijikita chini dakika 27 baadaye ikishuka kutoka usawa wa bahari kwa kasi ya maili nne kwa saa.

Vipande hivi viwili vikiwa chini  katika sakafu ya bahari ikiwa ni futi takribani 13,000 vimejitenga kwa futi 2000 vikielekea pande tofauti.

Inaonekana Titan ikiwa na abiria wake watano inaonekana ilikaribia kufika kunakokusudiwa yaani kiasi cha maili 2.4  kwenye sakafu ya Bahari ya Atlantic kabla ya kuzidiwa na kufumuka.

Bahari ya Atlantic ambayio ipo Kaskazini na Kusini mwa Marekani kwa upoande wa Magharibi huku Ulaya na Afrika kwa upande wa mashariki inaungana na bahari ya Arctic kw aupande wa kaskazini na kusini bahari ya Southern. Wanasayansi wanagawa bahari ya Atlantic mara mbili yaani beseni la Kaskazini kama North Atlantic na beseni la kusini kama South Atlantic.

Watalii hawa sio tu walikuwa wanakumbana na hali isiyo kawaida kwa bahari kuu hii ya pili kwa ukubwa duniani ambhayo hutengeneza mustakabali wa hali za hewa tofauti na upigaji wa vimbunga visivyokuwa vya kawaida eneo hilo lenye pia pomboo na kasa wa baharini.

Bahari hii yenye zaidi ya maili za mraba milioni 41 ndio nyumbani kwa mabaki ya meli kubwa duniani nyakati hizo ya Titanic baada ya kusakwa kwa miaka kadhaa Septemb 1, 1985 ikiwa imejitukliza katika futi 13,000 umbali wa mali za baharini 400  sawa na kilometa 740  kutoka Newfoundland, Canada. Mbaaki haya ambayo omo  ipo kwingine na shetri kwingine ipo katika eneo la 41°43′57′′ kaskazini na 49°56′49′′ magharibi.

Kiukweli baada ya kubainikwa Titanic imekaa eneo gani, watu walianza kuwania kiutalii na pia kuitumia na mwaka 1997 James Cameron alitengeneza filamu ya  Titanic.

Kampuni ya OceanGate Inc.  inayomilikuwa na wamarekani mmoja ikiwa katika eneo la Everett, Washington, ndilo limetengeneza nyambizi zinazotumika katika sekta ya utalii, viwanda, utafiti na uvumbuzi. Kampuni hii ilianzishwa na watu wawili Stockton Rush na Guillermo Söhnlein mwaka 2009

Walipoanza walinunua nyambizi mbili na baadaye kuunda za kwao Cyclops 1  na 2 ambayo waliibatiza Titan.  Mwaka 2021, OceanGate walianza kufanya biashara ya utalii kuwapeleka watu kwenye mabaki ya Titanic kwa lengo la utalii. Mwaka jana, 2022, bei ya mtalii mmoja katika safari ya OceanGate kuelekea mabaki ya Titanic ilikuwa ni dola za Marekani 250,000 sawa na  Sh 601,000,000 kwa mtu mmoja.

Juni 18, 2023 Titan iliua  watu watano waliokuwa wakielekea ikwenye mabaki ya Titanic akiwemo mmoja wa wamiliki Rush. Timu ya waokoaji ya kimataifa ilibaini mabaki Juni 22, 2023 karibu kabisa na  omo la Titanic.

Nani ni Stockton Rush

Stockton Rush anasema katika maihsa yake alipenda sana kukabili changamoto za anga za juu na akiwa bado kijana miaka 18 alishakuwa na leseni ya urubani.

Akiwa mkubwa alihamisha hamu zake hizo ikiwamo kuwa mtu wa kwanza kwenda Mars na kujikita katika utafiti wa bahari. Rush alitengeneza utajii mkubwa baada ya kuwekeza urithi wake katika kampuni za teknolojia ya kihandisi na kuamua kunua sabmarini.

Katika hekaheka hizo alibaini kwamba kusonga mbele kwa kuwa kulikuwa nasabmarini 100 tu zinaozmilikuwa na watu binafsi. Aliamua kutengeneza  ya kwake wenyewe. Mwaka 2006 alitengeneza Kittredge K-350 ambayo aliibatiza Suds.

Uzoefu wa Rush na utafiti aliokuwa anaufanya alibaini kwamba kuna biashara kubwa ambayo jamii bado kuishughulikia nayo utalii wa baharini kwa kutumia nyambizi.

Akajikita katika kuangalia sheria na taratibu kisha tamaa ya kutalii kwenye sakafu ya bahari, akabini akianzisha biashara hiyo hatakuwa na shaka , inalipa.

Kwa kutumia vyombo vyake mwaka 1986 alianzisha utalii wa sakafu ya bahari kwa kutumia sabmarini kupitia kampuni yake ya Atlantis Adventures ambapo watalii walipelekwa katika kisiwa cha Grand Cayman . Mwaka 2003, zaidi ya watu milioni 2  walifanya utalii huo wa chini ya bahari lakini eneo salama ambapo alijipatia dola za Marekani milioni 150  sawa na Sh 360,600,000,000.

Mwaka 2009-2013 Stockton Rush alifanya maendeleo makubwa katika biashara hizo ikiwamo ya kuanzisha OceanGate akiwa na Guillermo Söhnlein huko Seattle mwaka 2009.

Kwa mujibu wa Söhnlein,kampuni hiyo ilianzihwa kwa lengo la kuanzisha nyambizi zinazoweza kubeba watu watano za kutosha ili kukodisha kwa watu na kampuni binafsi.

Mwaka  2023 aliiambia Sky News kwamba  wanatengeneza nyambizi kwa ajili ya kufungua mipaka ya utalii katika sakafu ya bahari kwa binadamu wote.

Kampuni hiyo nyambizi yake ya kwanza ilikuwa Antipodes, iliyokuwa imetumika na ilikuwa na uwezo wa abiria watano .

Kati ya mwaka 2010 na 2013 kampuni hiyo iliwezesha upigaji mbizi 130 wakitumia Antipodes.

Kampuni hiyo iliendesha shughuli hizo kwa kusafirisha watafiti, kukodisha na kusafirisha watalii waliowaita wanasayansi wakazi.

Söhnlein alikadiria kwamba mwaka 2012  abiria wato walilipa kati ya Dola za Marekani 7,500 na dola 40,000  kwa kila mwanasayansi huyo ikitegemewa aina ya safari.

OceanGate ilitengeneza nyambizi yake Cyclops, ambayo waliita Cyclops 1 na kati ya mwaka 2016-2023 walifanya maendeleo makubwa japo mmoja wa waanzilishi alijitoa na kubakiza hisa chache.

Mwaka  2019 OceanGate ilianza kujipanga kutengeneza Cyclops 3 na Cyclops 4 lengo likiwa ni kuweza kufika  mita 6,000  ( sawa na futi 20,000) na mwaka 2021 OceanGate ilifanya jaribio lake la kwanza la kuelekea katika mabaki ya meli ya Titanic ndani ya Titan.

Kifo cha  Rush huenda kikabadili mwelekeo wa kampuni lakini tayari kuna shaka na jambo lenyewe.

Kuna sababu ya mgandamizo

Titan  unaweza kusema pasi shaka ilifumuliwa na mgandamizo wa maji ambapo kwa kiingereza unaitwa "catastrophic implosion"

na kumuua Stockton Rush III ambaye kimsingi ni mwanaanga wa anga za juu na rubani  akiwa amefanyakazi na Shirika la Utafiti wa Anga za juu (NASA).

 Rush akiwa na mfanyakazi mwingine mwaka 2021 wakati wa majira ya kiangazi walifika katika mabaki ya Titanic.

James Cameron  amemshutumu mwanzilishi wa chombo hicho kwa kuangalia zaidikibinafsi na kutioweka mmbele usalama.

David Pogue, mwandishi wa CBS a,baye alikwenda katika safari ya 2021 na Rush anasema  Titan haikuwa imetengenezwa na chuma cha kawaida bali na malighafi ambazo hazijajaribiwa kuhimili mgandamizo wa maji.

Rob McCallum,m,vumbizi ambaye pia alikuwa mshauri OceanGate, aliwahi kumweleza Rush aachane na kubadilisha msingi wa kawaida wa uumbaji wa nyambizi na kuwa na urahisi inapogusa  kwenye kina cha Titanic.

Katika email kwa Rush, Machi 2018, McCallum alisema: "Unataka kutumia teknolojia isiyo ya kiwango katika sehemu yenye changamoto sana ya mgandamizo. Kadiri ninavyothamini  suala la ujasiriamali na uvumbuzi, kitendo chako kinaweza kuweka tasnia nzima matatani.

"Kupeleka chombo  chini katika kina cha mita 4,000 katikati ya Atlantiki sio mchezo hapo si mahali unapoweza kukata kona."

 Rush, hakujibu vyema alisema kwamba amechoshwa nna watu wanaozuia uvumbuzi kwa hoja ya kuangalia usalama kwanza.

Usalama ulikuwa "kuhusu utamaduni, sio makaratasi", alisema. Alizungumza juu ya kuhitaji "muundo wa busara, majaribio ya kina, na idhini ya washiriki", lakini akasema kipande cha karatasi hakikuhakikishia usalama wa sehemu ndogo.

Miezi kadhaa iliyopita mmoja wa wafanyakazi wa zamani wa OceanGate ,David Lochridge alisema kwamba kuna vitu vibngi ambavyo vilionekana kuwa tishio kwa usalama wa nyambizi hiyo.

Mwaka 2018, Jamii ya Marine Technology Society  aliiandikia OceanGate ikituhumu madai yasiyokuwa na ukweli ya usalama wa nyambizi hiyo.

Mgandamizi mkubwa unaamini kwamba ulisababisha chombo hicho kuvunjika vipande vipande na kusababisha maafa kwa Ofisa Mtendaji Mkuu wa OceanGate CEO Stockton Rush, 61;veterani wa Kikosi cha maji cha Ufaransa Paul-Henri (PH) Nargeolet, 77; bilionea kwa Kiingereza Hamish Harding, 58; Mfanyabiashara wa Pakistan Shahzada Dawood, 41;  na mtoto wake mwenye umri wa miaka 19 Suleman.

Kufumuka kwa sabmarini hiyo kumeelezwa kuwa kumetokana napresha ya ndani kuwa ndogo zaidi kuliko mgandamizo wa nje

Wakati chombo aina ya nyambizi kinaingia chini baharini kinachofanyia ni kuwa presha ya ndani ni kubwa zaidi kuliko mazingira, au maji yaliyopo nje ya chombo.

Inaaminika kwambaTitan ilizidiwa na kiasi cha mgandamizi unaofikia pauni 5,500 na 6,000 kwa inchi moja ya mraba. Huu ni mgandamizi mkubwa kwani ukilinganisha na shinikizo la angahewa kwenye usawa wa bahari la pauni 14.7 kwa kila inchi ya mraba.

Ingawa bado haijafahamika ni nini  hasa kilitokea na kusababisha Titan kuharibika, kuna uwezekano kuwa kuna kitu kilisababisha kuvuja kwa mgandamizo wa ndani na hivyo kutoa nguvu kubwa kwa mgandamizo wa ndani.

Roderick Smith, profesa wa uhandisi katika Chuo cha Imperial London, anasema kwamba uwezekano huo ulitokana na "kushindwa kwa shinikizo la ndani eneo la omo " lakini hii haitajulikna  mpaka mabaki yote yawe yamekusanywa na kuangaliwa sababu.

Hata hivyo Smith anasema kwamba jinsi mfumo huo ulivyokuwa kutakuwa na shida kubwa kuweza kumaizi sababu.

 Kiukweli anasema Smith ili chombo kiweze kuwa salama katika kina kirefu kinahitaji kuwa na  umbo ambalo huruhusu kustahimili shinikizo sawa kwa pande zote.

Aileen Maria Marty, mwanamaji wa jeshi la Marekani mstaafu anasema kwamba mgandamizo hufumua chombo katika sekunde nchache sana.

"Jambo lote hutukia hata kabla ya watu walio ndani hata kugundua kuwa kuna shida."

 Dk Dale Molé anaamini kwamba tukio lillitokea haraka kiasi ya kwamba hata abiria wenyewe hawakujua nini kimewapiga.

mwisho

Makala haya yaliytolewa kwa mara ya kwanza na HABARILEO

 

COMMENTS

Name

Anga,11,Arusha,27,Burudani,302,burundani,1,come rain,1,come sun,1,Crazy in Love kama wimbo kama wao wenyewe,1,dahh sijui kweli mbona shida,1,Dar utakuja je tumejiandaa,1,daraja sahau nini,1,demokrasia ya upanga,1,Dodoma,77,Dole tupu vijana wa zamani,1,Duhh bibie endeleza libeneke,1,Duhh kaisikie Walibana,1,duhh kwa mbagala mama lazima awe supa,1,Fedha za maiti haziliwi bure,1,Fedha za watu kwa maendeleo ya watu,1,Fikira,14,filamu,238,Filamu ndio kielelezo cha ukuzi wa taifa,1,flamu,7,Gandamiza Kibara baba ake,1,Habari,4816,habari. dodoma,24,hadithi,19,hakika tumeweka historia,1,hakuna noma jongwe,1,hapa kwetu inakuwaje vile,1,hasira hasara,1,hata maji,1,hataki masikhara na maisha yake,1,hatubonyezi kizenji,1,haya ndiyo mambo ya Ulaya,1,haya si yangu ni ya mdau mwenye hasira,1,haya wabongo na mambo kutoka nje,1,He he he wananikumbusha upishi wa shaba,1,Headline,1,Hii hurejesha uhai,1,Hii iko sawa kweli?,1,Hii imekaa vizuri,1,Hii inakaaje vile,1,Hii kweli noma,1,Hii maana yake Moro kuna uhaba wa chakula,1,Hii mexico,1,Hii mihasira mingine bwana,1,Hii ndio moro sio mpaka dar,1,hii ni hatari,1,Hii ni kiboko anayetaka kubisha ajibishie tu,1,Hii ni moja ya staili za kunyoa nywele,1,Hii si lukwangule,1,hii staili mpya,1,hili ni jengo pacha la malaysia ghorofa 88,1,Hivi ni ngoma tu,1,hivi nini siri za serikali,1,hivi sisi tunajua kama kuna vitu vya aina hii,1,hivi vitu bwana,1,Hiyo ndiyo gharama ya demokrasia,1,Hizi imani nyingine ni hatari,1,Hizi takwimu hizi mhh,1,Hongera bibie,1,Hongera dada etu kwa kutuletea kaka etu (shemeji) kwani mwenye dada hakosi shemeji,1,Hongera sana,1,huhitaji mifedha kuwa msafi,1,Huko Ulaya,1,Huu ndio ustaarabu,1,huu ujiko utakuwa mkubwa,1,imetosha,1,Inahitaji nidhamu fulani,1,inakuuma au...,1,Inakuwaje kama filamu yenyewe itahitaji busu la nguvu,1,Inaonekana watanzania hatukuwepo,1,Ipo kazi Maximo,1,Iringa,22,Isiwe mijineno tu manake mihela hubadili watu kweli,1,Itakuwa laki moja ya halali,1,jamani huu kama si ushamba kumbe nini,1,Jamani mbona Mungu anatupigania,1,Jamani watoto wanatakiwa kupendwa,1,jamani.. jamani ukiikosa Diamond usijutie,1,Je nyumbani hakuna vitu vya aina hii?Tuambie,1,je walikuwepo watu wa huduma ya kwanza,1,Je watanzania wanalipa kodi,1,jela kwa raha,1,Jolie,1,juhudi za lazima kuinua filamu,1,kama si kiwanda cha chumvi nani atawajua hawa,1,Kama kweli ndio kweli basi kila heri,1,Kama Mkristo naamini hilo hiyo si sahihi,1,kama unajua kuyarudi nenda Malta,1,kama wao wanaweza sisi je,1,Kamua baba waache wakanyagane,1,karibu nyumbani dada yote maisha tu,1,karibu Tatiii,1,KARIBUNI,1,Katavi,5,kaza buti hakuna kukata tamaa inalipa,1,kazi kwako mheshimiwa waziri wa madini,1,kazi na burudani,1,keep it up bloggers,1,kero ya usafiri sasa kwisha,1,Kila chenye roho na mwili kitaonja umauti,1,kila kitu kina vitu,1,Kila la Heri jamila,1,kila la heri kwani ni changamoto,1,Kipya,51,Kiuno bila mfupa,1,Kolelo mzimu ambao bado hai,1,KUBWA,1,Kudumisha urafiki wa dunia,1,Kuna dalili za wasomi kukubali Uafrika,1,kuna makala humu humu ndani ya blogu sijui mnasemaje,1,Kuu,113,kwa mara nyingine tena Tigo imewezesha,1,Kwa mchanganyiko huu muungano lazima udumu,1,Kwa mihasira hajambo,1,kweli,1,Kweli ina mkono mrefu tuone,1,Kweli duniani tunatofautiana,1,la maana ni kuwa na jiko au vipi,1,labda halitabadilika tena,1,lakini mwafaka lazima,1,lengo ni kutafakari,1,leteni vitu tuvione,1,lets us,1,Lucy wanakuelewa hawa...,1,Lukwangule nyumbani kwetu,2,M ungu bariki mikono ya madaktari wafanikiwe,1,MAARUFU,1,maendeleo ya soka siku zote yanahitaji fedha ili yapatikane,1,maisha ni vyema kuyaangalia,1,MAJIBU,1,makala,51,mama ni mama tu anapendeza,1,mambo mengine we angalia tu,1,mambo msimamo,1,mambo sasa mchanganyiko,1,Mara nyingine huona tunakotoka kwa kuona wenzetu,1,Mashabiki wa rhumba mpooooooooo,1,Masitaa,12,Maskani,1,MASOKO,3,Masupa staa mnaoinukia mpoo,1,Matamasha,6,mavazi ya kuogelea yanaposhindaniwa,1,Mbeya,11,Mchakamchaka anti Asmah,1,Mchanganyiko,81,MCHANYATO,1,mchezo,5,mengi wanayoyaita siri ni public information,1,mfumuko wa bei mpaka noma,1,Mhh sijui watu wa Sua ambao wako huko wanasemaje,1,Mhh ugua pole dada watu wanataka burudani,1,Michezo,501,Michezo maalum inatakiwa kupigiwa debe,1,miguu,1,miguu babu,1,Mikataba mingine ama hakika tuiangalie hata wakopeshaji nao wanatugeuza sakala,1,MIMI NI KISURA NAJITAMBUA,1,Mimi sijajua hasa kumetokea nini kwani ninavyojua hawa huwa na ungalizi wa hali ya juu,1,Mimi simo,1,mimi sisemi,1,mkiwa chumvi basi mkoze,1,Mkiwa taa mulikeni,1,Mnaonaje je hii imekaa vyema,1,Mnaweza wakwetu hapa,1,Morogoro,51,mrithi wa mwanadada Whitney Houston,1,Mtwara,4,Mungu aiweke mahali pema roho yake,4,Mungu amrehemu,1,Mungu amweke pema peponi,1,Mungu awabariki sana,1,Mungu awe nao,1,Mungu ibariki Tanzania,1,Mungu tuepushe na imani hizi za kishirikina,1,mungu tufanye tuwe na upendo,1,Mungu twaomba utuhurumie,1,Muziki,350,muziki na fasheni,5,Mwanahabari,33,Mwanza,6,Mwendo mdundo dada,1,Mwenge huo utakimbizwa duniani kwa siku 130,1,Mwenge wa olimpiki ni ishara ya urafiki,1,Mzee wa Farasi nakupa saluti,1,Mzimbabwe huyu kutoka kwa mama mkali,1,N i dar mpaka Moro au bao tatu bila,1,Na sisi je,1,Naam kama haiwezekani hapa,1,Nairobi waanzisha tena utalii,1,namna bora ya kusaidia jamii,1,nani abebe hukumu na lawama,1,nani asiyejua utamu wa pipi,1,Nani kama baba,1,naona inafaa kuchangia mimi sitoi hoja,1,ndoa za mastaa huwa na mgogoro,1,nenda mwaya nenda,1,New Zanzibar Modern Taarab na wapenzi big up,1,news,5,Ni bikini kwa kwenda mbele,1,Ni Dar mpaka Moro au.. tatu bila,1,ni furaha za muungano,1,Ni kazi ngumu yenye kuhifadhi utamaduni,1,Ni kuchakarika kuonyesha urafiki na biashara pia,1,ni mfumuko wa bei au mfumuko wa nchi,1,Ni muhimu kutazama afya yako,1,ni muziki kwa kwenda mbele,1,Ni muziki mpaka China,1,Ni raha tupu,1,Ni Serengeti Premium Lager,1,Ni Tigo na mawasiliano ya kisasa,1,Ni wakati wa kuujadili utamaduni,1,Ni zaidi ya jazz,1,Nitasubiri and welcome home,1,nje je?,1,NUKUU YA LEO,1,nyie mnasemaje kuhusu hili,1,Ona Kolelo na sindikizwa na Wazee wa Gwasuma,1,ona vya dunia,1,One step ahead,1,patna mwingine mjamzito,1,Pengine anamuogopa Jada Pinkett manake kwa wivu..,1,picha,494,Pole Jamila hayo ndiyo mashindano,1,poleni sana,1,poleni sana wanyalukolo,1,Powa sana,1,Profesa jamaa wanakumaindi,1,Roho za marehemu zipate pumziko la milele,1,Ruvuma,9,sakata dansi mpaka kwenye kilele cha dunia,1,sasa kumebakia ugonjwa mmoja polisi kuendesha mashtaka,1,sasa mifedha kila mahali hongereni,1,Sasa ni mavuno,1,Sasa ni wakati wa kutafuta upenyo ndani ya IDOLS,1,SAYANSI,1,SAYANSI ANGA,1,See Uluguru Montains,1,serikali inataka kujihami kwanini,1,Show of support Big Up Madame,1,Si kitu kidogo hata kidogo,1,si unajua tena namie naimwaga hivyo hivyo,1,Siasa,346,siasa habari,2,Sijui kama City wanajua Mbagala noma,1,Sijui tunaishi karne gani yailahi,1,Sinema,9,sio advencha....kaaa ...niko kibaruani,1,Sisi ndio tunaanza vitongoji,1,Sisi yetu macho na masikio,1,Slow slow jamani,1,sto,1,tabasamu kali la mwenge wa olimpiki,1,Tabora,1,Tazama Waziri Mkuu Pinda wasije wakapindisha maamuzi yako,1,TEKNOLOJIA,1,Thats big man game,1,This is crazy Africa,1,This is Mgeta,1,Tibet wamegeuza Olimpiki jukwaa la siasa,1,Titbits collection,1,Tubadili tamaduni,1,Tuchangie mambo yaive,1,tuendeleze sanaa,1,tuienzi na sisi mbona wizara haituambii,1,Tuipeleke kaskazini,1,Tuisaidie serikali shida ya Mererani,1,tujue namna ya kupumzika,1,Tulienda kustarehe au kufanya fujo,1,Tumsaidie mtototo huyu kurejea katika hali ya kawaida,1,tunahitaji haya,1,Tunajifunza kweli kutoka kwao,1,Tunapandisha chati tu,1,Tunasubiri,1,tunazidi kuhesabu siku,1,TUNAZISUBIRI ZA VINARA ADAR,1,Tuombe nafuu kwa wagonjwa,1,Tuombe rehema kwa mungu,1,Tuone yatufae,1,Tusingoje wengine watusemee,1,tutampa tafu kubwa Prof,1,tuuenzi utamaduni au vipi,1,Tuukuze na kuulinda,1,tuvipende,1,tuwalinde maalbino,1,Tuwe kweli wakweli,1,ubunifu siku zote hulipa,1,uchumi huzunguka kwa kuwawezesha wasukaji,1,udumu muungano,1,Ugonjwa huu wa sasa ni kitendawili,1,Ukiiona kolelo utaipenda,1,Ukirejea salama kila mtu anafurahi,1,Umelenga Mkuchika utamaduni unakufa,1,unaposaka uwakilishi wa dunia,1,urafiki,1,Usisahau wazee wa Ngwasuma,1,UTAMADUNI,1,Video,2,Vionjo vipya ndani ya Gwasuma,1,Vita dhidi ya ufisadi,1,vitongoji Miss Tanzania navyo vimeanza,1,Vitu vikali vyazidi kuingia Dar,1,Vituko,77,Vituo vya polisi Tanga vyatelekezwa,1,VIVALO,1,Wacha tujifue,2,Wadau ilitolewa kiingereza,1,wakali wa ubunifu,1,wala usibabaike mwakwetu hii noma,1,wanadamu wanapotaka kujua zaidi,1,wanasema mpaka kieleweke,1,Wanataka kujua mali za JK na wengine,1,Wanawake wenye mvuto: Monroe,1,Wapo mabinti wa matawi ya juu,1,watu wanapofanya weli kwenye sanaa,1,waweza kurejea enzi ya Moro jazz na Cuban malimba,1,Wazee tupo kusindikiza,1,waziri,1,welcome dar baby,1,Wenzetu wameona sisi tunangoja nini kuangalia,1,wewe unasemaje,1,wigo mpana wa utamaduni,1,wilaya ya 'Mbagala' mlie tu,1,Yaaani sijui itawezekana,1,Yaani wakati mwingine hata huelewi prioty over priority,1,yeye mbele sisi nyuma,1,Yote maisha dada,1,ZA MOTOMOTO,1,Zanzibar,79,zawadi zinatakiwa ziende shule,1,ZILIZOTIA FORA,1,zitachangia kupunguza makali ya bei za umeme,1,
ltr
item
Lukwangule Entertainment: TITAN: Sabmarini iliyoua mabilionea watano
TITAN: Sabmarini iliyoua mabilionea watano
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEivb1tl483SoqR0kXVDEPWDzd2KTnekTjPmFDHgtZ8olXLEmN29T-QP5UjxZ6783SIQzijtYXGwhD-t7mGxjPeO_7sHsmhc3SwRA1DsXNyikLcZzHIoQ_pdOgpuyv3aSMdbDb2AOFp2mrDYgaZMacGoplJPmXo9zJjN44beobXtAmZu5Fa8t4u95wXrRghx/s320/titan.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEivb1tl483SoqR0kXVDEPWDzd2KTnekTjPmFDHgtZ8olXLEmN29T-QP5UjxZ6783SIQzijtYXGwhD-t7mGxjPeO_7sHsmhc3SwRA1DsXNyikLcZzHIoQ_pdOgpuyv3aSMdbDb2AOFp2mrDYgaZMacGoplJPmXo9zJjN44beobXtAmZu5Fa8t4u95wXrRghx/s72-c/titan.jpg
Lukwangule Entertainment
https://lukwangule.blogspot.com/2023/07/titan-sabmarini-iliyoua-mabilionea.html
https://lukwangule.blogspot.com/
http://lukwangule.blogspot.com/
http://lukwangule.blogspot.com/2023/07/titan-sabmarini-iliyoua-mabilionea.html
true
934549962738256429
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy