FARM 17: Chimbuko la Ukombozi Kusini mwa Afrika

KATIKA Kata ya Kipara mtua, Tarafa ya Naipanga , Wilaya ya Nachingwea kiasi cha kilometa 34 kutoka mji wa Nachingwea uliopo mkoani Lindi un...

KATIKA Kata ya Kipara mtua, Tarafa ya Naipanga , Wilaya ya Nachingwea kiasi cha kilometa 34 kutoka mji wa Nachingwea uliopo mkoani Lindi unakutana na eneo maarufu katika ukombozi wa bara la Afrika, Farm 17. Historia ya Farm 17 inaanzia miaka ya 1947 baada ya Vita Kuu ya Pili ya Dunia, wakati Serikali ya wakoloni wa Uingereza ilipoona inafaa kuwatafutia askari wake eneo la ajira kwa kuwakopesha wapiganaji hao fedha na kuanzisha mashamba ya karanga eneo la Nachingwea kupitia kampuni ya John Molem. Kupitia mpango huo mashamba 18 yalianzishwa yakipewa majina kuanzia Farm one hadi Farm 18. Hata hivyo kutokana na sababu mbalimbali mashamba hayo hayakuendelea na Waingereza hao kuamua kuondoka na kwenda kuishi Afrika ya Kusini. Ni katika eneo hili ambalo hivi sasa kuna shule ya Sekondari iliyoazishwa na wananchi yalikuwa ni makazi ya waliokuwa wapigania uhuru kutoka nchi za Kusini mwa Afrika, zikiwamo Msumbiji, Angola na Afrika ya Kusini ambazo kwa miaka kadhaa zilihenyeshwa na wareno na makaburu waliokuwa wakiendesha siasa za ubaguzi wa rangi, pia Zimbabwe ambayo iikuwa chini ya utawala wa Waingereza na baadae muasi Ian Smith hadi 1980 ilipopata uhuru wake. Hapa ni mahali walipowahi kuishi viongozi wa wapiganaji wa vita vya ukombozi wakiwamo Rais Zimbabwe, Robert Mugabe na viongozi wawili wa Msumbiji ambao wote ni marehemu kwa sasa, Edward Mondlane na mrithi wake, Samora Machel. Kwa maana hiyo, unapozungumzia harakati za uhuru au ukombozi Kusini mwa Afrika ambazo kwa kiasi kikubwa ziliongozwa na Tanzania chini ya Hayati Mwalimu Nyerere, huwezi kukosa kutaja wilaya ya Nachingwea, hususan eneo la Farm 17. Katika eneo hili ndipo kulikozaliwa askari jasiri waliofundwa ambao walipelekwa mastari wa mbele nchini msumbiji, Zimbabwe na Angola kufanya vitu vilivyowalazimisha wakoloni kuketi meza moja kuzungumzia uhuru. Ni rahisi kufika eneo hili ukiwa unatokea Dar es salaam ingawa kutokana na maboresho makubwa katika barabara nyingine zinazokupeleka Nachingwea. Ukitoka dar es salaam unakuwa umekata umbali wa kilometa 614.1 na kwa kutumia basi unaweza kuchukua saa hadi nane. Umaarufu wa eneo hili la Farm 17 umeanzia mbali, ukianzia na mji wenyewe wa Nachingwea ambapo katika miaka ya 1950 ilipitwa na reli inayokwenda katika mashamba ya karanga mojawapo likiwa ni hilo la Farm 17 ambalo lilibadilishwa kuwa ngome ya wapigania uhuru. Kiukweli Nachingwea ina mambo mengi ya kujivunia kwa mujibu wa Mkuu wa wilaya, Mohamed Hassan Moyo lakini kubwa ni kuwa mji wa ukombozi katika kusaidia nchi nyingi kujikomboa na kujipatia uhuru. Akinakiliwa na tovuti ya wilaya hiyo, Mkuu huyo wa wilaya alisema mojawapo ya shughuli ambayo ni nguzo muhimu kwa Wilaya ya Nachingwea hasa katika kuchangia uchumi wa Taifa, wilaya na mtu mmoja mmoja ni utalii na utalii wenye hisia kubwa ni wa shamba hilo ambalo limezalisha wapigania uhuru lakini pia likiwa na historia ya kilimo cha karanga na reli. Mkurugenzi wa Halmashauri ya Nachingwea, Injinia Chionda Alli Mfaume akizungumza kwa njia ya simu anasema kimsingi Mji wa Nachingwea unasikika kutokana na historia yake ya ukombozi. Mji huu ulihifadhi wapigania uhuru wa nchi za Msumbiji, Angola, Namibia, Afrika kusini na Zimbabwe na uliwatoa salama viongozi wa matraifa ya Msumbiji, Zimbabwe na namibia ambao walikuwa wanatumia makao hayo kama ngome yao. "Kuna historia nzuri sana ya watanzania na walimwengu wengine kujifunza. Tumefungua eneo hili kwa utalii wa ndani kwa sababu bado tunaendelea kuzungumza na wadau wengine kuimarisha maeneo haya ya zamani hasa mahandaki" anasema Mfaume. Anasema eneo hilo lenye historia njema ya harakati za kupigania uhuru ni eneo ambalo limejaa historia pevu na linastahili kuhifadhiwa na wilaya ya Nachingwea kwa kutumia vyanzo vyake inafanya kila linalowezekana ili miundombinu yake ikikamilika iwe kivututio si kwa watalii wa ndani pekee bali na jumuiya ya kimataifa inayotaka kujua mahali ambapo wapigania uhuru walisukwa kijeshi na kisiasa kukomboa nchi zao. "Tulifanya tamasha kubwa katika eneo hili la Farm 17 wakati wa Siku ya utalii duniani, lengo letu lilikuwa kuweka wazi eneo hili na pia kuhimiza utalii wa ndani na kuelezea changamoto tunazokumbana nazo katika kuhifadhi eneo hili ili watu wengi zaidi wajitokeze kuona fahari ya uhifadhi" anasema Mfaume. Anasema wamefanya mazungumzo na balozi wa Msumbiji nchini waliotembelea eneo hilo pamoja na balozi wa Zimbambwe nchini Tanzania, Balozi Lt. Gen.(Mstaafu) Anselem Nhamo Sanyatwe mwenye sifa ya pekee kabisa kwamba alishawahi kuishi katika shamba hilo hivyo lipo moyoni mwake. Anasema balozi huyo alitembelea Farm 17 hivi karibuni na kuelezea jinsi anavyolifahamu na kusema Tanzania kupitia rais wa kwanza wa Tanzania Mwalimu Julius Nyerere ilikuwa ni sehemu ya uhuru wao na Tanzania hakika ni nyumbani kwao. Balozi Anselem anasema alikuwa mmoja ya askari 6,000 wa Zimbambwe waliopata mafunzo eneo la kambi ya Farm 17 baada ya kuondoka kwa wapiganaji wa Msumbiji mwaka 1975 .Anasema makundi ya wapiganaji wa Zimbabwe yaliingia Farm 17 mwaka 1976. Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mfaume, balozi alionesha nia ya kushirikiana na halmashauri katika kuhifadhi eneo hilo. Ingawa Wizara ya Michezo,Utamaduni na Sanaa kupitia programu ya urithi wa ukombozi wa nchi za Afrika @urithiwaukombozi imeanza juhudi zao za kukusanya, kuweka kumbukumbu, kuhifadhi na kuendeleza historia ya ukombozi wa Afrika iliyotokana na harakati za kupigania uhuru, wao Nachingwea kwa nafasi waliyonayo wanataka kulitumia eneo hilo kukuza kipato na pia kuhifadhi historia hiyo adhimu. Katika eneo hilo la kumbkumbu ya wapigania uhuru kumeanzishwa shule ya sekondari ya Farm 17 ikiwa na lengo la kuendelea kuhifadhi majengo mbalimbali yaliyokuwa yakitumika kama Ofisi za utawala,Maghala ya chakula,Maghala ya silaha, Jiko na kumbi Nyumba za walinzi na viongozi,Mahandaki na Nyumba ya Samora Machel, rais wa kwanza wa Msumbiji huru aliyekufa katika ajali ya ndege. "Farm 17 ni eneo jema kwa wale ambao wanapenda kujua hasa msingi wa mapambano kusini mwa Afrika namna watu walivyofunza na kujihami. Hapa pana majengo mbalimbali japo mengine mengine yanatumika kwa shule ya sekondari na shule ya msingi, lipo jengo moja ambalo lilijengwa na Rais Samora kama ngome yake wakati wa vita vya Msumbiji.," anasema Mfaume. Anasema kinachofurahisha ni namna jengo hilo la chini kwa chini, lilivyoungwa kama barabara ilitumika kuelekea uwanja wa ndege uliokuwa jirani. "Ukiingia ndani unaona eneo zima,unaona ngome ya kujificha na maadui wakati wa vita na hii ndio ilivyokuwa wakatika wa mapambano kati ya wapigania uhuru na vikosi vya wareno," anasema Mfaume. Kulikuwa na kila sababu ya eneo hili kujengwa kivita na kingome zaidi kwani kilometa 110 kutoka Nachingwea mjini palikuwa na makambi ya wakimbizi wa Msumbiji eneo la Matekwe na haikujulikana kama wote walioingia hapo ni wale wanaoifagilia Frelimo au kuna maajenti wa wareno. Ukitafuta historia ya eneo la Matekwe katika mtandao unakutana na simulizi za mzee Salumu Mohamed Migomba akisema kwamba watu walianza kufika eneo hilo kwa kuletwa na serikali mwanzoni mwa miaka ya 1960. Anasema watu walianza kujenga mji hadi pale miaka ya 1967 alipofika waziri mkuu wa Tanzania wakati huo Mzee Rashid Mfaume Kawawa kuwaomba wananchi kuwapokea wageni kutoka Msumbiji wasiopungua 15,000. Ukifika eneo la Matekwe utakayakuta majengo tofauti ambayo yalitumiwa na wakimbizi, viongozi na majengo ya shughuli za jamii wakati huo ambayo hadi sasa yanaendelea kutumiwa kama ofisi za kijiji, zahanati, kanisa, shule. Baada ya Msumbiji kupata uhuru Juni 25, 1975 mambo mengi ya hapa yalibadilika katika maeneo hayo mawili. Ikumbukwe kwamba Samora alichaguliwa kuwa kiongozi baada ya kuuawa kwa Mondlane kiongozi wa kwanza wa Frelimo kwa bomu lilikuwa katika barua. Mwalimu Longnus Nambole , Mkuu wa kwanza wa sekondari ya Farm 17 anasema kwamba kuna kila sababu ya serikali na wadau wengine kushirikiana kutunza eneo hilo kwani. Pamoja na kuwa na majengo ya kambi za wapigania uhuru, kazi hiyo ilipomalizika awali yaligeuzwa kuwa chuo cha kufundishia wanajeshi. Chuo hiki kilikuwa kinatoa mafunzo kwa maafisa kwa jeshi kutoka nje ya nchi pamoja na mafunzo ya awali kwa askari wanaoanza. Desemba 1992 chuo hicho kilivunjwa na kuhamishiwa Mgulani Dar es salaam. Farm 17 hakika ni kumbukumbu njema na kama eneo hilo litaboreshwa, litazalisha ajira kwa wananchi lingevuta watalii kutoka maeneo mbalimbali Duniani na pia kuchangia pato la taifa. Imeandikwa na: Rahel Pallangyo

COMMENTS

Name

Anga,11,Arusha,27,Burudani,302,burundani,1,come rain,1,come sun,1,Crazy in Love kama wimbo kama wao wenyewe,1,dahh sijui kweli mbona shida,1,Dar utakuja je tumejiandaa,1,daraja sahau nini,1,demokrasia ya upanga,1,Dodoma,77,Dole tupu vijana wa zamani,1,Duhh bibie endeleza libeneke,1,Duhh kaisikie Walibana,1,duhh kwa mbagala mama lazima awe supa,1,Fedha za maiti haziliwi bure,1,Fedha za watu kwa maendeleo ya watu,1,Fikira,14,filamu,238,Filamu ndio kielelezo cha ukuzi wa taifa,1,flamu,7,Gandamiza Kibara baba ake,1,Habari,4816,habari. dodoma,24,hadithi,19,hakika tumeweka historia,1,hakuna noma jongwe,1,hapa kwetu inakuwaje vile,1,hasira hasara,1,hata maji,1,hataki masikhara na maisha yake,1,hatubonyezi kizenji,1,haya ndiyo mambo ya Ulaya,1,haya si yangu ni ya mdau mwenye hasira,1,haya wabongo na mambo kutoka nje,1,He he he wananikumbusha upishi wa shaba,1,Headline,1,Hii hurejesha uhai,1,Hii iko sawa kweli?,1,Hii imekaa vizuri,1,Hii inakaaje vile,1,Hii kweli noma,1,Hii maana yake Moro kuna uhaba wa chakula,1,Hii mexico,1,Hii mihasira mingine bwana,1,Hii ndio moro sio mpaka dar,1,hii ni hatari,1,Hii ni kiboko anayetaka kubisha ajibishie tu,1,Hii ni moja ya staili za kunyoa nywele,1,Hii si lukwangule,1,hii staili mpya,1,hili ni jengo pacha la malaysia ghorofa 88,1,Hivi ni ngoma tu,1,hivi nini siri za serikali,1,hivi sisi tunajua kama kuna vitu vya aina hii,1,hivi vitu bwana,1,Hiyo ndiyo gharama ya demokrasia,1,Hizi imani nyingine ni hatari,1,Hizi takwimu hizi mhh,1,Hongera bibie,1,Hongera dada etu kwa kutuletea kaka etu (shemeji) kwani mwenye dada hakosi shemeji,1,Hongera sana,1,huhitaji mifedha kuwa msafi,1,Huko Ulaya,1,Huu ndio ustaarabu,1,huu ujiko utakuwa mkubwa,1,imetosha,1,Inahitaji nidhamu fulani,1,inakuuma au...,1,Inakuwaje kama filamu yenyewe itahitaji busu la nguvu,1,Inaonekana watanzania hatukuwepo,1,Ipo kazi Maximo,1,Iringa,22,Isiwe mijineno tu manake mihela hubadili watu kweli,1,Itakuwa laki moja ya halali,1,jamani huu kama si ushamba kumbe nini,1,Jamani mbona Mungu anatupigania,1,Jamani watoto wanatakiwa kupendwa,1,jamani.. jamani ukiikosa Diamond usijutie,1,Je nyumbani hakuna vitu vya aina hii?Tuambie,1,je walikuwepo watu wa huduma ya kwanza,1,Je watanzania wanalipa kodi,1,jela kwa raha,1,Jolie,1,juhudi za lazima kuinua filamu,1,kama si kiwanda cha chumvi nani atawajua hawa,1,Kama kweli ndio kweli basi kila heri,1,Kama Mkristo naamini hilo hiyo si sahihi,1,kama unajua kuyarudi nenda Malta,1,kama wao wanaweza sisi je,1,Kamua baba waache wakanyagane,1,karibu nyumbani dada yote maisha tu,1,karibu Tatiii,1,KARIBUNI,1,Katavi,5,kaza buti hakuna kukata tamaa inalipa,1,kazi kwako mheshimiwa waziri wa madini,1,kazi na burudani,1,keep it up bloggers,1,kero ya usafiri sasa kwisha,1,Kila chenye roho na mwili kitaonja umauti,1,kila kitu kina vitu,1,Kila la Heri jamila,1,kila la heri kwani ni changamoto,1,Kipya,51,Kiuno bila mfupa,1,Kolelo mzimu ambao bado hai,1,KUBWA,1,Kudumisha urafiki wa dunia,1,Kuna dalili za wasomi kukubali Uafrika,1,kuna makala humu humu ndani ya blogu sijui mnasemaje,1,Kuu,113,kwa mara nyingine tena Tigo imewezesha,1,Kwa mchanganyiko huu muungano lazima udumu,1,Kwa mihasira hajambo,1,kweli,1,Kweli ina mkono mrefu tuone,1,Kweli duniani tunatofautiana,1,la maana ni kuwa na jiko au vipi,1,labda halitabadilika tena,1,lakini mwafaka lazima,1,lengo ni kutafakari,1,leteni vitu tuvione,1,lets us,1,Lucy wanakuelewa hawa...,1,Lukwangule nyumbani kwetu,2,M ungu bariki mikono ya madaktari wafanikiwe,1,MAARUFU,1,maendeleo ya soka siku zote yanahitaji fedha ili yapatikane,1,maisha ni vyema kuyaangalia,1,MAJIBU,1,makala,51,mama ni mama tu anapendeza,1,mambo mengine we angalia tu,1,mambo msimamo,1,mambo sasa mchanganyiko,1,Mara nyingine huona tunakotoka kwa kuona wenzetu,1,Mashabiki wa rhumba mpooooooooo,1,Masitaa,12,Maskani,1,MASOKO,3,Masupa staa mnaoinukia mpoo,1,Matamasha,6,mavazi ya kuogelea yanaposhindaniwa,1,Mbeya,11,Mchakamchaka anti Asmah,1,Mchanganyiko,81,MCHANYATO,1,mchezo,5,mengi wanayoyaita siri ni public information,1,mfumuko wa bei mpaka noma,1,Mhh sijui watu wa Sua ambao wako huko wanasemaje,1,Mhh ugua pole dada watu wanataka burudani,1,Michezo,501,Michezo maalum inatakiwa kupigiwa debe,1,miguu,1,miguu babu,1,Mikataba mingine ama hakika tuiangalie hata wakopeshaji nao wanatugeuza sakala,1,MIMI NI KISURA NAJITAMBUA,1,Mimi sijajua hasa kumetokea nini kwani ninavyojua hawa huwa na ungalizi wa hali ya juu,1,Mimi simo,1,mimi sisemi,1,mkiwa chumvi basi mkoze,1,Mkiwa taa mulikeni,1,Mnaonaje je hii imekaa vyema,1,Mnaweza wakwetu hapa,1,Morogoro,51,mrithi wa mwanadada Whitney Houston,1,Mtwara,4,Mungu aiweke mahali pema roho yake,4,Mungu amrehemu,1,Mungu amweke pema peponi,1,Mungu awabariki sana,1,Mungu awe nao,1,Mungu ibariki Tanzania,1,Mungu tuepushe na imani hizi za kishirikina,1,mungu tufanye tuwe na upendo,1,Mungu twaomba utuhurumie,1,Muziki,350,muziki na fasheni,5,Mwanahabari,33,Mwanza,6,Mwendo mdundo dada,1,Mwenge huo utakimbizwa duniani kwa siku 130,1,Mwenge wa olimpiki ni ishara ya urafiki,1,Mzee wa Farasi nakupa saluti,1,Mzimbabwe huyu kutoka kwa mama mkali,1,N i dar mpaka Moro au bao tatu bila,1,Na sisi je,1,Naam kama haiwezekani hapa,1,Nairobi waanzisha tena utalii,1,namna bora ya kusaidia jamii,1,nani abebe hukumu na lawama,1,nani asiyejua utamu wa pipi,1,Nani kama baba,1,naona inafaa kuchangia mimi sitoi hoja,1,ndoa za mastaa huwa na mgogoro,1,nenda mwaya nenda,1,New Zanzibar Modern Taarab na wapenzi big up,1,news,5,Ni bikini kwa kwenda mbele,1,Ni Dar mpaka Moro au.. tatu bila,1,ni furaha za muungano,1,Ni kazi ngumu yenye kuhifadhi utamaduni,1,Ni kuchakarika kuonyesha urafiki na biashara pia,1,ni mfumuko wa bei au mfumuko wa nchi,1,Ni muhimu kutazama afya yako,1,ni muziki kwa kwenda mbele,1,Ni muziki mpaka China,1,Ni raha tupu,1,Ni Serengeti Premium Lager,1,Ni Tigo na mawasiliano ya kisasa,1,Ni wakati wa kuujadili utamaduni,1,Ni zaidi ya jazz,1,Nitasubiri and welcome home,1,nje je?,1,NUKUU YA LEO,1,nyie mnasemaje kuhusu hili,1,Ona Kolelo na sindikizwa na Wazee wa Gwasuma,1,ona vya dunia,1,One step ahead,1,patna mwingine mjamzito,1,Pengine anamuogopa Jada Pinkett manake kwa wivu..,1,picha,494,Pole Jamila hayo ndiyo mashindano,1,poleni sana,1,poleni sana wanyalukolo,1,Powa sana,1,Profesa jamaa wanakumaindi,1,Roho za marehemu zipate pumziko la milele,1,Ruvuma,9,sakata dansi mpaka kwenye kilele cha dunia,1,sasa kumebakia ugonjwa mmoja polisi kuendesha mashtaka,1,sasa mifedha kila mahali hongereni,1,Sasa ni mavuno,1,Sasa ni wakati wa kutafuta upenyo ndani ya IDOLS,1,SAYANSI,1,SAYANSI ANGA,1,See Uluguru Montains,1,serikali inataka kujihami kwanini,1,Show of support Big Up Madame,1,Si kitu kidogo hata kidogo,1,si unajua tena namie naimwaga hivyo hivyo,1,Siasa,346,siasa habari,2,Sijui kama City wanajua Mbagala noma,1,Sijui tunaishi karne gani yailahi,1,Sinema,9,sio advencha....kaaa ...niko kibaruani,1,Sisi ndio tunaanza vitongoji,1,Sisi yetu macho na masikio,1,Slow slow jamani,1,sto,1,tabasamu kali la mwenge wa olimpiki,1,Tabora,1,Tazama Waziri Mkuu Pinda wasije wakapindisha maamuzi yako,1,TEKNOLOJIA,1,Thats big man game,1,This is crazy Africa,1,This is Mgeta,1,Tibet wamegeuza Olimpiki jukwaa la siasa,1,Titbits collection,1,Tubadili tamaduni,1,Tuchangie mambo yaive,1,tuendeleze sanaa,1,tuienzi na sisi mbona wizara haituambii,1,Tuipeleke kaskazini,1,Tuisaidie serikali shida ya Mererani,1,tujue namna ya kupumzika,1,Tulienda kustarehe au kufanya fujo,1,Tumsaidie mtototo huyu kurejea katika hali ya kawaida,1,tunahitaji haya,1,Tunajifunza kweli kutoka kwao,1,Tunapandisha chati tu,1,Tunasubiri,1,tunazidi kuhesabu siku,1,TUNAZISUBIRI ZA VINARA ADAR,1,Tuombe nafuu kwa wagonjwa,1,Tuombe rehema kwa mungu,1,Tuone yatufae,1,Tusingoje wengine watusemee,1,tutampa tafu kubwa Prof,1,tuuenzi utamaduni au vipi,1,Tuukuze na kuulinda,1,tuvipende,1,tuwalinde maalbino,1,Tuwe kweli wakweli,1,ubunifu siku zote hulipa,1,uchumi huzunguka kwa kuwawezesha wasukaji,1,udumu muungano,1,Ugonjwa huu wa sasa ni kitendawili,1,Ukiiona kolelo utaipenda,1,Ukirejea salama kila mtu anafurahi,1,Umelenga Mkuchika utamaduni unakufa,1,unaposaka uwakilishi wa dunia,1,urafiki,1,Usisahau wazee wa Ngwasuma,1,UTAMADUNI,1,Video,2,Vionjo vipya ndani ya Gwasuma,1,Vita dhidi ya ufisadi,1,vitongoji Miss Tanzania navyo vimeanza,1,Vitu vikali vyazidi kuingia Dar,1,Vituko,77,Vituo vya polisi Tanga vyatelekezwa,1,VIVALO,1,Wacha tujifue,2,Wadau ilitolewa kiingereza,1,wakali wa ubunifu,1,wala usibabaike mwakwetu hii noma,1,wanadamu wanapotaka kujua zaidi,1,wanasema mpaka kieleweke,1,Wanataka kujua mali za JK na wengine,1,Wanawake wenye mvuto: Monroe,1,Wapo mabinti wa matawi ya juu,1,watu wanapofanya weli kwenye sanaa,1,waweza kurejea enzi ya Moro jazz na Cuban malimba,1,Wazee tupo kusindikiza,1,waziri,1,welcome dar baby,1,Wenzetu wameona sisi tunangoja nini kuangalia,1,wewe unasemaje,1,wigo mpana wa utamaduni,1,wilaya ya 'Mbagala' mlie tu,1,Yaaani sijui itawezekana,1,Yaani wakati mwingine hata huelewi prioty over priority,1,yeye mbele sisi nyuma,1,Yote maisha dada,1,ZA MOTOMOTO,1,Zanzibar,79,zawadi zinatakiwa ziende shule,1,ZILIZOTIA FORA,1,zitachangia kupunguza makali ya bei za umeme,1,
ltr
item
Lukwangule Entertainment: FARM 17: Chimbuko la Ukombozi Kusini mwa Afrika
FARM 17: Chimbuko la Ukombozi Kusini mwa Afrika
Lukwangule Entertainment
https://lukwangule.blogspot.com/2023/10/farm-17-chimbuko-la-ukombozi-kusini-mwa.html
https://lukwangule.blogspot.com/
http://lukwangule.blogspot.com/
http://lukwangule.blogspot.com/2023/10/farm-17-chimbuko-la-ukombozi-kusini-mwa.html
true
934549962738256429
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy