TanTrade ni zaidi ya 'maonesho ya sabasaba'

.Wanasababisha mchakato wa mageuzi katika biashara Na Mwandishi Wetu MAMLAKA ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) ilianzishwa kw...

.Wanasababisha mchakato wa mageuzi katika biashara Na Mwandishi Wetu MAMLAKA ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) ilianzishwa kwa Sheria ya Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania namba 4 ya mwaka 2009 iliyofuta Sheria ya Bodi ya Biashara ya Nje namba 5 ya mwaka 1978 na Sheria ya Bodi ya Biashara ya Ndani namba 15 ya mwaka 1973 ni zaidi ya kufanya maonesho ya kimataifa ya biashara kama watu walivyozoea ya sabasaba. Ikiwa kama mamlaka ina kazi kubwa ya kudhibiti shughuli zinazohusiana na biashara ya ndani na nje ambayo hapo awali ilifanywa na Bodi ya Biashara ya Nje na Bodi ya Biashara ya Ndani. Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade, Latifa Khamis akizungumza na wahariri wa vyombo vya habari nchini hivi karibuni ikiwa ni mwendelezo wa vikao vinavyoratibiwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina vya taasisi za umma na makampuni ambayo serikali yanahisa kujieleza kwa umma anasema kazi kubwa ya mamlaka hiyo ni kutafuta masoko na uwekezaji. Maelezo ya Mkurugenzi Mkuu Latifa ambayo alitoa katika mada yake na kufafanua zaidi katika maswali na majibu yana akisi kitu ambacho watanzania wengi hawakijui kuwa sheria ya kuanzisha TanTrade pamoja na kuwa hatua kubwa katika kuimarisha mchakato wa mageuzi ya biashara nchini Tanzania, kazi yake ni kuendeleza biashara za ndani na nje na kudhibiti maonesho ya biashara ya yanayofanyika Tanzania yakiwemo ya kimataifa. Lengo la msingi kuwapo kwa mamlaka hiyo ni kukabiliana na vikwazo vinavyowakabili wafanyabiashara, wauzaji bidhaa nje na wazalishaji wa bidhaa na huduma kwa nia ya kuongeza utendaji wa sekta ya biashara katika uchumi na hapa kuna kitu kinaitwa branding ambacho kinatengenezewa pamoja mambo mengine mkakati. Ukiangalia maelezo ya Mkurugrenzi Mkuu Latifa kwa ujumla wake moja ya jukumu kubwa na muhimu la Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE) ni kusaidia uwekaji wa mazingira rafiki kwa bidhaa na huduma zinazozalishwa nchini ili kuyafikia masoko ya ndani, kikanda na kimataifa. Lakini pia wana jukumu jingine la kutambua na kushauri mbinu bora za kutatua changamoto zinazokwamisha maendeleo ya biashara katika mnyororo wa thamani na kutoa ushauri na mafunzo kwa Jumuiya ya Wafanyabiashara juu ya namna bora ya kusimamia shughuli za biashara ya ndani na za nje . Pia ina jukumu la kujenga na kukuza utamaduni wa kuuza bidhaa nje kwa wafanyabiashara wadogo, wa kati na wakubwa kwa njia mbalimbali. Ukitazama majukumu hayo unatambua kwamba shughuli ya Tantrade ambayo pia kwa miaka mitano wamefanikiwa kuratibu matukio mbalimbali ikiwemo programu za utafiti, makongamano na misafara ya kibiashara, maonesho na mikutano ya kuunganisha wazalishaji na wanunuzi ambayo yameongeza makusanyo katika mfuko wa Hazina kwa asilimia 20.15 kwa kipindi cha miaka mitano, ni kusukuma na kuhakikisha uendelevu wa biashara ya Tanzania katika soko la dunia. Akizungumzia ufanisi unaowezesha na wao kusonga mbele Latifa anasema:“Katika kipindi cha miaka mitano TanTrade ilipanga kukusanya jumla ya shilingi 52,562,298,340 na imefanikiwa kukusanya shilingi 40,004,650,548 sawa na asilimia 76. "Ni kutoka vyanzo mbalimbali ikiwa ni pamoja na ruzuku kutoka Serikali Kuu kwa ajili ya mishahara na miradi ya maendeleo na vyanzo vya mapato ya ndani ikiwemo ada inayotozwa kwenye uratibu na usimamizi wa maonesho, upangaji wakati usio wa maonesho pamoja na ushiriki na viingilio vya Maonesho ya DITF.” Anasema kuwa, maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya Sabasaba ambayo yamekuwa yakifanyika kila mwaka yamezidi kuongeza thamani yake kwa kipindi cha miaka mitano kutokana namna yanavyofanya kuwaweka karibu wafanyabiashara wa ndani na nje katika hali ya kutafuta masoko ya uhakika ya bidhaa. Mkurugenzi huyo anasema,kampuni za ndani na nje, washiriki, idadi ya nchi zilizoshiriki maonesho hayo, watembelea maonesho pamoja na ajira zilizozalishwa vimeongezeka na hivyo yamezidi kuongeza wigo wa biashara za ndani na nje ya nchi. Kwa kuzingatia uanzishwaji wake mamlaka hii kwa kutumia wataalamu wake wa ndani wamefanya mambo makubwa ya kuweka thamani katika mnyororo wa bidhaa ambazo Tanzania ina fursa nazo sana nchi za nje baada ya kufanya utafiti na kuridhika na mwenendo wake. “TanTrade imekamilisha maombi ya ufadhili ya kuendeleza rajamu (branding) ya Taifa ya Viungo (Tanzania Spice Label) kwa kushirikiana na Kituo cha Biashara cha Kimataifa (ITC) pamoja na wadau wa sekta ya viungo. "Hadi Agosti, 2023 TanTrade imekamilisha rajamu ya iliki, tangawizi, mdalasini, pilipili manga na karafuu vilevile, mamlaka inaendelea na taratibu za kukamilisha rajamu za bidhaa nyingine ikiwemo asali, korosho, kahawa na chai pamoja na mafunzo kwa wafanyabiashara 6,979 kupitia programu 26 ili kuimarisha uwezo wa kujiendesha kiushindani.” anasema Latifa akidhihirisha kwamba Mamlaka anayoongoza ni zaidi ya kuonekana ikiratibu maonesho ya Sabasaba katika viwanja vya Mwalimu Nyerere, Barabaa ya Kilwa. Latifa anasema, mamlaka hiyo imeendelea kusaka masoko nje ya nchi ya bidhaa mbalimbali zinazolishwa nchini ikiwemo mazao ya biashara na madini ili kuongeza wigo wa uzalishwaji na kuongeza thamani ya mnyororo kwa wazalishaji. Kutokana na mazingira yake chini ya usimamizi madhuubuti wa Latifa,TanTrade imefanya uchambuzi wa takwimu katika mfumo wa ITC kutambua bidhaa zinazohitajika kwenye masoko mbalimbali duniani.Nchi ambazo zinaonekana kuhitaji bidhaa za kilimo na madini kutoka Tanzania ni pamoja na India, Umoja wa Falme za Kiarabu, Uswisi, Vietnam, China, Pakistani, Japani, Marekani, Oman, Qatar, Kuwait na Saudi Arabia. Watanzania wa kawaida kwa sasa wanapaswa kutambua kwamba Mamlaka hii ipo kwa ajili ya kuendeleza masoko ya bidhaa zao iwe kwa wajasirimali wadogo, wakati na wakubwa kinachostahili ni kupenya katika soko na kuwa na ushirikiano ili kuwa na soko endelevu la bidhaa ambazo zinafanikiwa kuuzwa nje. Latifa anasema kwamba Tantrade wanajukumu kubwa la kukuza na kuendeleza biashara ya ndani na nje ya nchi ili kukuza uchumi wa Tanzania kuupaisha na kuifanya kuwa endelevukwa kuhakikisha Tanzania inakuwa kitovu cha bidhaa mbalimbali zinazotokana na mnyororo wa kilimo, ufugaji, madini na viungo. "Sisi hatutangazi fursa kama haina vigezo, mara nyingi fursa tunazozitangaza sisi zina vigezo tofauti na matangazo ya taasisi nyingine mtaona wengine wanatangaza fursa ya soko la nazi tu kamaliza, lakini TanTrade inakuwa na maelezo ya kitaalamu." "Na kama halina maelezo ya kitaalamu hatuwezi kutangaza mpaka tumefanya hivyo kujiridhisha kabisa kikamilifu. Kwa kuzingatia kanuni zake za undeshaji ni dhahiri kuwa TanTrade inaihitaji ushirikiano ili kuweza kusaidia kukuza sekta ya biashara, lengo likiwa ni kuifanya sekta ya biashara na uwekezaji iwe na tija . haya yanafanyika huku bidhaa za Tanzania nje ya nchi badi zikikabiliwa na changamoto ndogo ndogo hasa kutokuwa na uendelevu wa oda kwani wengi wengi wakuipeleka mara mbili, tatu anakimbia. "Shida mtu hana uwezo ni peke yake anakuwa mchoyo, badala ashirikishe na wengine hawezi lazima tushirikiane kuimarisha biashara kupitia taaluma yenu. "Mbali na hilo, biashara yetu huko nje imekabiliwa na utapeli, kuna baadhi ya watu wanapeleka bidhaa zinakuwa hazina ubora sana mfano zina mawe. "Lakini, kama mamlaka tumekuwa tunakaa nao lengo letu ni ku-protect image ya nchi yetu iwe nzuri ili bidhaa zetu ziweze kuuzika na kuthaminika. Tantrade ikiwa kwa mwaka wa fedha 2023/2024 imejipanga kufanya mambo mbalimbali ikiwemo; kuendelea kuratibu shughuli za utafutaji masoko na ukuzaji biashara ili kuunganisha wazalishaji, kuendelea na taratibu za uanzishwaji wa Dawati la Waambata wa Kibiashara kwenye Ubalozi mbalimbali wa kimkakati wa Tanzania nje ya nchi,sambamba na kuendeleza ushirikiano na Ubalozi nje ya Nchi katika kutangaza fursa za masoko ya bidhaa na mazao yanayozalishwa nchini, kuratibu ushiriki wa Tanzania kwenye Maonesho ya Expo 2025 Osaka, Japani inadhirisha kwa wananchia kwamba yenyewe ipo kikazi zaidi na si kuratibu tu maonesho ya sabasaba. "Tuna vipaumbele kuhusu Japan kila wizara, kila sekta inaandaa kipaimbele chake, tuna kamati ambayo ni kubwa zaidi, kwani dunia yote itakuwa pamoja katika kijiji kimoja. "Sisi katika kuji-expose lazima tuwe na mikakati ambayo mpaka sasa tumeiandaa kila wizara itatupa kipaumbele chake, muonekano wa banda la Tanzania utaonekana kwa vipaumbele na mwelekeo wa nchi. "Anayeingia anaona nini tunakwenda Japan wenzetu wemeendelea sana, tutakuwa na bidhaa za kipaumbele, sekta miradi na project au innovation (ubunifu)." Katika mkutano huo na waandishi wa habari pia latifa alizungumzia wanavyofuatilia mikataba ya kibiashara iliyofungwa na nchi hii. "Kuna mikataba ya biashara ambayo tumeifunga kupitia matukio mbalimbali, hivyo TanTrade inaendelea kufuatilia mikataba ya makubaliano ya kibiashara ambayo imesainiwa katika matukio mbalimbali. "Ambapo jumla ya mikataba 46 yenye thamani ya shilingi trilioni 17.53 ikiwemo mikubwa ya bandari imesainiwa. "Baada ya bandari, kuna miradi mingine mkubwa itakuja. Sisi ndio kazi yetu kutafuta masoko na uwekezaji. Katika mazingira ya sasa lazima tufanye PPP (Ushirikiano wa Sekta Binafsi na Umma) kwani ni muhimu sana." mwisho

COMMENTS

Name

Anga,11,Arusha,27,Burudani,302,burundani,1,come rain,1,come sun,1,Crazy in Love kama wimbo kama wao wenyewe,1,dahh sijui kweli mbona shida,1,Dar utakuja je tumejiandaa,1,daraja sahau nini,1,demokrasia ya upanga,1,Dodoma,77,Dole tupu vijana wa zamani,1,Duhh bibie endeleza libeneke,1,Duhh kaisikie Walibana,1,duhh kwa mbagala mama lazima awe supa,1,Fedha za maiti haziliwi bure,1,Fedha za watu kwa maendeleo ya watu,1,Fikira,14,filamu,238,Filamu ndio kielelezo cha ukuzi wa taifa,1,flamu,7,Gandamiza Kibara baba ake,1,Habari,4816,habari. dodoma,24,hadithi,19,hakika tumeweka historia,1,hakuna noma jongwe,1,hapa kwetu inakuwaje vile,1,hasira hasara,1,hata maji,1,hataki masikhara na maisha yake,1,hatubonyezi kizenji,1,haya ndiyo mambo ya Ulaya,1,haya si yangu ni ya mdau mwenye hasira,1,haya wabongo na mambo kutoka nje,1,He he he wananikumbusha upishi wa shaba,1,Headline,1,Hii hurejesha uhai,1,Hii iko sawa kweli?,1,Hii imekaa vizuri,1,Hii inakaaje vile,1,Hii kweli noma,1,Hii maana yake Moro kuna uhaba wa chakula,1,Hii mexico,1,Hii mihasira mingine bwana,1,Hii ndio moro sio mpaka dar,1,hii ni hatari,1,Hii ni kiboko anayetaka kubisha ajibishie tu,1,Hii ni moja ya staili za kunyoa nywele,1,Hii si lukwangule,1,hii staili mpya,1,hili ni jengo pacha la malaysia ghorofa 88,1,Hivi ni ngoma tu,1,hivi nini siri za serikali,1,hivi sisi tunajua kama kuna vitu vya aina hii,1,hivi vitu bwana,1,Hiyo ndiyo gharama ya demokrasia,1,Hizi imani nyingine ni hatari,1,Hizi takwimu hizi mhh,1,Hongera bibie,1,Hongera dada etu kwa kutuletea kaka etu (shemeji) kwani mwenye dada hakosi shemeji,1,Hongera sana,1,huhitaji mifedha kuwa msafi,1,Huko Ulaya,1,Huu ndio ustaarabu,1,huu ujiko utakuwa mkubwa,1,imetosha,1,Inahitaji nidhamu fulani,1,inakuuma au...,1,Inakuwaje kama filamu yenyewe itahitaji busu la nguvu,1,Inaonekana watanzania hatukuwepo,1,Ipo kazi Maximo,1,Iringa,22,Isiwe mijineno tu manake mihela hubadili watu kweli,1,Itakuwa laki moja ya halali,1,jamani huu kama si ushamba kumbe nini,1,Jamani mbona Mungu anatupigania,1,Jamani watoto wanatakiwa kupendwa,1,jamani.. jamani ukiikosa Diamond usijutie,1,Je nyumbani hakuna vitu vya aina hii?Tuambie,1,je walikuwepo watu wa huduma ya kwanza,1,Je watanzania wanalipa kodi,1,jela kwa raha,1,Jolie,1,juhudi za lazima kuinua filamu,1,kama si kiwanda cha chumvi nani atawajua hawa,1,Kama kweli ndio kweli basi kila heri,1,Kama Mkristo naamini hilo hiyo si sahihi,1,kama unajua kuyarudi nenda Malta,1,kama wao wanaweza sisi je,1,Kamua baba waache wakanyagane,1,karibu nyumbani dada yote maisha tu,1,karibu Tatiii,1,KARIBUNI,1,Katavi,5,kaza buti hakuna kukata tamaa inalipa,1,kazi kwako mheshimiwa waziri wa madini,1,kazi na burudani,1,keep it up bloggers,1,kero ya usafiri sasa kwisha,1,Kila chenye roho na mwili kitaonja umauti,1,kila kitu kina vitu,1,Kila la Heri jamila,1,kila la heri kwani ni changamoto,1,Kipya,51,Kiuno bila mfupa,1,Kolelo mzimu ambao bado hai,1,KUBWA,1,Kudumisha urafiki wa dunia,1,Kuna dalili za wasomi kukubali Uafrika,1,kuna makala humu humu ndani ya blogu sijui mnasemaje,1,Kuu,113,kwa mara nyingine tena Tigo imewezesha,1,Kwa mchanganyiko huu muungano lazima udumu,1,Kwa mihasira hajambo,1,kweli,1,Kweli ina mkono mrefu tuone,1,Kweli duniani tunatofautiana,1,la maana ni kuwa na jiko au vipi,1,labda halitabadilika tena,1,lakini mwafaka lazima,1,lengo ni kutafakari,1,leteni vitu tuvione,1,lets us,1,Lucy wanakuelewa hawa...,1,Lukwangule nyumbani kwetu,2,M ungu bariki mikono ya madaktari wafanikiwe,1,MAARUFU,1,maendeleo ya soka siku zote yanahitaji fedha ili yapatikane,1,maisha ni vyema kuyaangalia,1,MAJIBU,1,makala,51,mama ni mama tu anapendeza,1,mambo mengine we angalia tu,1,mambo msimamo,1,mambo sasa mchanganyiko,1,Mara nyingine huona tunakotoka kwa kuona wenzetu,1,Mashabiki wa rhumba mpooooooooo,1,Masitaa,12,Maskani,1,MASOKO,3,Masupa staa mnaoinukia mpoo,1,Matamasha,6,mavazi ya kuogelea yanaposhindaniwa,1,Mbeya,11,Mchakamchaka anti Asmah,1,Mchanganyiko,81,MCHANYATO,1,mchezo,5,mengi wanayoyaita siri ni public information,1,mfumuko wa bei mpaka noma,1,Mhh sijui watu wa Sua ambao wako huko wanasemaje,1,Mhh ugua pole dada watu wanataka burudani,1,Michezo,501,Michezo maalum inatakiwa kupigiwa debe,1,miguu,1,miguu babu,1,Mikataba mingine ama hakika tuiangalie hata wakopeshaji nao wanatugeuza sakala,1,MIMI NI KISURA NAJITAMBUA,1,Mimi sijajua hasa kumetokea nini kwani ninavyojua hawa huwa na ungalizi wa hali ya juu,1,Mimi simo,1,mimi sisemi,1,mkiwa chumvi basi mkoze,1,Mkiwa taa mulikeni,1,Mnaonaje je hii imekaa vyema,1,Mnaweza wakwetu hapa,1,Morogoro,51,mrithi wa mwanadada Whitney Houston,1,Mtwara,4,Mungu aiweke mahali pema roho yake,4,Mungu amrehemu,1,Mungu amweke pema peponi,1,Mungu awabariki sana,1,Mungu awe nao,1,Mungu ibariki Tanzania,1,Mungu tuepushe na imani hizi za kishirikina,1,mungu tufanye tuwe na upendo,1,Mungu twaomba utuhurumie,1,Muziki,350,muziki na fasheni,5,Mwanahabari,33,Mwanza,6,Mwendo mdundo dada,1,Mwenge huo utakimbizwa duniani kwa siku 130,1,Mwenge wa olimpiki ni ishara ya urafiki,1,Mzee wa Farasi nakupa saluti,1,Mzimbabwe huyu kutoka kwa mama mkali,1,N i dar mpaka Moro au bao tatu bila,1,Na sisi je,1,Naam kama haiwezekani hapa,1,Nairobi waanzisha tena utalii,1,namna bora ya kusaidia jamii,1,nani abebe hukumu na lawama,1,nani asiyejua utamu wa pipi,1,Nani kama baba,1,naona inafaa kuchangia mimi sitoi hoja,1,ndoa za mastaa huwa na mgogoro,1,nenda mwaya nenda,1,New Zanzibar Modern Taarab na wapenzi big up,1,news,5,Ni bikini kwa kwenda mbele,1,Ni Dar mpaka Moro au.. tatu bila,1,ni furaha za muungano,1,Ni kazi ngumu yenye kuhifadhi utamaduni,1,Ni kuchakarika kuonyesha urafiki na biashara pia,1,ni mfumuko wa bei au mfumuko wa nchi,1,Ni muhimu kutazama afya yako,1,ni muziki kwa kwenda mbele,1,Ni muziki mpaka China,1,Ni raha tupu,1,Ni Serengeti Premium Lager,1,Ni Tigo na mawasiliano ya kisasa,1,Ni wakati wa kuujadili utamaduni,1,Ni zaidi ya jazz,1,Nitasubiri and welcome home,1,nje je?,1,NUKUU YA LEO,1,nyie mnasemaje kuhusu hili,1,Ona Kolelo na sindikizwa na Wazee wa Gwasuma,1,ona vya dunia,1,One step ahead,1,patna mwingine mjamzito,1,Pengine anamuogopa Jada Pinkett manake kwa wivu..,1,picha,494,Pole Jamila hayo ndiyo mashindano,1,poleni sana,1,poleni sana wanyalukolo,1,Powa sana,1,Profesa jamaa wanakumaindi,1,Roho za marehemu zipate pumziko la milele,1,Ruvuma,9,sakata dansi mpaka kwenye kilele cha dunia,1,sasa kumebakia ugonjwa mmoja polisi kuendesha mashtaka,1,sasa mifedha kila mahali hongereni,1,Sasa ni mavuno,1,Sasa ni wakati wa kutafuta upenyo ndani ya IDOLS,1,SAYANSI,1,SAYANSI ANGA,1,See Uluguru Montains,1,serikali inataka kujihami kwanini,1,Show of support Big Up Madame,1,Si kitu kidogo hata kidogo,1,si unajua tena namie naimwaga hivyo hivyo,1,Siasa,346,siasa habari,2,Sijui kama City wanajua Mbagala noma,1,Sijui tunaishi karne gani yailahi,1,Sinema,9,sio advencha....kaaa ...niko kibaruani,1,Sisi ndio tunaanza vitongoji,1,Sisi yetu macho na masikio,1,Slow slow jamani,1,sto,1,tabasamu kali la mwenge wa olimpiki,1,Tabora,1,Tazama Waziri Mkuu Pinda wasije wakapindisha maamuzi yako,1,TEKNOLOJIA,1,Thats big man game,1,This is crazy Africa,1,This is Mgeta,1,Tibet wamegeuza Olimpiki jukwaa la siasa,1,Titbits collection,1,Tubadili tamaduni,1,Tuchangie mambo yaive,1,tuendeleze sanaa,1,tuienzi na sisi mbona wizara haituambii,1,Tuipeleke kaskazini,1,Tuisaidie serikali shida ya Mererani,1,tujue namna ya kupumzika,1,Tulienda kustarehe au kufanya fujo,1,Tumsaidie mtototo huyu kurejea katika hali ya kawaida,1,tunahitaji haya,1,Tunajifunza kweli kutoka kwao,1,Tunapandisha chati tu,1,Tunasubiri,1,tunazidi kuhesabu siku,1,TUNAZISUBIRI ZA VINARA ADAR,1,Tuombe nafuu kwa wagonjwa,1,Tuombe rehema kwa mungu,1,Tuone yatufae,1,Tusingoje wengine watusemee,1,tutampa tafu kubwa Prof,1,tuuenzi utamaduni au vipi,1,Tuukuze na kuulinda,1,tuvipende,1,tuwalinde maalbino,1,Tuwe kweli wakweli,1,ubunifu siku zote hulipa,1,uchumi huzunguka kwa kuwawezesha wasukaji,1,udumu muungano,1,Ugonjwa huu wa sasa ni kitendawili,1,Ukiiona kolelo utaipenda,1,Ukirejea salama kila mtu anafurahi,1,Umelenga Mkuchika utamaduni unakufa,1,unaposaka uwakilishi wa dunia,1,urafiki,1,Usisahau wazee wa Ngwasuma,1,UTAMADUNI,1,Video,2,Vionjo vipya ndani ya Gwasuma,1,Vita dhidi ya ufisadi,1,vitongoji Miss Tanzania navyo vimeanza,1,Vitu vikali vyazidi kuingia Dar,1,Vituko,77,Vituo vya polisi Tanga vyatelekezwa,1,VIVALO,1,Wacha tujifue,2,Wadau ilitolewa kiingereza,1,wakali wa ubunifu,1,wala usibabaike mwakwetu hii noma,1,wanadamu wanapotaka kujua zaidi,1,wanasema mpaka kieleweke,1,Wanataka kujua mali za JK na wengine,1,Wanawake wenye mvuto: Monroe,1,Wapo mabinti wa matawi ya juu,1,watu wanapofanya weli kwenye sanaa,1,waweza kurejea enzi ya Moro jazz na Cuban malimba,1,Wazee tupo kusindikiza,1,waziri,1,welcome dar baby,1,Wenzetu wameona sisi tunangoja nini kuangalia,1,wewe unasemaje,1,wigo mpana wa utamaduni,1,wilaya ya 'Mbagala' mlie tu,1,Yaaani sijui itawezekana,1,Yaani wakati mwingine hata huelewi prioty over priority,1,yeye mbele sisi nyuma,1,Yote maisha dada,1,ZA MOTOMOTO,1,Zanzibar,79,zawadi zinatakiwa ziende shule,1,ZILIZOTIA FORA,1,zitachangia kupunguza makali ya bei za umeme,1,
ltr
item
Lukwangule Entertainment: TanTrade ni zaidi ya 'maonesho ya sabasaba'
TanTrade ni zaidi ya 'maonesho ya sabasaba'
Lukwangule Entertainment
https://lukwangule.blogspot.com/2023/10/tantrade-ni-zaidi-ya-maonesho-ya.html
https://lukwangule.blogspot.com/
http://lukwangule.blogspot.com/
http://lukwangule.blogspot.com/2023/10/tantrade-ni-zaidi-ya-maonesho-ya.html
true
934549962738256429
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy