Jenerali Mirisho Sam Hagai Sarakikya ni mmoja wakuu wa majeshi tisa waliongoza Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania ( JWTZ) tangu kuanz...
Anasema wakati anateuliwa na kukabidhiwa madaraka ya ukuu wa jeshi alikuwa kijana mdogo na kustaajabu sana, lakini alikubali mzigo aliopewa na kuacha kwenda masomoni Uingereza.
"Niliteuliwa wakati jeshi halipo, askari wote walioasi walikuwa wamefukuzwa, Mwalimu Nyerere akaniambia nakuteua ukaunde jeshi jipya," anasema Jenerali Sarakikiya ambaye alisema Mwalimu Nyerere alimpa kazi hiyo kwa kuona ulazima wa kuwa na jeshina kusema alikubali kazi hiyo na kuianza.
Maasi ya tarehe 20 Januari 1964 yalianzia Collito Barracks (Lugalo Dar es Salaam) na baadaye kuenea hadi Kalewa Barracks iliyokuwa Tabora. Hata hivyo maasi hayakuishia Tabora bali hata Kombania mpya iliyokuwa imepelekwa Nachingwea, kwa maandalizi ya kuanzisha kikosi kipya cha tatu hapa Tanzania nayo askari wake walijiingiza katika maasi hayo.
Anasema askari waliokuwa wamebaki walikuwa maofisa na wale ambao walikuwa likizo wakati maasi yanatokea yaliyosababishwa pamoja mambo mengine madaraka , nyongeza ya mshahara na kupinga kuondolewa kwa nafuu katika bidhaa wanazonunua, kwa kurejeshewa ushuru.
Anasema askari na maofisa hao wachache ambao ndio kitovu cha TPDF alianza harakati za kutengeneza jeshi upya ambao walikuwa ni askari wa miguu waliohitimu Septemba Mosi mwaka huo.
Kazi yake ya pili aliyoifanya ni kjuunda kwa kikosi cha anga wa upande wa uchukuzi kabla ya kuwezesha kuwepoo kwa kikosi cha wapiganaji cha anga na wanamaji.
"Ndio kazi za kwanza kufanya na kuweka misingi mizuri" anasema Jenerali Sarakikya.
Anasema katika kupanua na kuwa na jeshi lenye maareifa makubwa, mkuu huyo wa jeshi ambaye amesomea mizinga midogo na mikubwa na utaalamu mwingine wa kijeshi walihitaji maofisa zaidi na hivyo akaanzisha chuo (Monduli) hasa baada ya Waingereza ambao tulizozana nao mwaka 1965 kwa sababu ya Rhodesia kukataa kupokea wanafunzi kutoka Tanzania.
Anasema chuo hicho kilichoanzia Dar mwaka 1969 kwa kutumia chuo cha Polisi amesema killenga kutengeneza maofisa na poia kuwa sehemu ya maarifa kwa wanajeshi.
Alisema sababu ya kuanza Dar es salaam ni kuwa na uhakika na walimu kwani wanajeshi wanajifunza mambo mengi ukiachia mbali suala la ulinzi na usalama.
"Askari wanafundishwa uzalendo, uaminmifu,utiii, upendo wa watu wako na nchi yako,, kazi kwanza maswali baadae.." anasema na kuongeza kuwa jeshi lazima liendelee kufuata misngi iliyowekwa kwa ajili ya ustawi wa taifa.
Jenerali Sarakikya ambaye pia alihudumu katika balozi kwanza Nigeria na kisha Ethiopia anasema maasi ya wakati ule hayakulenga kuchukua serikali lakini kufikisha madai ya kutaka mabadiliko.
Jenerali Sarakikya askari mkimya lakini shupavu akiwa amekabidhiwa madaraka akiwa kijana ameonesha uaminifu wa hali ya juu na kumfanya kuwa mwenye historia ndefu ya ujasiri.
Akizungumza katika chaneli hiyo ya ulinzi alionekana kutokuwa na kiburi kuhusu mafanikio yake binafsi. Akipendelea michezo, riadha na kupanda milima, anaamini siasa ni kazi ya wanasiasa, mpaka katika uzee wake anaitaka jamii kuendelea kuwa ya kizalendo.
Wakati kuna maadhimisho makubwa ya kijeshi yanayofanyika kati ya mwezi huu hadi Septemba kuonesha ukuaji wa jeshi hilo ambalo kwa sasa linakamandi zaidi ya tano kutoka vikosi vitatu vya awali. Kamandi hizo zikiwa za Makao makuu, Nchi kavu,anga, wanamaji,jeshi la akiba na JKT, Jenerali huyo anasema wakuu wote wa majeshi waliopita baada yake wamefanya vyema katika kuliimarisha jeshi.
Viongozi waliopita katika nafasi ya Ukuu wa Jeshi baada ya yeye ni Jenerali Abdallah Twalipo (1974-1980),Jenerali David Msuguri (1980-1988), Jenerali Mwita Kiaro (1988-1994), Jenerali Robert Mboma (1994-2001),Jenerali George Waitara (2001-2007), Jenerali Davis Mwamunyange (2007-2017), Jenerali Venance Mabeyo (2017-2022) na kuanzia mwaka 2022 mpaka sasa jeshi linaongozwa na Jenerali Jacob Mkunda.
Jenerali Mirisho Sam Hagai Sarakikya ni mmoja wakuu wa majeshi tisa waliongoza Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania ( JWTZ) tangu kuanzishwa kwake mwaka 1964. Kwa sasa jeshi hilo linaongozwa na Jenerali Jacob Mkunda.
Mzee huyu mwenye umri wa miaka 86 kwa sasa, unaweza kusema ni mmoja wa viongozi wa kijeshi walioweka msingi imara wa jeshi lililopo sasa hasa kwa kuzingatia namna alivyopatiwa madaraka, maagizo aliyopewa na kazi aliyoifanya kufuma JWTZ kuwa lilivyo sasa lenye nidhamu na uzalendo.
Jenerali Mrisho Sam Hagai Sarakikya aliyezaliwa 1934, Meru, amesoma shule ya msingi ya Nkoaranga na kuingia sekondari ya Old Moshi na kumalizia Tabora kabla ya kujiunga na jeshi mwaka 1958 na kupelekwa chuo cha kijeshi cha Royal Military Academy Sandhurst.
Mkuu huyu wa kwanza kabisa wa majeshi ya Tanzania, mwafrika Mtanzania , aliongoza nafasi hiyo ya Ukuu wa Majeshi kuanzia Mwaka 1964 hadi mwaka 1974 akishikilia rekodi ya kuongoza Cheo hicho cha ukuu wa Majeshi akiwa na umri mdogo zaidi kwani aliteuliwa na Mwalimu Julius Kambarage Nyerere akiwa na umri wa miaka 30 tu baada ya kutokea uasi jeshini na kuundwa upya kwa jeshi.
Akizungumza na Chaneli ya Ulinzi na JKT, Jenerali Sarakikya amesema kwamba jeshi hilo limetoka mbali na kwamba kwa kuendelea kuenzi misingi ya kuundwa kwake jeshi hilo limeendelea kuwa imara na kuheshimika duniani likifanya kazi zake nyumbani na kimataifa kwa weledi mkubwa.
"Jeshi letu ni timamu sana kutokana na kutoondoka katika misingi yake... uzalendo, uhodari na ushupavu, sio legelege" anasema Jenerali Sarakikya wakati wa mahojiano na kueleza kuwa kazi zilizofanywa Seychelss, Msumbiji, Uganda,Lebanon , DRC ni kazi nzuri mno na hiyo inawezekana kwa kubaki katika msingi.
COMMENTS