Wajua asili ya vifaa vya kuashiria muungano?

Wajua asili ya vifaa vya kuashiria muungano?

Kuna Makala iliandikwa mwaka 2008 inazungumzia asili ya vifaa vilivyotumika kuashiria Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Mwandishi, Victori...


Kuna Makala iliandikwa mwaka 2008 inazungumzia asili ya vifaa vilivyotumika kuashiria Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Mwandishi, Victoria Godfrey, anaeleza kuwa chungu kilichotumiwa kuchanganya udongo kilitoka kwa Wanyakyusa (Mbeya), vibuyu vilitoka Umasaini, na udongo ulitoka Ikulu za Dar es Salaam na Zanzibar. Vifaa hivi vimehifadhiwa kwenye Makumbusho ya Taifa. Mwandishi anahimiza watu wenye fikira kutafakari kwa nini vifaa hivyo mahususi vilichaguliwa.

https://lukwangule.blogspot.com/2008/04/wajua-asili-ya-vifaa-vya-kuashiria.html



Miaka 11 iliyopita Jumamosi, Aprili 26, 2014 gazeti la Mwananchi liliandika hivi:


Wakati  Watanzania wakiadhimisha miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar,  siku ulipochanganywa udongo wa pande mbili za Muungano kulikuwa na mazingira ya ajabu na mabadiliko ya vipindi vya hali ya hewa vilivyowababaisha na kuwashangaza watu wengi waliohudhuria sherehe hizo.


Sherehe za kuchanganya udongo wa pande mbili uliowekwa kwenye vibuyu viwili tofauti zilifanyika Aprili 26, 1964 kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam na Mwalimu Nyerere alichanganya udongo kwa kuumimina ndani ya chungu kuashiria Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.


Mmoja kati ya watu  waliobeba udongo wa Zanzibar na kuchanganywa na ule wa Tanganyika,  Hassan Omar Mzee (66) akihojiwa na Mwananchi nyumbani kwake huko Kibweni nje ya Mji wa Unguja, anaitaja siku hiyo ilikuwa ya aina yake atakayoikumbuka maishani. Wakati wa tukio hilo alikuwa na  umri wa miaka 16.


Hassan anasema kazi ya kuchanganya udogo wa Tanganyika na Zanzibar ilianza  saa tatu asubuhi na kukiwa na manyunyu ya mvua, jua lisilounguza likiwaka na kupotea na mawingu yaliyokuwa na kivuli  cha ubaridi yakiwa yametulizana juu ya anga huku ukimya ukitawala eneo la uwanja.


Anasimulia kuwa lilikuwa tukio la aina yake ambalo liliwashangaza viongozi wengi wa nje na ndani, waliohudhuria na kushuhudia kitendo hicho cha kijasiri na cha kihistoria kilichofanywa na viongozi wa mataifa ya Tanganyika na Zanzibar, Mwalimu Julius Nyerere na Sheikh Abeid Amani Karume (wote kwa sasa ni marehemu).



Mshangao huo unatokana na mazimio ya harakati za vikao vingi vya viongozi wa Kiafrika, walikuwa na lengo la kuungana baada ya kujikomboa kutoka kwenye ukoloni, lakini  maazimio hayo yaliwashinda viongozi wengi  pia Nyerere na Karume walitekeleza kwa vitendo.


Anasema siyo Mwalimu Nyerere wala Mzee Karume walionekana kuwa na hofu ya kupoteza madaraka ya nchi zao, hawakutaka kuendekeza fahari ya vyeo vyao na badala yake walichokitanguliza mbele ni  nia na azma ya kujenga umoja wa kitaifa wa watu wao.


Jamhuri ya watu wa Zanzibar na ile ya Tanganyika ndipo zilipokufa. Mabeberu na wakoloni wakipigwa na butwaa kuona kitendo hicho kikitokea na viongozi wa pande mbili wakiwa na nyuso za furaha na bashasha pia wananchi wengine wakionekana kutokwa na machozi ya furaha kutokana na tukio hilo.


Akielezea tukio hilo, Hassan anawataja wenzake wengine watatu walioshiriki katika kazi ya kubeba udongo wa pande mbili za Muungano  ni Hassan Kheir Mrema na Sifaheri Kunda kutoka Tanzania Bara na Khadija Abbas kutoka Zanzibar.


Wenzao wanawake walibeba vibuyu vidogo na vikubwa vyenye udongo na wanaume walibeba chungu kimoja kilichochanganyiwa udongo, tukio lilifanyika katikati ya Uwanja wa Taifa ambako jukwaa maalumu lilijengwa.


“Siku hiyo tuliamka mapema tukiwa tumepewa mavazi maalumu, wanaume tulivaa shati na suruali zilizoshonwa kwa vitenge, wenzetu wa kike walivaa mavazi maalumu ya khanga zilizozingatia utamaduni wa Mwafrika,” anaeleza Hassan.


Anasema kabla ya kazi hiyo kufanyika, kulikuwa na  mazoezi ya vitendo wiki moja nyuma yake,  jinsi ya utaratibu mzima utakavyokuwa  hadi kuchanganywa udongo wakiongozwa na Bi Mwakemwa, ndiye aliyekuwa mwenyeji wao tokea walipowasili Dar es Salaam na kupiga kambi Uwanja wa Taifa.  Hassan anaeleza  ilipofika saa tatu juu ya alama wananchi kutoka Tanganyika na Zanzibar walikusanyika na kukaa kwenye jukwaa la Uwanja wa Taifa kwa utulivu, wakisubiri kuona na kushuhudia tukio la  kihistoria likifanyika ili kuziunganisha nchi mbili kuwa Taifa moja.


Anaeleza baada ya kazi hiyo kukamilika, akiwa na wenzake waliondoka hadi kwenye jukwaa kuu wakiwa na vifaa vilivyotumika kubeba udongo na baadaye  kwenda kukaa sehemu waliopangiwa kabla ya kuanza safari ya kuelekea Ikulu ya Dar es Salaam.



Anaeleza  walipofika Ikulu kulikuwa na tukio kubwa la kihistoria na ulipandwa mti wa mwembe wa kumbukumbu ya Muungano, uliopandwa na Mwalimu Julius Nyerere akishirikiana Mzee Karume, ukapewa jina la  mwembe wa Muungano.


“Mimi nilimkabidhi galoni lililokuwa na maji Mwalimu Nyerere ili kuumwagia mti uliopandwa, Hassan Kheri alimkabidhi Mzee Karume galoni jingine na kuumwagia mwembe huo, hadi leo mwembe huo upo, ni mkubwa kuliko yote ndani ya uzio wa Ikulu,” anasema Hassan akiwa bado anaonyesha kuwa na hamu ya tukio hilo.


Baada ya kumalizika kazi hiyo, sehemu ya udongo uliobakia na vifaa vilivyotumika vilipelekwa kwenye  Makumbusho ya Taifa, hadi leo vitu hivyo vinaoonekana na kushuhudiwa na wanaokwenda kuitembelea makumbusho hiyo.


“Udongo wa Zanzibar uliochanganywa na ule wa Tanganyika ulitoka eneo la Kizimbani hapa Unguja, ule wa Tanganyika ulichotwa maeneo ya Dar es Salaam, udongo toka maeneo hayo sasa umeliunganisha taifa zima na mipaka yake, sasa tuna Taifa moja la Tanzania na kiti kimoja Umoja wa Mataifa, ” anasema Hassan.


Safari yao kutoka Unguja hadi Dar es Salaam


Akiwa mwanafunzi wa Chuo cha Ufundi Zanzibar  mwaka 1964,  pia  Katibu Mipango wa Umoaj wa Vijana wa  ASP ‘Youth League’, jina lake liliteuliwa kuwa katika orodha ya watakaoshiriki tukio la kuzaliwa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Maandalizi ya safari yao yalifanywa na Mwenyekiti wa ASP Youth League ,hayati Seif Bakari Omar mmoja kati ya watu 14 wa mstari wa mbele katika Mapinduzi ya Zanzibar, yakiratibiwa na Katibu Mipango wa ASP  hayati Abdallah Said Natepe.


Uteuzi na kupendekezwa majina ya vijana 100 kutoka Zanzibar ambao waliungana na wenzao wa Tanganyika ulifanywa na Halmashauri Kuu ya ASP Youth League,  wiki moja kabla ya siku ya Muungano walichezeshwa gwaride la Muungano, nyakati  za asubihi na jioni wakiongozwa na Bi Mwakemwa.


Vijana kutoka Zanzibar waliondoka kwa kutumia usafiri wa meli hadi  Dar es Salaam, wakapokewa na wenzao kwa furaha, hata hivyo wakati huo hakufahamu kama atapangwa kuwa mmoja kati ya vijana watakaobeba udongo kutoka Zanzibar.


Walipofika na meli yao kutia nanga, wakateremka na kupanda magari yaliyowapeleka kwenye maeneo waliopangiwa kuishi na kufanya mazoezi, kabla ya siku ya tukio hilo kufika.


Hapo ndipo tulipoteuliwa na kuanza kufanya mazoezi ya vitendo katika eneo la uchanganyaji udongo huku wenzao wengine wakicheza gwaride la halaiki ya Muungano. Muda wote walikuwa wenye furaha na wakati mwingi kabla na baada ya kuamka walikuwa wakiimba nyimbo za kulisifia taifa jipya.


Baada ya kumalizika tukio la uchanganyaji udongo kulifanyika karamu na dhifa kubwa ikulu, viongozi wote wa Tanganyika na Zanzibar walihudhuria kabla ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano kurudi Zanzibar,  kupokewa kwa maandamano makubwa huko Maisara Suleiman, Unguja na Tibirinzi kisiwani Pemba.


Je, Muungano ulipata baraka za wananchi wa Zanzibar?


Hassan anasema hilo halikuwa ni jambo la siri. Kwa miaka mingi ASP iliweka dhamira ya  wananchi wa Zanzibar kuungana na wenzao wa Tanganyika  huku mara kadhaa wananchi wakiulizwa hadharani wakiuunga mkono mpango huo.


Mzee Karume katika mikutano mingi ya ASP aliyoifanya Zanzibar na Pemba  alisikika akiwauliza wananchi “...Je, wananchi mko tayari kwa union na Tanganyika,…wananchi walimjibu bila ya kubabaika  …tuko tayari kwa masilahi ya Afrika yote, Mapinduzi na usalama wa nchi zetu,” anasema Hassan.


Name

Anga,11,Arusha,27,Burudani,317,burundani,1,come rain,1,come sun,1,Crazy in Love kama wimbo kama wao wenyewe,1,dahh sijui kweli mbona shida,1,Dar utakuja je tumejiandaa,1,daraja sahau nini,1,demokrasia ya upanga,1,Dodoma,78,Dole tupu vijana wa zamani,1,Duhh bibie endeleza libeneke,1,Duhh kaisikie Walibana,1,duhh kwa mbagala mama lazima awe supa,1,Fedha za maiti haziliwi bure,1,Fedha za watu kwa maendeleo ya watu,1,Fikira,14,filamu,249,Filamu ndio kielelezo cha ukuzi wa taifa,1,flamu,7,Gandamiza Kibara baba ake,1,haba,1,Habari,5078,habari dodoma,29,habari. dodoma,32,habaria,1,hadithi,19,hakika tumeweka historia,1,hakuna noma jongwe,1,hapa kwetu inakuwaje vile,1,hasira hasara,1,hata maji,1,hataki masikhara na maisha yake,1,hatubonyezi kizenji,1,haya ndiyo mambo ya Ulaya,1,haya si yangu ni ya mdau mwenye hasira,1,haya wabongo na mambo kutoka nje,1,He he he wananikumbusha upishi wa shaba,1,Headline,1,Hii hurejesha uhai,1,Hii iko sawa kweli?,1,Hii imekaa vizuri,1,Hii inakaaje vile,1,Hii kweli noma,1,Hii maana yake Moro kuna uhaba wa chakula,1,Hii mexico,1,Hii mihasira mingine bwana,1,Hii ndio moro sio mpaka dar,1,hii ni hatari,1,Hii ni kiboko anayetaka kubisha ajibishie tu,1,Hii ni moja ya staili za kunyoa nywele,1,Hii si lukwangule,1,hii staili mpya,1,hili ni jengo pacha la malaysia ghorofa 88,1,Hivi ni ngoma tu,1,hivi nini siri za serikali,1,hivi sisi tunajua kama kuna vitu vya aina hii,1,hivi vitu bwana,1,Hiyo ndiyo gharama ya demokrasia,1,Hizi imani nyingine ni hatari,1,Hizi takwimu hizi mhh,1,Hongera bibie,1,Hongera dada etu kwa kutuletea kaka etu (shemeji) kwani mwenye dada hakosi shemeji,1,Hongera sana,1,huhitaji mifedha kuwa msafi,1,Huko Ulaya,1,Huu ndio ustaarabu,1,huu ujiko utakuwa mkubwa,1,imetosha,1,Inahitaji nidhamu fulani,1,inakuuma au...,1,Inakuwaje kama filamu yenyewe itahitaji busu la nguvu,1,Inaonekana watanzania hatukuwepo,1,Ipo kazi Maximo,1,Iringa,22,Isiwe mijineno tu manake mihela hubadili watu kweli,1,Itakuwa laki moja ya halali,1,jamani huu kama si ushamba kumbe nini,1,Jamani mbona Mungu anatupigania,1,Jamani watoto wanatakiwa kupendwa,1,jamani.. jamani ukiikosa Diamond usijutie,1,Je nyumbani hakuna vitu vya aina hii?Tuambie,1,je walikuwepo watu wa huduma ya kwanza,1,Je watanzania wanalipa kodi,1,jela kwa raha,1,Jolie,1,juhudi za lazima kuinua filamu,1,kama si kiwanda cha chumvi nani atawajua hawa,1,Kama kweli ndio kweli basi kila heri,1,Kama Mkristo naamini hilo hiyo si sahihi,1,kama unajua kuyarudi nenda Malta,1,kama wao wanaweza sisi je,1,Kamua baba waache wakanyagane,1,karibu nyumbani dada yote maisha tu,1,karibu Tatiii,1,KARIBUNI,1,Katavi,5,kaza buti hakuna kukata tamaa inalipa,1,kazi kwako mheshimiwa waziri wa madini,1,kazi na burudani,1,keep it up bloggers,1,kero ya usafiri sasa kwisha,1,Kila chenye roho na mwili kitaonja umauti,1,kila kitu kina vitu,1,Kila la Heri jamila,1,kila la heri kwani ni changamoto,1,Kipya,51,Kiuno bila mfupa,1,Kolelo mzimu ambao bado hai,1,KUBWA,1,Kudumisha urafiki wa dunia,1,Kuna dalili za wasomi kukubali Uafrika,1,kuna makala humu humu ndani ya blogu sijui mnasemaje,1,Kuu,113,kwa mara nyingine tena Tigo imewezesha,1,Kwa mchanganyiko huu muungano lazima udumu,1,Kwa mihasira hajambo,1,kweli,1,Kweli ina mkono mrefu tuone,1,Kweli duniani tunatofautiana,1,la maana ni kuwa na jiko au vipi,1,labda halitabadilika tena,1,lakini mwafaka lazima,1,lengo ni kutafakari,1,leteni vitu tuvione,1,lets us,1,Lucy wanakuelewa hawa...,1,Lukwangule nyumbani kwetu,2,M ungu bariki mikono ya madaktari wafanikiwe,1,MAARUFU,1,maendeleo ya soka siku zote yanahitaji fedha ili yapatikane,1,maisha ni vyema kuyaangalia,1,MAJIBU,1,makala,52,mama ni mama tu anapendeza,1,mambo mengine we angalia tu,1,mambo msimamo,1,mambo sasa mchanganyiko,1,Mara nyingine huona tunakotoka kwa kuona wenzetu,1,Mashabiki wa rhumba mpooooooooo,1,Masitaa,12,Maskani,1,MASOKO,3,Masupa staa mnaoinukia mpoo,1,Matamasha,6,mavazi ya kuogelea yanaposhindaniwa,1,Mbeya,11,Mchakamchaka anti Asmah,1,Mchanganyiko,81,MCHANYATO,1,mchezo,5,mengi wanayoyaita siri ni public information,1,mfumuko wa bei mpaka noma,1,Mhh sijui watu wa Sua ambao wako huko wanasemaje,1,Mhh ugua pole dada watu wanataka burudani,1,Michezo,518,Michezo maalum inatakiwa kupigiwa debe,1,miguu,1,miguu babu,1,Mikataba mingine ama hakika tuiangalie hata wakopeshaji nao wanatugeuza sakala,1,MIMI NI KISURA NAJITAMBUA,1,Mimi sijajua hasa kumetokea nini kwani ninavyojua hawa huwa na ungalizi wa hali ya juu,1,Mimi simo,1,mimi sisemi,1,mkiwa chumvi basi mkoze,1,Mkiwa taa mulikeni,1,Mnaonaje je hii imekaa vyema,1,Mnaweza wakwetu hapa,1,Morogoro,51,mrithi wa mwanadada Whitney Houston,1,Mtwara,4,Mungu aiweke mahali pema roho yake,4,Mungu amrehemu,1,Mungu amweke pema peponi,1,Mungu awabariki sana,1,Mungu awe nao,1,Mungu ibariki Tanzania,1,Mungu tuepushe na imani hizi za kishirikina,1,mungu tufanye tuwe na upendo,1,Mungu twaomba utuhurumie,1,Muziki,353,muziki na fasheni,6,Mwanahabari,33,Mwanza,6,Mwendo mdundo dada,1,Mwenge huo utakimbizwa duniani kwa siku 130,1,Mwenge wa olimpiki ni ishara ya urafiki,1,Mzee wa Farasi nakupa saluti,1,Mzimbabwe huyu kutoka kwa mama mkali,1,N i dar mpaka Moro au bao tatu bila,1,Na sisi je,1,Naam kama haiwezekani hapa,1,Nairobi waanzisha tena utalii,1,namna bora ya kusaidia jamii,1,nani abebe hukumu na lawama,1,nani asiyejua utamu wa pipi,1,Nani kama baba,1,naona inafaa kuchangia mimi sitoi hoja,1,ndoa za mastaa huwa na mgogoro,1,nenda mwaya nenda,1,New Zanzibar Modern Taarab na wapenzi big up,1,news,5,Ni bikini kwa kwenda mbele,1,Ni Dar mpaka Moro au.. tatu bila,1,ni furaha za muungano,1,Ni kazi ngumu yenye kuhifadhi utamaduni,1,Ni kuchakarika kuonyesha urafiki na biashara pia,1,ni mfumuko wa bei au mfumuko wa nchi,1,Ni muhimu kutazama afya yako,1,ni muziki kwa kwenda mbele,1,Ni muziki mpaka China,1,Ni raha tupu,1,Ni Serengeti Premium Lager,1,Ni Tigo na mawasiliano ya kisasa,1,Ni wakati wa kuujadili utamaduni,1,Ni zaidi ya jazz,1,Nitasubiri and welcome home,1,nje je?,1,NUKUU YA LEO,1,nyie mnasemaje kuhusu hili,1,Ona Kolelo na sindikizwa na Wazee wa Gwasuma,1,ona vya dunia,1,One step ahead,1,patna mwingine mjamzito,1,Pengine anamuogopa Jada Pinkett manake kwa wivu..,1,picha,494,Pole Jamila hayo ndiyo mashindano,1,poleni sana,1,poleni sana wanyalukolo,1,Powa sana,1,Profesa jamaa wanakumaindi,1,Roho za marehemu zipate pumziko la milele,1,Ruvuma,9,sakata dansi mpaka kwenye kilele cha dunia,1,sasa kumebakia ugonjwa mmoja polisi kuendesha mashtaka,1,sasa mifedha kila mahali hongereni,1,Sasa ni mavuno,1,Sasa ni wakati wa kutafuta upenyo ndani ya IDOLS,1,SAYANSI,3,SAYANSI ANGA,3,See Uluguru Montains,1,serikali inataka kujihami kwanini,1,Show of support Big Up Madame,1,Si kitu kidogo hata kidogo,1,si unajua tena namie naimwaga hivyo hivyo,1,Siasa,346,siasa habari,2,Sijui kama City wanajua Mbagala noma,1,Sijui tunaishi karne gani yailahi,1,Sinema,9,sio advencha....kaaa ...niko kibaruani,1,Sisi ndio tunaanza vitongoji,1,Sisi yetu macho na masikio,1,Slow slow jamani,1,sto,1,tabasamu kali la mwenge wa olimpiki,1,Tabora,1,Tazama Waziri Mkuu Pinda wasije wakapindisha maamuzi yako,1,TEKNOLOJIA,1,Thats big man game,1,This is crazy Africa,1,This is Mgeta,1,Tibet wamegeuza Olimpiki jukwaa la siasa,1,Titbits collection,1,Tubadili tamaduni,1,Tuchangie mambo yaive,1,tuendeleze sanaa,1,tuienzi na sisi mbona wizara haituambii,1,Tuipeleke kaskazini,1,Tuisaidie serikali shida ya Mererani,1,tujue namna ya kupumzika,1,Tulienda kustarehe au kufanya fujo,1,Tumsaidie mtototo huyu kurejea katika hali ya kawaida,1,tunahitaji haya,1,Tunajifunza kweli kutoka kwao,1,Tunapandisha chati tu,1,Tunasubiri,1,tunazidi kuhesabu siku,1,TUNAZISUBIRI ZA VINARA ADAR,1,Tuombe nafuu kwa wagonjwa,1,Tuombe rehema kwa mungu,1,Tuone yatufae,1,Tusingoje wengine watusemee,1,tutampa tafu kubwa Prof,1,tuuenzi utamaduni au vipi,1,Tuukuze na kuulinda,1,tuvipende,1,tuwalinde maalbino,1,Tuwe kweli wakweli,1,ubunifu siku zote hulipa,1,uchumi huzunguka kwa kuwawezesha wasukaji,1,udumu muungano,1,Ugonjwa huu wa sasa ni kitendawili,1,Ukiiona kolelo utaipenda,1,Ukirejea salama kila mtu anafurahi,1,Umelenga Mkuchika utamaduni unakufa,1,unaposaka uwakilishi wa dunia,1,urafiki,1,urembo,1,Usisahau wazee wa Ngwasuma,1,UTALII,1,UTAMADUNI,3,Video,2,Vionjo vipya ndani ya Gwasuma,1,Vita dhidi ya ufisadi,1,vitongoji Miss Tanzania navyo vimeanza,1,Vitu vikali vyazidi kuingia Dar,1,Vituko,77,Vituo vya polisi Tanga vyatelekezwa,1,VIVALO,1,Wacha tujifue,2,Wadau ilitolewa kiingereza,1,wakali wa ubunifu,1,wala usibabaike mwakwetu hii noma,1,wanadamu wanapotaka kujua zaidi,1,wanasema mpaka kieleweke,1,Wanataka kujua mali za JK na wengine,1,Wanawake wenye mvuto: Monroe,1,Wapo mabinti wa matawi ya juu,1,watu wanapofanya weli kwenye sanaa,1,waweza kurejea enzi ya Moro jazz na Cuban malimba,1,Wazee tupo kusindikiza,1,waziri,1,welcome dar baby,1,Wenzetu wameona sisi tunangoja nini kuangalia,1,wewe unasemaje,1,wigo mpana wa utamaduni,1,wilaya ya 'Mbagala' mlie tu,1,Yaaani sijui itawezekana,1,Yaani wakati mwingine hata huelewi prioty over priority,1,yeye mbele sisi nyuma,1,Yote maisha dada,1,ZA MOTOMOTO,1,Zanzibar,79,zawadi zinatakiwa ziende shule,1,ZILIZOTIA FORA,1,zitachangia kupunguza makali ya bei za umeme,1,
ltr
item
Lukwangule Entertainment: Wajua asili ya vifaa vya kuashiria muungano?
Wajua asili ya vifaa vya kuashiria muungano?
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjbOWxGmXxFA5rVarXzQ2oEPIepEQn6YHAAirHRSNWqIgmGWDkogf71QW62QGCiG4ASAxMEbrA4o6f-22d7eJvQ9B4Ys_gidR93bLPCNPBlEIRM27_yFR_eENeHBTvOAkAdqogiKD6deb4lZYhfiIRiNewKJuB2ub3PT2Ap552nUL717BSMR81V0ifsH1y0/s320/Historia-ya-Muungano-wa-Tanganyika-na-Zanzibar_1.webp
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjbOWxGmXxFA5rVarXzQ2oEPIepEQn6YHAAirHRSNWqIgmGWDkogf71QW62QGCiG4ASAxMEbrA4o6f-22d7eJvQ9B4Ys_gidR93bLPCNPBlEIRM27_yFR_eENeHBTvOAkAdqogiKD6deb4lZYhfiIRiNewKJuB2ub3PT2Ap552nUL717BSMR81V0ifsH1y0/s72-c/Historia-ya-Muungano-wa-Tanganyika-na-Zanzibar_1.webp
Lukwangule Entertainment
https://lukwangule.blogspot.com/2025/04/wajua-asili-ya-vifaa-vya-kuashiria.html
https://lukwangule.blogspot.com/
http://lukwangule.blogspot.com/
http://lukwangule.blogspot.com/2025/04/wajua-asili-ya-vifaa-vya-kuashiria.html
true
934549962738256429
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy