DKT. BITEKO AZINDUA PROGRAMU YA UGAWAJI MAJIKO YA UMEME KWA BEI YA RUZUKU KWA WAFANYAKAZI WA TANESCO

     Awapongeza TANESCO kutekeleza maoni ya Rais Samia kwa vitendo     Imeelezwa kuwa, matumizi ya nishati safi ya kupikia ni ajenda  ya kit...


 


 

📌 Awapongeza TANESCO kutekeleza maoni ya Rais Samia kwa vitendo

 

 

Imeelezwa kuwa, matumizi ya nishati safi ya kupikia ni ajenda  ya kitaifa inayolenga kuhamasisha wananchi kutumia nishati safi na salama ya kupikia ikiwemo nishati ya umeme.

 

Aidha, takwimu za mwaka 2022 zinaonesha kuwa Watanzania wanaotumia nishati ya umeme kwa ajili ya kupikia ni asilimia 4.2 tu huku ikitajwa kuwa idadi hiyo ni ndogo ikilinganishwa na idadi ya watanzania waliopo.

 

Akizungumza Agosti 14, 2025 jijini Dodoma wakati akizindua Mpango wa Ugawaji Majiko ya Kupikia kwa Umeme kwa Wafanyakazi wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amesema kuwa kutokana na historia ya siku za nyuma Watanzania walidhani kuwa kupika kwa umeme  ni ghali zaidi tatizo ambalo lilisababishwa na masuala mengi ikiwemo elimu kuhusu unafuu wa gharama kwa matumizi ya umeme.

 

“Utafiti wa TANESCO unaonesha kuwa kupikia kwa nishati ya umeme, hasa kwa kutumia majiko janja yenye ufanisi  ni nafuu zaidi kuliko wanavyofikiria wengi miongoni mwetu katika jamii tunazoishi. Utafiti huo unaonesha kuwa, majiko janja ya umeme yanaweza kutumia chini ya uniti moja (1) ya umeme ambayo ni sawa na chini ya shilingi za Kitanzania 352 kuandaa mlo mmoja,” amesema Dkt. Biteko.







 

Amefafanua kuwa matumizi ya umeme kwa ajili ya kupikia ni nafuu kuliko nishati nyingine hivyo Watanzania hawana haja ya kuogopa kutumia umeme. Aidha, hatua ya Ugawaji Majiko ya Kupikia kwa Umeme kwa Wafanyakazi  TANESCO itakuwa  hatua muhimu katika mabadiliko kwa kuwa wafanyakazi hao  wa TANESCO watakuwa  mabalozi wa matumizi ya nishati safi ya kupikia hususan majiko ya umeme  katika jamii.

 

“ Kupitia mpango huu, nimejulishwa kuwa  TANESCO, kwa kushirikianana Taasisi ya Modern Energy Cooking Services (MECS) chini ya Serikali ya Uingereza imeweza kununua zaidi ya majiko 11,000. Majiko haya yatawafikia wafanyakazi wote waTANESCO kwa mpango wa mfuko wa mzunguko (revolving fund). Pia zimewekwa mbinu bunifu za ugharamiaji ambazo ni rafiki kwa kila mtumiaji,”amesisitiza Dkt. Biteko.

 

 Amewapongeza wafanyakazi wa TANESCO kuwa kufanya kazi kubwa ya kuwahudumia Watanzania kwa kuboresha utoaji wa huduma ya umeme nchini na kuwaasa kuwa wabunifu zaidi katika kutekeleza majukumu yao sambamba na kuwa mabalozi wa mabadiliko chanya kwa jamii.

 

Kuhusu  programu hiyo ya Ugawaji wa Majiko ya Kupikia  kwa Umeme amesema hapo baadaye itahusisha wateja wa TANESCO  wanaojiunga na huduma ya umeme.

 

 “ Wateja hao watapatiwa majiko na watalipa kidogo kidogo kupitia manunuzi ya umeme (On bill financing) ilikuleta manufaa zaidi kwa jamii nzima ya Tanzania. Nawaomba TANESCO kuharakisha jambo hili iliwananchi waweze kunufaikana program hii muhimu,” ameeleza Dkt. Biteko.

 






Aidha, ametoa wito kwa Taasisi za Umma na Binafsi kujifunza kutoka TANESCO na kaungalia namna ambavyo watumishi wao wanaweza kunufaika na programu hiyo na kuchochoea matumizi ya nishati safi ya kupikia hususani kwa kutumia umeme.

 

Katika hatua nyingine, Dkt. Biteko amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwa kinara wa ajenda wa nishati safi ya kupikia na kuelekeza wananchi wahamasishwe katika matumizi wa nishati safi ya kupikia.

 

Amebainisha kuwa  hakuna mafanikio yoyote yaliyopatikana katika nishati ya umeme na mafuta bila kumtaja Rais Samia ambaye ametoa msukumo mkubwa katika seka hiyo si tu nchini Tanzania bali Afrika na duniani kote.

 

 Aidha, amesema kuhusu hali ya umeme nchini, takwimu zinaonesha kuwa, hadi kufikia Julai 2025, Tanzania ilikuwa na uwezo wa kuzalisha jumla ya megawati 2,720. Ambapo mahitaji ya umeme kwenye Gridi ya Taifa yamefikia megawati 1,921 pekee.

 

Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Judith Kapinga kwa upande wake, amesema kuwa, tukio la ugawaji wa majiko ya umeme kwa bei ya ruzuku kwa Wafanyakazi wa TANESCO  ni sehemu ya utekelezaji wa Mkakati wa Nishagi Safi ya Kupikia ambayo kinara wake ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan.

 

Amesema zoezi hilo la ugawaji majiko hayo ya umeme ni kielelezo cha kuwa, Wizara ya Nishati na Taasisi zake zinaibeba Ajenda ya Nishati  Safi ya Kupikia kwa  vitendo na pia inawafanya wafanyakazi kuwa  vinara na mabalozi wa nishati safi ya kupikia.

 

Aidha, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule amemshukuru Rais Samia kwa kuimarisha miradi ya nishati katika Mkoa husika kwani katika kipindi cha miaka minne ametoa shilingi bilioni 214.3 ambazo zimekamilisha miradi ya umeme vijijini na kupekeka umeme kwenye miradi mbalimbali ikiwemo umwagiliaji, afya na maji.

 

Kuhusu Nishati Safi ya Kupikia, amesema katika Mkoa wa Dodoma majiko ya gesi takriban 10,000 yamefikia wananchi, pia  miradi ya umeme jua na upepo imefikia miradi mbalimbali ikiwemo ya umwagiliaji, na taasisi mbalimbali zinatumia nishati safi ya kupikia ikiwemo vikosi vyote vya Ulinzi na Usalama pamoja na  Shule mbalimbali.

 

Awali, Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Lazaro Twange alisema kuwa, tukio la ugawaji wa majiko ya umeme kwa TANESCO ni muhimu kwani  ni sehemu ya mpango mkakati wa kuitikia wito wa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan wa kuhakikisha kuwa ifikapo 2034 asilimia 80 ya wananchi wanatumia nishati safi ya kupikia.


 

Amesema majiko yatakayosambazwa ni 11,000  na yatafikia watumishi wote wa TANESCO, na hivyo ametoa wito kwa wafanyakazi kutumia majiko hayo na kuwa mabalozi wa kuhamasisha matumizi ya nisahati safi ya iupilia..

 

Mpango huo wa ugawaji majiko ya umeme amesema.kuwa, unahusisha utoaji wa elimu,  usambazaji majiko na pia wananchi kukopeshwa majiko ya umeme ambapo baadaye wataweza kulipa jinsi wanavyolipia umeme lengo likiwa ni kuongeza watu wanaotumia umeme kupikia na hivyo shirika kuongeza mapato.

 

Mwakilishi wa mradi wa MECS uliopo chini ya Serikali ya Uingereza,  ambao ndio umetoa majiko hayo ya umeme   kwa wafanyakazi wa TANESCO kwa bei ya ruzuku, Charles Barnabas amesema majiko hayo yanatumia umeme kidogo.

 

Amesema pia wana kampeni ya kitaifa ya Pika smart ambayo wanafanya na Tanesco ya kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia kwa kutumia majiko ya umeme.

 

Mwisho


COMMENTS

Name

Anga,11,Arusha,27,Burudani,346,burundani,2,come rain,1,come sun,1,Crazy in Love kama wimbo kama wao wenyewe,1,dahh sijui kweli mbona shida,1,Dar utakuja je tumejiandaa,1,daraja sahau nini,1,demokrasia ya upanga,1,Dodoma,78,Dole tupu vijana wa zamani,1,Duhh bibie endeleza libeneke,1,Duhh kaisikie Walibana,1,duhh kwa mbagala mama lazima awe supa,1,Fedha za maiti haziliwi bure,1,Fedha za watu kwa maendeleo ya watu,1,Fikira,14,filamu,253,Filamu ndio kielelezo cha ukuzi wa taifa,1,flamu,7,Gandamiza Kibara baba ake,1,haba,1,habar,1,Habari,5293,habari dodoma,31,habari. dodoma,32,habaria,1,hadithi,19,hakika tumeweka historia,1,hakuna noma jongwe,1,hapa kwetu inakuwaje vile,1,hasira hasara,1,hata maji,1,hataki masikhara na maisha yake,1,hatubonyezi kizenji,1,haya ndiyo mambo ya Ulaya,1,haya si yangu ni ya mdau mwenye hasira,1,haya wabongo na mambo kutoka nje,1,He he he wananikumbusha upishi wa shaba,1,Headline,1,Hii hurejesha uhai,1,Hii iko sawa kweli?,1,Hii imekaa vizuri,1,Hii inakaaje vile,1,Hii kweli noma,1,Hii maana yake Moro kuna uhaba wa chakula,1,Hii mexico,1,Hii mihasira mingine bwana,1,Hii ndio moro sio mpaka dar,1,hii ni hatari,1,Hii ni kiboko anayetaka kubisha ajibishie tu,1,Hii ni moja ya staili za kunyoa nywele,1,Hii si lukwangule,1,hii staili mpya,1,hili ni jengo pacha la malaysia ghorofa 88,1,Hivi ni ngoma tu,1,hivi nini siri za serikali,1,hivi sisi tunajua kama kuna vitu vya aina hii,1,hivi vitu bwana,1,Hiyo ndiyo gharama ya demokrasia,1,Hizi imani nyingine ni hatari,1,Hizi takwimu hizi mhh,1,Hongera bibie,1,Hongera dada etu kwa kutuletea kaka etu (shemeji) kwani mwenye dada hakosi shemeji,1,Hongera sana,1,huhitaji mifedha kuwa msafi,1,Huko Ulaya,1,Huu ndio ustaarabu,1,huu ujiko utakuwa mkubwa,1,imetosha,1,Inahitaji nidhamu fulani,1,inakuuma au...,1,Inakuwaje kama filamu yenyewe itahitaji busu la nguvu,1,Inaonekana watanzania hatukuwepo,1,Ipo kazi Maximo,1,Iringa,22,Isiwe mijineno tu manake mihela hubadili watu kweli,1,Itakuwa laki moja ya halali,1,jamani huu kama si ushamba kumbe nini,1,Jamani mbona Mungu anatupigania,1,Jamani watoto wanatakiwa kupendwa,1,jamani.. jamani ukiikosa Diamond usijutie,1,Je nyumbani hakuna vitu vya aina hii?Tuambie,1,je walikuwepo watu wa huduma ya kwanza,1,Je watanzania wanalipa kodi,1,jela kwa raha,1,Jolie,1,juhudi za lazima kuinua filamu,1,kama si kiwanda cha chumvi nani atawajua hawa,1,Kama kweli ndio kweli basi kila heri,1,Kama Mkristo naamini hilo hiyo si sahihi,1,kama unajua kuyarudi nenda Malta,1,kama wao wanaweza sisi je,1,Kamua baba waache wakanyagane,1,karibu nyumbani dada yote maisha tu,1,karibu Tatiii,1,KARIBUNI,1,Katavi,5,kaza buti hakuna kukata tamaa inalipa,1,kazi kwako mheshimiwa waziri wa madini,1,kazi na burudani,1,keep it up bloggers,1,kero ya usafiri sasa kwisha,1,Kila chenye roho na mwili kitaonja umauti,1,kila kitu kina vitu,1,Kila la Heri jamila,1,kila la heri kwani ni changamoto,1,Kipya,51,Kiuno bila mfupa,1,Kolelo mzimu ambao bado hai,1,KUBWA,1,Kudumisha urafiki wa dunia,1,Kuna dalili za wasomi kukubali Uafrika,1,kuna makala humu humu ndani ya blogu sijui mnasemaje,1,Kuu,113,kwa mara nyingine tena Tigo imewezesha,1,Kwa mchanganyiko huu muungano lazima udumu,1,Kwa mihasira hajambo,1,kweli,1,Kweli ina mkono mrefu tuone,1,Kweli duniani tunatofautiana,1,la maana ni kuwa na jiko au vipi,1,labda halitabadilika tena,1,lakini mwafaka lazima,1,lengo ni kutafakari,1,leteni vitu tuvione,1,lets us,1,Lucy wanakuelewa hawa...,1,Lukwangule nyumbani kwetu,2,M ungu bariki mikono ya madaktari wafanikiwe,1,MAARUFU,1,maendeleo ya soka siku zote yanahitaji fedha ili yapatikane,1,maisha ni vyema kuyaangalia,1,MAJIBU,1,makala,52,mama ni mama tu anapendeza,1,mambo mengine we angalia tu,1,mambo msimamo,1,mambo sasa mchanganyiko,1,Mara nyingine huona tunakotoka kwa kuona wenzetu,1,Mashabiki wa rhumba mpooooooooo,1,Masitaa,12,Maskani,1,MASOKO,3,Masupa staa mnaoinukia mpoo,1,Matamasha,6,mavazi ya kuogelea yanaposhindaniwa,1,Mbeya,11,Mchakamchaka anti Asmah,1,Mchanganyiko,81,MCHANYATO,1,mchezo,5,mengi wanayoyaita siri ni public information,1,mfumuko wa bei mpaka noma,1,Mhh sijui watu wa Sua ambao wako huko wanasemaje,1,Mhh ugua pole dada watu wanataka burudani,1,Michezo,557,Michezo maalum inatakiwa kupigiwa debe,1,miguu,1,miguu babu,1,Mikataba mingine ama hakika tuiangalie hata wakopeshaji nao wanatugeuza sakala,1,MIMI NI KISURA NAJITAMBUA,1,Mimi sijajua hasa kumetokea nini kwani ninavyojua hawa huwa na ungalizi wa hali ya juu,1,Mimi simo,1,mimi sisemi,1,miochezo,1,mkiwa chumvi basi mkoze,1,Mkiwa taa mulikeni,1,Mnaonaje je hii imekaa vyema,1,Mnaweza wakwetu hapa,1,Morogoro,51,mrithi wa mwanadada Whitney Houston,1,Mtwara,4,Mungu aiweke mahali pema roho yake,4,Mungu amrehemu,1,Mungu amweke pema peponi,1,Mungu awabariki sana,1,Mungu awe nao,1,Mungu ibariki Tanzania,1,Mungu tuepushe na imani hizi za kishirikina,1,mungu tufanye tuwe na upendo,1,Mungu twaomba utuhurumie,1,Muziki,356,muziki na fasheni,6,Mwanahabari,33,Mwanza,6,Mwendo mdundo dada,1,Mwenge huo utakimbizwa duniani kwa siku 130,1,Mwenge wa olimpiki ni ishara ya urafiki,1,Mzee wa Farasi nakupa saluti,1,Mzimbabwe huyu kutoka kwa mama mkali,1,N i dar mpaka Moro au bao tatu bila,1,Na sisi je,1,Naam kama haiwezekani hapa,1,Nairobi waanzisha tena utalii,1,namna bora ya kusaidia jamii,1,nani abebe hukumu na lawama,1,nani asiyejua utamu wa pipi,1,Nani kama baba,1,naona inafaa kuchangia mimi sitoi hoja,1,ndoa za mastaa huwa na mgogoro,1,nenda mwaya nenda,1,New Zanzibar Modern Taarab na wapenzi big up,1,news,5,Ni bikini kwa kwenda mbele,1,Ni Dar mpaka Moro au.. tatu bila,1,ni furaha za muungano,1,Ni kazi ngumu yenye kuhifadhi utamaduni,1,Ni kuchakarika kuonyesha urafiki na biashara pia,1,ni mfumuko wa bei au mfumuko wa nchi,1,Ni muhimu kutazama afya yako,1,ni muziki kwa kwenda mbele,1,Ni muziki mpaka China,1,Ni raha tupu,1,Ni Serengeti Premium Lager,1,Ni Tigo na mawasiliano ya kisasa,1,Ni wakati wa kuujadili utamaduni,1,Ni zaidi ya jazz,1,Nitasubiri and welcome home,1,nje je?,1,NUKUU YA LEO,1,nyie mnasemaje kuhusu hili,1,Ona Kolelo na sindikizwa na Wazee wa Gwasuma,1,ona vya dunia,1,One step ahead,1,patna mwingine mjamzito,1,Pengine anamuogopa Jada Pinkett manake kwa wivu..,1,picha,494,Pole Jamila hayo ndiyo mashindano,1,poleni sana,1,poleni sana wanyalukolo,1,Powa sana,1,Profesa jamaa wanakumaindi,1,Roho za marehemu zipate pumziko la milele,1,Ruvuma,9,sakata dansi mpaka kwenye kilele cha dunia,1,sasa kumebakia ugonjwa mmoja polisi kuendesha mashtaka,1,sasa mifedha kila mahali hongereni,1,Sasa ni mavuno,1,Sasa ni wakati wa kutafuta upenyo ndani ya IDOLS,1,SAYANSI,5,SAYANSI ANGA,3,See Uluguru Montains,1,serikali inataka kujihami kwanini,1,Show of support Big Up Madame,1,Si kitu kidogo hata kidogo,1,si unajua tena namie naimwaga hivyo hivyo,1,Siasa,346,siasa habari,2,Sijui kama City wanajua Mbagala noma,1,Sijui tunaishi karne gani yailahi,1,Sinema,13,sio advencha....kaaa ...niko kibaruani,1,Sisi ndio tunaanza vitongoji,1,Sisi yetu macho na masikio,1,Slow slow jamani,1,sto,1,tabasamu kali la mwenge wa olimpiki,1,Tabora,1,Tazama Waziri Mkuu Pinda wasije wakapindisha maamuzi yako,1,TEKNOLOJIA,1,Thats big man game,1,This is crazy Africa,1,This is Mgeta,1,Tibet wamegeuza Olimpiki jukwaa la siasa,1,Titbits collection,1,Tubadili tamaduni,1,Tuchangie mambo yaive,1,tuendeleze sanaa,1,tuienzi na sisi mbona wizara haituambii,1,Tuipeleke kaskazini,1,Tuisaidie serikali shida ya Mererani,1,tujue namna ya kupumzika,1,Tulienda kustarehe au kufanya fujo,1,Tumsaidie mtototo huyu kurejea katika hali ya kawaida,1,tunahitaji haya,1,Tunajifunza kweli kutoka kwao,1,Tunapandisha chati tu,1,Tunasubiri,1,tunazidi kuhesabu siku,1,TUNAZISUBIRI ZA VINARA ADAR,1,Tuombe nafuu kwa wagonjwa,1,Tuombe rehema kwa mungu,1,Tuone yatufae,1,Tusingoje wengine watusemee,1,tutampa tafu kubwa Prof,1,tuuenzi utamaduni au vipi,1,Tuukuze na kuulinda,1,tuvipende,1,tuwalinde maalbino,1,Tuwe kweli wakweli,1,ubunifu siku zote hulipa,1,uchumi huzunguka kwa kuwawezesha wasukaji,1,udumu muungano,1,Ugonjwa huu wa sasa ni kitendawili,1,Ukiiona kolelo utaipenda,1,Ukirejea salama kila mtu anafurahi,1,Umelenga Mkuchika utamaduni unakufa,1,unaposaka uwakilishi wa dunia,1,urafiki,1,urembo,1,Usisahau wazee wa Ngwasuma,1,UTALII,1,UTAMADUNI,3,Video,2,Vionjo vipya ndani ya Gwasuma,1,Vita dhidi ya ufisadi,1,vitongoji Miss Tanzania navyo vimeanza,1,Vitu vikali vyazidi kuingia Dar,1,Vituko,77,Vituo vya polisi Tanga vyatelekezwa,1,VIVALO,1,Wacha tujifue,2,Wadau ilitolewa kiingereza,1,wakali wa ubunifu,1,wala usibabaike mwakwetu hii noma,1,wanadamu wanapotaka kujua zaidi,1,wanasema mpaka kieleweke,1,Wanataka kujua mali za JK na wengine,1,Wanawake wenye mvuto: Monroe,1,Wapo mabinti wa matawi ya juu,1,watu wanapofanya weli kwenye sanaa,1,waweza kurejea enzi ya Moro jazz na Cuban malimba,1,Wazee tupo kusindikiza,1,waziri,1,welcome dar baby,1,Wenzetu wameona sisi tunangoja nini kuangalia,1,wewe unasemaje,1,wigo mpana wa utamaduni,1,wilaya ya 'Mbagala' mlie tu,1,Yaaani sijui itawezekana,1,Yaani wakati mwingine hata huelewi prioty over priority,1,yeye mbele sisi nyuma,1,Yote maisha dada,1,ZA MOTOMOTO,1,Zanzibar,79,zawadi zinatakiwa ziende shule,1,ZILIZOTIA FORA,1,zitachangia kupunguza makali ya bei za umeme,1,
ltr
item
Lukwangule Entertainment: DKT. BITEKO AZINDUA PROGRAMU YA UGAWAJI MAJIKO YA UMEME KWA BEI YA RUZUKU KWA WAFANYAKAZI WA TANESCO
DKT. BITEKO AZINDUA PROGRAMU YA UGAWAJI MAJIKO YA UMEME KWA BEI YA RUZUKU KWA WAFANYAKAZI WA TANESCO
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgUiZxfCAzByAamcJxeMMVEjhFvINsS8x9F1g6QwaZApRvYgBmh6IHBXTiUwfQvnjSEwKMDt-OGgqNdS1Nr82JiPqJZ2fPYiTwE5kMfPJqATByWlSTBkQzx_HV4Tft15hZJ9dCYzWf2f3E2iP2m8SQNxclhuhakXoeJ05c6Tj9XiXk44N1H1-4emnrYrUp2/s320/KNK_7005%20(1).jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgUiZxfCAzByAamcJxeMMVEjhFvINsS8x9F1g6QwaZApRvYgBmh6IHBXTiUwfQvnjSEwKMDt-OGgqNdS1Nr82JiPqJZ2fPYiTwE5kMfPJqATByWlSTBkQzx_HV4Tft15hZJ9dCYzWf2f3E2iP2m8SQNxclhuhakXoeJ05c6Tj9XiXk44N1H1-4emnrYrUp2/s72-c/KNK_7005%20(1).jpg
Lukwangule Entertainment
https://lukwangule.blogspot.com/2025/08/dkt-biteko-azindua-programu-ya-ugawaji.html
https://lukwangule.blogspot.com/
http://lukwangule.blogspot.com/
http://lukwangule.blogspot.com/2025/08/dkt-biteko-azindua-programu-ya-ugawaji.html
true
934549962738256429
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy