RAIS SAMIA AWAKARIBISHA IKULU TAIFA STARS KWA CHAKULA CHA MCHANA

Na Rahel Pallangyo RAIS Samia Suluhu Hassan amewaalika wachezaji na benchi la ufundi la timu ya Taifa, Taifa Stars, kwa chakula cha mchana I...




Na Rahel Pallangyo


RAIS Samia Suluhu Hassan amewaalika wachezaji na benchi la ufundi la timu ya Taifa, Taifa Stars, kwa chakula cha mchana Ikulu, Januari 10, 2026. Mwaliko huo ni ishara ya kutambua mchango wao na heshima waliyoipa nchi baada ya kufuzu hatua ya 16 bora katika michuano ya AFCON 2025 nchini Morocco.

Hayo yameelezwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Profesa Palamagamba Kabudi, wakati wa mapokezi ya timu hiyo kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Dar es Salaam. Timu hiyo imerejea nchini ikitokea Rabat, Morocco kwa kutumia ndege ya Boeing 787-8 Dreamliner iliyotolewa na Rais Samia.

Profesa Kabudi amesema kuwa kutokana na kiwango kilichooneshwa, Tanzania sasa imeingia rasmi katika orodha ya timu washindani barani Afrika na si washiriki pekee. 



Alisema wachezaji wameonesha kiwango cha juu cha ushindani, nidhamu na kujitoa kwa hali ya juu na kulipa heshima kubwa taifa barani Afrika. 

“Taifa Stars wameonesha umahiri wa hali ya juu na kujitoa kwa hali yao yote. Kwa mafanikio haya, Tanzania sasa si mshiriki tu wa AFCON, bali ni mshindani wa kweli,” alisema Profesa Kabudi.

Amesema mafanikio hayo ni msingi imara kuelekea maandalizi ya AFCON 2027 itakayofanyika kwa pamoja nchini Tanzania, Kenya na Uganda.

“Rais ameniagiza nije niwapokee na nimshukuru kwa dhati kwa uwekezaji mkubwa alioufanya katika sekta ya michezo, ambao matunda yake yameanza kuonekana,” alisema Profesa Kabudi.



Amewashukuru wananchi wa Dar es Salaam na Watanzania kwa ujumla kwa kujitokeza kwa wingi kuipokea timu hiyo, huku akisisitiza umuhimu wa kulinda amani, umoja na mshikamano wa kitaifa.

"Amani ni msingi wa taifa letu. Taifa lolote linalothamini michezo hulinda amani, na Tanzania imeendelea kuwa mfano wa nchi inayokabiliana na changamoto zake kwa njia ya maridhiano,” alisisitiza.



Naye Kocha Mkuu wa Taifa Stars Miguel Gamondi alisema wachezaji walipambana kwa hali ya juu na wanastahili pongezi kubwa kutoka kwa Watanzania wote.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, alisema mkoa huo unaungana na serikali kuwapongeza Taifa Stars kwa kazi kubwa waliyoifanya, huku akibainisha kuwa maandalizi ya AFCON 2027 yanaendelea kwa kasi.

“Tumejipanga kikamilifu. Tumetuma kikosi maalum kwenda nchini Morocco kujifunza namna bora ya uendeshaji wa mashindano haya. Amani ndiyo msingi wa kila jambo, na tunahakikisha amani ya Dar es Salaam inalindwa wakati wote,” alisema Chalamila.

Aliongeza kuwa mkoa huo, kwa kushirikiana na sekta binafsi, unaendelea kuboresha miundombinu, ikiwemo ujenzi wa hoteli za nyota tano, huku akiahidi kuwa ifikapo 2027 hakutakuwa na barabara itakayofungwa wakati wa mashindano.





Mapokezi ya Taifa Stars yalipambwa na shamrashamra za kipekee zilizosheheni ladha ya sanaa na utamaduni wa Kitanzania. Vikundi vya ngoma za asili vilitumbuiza kwa madoido, vikicheza kwa ufundi wa hali ya juu huku sauti za ngoma na vigelegele vikitawala anga la uwanja huo, hali iliyoamsha ari na fahari ya kitaifa miongoni mwa mamia ya mashabiki waliojitokeza kuwapokea mashujaa hao.

Vituko vya sanaa na utamaduni viliwakilishwa vyema na vibunifu mbalimbali, ikiwemo uwepo wa wahusika waliovalia mavazi ya vikaragosi ya dubu wakubwa wa rangi za kijani, bluu na nyeusi, ambayo ni rangi za bendera ya taifa. Ubunifu huu uliwavutia watu wengi, hususan watoto na vijana, na kufanya mazingira ya uwanja wa ndege kuwa kama tamasha kubwa la kijamii lililojaa furaha na amani.

Wachezaji wa Taifa Stars walionekana wenye bashasha wakizungukwa na viongozi pamoja na mashabiki, huku wakisindikizwa kila hatua na umati uliokuwa ukiimba nyimbo za ushindi. Muingiliano huu wa sanaa, ngoma, na mavazi ya utamaduni ulionyesha jinsi michezo inavyoweza kuunganisha taifa na kutoa fursa kwa wasanii kuonyesha vipaji vyao katika matukio makubwa ya kihistoria kama hayo.



Katika mashindano hayo yaliyoanza Desemba 21 mwaka jana kwenye makundi Taifa Stars ilifungwa na Nigeria 2-1 katika mchezo wa kwanza na kutoka sare ya 1-1 dhidi ya Uganda na Tunisia.

Kwa kufika hatua ya 16 bora Taifa Stars imevuna Sh Bilioni 1.9 pia imepokea Sh milioni 300 kama zawadi ya kila goli, mechi dhidi ya Uganda Sh milioni 100 na mechi ya Tunisia sh milioni 200.

Taifa Stars imeshiriki kwa mara ya nne katika michuano ya AFCON tangu kuanzishwa kwake mwaka 1957 ambapo ilishiriki mwaka 1980, 2019 na 2023 na safari hii wamevuka hatua ya makundi kwa mara ya kwanza.


COMMENTS

Name

Anga,11,Arusha,27,Burudani,379,burundani,2,come rain,1,come sun,1,Crazy in Love kama wimbo kama wao wenyewe,1,dahh sijui kweli mbona shida,1,Dar utakuja je tumejiandaa,1,daraja sahau nini,1,demokrasia ya upanga,1,Dodoma,78,Dole tupu vijana wa zamani,1,Duhh bibie endeleza libeneke,1,Duhh kaisikie Walibana,1,duhh kwa mbagala mama lazima awe supa,1,Fedha za maiti haziliwi bure,1,Fedha za watu kwa maendeleo ya watu,1,Fikira,14,filamu,271,Filamu ndio kielelezo cha ukuzi wa taifa,1,flamu,7,Gandamiza Kibara baba ake,1,haba,1,habar,2,Habari,6046,habari dodoma,38,habari. dodoma,32,habaria,1,hadithi,23,hakika tumeweka historia,1,hakuna noma jongwe,1,hapa kwetu inakuwaje vile,1,hasira hasara,1,hata maji,1,hataki masikhara na maisha yake,1,hatubonyezi kizenji,1,haya ndiyo mambo ya Ulaya,1,haya si yangu ni ya mdau mwenye hasira,1,haya wabongo na mambo kutoka nje,1,He he he wananikumbusha upishi wa shaba,1,Headline,1,Hii hurejesha uhai,1,Hii iko sawa kweli?,1,Hii imekaa vizuri,1,Hii inakaaje vile,1,Hii kweli noma,1,Hii maana yake Moro kuna uhaba wa chakula,1,Hii mexico,1,Hii mihasira mingine bwana,1,Hii ndio moro sio mpaka dar,1,hii ni hatari,1,Hii ni kiboko anayetaka kubisha ajibishie tu,1,Hii ni moja ya staili za kunyoa nywele,1,Hii si lukwangule,1,hii staili mpya,1,hili ni jengo pacha la malaysia ghorofa 88,1,Hivi ni ngoma tu,1,hivi nini siri za serikali,1,hivi sisi tunajua kama kuna vitu vya aina hii,1,hivi vitu bwana,1,Hiyo ndiyo gharama ya demokrasia,1,Hizi imani nyingine ni hatari,1,Hizi takwimu hizi mhh,1,Hongera bibie,1,Hongera dada etu kwa kutuletea kaka etu (shemeji) kwani mwenye dada hakosi shemeji,1,Hongera sana,1,huhitaji mifedha kuwa msafi,1,Huko Ulaya,1,Huu ndio ustaarabu,1,huu ujiko utakuwa mkubwa,1,imetosha,1,Inahitaji nidhamu fulani,1,inakuuma au...,1,Inakuwaje kama filamu yenyewe itahitaji busu la nguvu,1,Inaonekana watanzania hatukuwepo,1,Ipo kazi Maximo,1,Iringa,22,Isiwe mijineno tu manake mihela hubadili watu kweli,1,Itakuwa laki moja ya halali,1,jamani huu kama si ushamba kumbe nini,1,Jamani mbona Mungu anatupigania,1,Jamani watoto wanatakiwa kupendwa,1,jamani.. jamani ukiikosa Diamond usijutie,1,Je nyumbani hakuna vitu vya aina hii?Tuambie,1,je walikuwepo watu wa huduma ya kwanza,1,Je watanzania wanalipa kodi,1,jela kwa raha,1,Jolie,1,juhudi za lazima kuinua filamu,1,kama si kiwanda cha chumvi nani atawajua hawa,1,Kama kweli ndio kweli basi kila heri,1,Kama Mkristo naamini hilo hiyo si sahihi,1,kama unajua kuyarudi nenda Malta,1,kama wao wanaweza sisi je,1,Kamua baba waache wakanyagane,1,karibu nyumbani dada yote maisha tu,1,karibu Tatiii,1,KARIBUNI,1,Katavi,5,kaza buti hakuna kukata tamaa inalipa,1,kazi kwako mheshimiwa waziri wa madini,1,kazi na burudani,1,keep it up bloggers,1,kero ya usafiri sasa kwisha,1,Kila chenye roho na mwili kitaonja umauti,1,kila kitu kina vitu,1,Kila la Heri jamila,1,kila la heri kwani ni changamoto,1,Kipya,51,Kiuno bila mfupa,1,Kolelo mzimu ambao bado hai,1,KUBWA,1,Kudumisha urafiki wa dunia,1,Kuna dalili za wasomi kukubali Uafrika,1,kuna makala humu humu ndani ya blogu sijui mnasemaje,1,Kuu,113,kwa mara nyingine tena Tigo imewezesha,1,Kwa mchanganyiko huu muungano lazima udumu,1,Kwa mihasira hajambo,1,kweli,1,Kweli ina mkono mrefu tuone,1,Kweli duniani tunatofautiana,1,la maana ni kuwa na jiko au vipi,1,labda halitabadilika tena,1,lakini mwafaka lazima,1,lengo ni kutafakari,1,leteni vitu tuvione,1,lets us,1,Lucy wanakuelewa hawa...,1,Lukwangule nyumbani kwetu,2,M ungu bariki mikono ya madaktari wafanikiwe,1,MAARUFU,1,maendeleo ya soka siku zote yanahitaji fedha ili yapatikane,1,maisha ni vyema kuyaangalia,1,MAJIBU,1,makala,52,mama ni mama tu anapendeza,1,mambo mengine we angalia tu,1,mambo msimamo,1,mambo sasa mchanganyiko,1,Mara nyingine huona tunakotoka kwa kuona wenzetu,1,Mashabiki wa rhumba mpooooooooo,1,Masitaa,12,Maskani,1,MASOKO,3,Masupa staa mnaoinukia mpoo,1,Matamasha,6,mavazi ya kuogelea yanaposhindaniwa,1,Mbeya,11,Mchakamchaka anti Asmah,1,Mchanganyiko,81,MCHANYATO,1,mchezo,6,mengi wanayoyaita siri ni public information,1,mfumuko wa bei mpaka noma,1,Mhh sijui watu wa Sua ambao wako huko wanasemaje,1,Mhh ugua pole dada watu wanataka burudani,1,Michezo,637,Michezo maalum inatakiwa kupigiwa debe,1,miguu,1,miguu babu,1,Mikataba mingine ama hakika tuiangalie hata wakopeshaji nao wanatugeuza sakala,1,MIMI NI KISURA NAJITAMBUA,1,Mimi sijajua hasa kumetokea nini kwani ninavyojua hawa huwa na ungalizi wa hali ya juu,1,Mimi simo,1,mimi sisemi,1,miochezo,1,mkiwa chumvi basi mkoze,1,Mkiwa taa mulikeni,1,Mnaonaje je hii imekaa vyema,1,Mnaweza wakwetu hapa,1,Morogoro,51,mrithi wa mwanadada Whitney Houston,1,Mtwara,4,Mungu aiweke mahali pema roho yake,4,Mungu amrehemu,1,Mungu amweke pema peponi,1,Mungu awabariki sana,1,Mungu awe nao,1,Mungu ibariki Tanzania,1,Mungu tuepushe na imani hizi za kishirikina,1,mungu tufanye tuwe na upendo,1,Mungu twaomba utuhurumie,1,Muziki,370,muziki na fasheni,18,Mwanahabari,33,Mwanza,6,Mwendo mdundo dada,1,Mwenge huo utakimbizwa duniani kwa siku 130,1,Mwenge wa olimpiki ni ishara ya urafiki,1,Mzee wa Farasi nakupa saluti,1,Mzimbabwe huyu kutoka kwa mama mkali,1,N i dar mpaka Moro au bao tatu bila,1,Na sisi je,1,Naam kama haiwezekani hapa,1,Nairobi waanzisha tena utalii,1,namna bora ya kusaidia jamii,1,nani abebe hukumu na lawama,1,nani asiyejua utamu wa pipi,1,Nani kama baba,1,naona inafaa kuchangia mimi sitoi hoja,1,ndoa za mastaa huwa na mgogoro,1,nenda mwaya nenda,1,New Zanzibar Modern Taarab na wapenzi big up,1,news,5,Ni bikini kwa kwenda mbele,1,Ni Dar mpaka Moro au.. tatu bila,1,ni furaha za muungano,1,Ni kazi ngumu yenye kuhifadhi utamaduni,1,Ni kuchakarika kuonyesha urafiki na biashara pia,1,ni mfumuko wa bei au mfumuko wa nchi,1,Ni muhimu kutazama afya yako,1,ni muziki kwa kwenda mbele,1,Ni muziki mpaka China,1,Ni raha tupu,1,Ni Serengeti Premium Lager,1,Ni Tigo na mawasiliano ya kisasa,1,Ni wakati wa kuujadili utamaduni,1,Ni zaidi ya jazz,1,Nitasubiri and welcome home,1,nje je?,1,NUKUU YA LEO,1,nyie mnasemaje kuhusu hili,1,Ona Kolelo na sindikizwa na Wazee wa Gwasuma,1,ona vya dunia,1,One step ahead,1,patna mwingine mjamzito,1,Pengine anamuogopa Jada Pinkett manake kwa wivu..,1,picha,494,Pole Jamila hayo ndiyo mashindano,1,poleni sana,1,poleni sana wanyalukolo,1,Powa sana,1,Profesa jamaa wanakumaindi,1,Roho za marehemu zipate pumziko la milele,1,Ruvuma,9,sakata dansi mpaka kwenye kilele cha dunia,1,sasa kumebakia ugonjwa mmoja polisi kuendesha mashtaka,1,sasa mifedha kila mahali hongereni,1,Sasa ni mavuno,1,Sasa ni wakati wa kutafuta upenyo ndani ya IDOLS,1,SAYANSI,5,SAYANSI ANGA,7,See Uluguru Montains,1,serikali inataka kujihami kwanini,1,Show of support Big Up Madame,1,Si kitu kidogo hata kidogo,1,si unajua tena namie naimwaga hivyo hivyo,1,Siasa,346,siasa habari,2,Sijui kama City wanajua Mbagala noma,1,Sijui tunaishi karne gani yailahi,1,Sinema,17,sio advencha....kaaa ...niko kibaruani,1,Sisi ndio tunaanza vitongoji,1,Sisi yetu macho na masikio,1,Slow slow jamani,1,sto,1,tabasamu kali la mwenge wa olimpiki,1,Tabora,1,Tazama Waziri Mkuu Pinda wasije wakapindisha maamuzi yako,1,TEKNOLOJIA,1,Thats big man game,1,This is crazy Africa,1,This is Mgeta,1,Tibet wamegeuza Olimpiki jukwaa la siasa,1,Titbits collection,1,Tubadili tamaduni,1,Tuchangie mambo yaive,1,tuendeleze sanaa,1,tuienzi na sisi mbona wizara haituambii,1,Tuipeleke kaskazini,1,Tuisaidie serikali shida ya Mererani,1,tujue namna ya kupumzika,1,Tulienda kustarehe au kufanya fujo,1,Tumsaidie mtototo huyu kurejea katika hali ya kawaida,1,tunahitaji haya,1,Tunajifunza kweli kutoka kwao,1,Tunapandisha chati tu,1,Tunasubiri,1,tunazidi kuhesabu siku,1,TUNAZISUBIRI ZA VINARA ADAR,1,Tuombe nafuu kwa wagonjwa,1,Tuombe rehema kwa mungu,1,Tuone yatufae,1,Tusingoje wengine watusemee,1,tutampa tafu kubwa Prof,1,tuuenzi utamaduni au vipi,1,Tuukuze na kuulinda,1,tuvipende,1,tuwalinde maalbino,1,Tuwe kweli wakweli,1,ubunifu siku zote hulipa,1,uchumi huzunguka kwa kuwawezesha wasukaji,1,udumu muungano,1,Ugonjwa huu wa sasa ni kitendawili,1,Ukiiona kolelo utaipenda,1,Ukirejea salama kila mtu anafurahi,1,Umelenga Mkuchika utamaduni unakufa,1,unaposaka uwakilishi wa dunia,1,urafiki,1,urembo,1,Usisahau wazee wa Ngwasuma,1,UTALII,1,UTAMADUNI,4,Video,2,Vionjo vipya ndani ya Gwasuma,1,Vita dhidi ya ufisadi,1,vitongoji Miss Tanzania navyo vimeanza,1,Vitu vikali vyazidi kuingia Dar,1,Vituko,77,Vituo vya polisi Tanga vyatelekezwa,1,VIVALO,1,Wacha tujifue,2,Wadau ilitolewa kiingereza,1,wakali wa ubunifu,1,wala usibabaike mwakwetu hii noma,1,wanadamu wanapotaka kujua zaidi,1,wanasema mpaka kieleweke,1,Wanataka kujua mali za JK na wengine,1,Wanawake wenye mvuto: Monroe,1,Wapo mabinti wa matawi ya juu,1,watu wanapofanya weli kwenye sanaa,1,waweza kurejea enzi ya Moro jazz na Cuban malimba,1,Wazee tupo kusindikiza,1,waziri,1,welcome dar baby,1,Wenzetu wameona sisi tunangoja nini kuangalia,1,wewe unasemaje,1,wigo mpana wa utamaduni,1,wilaya ya 'Mbagala' mlie tu,1,Yaaani sijui itawezekana,1,Yaani wakati mwingine hata huelewi prioty over priority,1,yeye mbele sisi nyuma,1,Yote maisha dada,1,ZA MOTOMOTO,1,Zanzibar,79,zawadi zinatakiwa ziende shule,1,ZILIZOTIA FORA,1,zitachangia kupunguza makali ya bei za umeme,1,
ltr
item
Lukwangule Entertainment: RAIS SAMIA AWAKARIBISHA IKULU TAIFA STARS KWA CHAKULA CHA MCHANA
RAIS SAMIA AWAKARIBISHA IKULU TAIFA STARS KWA CHAKULA CHA MCHANA
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEio_lFZ0Pa_4sIIJF__IK3SmpkdQLosVCZq-4nQ2G7p1ALLHmnrMXvSdrbJCx4_WIg58TaHXL5J_8r_ZQLGrGbfEc57DEJrCFPI1gST7Ef7AD9-X7qrGeHh-FupWQlZTwS0qSr7oGzGFhI574hMAPQxrP5OGAOl7WZr2H3t5g_qjmvZ6hrrmc2aBXSxDlMG/s320/CY8A8726.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEio_lFZ0Pa_4sIIJF__IK3SmpkdQLosVCZq-4nQ2G7p1ALLHmnrMXvSdrbJCx4_WIg58TaHXL5J_8r_ZQLGrGbfEc57DEJrCFPI1gST7Ef7AD9-X7qrGeHh-FupWQlZTwS0qSr7oGzGFhI574hMAPQxrP5OGAOl7WZr2H3t5g_qjmvZ6hrrmc2aBXSxDlMG/s72-c/CY8A8726.jpg
Lukwangule Entertainment
https://lukwangule.blogspot.com/2026/01/rais-samia-awakaribisha-ikulu-taifa.html
https://lukwangule.blogspot.com/
http://lukwangule.blogspot.com/
http://lukwangule.blogspot.com/2026/01/rais-samia-awakaribisha-ikulu-taifa.html
true
934549962738256429
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy