SIMON MKINA WA PAMBAZUKO ONLINE ATWAA USHINDI WA JUMLA EJAT 2025

Mwanahabari Simon Mkina wa Pambazuko Online ameibuka mshindi bora wa jumla katika Tuzo za 16 za Umahiri wa Uandishi wa Habari Tanzania (EJAT...




Mwanahabari Simon Mkina wa Pambazuko Online ameibuka mshindi bora wa jumla katika Tuzo za 16 za Umahiri wa Uandishi wa Habari Tanzania (EJAT) mwaka 2025 zilizofanyika jijini Dar es Salaam na kukabidhiwa hundi ya shilingi milioni tatu na mgeni rasmi, Rais wa Mahakama ya Afrika Mashariki, Jaji Nestor Kayobera. 

Mkina aling’ara vilivyo katika usiku huo wa tuzo zinazoandaliwa na Baraza la Habari Tanzania (MCT) kwa kunyakua pia Tuzo ya Habari Bora ya Afya pamoja na Tuzo ya Uandishi Bora wa Habari za Uchunguzi. 



Gazeti la Jamhuri nalo lilionyesha ubabe wake kwa kutwaa Tuzo ya Mahojiano Bora ya Mwaka kupitia mahojiano mahiri yaliyofanywa na Mhariri wake, Manyerere Jacton, na Waziri Mkuu mstaafu Jaji Joseph Warioba, huku gazeti hilo likiongeza tuzo nyingine mikononi mwao ambayo ni Tuzo ya Uhifadhi ya Mwalimu Julius Nyerere.

Orodha ya washindi wa umahiri wa uandishi iliendelea kutawaliwa na weledi mkubwa ambapo Julius Maricha wa Gazeti la Mwananchi alishinda Tuzo ya Afya ya Uzazi, huku Philip Mwihava wa Clouds FM akitwaa Tuzo ya Habari Bora ya Elimu na kumwacha Leonard Mubale wa Trigen Media katika nafasi ya pili. Tuzo ya Habari Bora ya Siasa ilienda kwa Antony Rwekaza wa Watetezi TV, nayo Tuzo ya Michezo ikanyakuliwa na Mackriner Siyovelwa wa Crown Media.

Ushindani uliendelea kuwa mkali katika vipengele vingine ambapo Devotha Kihwelo wa gazeti la Mwananchi alitunukiwa Tuzo ya Utawala Bora, huku Joseph Kirati wa The Chanzo akiondoka na Tuzo ya Picha Bora ya Habari. Mwanahabari Abel Kilumbu wa EATV alifanya kweli kwa kutwaa Tuzo ya Habari Bora ya Video, Sauti, Maandishi na Picha, huku Daniel Samson wa Nukta Afrika akijitwalia Tuzo ya Maudhui Bora ya Mtandao. 

Katika tuzo maalum za umahiri wa kipekee, Manyerere Jacton alitangazwa kuwa Mhariri Bora wa Mwaka, Sanula Athanas wa gazeti la Nipashe akatwaa Tuzo ya Mwanahabari Mbobevu na Mchambuzi Mahiri, Esau Ng’umbi wa Nukta Afrika akatawazwa kuwa Mwanahabari Mchanga Bora wa Mwaka, na Neema Abel wa The Guardian akaibuka kidedea kama Mwanahabari Bora Mwanamke wa Mwaka.

Katika upande wa taasisi, Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) iliibuka kidedea kwa kushinda Tuzo ya Chombo Bora cha Habari cha Serikali Kinachotii Sheria zaidi, ushindi ambao Mkurugenzi Mtendaji wa TSN, Asha Dachi, amebainisha kuwa ni uthibitisho thabiti wa namna taasisi hiyo inavyosimamia viwango vya taaluma, maadili, na weledi tangu kuanzishwa kwake. 



Dachi alipongeza juhudi za wahariri na timu nzima ya wanahabari akieleza kuwa msingi wa mafanikio ya TSN unaanzia kwenye mchakato thabiti wa ajira na mafunzo ya kitaaluma yanayowajenga watumishi kufanya kazi kwa kuzingatia sera na utumishi wa umma. 



Ushindi wa TSN ulienda sambamba na mafanikio ya Mhariri Msaidizi wa gazeti la HabariLEO, Halima Mlacha, aliyetwaa Tuzo ya Uandishi Bora wa Habari za Afya ya Uzazi iliyodhaminiwa na MSI Tanzania, hatua ambayo Dachi aliiitaja kama chachu kwa waandishi wa Daily News, HabariLEO, na majukwaa ya kidijiti ya TSN kuendelea kuzalisha kazi za uchunguzi zenye ubora na athari chanya kwa jamii.

Kwenye kundi la vyombo binafsi, kampuni ya Azam Media ilijizolea sifa kwa kushinda Tuzo ya Chombo Bora cha Habari Binafsi Kinachotii Sheria huku Nukta Afrika ikishika nafasi ya pili, ingawa Nukta Afrika haikuondoka patupu kwani ilinyakua Tuzo ya Uandishi Bora wa Habari za Ugonjwa wa Sikoseli. 

Kilele cha hafla hiyo kilipambwa na uzinduzi wa kumbukumbu ya miaka 30 tangu kuanzishwa kwa MCT, ambapo baraza hilo lilitambua mchango wa viongozi 10 walioacha alama katika maendeleo yake akiwemo Jaji Joseph Warioba, Profesa Issa Shivji, Geoffrey Mmari, Anthony Ngaiza, na Kajubi Mukajanga. Aidha, Dk Samwilu Mwaffisi alitunukiwa Tuzo ya Heshima ya Mafanikio ya Maisha katika Uandishi wa Habari kama ishara ya kuthamini mchango wake wa kudumu na wa kihistoria katika kuijenga na kuisitawisha tasnia ya habari nchini Tanzania.

 MAJINA KAMILI WASHINDI WA EJAT HAYA HAPA

1. Dkt. Maurice Samwilu Mwaffisi - Tuzo ya Mafanikio ya Maisha katika Uandishi wa Habari (LAJA) 2025.

2. Simon Martha Mkina - Pambazuko Online, Mwanahabari Bora wa Mwaka 2025.

3. Simon Martha Mkina - Pambazuko Online, Tuzo ya Habari Bora ya Afya 2025 (Best Health Reporting 2025)

1. Sanula Athanas – Nipashe, Tuzo ya Habari Bora ya Elimu 2025 (Best Education Reporting 2025)

2. Anthony Rwekaza – Watetezi Online TV, Tuzo ya Habari Bora ya Siasa 2025 (Best Political Reporting 2025)

3. Mackriner Siyovelwa – Crown Media,Tuzo ya Habari Bora ya Michezo 2025 (Best Sports Reporting 2025)

4. Devotha Kihwelo - Mwananchi ,Tuzo ya Habari Bora ya Utawala Bora 2025 (Best Good Governance Reporting 2025)

5. Joseph Kirati – The Chanzo, Tuzo ya Picha Bora ya Habari 2025 (Best Photojournalist 2025)

6. Abel Kilumbu – EATV, Tuzo ya Habari Bora ya video, sauti, maandishi na picha (Best Multimedia Reporting 2025)

7. Isack Lukumay - Orkonerei FM, Tuzo ya Maudhui Bora ya Habari za Vijijini 2025 (Best Rural Reporting 2025)

8. Abdallah Kurwa – ITV, Tuzo ya Maudhui Bora ya Televisheni 2025 (Best Television Content 2025)

9. Daniel Samson – Nukta Africa, Tuzo ya Maudhui Bora ya Mtandaoni 2025 (Best Online Content 2025)

10. Esau Ng’umbi – Nukta Africa, Tuzo ya Ufanisi 2025: Mwanahabari Mchanga Bora wa Mwaka (Recognition Award 2025: The Best Youngest Journalist of the Year)

11. Neema Abel – The Guardin, Tuzo ya Ufanisi 2025: Mwanahabari Bora Mwanamke wa Mwaka (Recognition Award 2025: Best Woman Journalist of the Year)

12. Manyerere Jackton – Jamhuri Media, Tuzo ya Ufanisi 2025: Mhariri Bora wa Mwaka (Recognition Award 2025: Outstanding Editor of the Year 2025)

13. Sanula Athanas – Nipashe, Tuzo ya Mwanahabari Mbobevu na Mchambuzi Mahiri 2025 (Most Specialized Journalist of the Year 2025)

14.  Simon Martha Mkina - Pambazuko Online, Tuzo ya Uandishi Bora wa Uchunguzi wa Mwaka 2025 (Best Investigative Reporting 2025)

 TUZO VYOMBO VYA HABARI

 1. Azam Media Ltd - Tuzo ya Chombo cha Habari Binafsi Kinachotii Sheria Zaidi 2025 (Recognition Award 2025: The Most Compliant Private Media House of the Year)

2. Tanzania Standard Newspaper (TSN) - Tuzo ya Chombo cha Habari cha Serikali Kinachotii Sheria Zaidi 2025 (Recognition Award 2025: The Most Compliant Private Media House of the Year)

3. Jamhuri Newspaper - Tuzo ya Mahojiano Bora ya Gazeti 2025 (The Best Print Interview of the Year)

4. Nukta Africa - Tuzo ya Ubobevu na Umahiri wa Uandishi wa Habari za Ugonjwa wa Sikoseli 2025 (The Best Specialized Media House of the Year on Sickle cell reporting)

 

TUZO ZA WASHIRIKA (NCAA, MSI Tanzania na UWEZO Tanzania)

 1. Jamhuri Newspaper - Tuzo ya Uhifadhi ya Julius Nyerere 2025 (Recognition Award 2025: Mwalimu Julius Nyerere Conservation Award).

2. Julius Maricha – The Citizen, Tuzo ya Afya ya Uzazi ya MSI Tanzania (The MSI Tanzania Reproductive Health Reporting Award 2025).

3. Hamad Rashid -The royal Media, Tuzo ya Elimu ya Uwezo Tanzania (The Uwezo Tanzania Education Reporting Award 2025)

 TUZO ZA MAADHIMISHO YA MIAKA 30, YA BARAZA LA HABARI TANZANIA (MCT).

  Waliopata tuzo hii ni -;

 1. Mhe.Jaji Joseph Sinde Warioba

2. Prof. Geoffrey Mmari

3. Prof. Issa G. Shivji

4. Hayati Mhe. Jaji Mstaafu Robert Kisanga

5. Mhe. Jaji Thomas Mihayo

6. Hayati Mhe. Jaji Mstaafu Juxon Isaac Mlay

7. Mhe. Jaji Mstaafu Agusta Bubeshi

8. Ndg. Anthony Ngaiza

9. Ndg. Kajubi Mukajanga


COMMENTS

Name

Anga,12,Arusha,27,batiki,1,Burudani,447,burundani,2,come rain,1,come sun,1,Crazy in Love kama wimbo kama wao wenyewe,1,dahh sijui kweli mbona shida,1,Dar utakuja je tumejiandaa,1,daraja sahau nini,1,demokrasia ya upanga,1,Dodoma,78,Dole tupu vijana wa zamani,1,Duhh bibie endeleza libeneke,1,Duhh kaisikie Walibana,1,duhh kwa mbagala mama lazima awe supa,1,Fedha za maiti haziliwi bure,1,Fedha za watu kwa maendeleo ya watu,1,Fikira,14,filamu,287,Filamu ndio kielelezo cha ukuzi wa taifa,1,flamu,7,Gandamiza Kibara baba ake,1,haba,1,habar,3,Habari,7039,habari dodoma,39,habari. dodoma,32,habaria,1,hadithi,23,hakika tumeweka historia,1,hakuna noma jongwe,1,hapa kwetu inakuwaje vile,1,hasira hasara,1,hata maji,1,hataki masikhara na maisha yake,1,hatubonyezi kizenji,1,haya ndiyo mambo ya Ulaya,1,haya si yangu ni ya mdau mwenye hasira,1,haya wabongo na mambo kutoka nje,1,He he he wananikumbusha upishi wa shaba,1,Headline,1,Hii hurejesha uhai,1,Hii iko sawa kweli?,1,Hii imekaa vizuri,1,Hii inakaaje vile,1,Hii kweli noma,1,Hii maana yake Moro kuna uhaba wa chakula,1,Hii mexico,1,Hii mihasira mingine bwana,1,Hii ndio moro sio mpaka dar,1,hii ni hatari,1,Hii ni kiboko anayetaka kubisha ajibishie tu,1,Hii ni moja ya staili za kunyoa nywele,1,Hii si lukwangule,1,hii staili mpya,1,hili ni jengo pacha la malaysia ghorofa 88,1,Hivi ni ngoma tu,1,hivi nini siri za serikali,1,hivi sisi tunajua kama kuna vitu vya aina hii,1,hivi vitu bwana,1,Hiyo ndiyo gharama ya demokrasia,1,Hizi imani nyingine ni hatari,1,Hizi takwimu hizi mhh,1,Hongera bibie,1,Hongera dada etu kwa kutuletea kaka etu (shemeji) kwani mwenye dada hakosi shemeji,1,Hongera sana,1,huhitaji mifedha kuwa msafi,1,Huko Ulaya,1,Huu ndio ustaarabu,1,huu ujiko utakuwa mkubwa,1,imetosha,1,Inahitaji nidhamu fulani,1,inakuuma au...,1,Inakuwaje kama filamu yenyewe itahitaji busu la nguvu,1,Inaonekana watanzania hatukuwepo,1,Ipo kazi Maximo,1,Iringa,22,Isiwe mijineno tu manake mihela hubadili watu kweli,1,Itakuwa laki moja ya halali,1,jamani huu kama si ushamba kumbe nini,1,Jamani mbona Mungu anatupigania,1,Jamani watoto wanatakiwa kupendwa,1,jamani.. jamani ukiikosa Diamond usijutie,1,Je nyumbani hakuna vitu vya aina hii?Tuambie,1,je walikuwepo watu wa huduma ya kwanza,1,Je watanzania wanalipa kodi,1,jela kwa raha,1,Jolie,1,juhudi za lazima kuinua filamu,1,kama si kiwanda cha chumvi nani atawajua hawa,1,Kama kweli ndio kweli basi kila heri,1,Kama Mkristo naamini hilo hiyo si sahihi,1,kama unajua kuyarudi nenda Malta,1,kama wao wanaweza sisi je,1,Kamua baba waache wakanyagane,1,karibu nyumbani dada yote maisha tu,1,karibu Tatiii,1,KARIBUNI,1,Katavi,5,kaza buti hakuna kukata tamaa inalipa,1,kazi kwako mheshimiwa waziri wa madini,1,kazi na burudani,1,keep it up bloggers,1,kero ya usafiri sasa kwisha,1,Kila chenye roho na mwili kitaonja umauti,1,kila kitu kina vitu,1,Kila la Heri jamila,1,kila la heri kwani ni changamoto,1,Kipya,51,Kiuno bila mfupa,1,Kolelo mzimu ambao bado hai,1,KUBWA,1,Kudumisha urafiki wa dunia,1,Kuna dalili za wasomi kukubali Uafrika,1,kuna makala humu humu ndani ya blogu sijui mnasemaje,1,Kuu,113,kwa mara nyingine tena Tigo imewezesha,1,Kwa mchanganyiko huu muungano lazima udumu,1,Kwa mihasira hajambo,1,kweli,1,Kweli ina mkono mrefu tuone,1,Kweli duniani tunatofautiana,1,la maana ni kuwa na jiko au vipi,1,labda halitabadilika tena,1,lakini mwafaka lazima,1,lengo ni kutafakari,1,leteni vitu tuvione,1,lets us,1,Lucy wanakuelewa hawa...,1,Lukwangule nyumbani kwetu,2,M ungu bariki mikono ya madaktari wafanikiwe,1,MAARUFU,1,maendeleo ya soka siku zote yanahitaji fedha ili yapatikane,1,maisha ni vyema kuyaangalia,1,MAJIBU,1,makala,52,mama ni mama tu anapendeza,1,mambo mengine we angalia tu,1,mambo msimamo,1,mambo sasa mchanganyiko,1,Mara nyingine huona tunakotoka kwa kuona wenzetu,1,Mashabiki wa rhumba mpooooooooo,1,Masitaa,12,Maskani,1,MASOKO,3,Masupa staa mnaoinukia mpoo,1,Matamasha,6,mavazi ya kuogelea yanaposhindaniwa,1,Mbeya,11,Mchakamchaka anti Asmah,1,Mchanganyiko,81,MCHANYATO,1,mchezo,6,mengi wanayoyaita siri ni public information,1,mfumuko wa bei mpaka noma,1,Mhh sijui watu wa Sua ambao wako huko wanasemaje,1,Mhh ugua pole dada watu wanataka burudani,1,Michezo,738,Michezo maalum inatakiwa kupigiwa debe,1,miguu,1,miguu babu,1,Mikataba mingine ama hakika tuiangalie hata wakopeshaji nao wanatugeuza sakala,1,MIMI NI KISURA NAJITAMBUA,1,Mimi sijajua hasa kumetokea nini kwani ninavyojua hawa huwa na ungalizi wa hali ya juu,1,Mimi simo,1,mimi sisemi,1,miochezo,1,mkiwa chumvi basi mkoze,1,Mkiwa taa mulikeni,1,Mnaonaje je hii imekaa vyema,1,Mnaweza wakwetu hapa,1,Morogoro,51,mrithi wa mwanadada Whitney Houston,1,Mtwara,4,Mungu aiweke mahali pema roho yake,4,Mungu amrehemu,1,Mungu amweke pema peponi,1,Mungu awabariki sana,1,Mungu awe nao,1,Mungu ibariki Tanzania,1,Mungu tuepushe na imani hizi za kishirikina,1,mungu tufanye tuwe na upendo,1,Mungu twaomba utuhurumie,1,Muziki,376,muziki na fasheni,20,Mwanahabari,33,Mwanza,6,Mwendo mdundo dada,1,Mwenge huo utakimbizwa duniani kwa siku 130,1,Mwenge wa olimpiki ni ishara ya urafiki,1,Mzee wa Farasi nakupa saluti,1,Mzimbabwe huyu kutoka kwa mama mkali,1,N i dar mpaka Moro au bao tatu bila,1,Na sisi je,1,Naam kama haiwezekani hapa,1,Nairobi waanzisha tena utalii,1,namna bora ya kusaidia jamii,1,nani abebe hukumu na lawama,1,nani asiyejua utamu wa pipi,1,Nani kama baba,1,naona inafaa kuchangia mimi sitoi hoja,1,ndoa za mastaa huwa na mgogoro,1,nenda mwaya nenda,1,New Zanzibar Modern Taarab na wapenzi big up,1,news,5,Ni bikini kwa kwenda mbele,1,Ni Dar mpaka Moro au.. tatu bila,1,ni furaha za muungano,1,Ni kazi ngumu yenye kuhifadhi utamaduni,1,Ni kuchakarika kuonyesha urafiki na biashara pia,1,ni mfumuko wa bei au mfumuko wa nchi,1,Ni muhimu kutazama afya yako,1,ni muziki kwa kwenda mbele,1,Ni muziki mpaka China,1,Ni raha tupu,1,Ni Serengeti Premium Lager,1,Ni Tigo na mawasiliano ya kisasa,1,Ni wakati wa kuujadili utamaduni,1,Ni zaidi ya jazz,1,Nitasubiri and welcome home,1,nje je?,1,NUKUU YA LEO,1,nyie mnasemaje kuhusu hili,1,Ona Kolelo na sindikizwa na Wazee wa Gwasuma,1,ona vya dunia,1,One step ahead,1,patna mwingine mjamzito,1,Pengine anamuogopa Jada Pinkett manake kwa wivu..,1,picha,494,Pole Jamila hayo ndiyo mashindano,1,poleni sana,1,poleni sana wanyalukolo,1,Powa sana,1,Profesa jamaa wanakumaindi,1,Roho za marehemu zipate pumziko la milele,1,Ruvuma,9,sakata dansi mpaka kwenye kilele cha dunia,1,sasa kumebakia ugonjwa mmoja polisi kuendesha mashtaka,1,sasa mifedha kila mahali hongereni,1,Sasa ni mavuno,1,Sasa ni wakati wa kutafuta upenyo ndani ya IDOLS,1,SAYANSI,9,SAYANSI ANGA,12,See Uluguru Montains,1,serikali inataka kujihami kwanini,1,Show of support Big Up Madame,1,Si kitu kidogo hata kidogo,1,si unajua tena namie naimwaga hivyo hivyo,1,Siasa,346,siasa habari,2,Sijui kama City wanajua Mbagala noma,1,Sijui tunaishi karne gani yailahi,1,Sinema,17,sio advencha....kaaa ...niko kibaruani,1,Sisi ndio tunaanza vitongoji,1,Sisi yetu macho na masikio,1,Slow slow jamani,1,sto,1,tabasamu kali la mwenge wa olimpiki,1,Tabora,1,Tazama Waziri Mkuu Pinda wasije wakapindisha maamuzi yako,1,TEKNOLOJIA,1,Thats big man game,1,This is crazy Africa,1,This is Mgeta,1,Tibet wamegeuza Olimpiki jukwaa la siasa,1,Titbits collection,1,Tubadili tamaduni,1,Tuchangie mambo yaive,1,tuendeleze sanaa,1,tuienzi na sisi mbona wizara haituambii,1,Tuipeleke kaskazini,1,Tuisaidie serikali shida ya Mererani,1,tujue namna ya kupumzika,1,Tulienda kustarehe au kufanya fujo,1,Tumsaidie mtototo huyu kurejea katika hali ya kawaida,1,tunahitaji haya,1,Tunajifunza kweli kutoka kwao,1,Tunapandisha chati tu,1,Tunasubiri,1,tunazidi kuhesabu siku,1,TUNAZISUBIRI ZA VINARA ADAR,1,Tuombe nafuu kwa wagonjwa,1,Tuombe rehema kwa mungu,1,Tuone yatufae,1,Tusingoje wengine watusemee,1,tutampa tafu kubwa Prof,1,tuuenzi utamaduni au vipi,1,Tuukuze na kuulinda,1,tuvipende,1,tuwalinde maalbino,1,Tuwe kweli wakweli,1,ubunifu siku zote hulipa,1,uchumi huzunguka kwa kuwawezesha wasukaji,1,udumu muungano,1,Ugonjwa huu wa sasa ni kitendawili,1,Ukiiona kolelo utaipenda,1,Ukirejea salama kila mtu anafurahi,1,Umelenga Mkuchika utamaduni unakufa,1,unaposaka uwakilishi wa dunia,1,urafiki,1,urembo,1,Usisahau wazee wa Ngwasuma,1,UTALII,1,UTAMADUNI,4,Video,2,Vionjo vipya ndani ya Gwasuma,1,Vita dhidi ya ufisadi,1,vitongoji Miss Tanzania navyo vimeanza,1,Vitu vikali vyazidi kuingia Dar,1,Vituko,77,Vituo vya polisi Tanga vyatelekezwa,1,VIVALO,1,Wacha tujifue,2,Wadau ilitolewa kiingereza,1,wakali wa ubunifu,1,wala usibabaike mwakwetu hii noma,1,wanadamu wanapotaka kujua zaidi,1,wanasema mpaka kieleweke,1,Wanataka kujua mali za JK na wengine,1,Wanawake wenye mvuto: Monroe,1,Wapo mabinti wa matawi ya juu,1,watu wanapofanya weli kwenye sanaa,1,waweza kurejea enzi ya Moro jazz na Cuban malimba,1,Wazee tupo kusindikiza,1,waziri,1,welcome dar baby,1,Wenzetu wameona sisi tunangoja nini kuangalia,1,wewe unasemaje,1,wigo mpana wa utamaduni,1,wilaya ya 'Mbagala' mlie tu,1,Yaaani sijui itawezekana,1,Yaani wakati mwingine hata huelewi prioty over priority,1,yeye mbele sisi nyuma,1,Yote maisha dada,1,ZA MOTOMOTO,1,Zanzibar,79,zawadi zinatakiwa ziende shule,1,ZILIZOTIA FORA,1,zitachangia kupunguza makali ya bei za umeme,1,
ltr
item
Lukwangule Entertainment: SIMON MKINA WA PAMBAZUKO ONLINE ATWAA USHINDI WA JUMLA EJAT 2025
SIMON MKINA WA PAMBAZUKO ONLINE ATWAA USHINDI WA JUMLA EJAT 2025
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjGCHSKeuQ8obBsJzY5GQq5pnbD0NI9WF4HOEtgi-0nS1q09629xjN_1XZVw_527o_-urJgrf46vXs5xB1KVzdPgkRr56pe33C2mqT_8EdO1c87gTYxy95FYK_rcFean3Q1_cJLWQ5GqUpCfIHvpEqgOE1TLMQFdmPDyKzRXkX9XUILC-0jR38bOicVSj_-/s320/mkina1.jfif
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjGCHSKeuQ8obBsJzY5GQq5pnbD0NI9WF4HOEtgi-0nS1q09629xjN_1XZVw_527o_-urJgrf46vXs5xB1KVzdPgkRr56pe33C2mqT_8EdO1c87gTYxy95FYK_rcFean3Q1_cJLWQ5GqUpCfIHvpEqgOE1TLMQFdmPDyKzRXkX9XUILC-0jR38bOicVSj_-/s72-c/mkina1.jfif
Lukwangule Entertainment
https://lukwangule.blogspot.com/2026/05/simon-mkina-wa-pambazuko-online-atwaa.html
https://lukwangule.blogspot.com/
http://lukwangule.blogspot.com/
http://lukwangule.blogspot.com/2026/05/simon-mkina-wa-pambazuko-online-atwaa.html
true
934549962738256429
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy