MAKAMU WA RAIS ATOA MIEZI SITA KWA WIZARA YA BIASHARA KUJA NA SERA MAHUSUSI KWA STARTUPS

Makamu wa Rais, Mhe. Deogratius Ndejembi, ametoa miezi sita kwa Wizara ya Viwanda na Biashara kuandaa Sera mahususi ya biashara bunifu (st...




Makamu wa Rais, Mhe. Deogratius Ndejembi, ametoa miezi sita kwa Wizara ya Viwanda na Biashara kuandaa Sera mahususi ya biashara bunifu (startups), itakayosaidia vijana na wafanyabiashara kupata mitaji na hivyo kuongeza na kupanua  wigo wa ubunifu na biashara nchini ikiwa ni mkakati wa kuchochea ajira na kujenga uchumi unaotegemea maarifa na teknolojia kuelekea Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.

 Akifungua Wiki ya Biashara Bunifu (Startups Week) leo, Oktoba 19, 2026, katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC), Dar es Salaam, Ndejembi amesema Serikali inatambua mchango wa biashara bunifu katika kukuza uchumi na kuzalisha ajira, hivyo imejipanga kuweka mazingira yatakayowezesha mawazo ya vijana kukua na kuwa biashara kubwa zenye uwezo wa kuvutia uwekezaji na kushindana katika masoko ya ndani na nje.

 Amesema sera hiyo itazingatia mahitaji ya kipekee ya biashara bunifu, ambazo zina uwezo wa kukua kwa kasi na kuvutia uwekezaji mkubwa, tofauti na biashara ndogo na za kati (SMEs), huku akisisitiza umuhimu wa taasisi za fedha kuweka mifumo ya upatikanaji wa mitaji badala ya kutegemea mikopo pekee.

 Katika hatua hiyo, ameitaja Benki ya NMB kuwa miongoni mwa taasisi zilizoanza kuwezesha biashara bunifu, huku akieleza kuwa Serikali itaendelea kufungua fursa za masoko kupitia utaratibu wa kutenga asilimia 30 ya manunuzi ya umma kwa makundi maalumu na fedha za uwezeshaji zinazofikia Sh bilioni 200, ambazo vijana wenye biashara bunifu wanaweza kunufaika nazo.

 




Katika kuondoa changamoto za mazingira ya kufanyia kazi, Makamu wa Rais  ameielekeza Wizara ya Viwanda na Biashara kwa kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu kuanzisha kituo cha pamoja cha ubunifu (innovation centre), itakayowezesha  vijana kukutana, kubadilishana mawazo na kuunganishwa na wawekezaji wakubwa wa ndani na nje zikiwemo  Taasisi za fedha. Amesema ushirikiano na benki, kampuni za mawasiliano na wadau wengine unaweza kuwezesha upatikanaji wa maeneo ya kazi na huduma muhimu, ikiwemo intaneti ya bure, huku akisisitiza Chama cha Biashara Bunifu Tanzania kushirikishwa kikamilifu katika maandalizi ya sera hiyo.

 Aidha, Ndejembi amesema Tanzania ina fursa kubwa ya kukuza biashara bunifu kutokana na matumizi yanayoongezeka ya teknolojia na ukubwa wa soko la ndani na Afrika, akitaja takribani usajili milioni 120 wa simu nchini na watumiaji hai milioni 60, ambao asilimia kubwa wanatumia simu janja. Amewataja vijana Alvin na Ramadhan waliofanikiwa kuanzisha biashara bunifu na sasa ni Kampuni zenye mitaji mikubwa kama mifano ya uwezo wa Watanzania kutumia ubunifu kutengeneza fursa za kiuchumi, akisisitiza kuwa mazingira bora ya sera, mitaji na masoko yatawezesha biashara bunifu kuongeza mchango wake katika ajira na ukuaji wa uchumi kuelekea mwaka 2050.

 Akichangia mjadala katika ufunguzi wa wiki hiyo, Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Judith Kapinga, amesema Wizara hiyo si polisi wala mgambo wa kufunga biashara, bali jukumu lake ni kuhamasisha, kulea na kukuza biashara pamoja na mawazo bunifu ya Watanzania. Amesema kwa kushirikiana na sekta nyingine, Wizara itaendelea kuhakikisha hakuna biashara inayofungwa bila sababu za msingi za kisheria, isipokuwa zile zinazokiuka au kuendeshwa kinyume na sheria za nchi, akisisitiza kuwa dhamira ya Serikali ni kujenga mazingira yanayochochea ukuaji wa biashara badala ya kuzikwamisha.

 Kapinga amesema Wizara itaendelea kuhamasisha wananchi, hususan vijana, kubadili mitazamo na mienendo katika kufanya biashara, huku ikiimarisha ushirikiano na sekta binafsi kuhakikisha sera na sheria zinaendana na mabadiliko ya teknolojia na mahitaji ya biashara bunifu. Ameahidi kuwa kupitia Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade), Wizara itaendelea kuboresha mazingira ya biashara, kutangaza bidhaa na ubunifu wa Watanzania nje ya nchi na kuwezesha biashara bunifu kupenya katika masoko ya ndani na kimataifa.

Akitoa salamu za Mkoa wa Dar es Salaam, Mkuu wa Mkoa huo, Mhe. Albert Chalamila, amesema Dar es Salaam ni miongoni mwa wanufaika na wadau wakubwa wa biashara bunifu nchini, hivyo Mkoa utaendelea kuunga mkono jitihada za kukuza sekta hiyo kama sehemu ya kupanua fursa za kiuchumi na kuongeza ajira kwa vijana. Amesema Mkoa utaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali kuimarisha mazingira yanayochochea ubunifu na ukuaji wa biashara, ili kuwawezesha vijana kutumia maarifa na vipaji vyao kujiajiri, kuzalisha ajira na kuchangia maendeleo ya uchumi wa Mkoa na Taifa kwa ujumla.

 Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi ya Chama cha Biashara Bunifu Tanzania (Tanzania Startup Association), Bw. Paul Makanza, amesema chama hicho kilichoanzishwa mwaka 2020 kimeendelea kuwa kiungo muhimu katika kukuza biashara bunifu kupitia ushawishi, utafiti na ushiriki katika uandaaji wa sera zinazolenga kuboresha mazingira ya biashara nchini, hususan kwa vijana. Amesema chama hicho kimefanikiwa kuandaa ripoti ya mfumo wa biashara bunifu nchini (Startup Ecosystem Report), inayobainisha fursa na changamoto za sekta hiyo pamoja na namna inavyoweza kuchangia utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.

 Makanza amesema juhudi za chama hicho na wadau wake zimechangia kuzalishwa kwa takribani ajira 20,000 kupitia biashara bunifu, hatua inayoonyesha uwezo wa sekta hiyo kuwa kichocheo cha ukuaji wa uchumi na ajira kwa vijana. Hata hivyo, amesema changamoto ya upatikanaji wa mitaji na masoko bado inakwamisha ukuaji wa biashara nyingi bunifu, hivyo kusisitiza umuhimu wa kuimarisha ushirikiano kati ya Serikali, sekta binafsi na wadau wa ubunifu ili kuwezesha biashara hizo kukua na kuongeza mchango wake katika uchumi wa Taifa.

 Kabla ya kushiriki mjadala kuhusu biashara bunifu, Makamu wa Rais alitembelea mabanda ya maonesho ya wabunifu na wawekezaji, wakiwemo wadhamini wakuu wa tukio hilo, Benki ya NMB, ambayo hadi sasa imefanikiwa kufadhili biashara bunifu sita zilizoingia katika mfumo wa benki hiyo, huku nyingine tano zikiwa katika hatua za mwisho za uwezeshaji. Hata hivyo, changamoto ya upatikanaji wa dhamana kwa mikopo mikubwa imeendelea kuwa kikwazo kwa biashara bunifu zinazohitaji mitaji zaidi ili kupanua shughuli zake na kuongeza mchango wake katika uchumi wa Taifa. ‎

 


COMMENTS

Name

Anga,12,Arusha,27,batiki,1,Burudani,476,burundani,2,come rain,1,come sun,1,Crazy in Love kama wimbo kama wao wenyewe,1,dahh sijui kweli mbona shida,1,Dar utakuja je tumejiandaa,1,daraja sahau nini,1,demokrasia ya upanga,1,Dodoma,78,Dole tupu vijana wa zamani,1,Duhh bibie endeleza libeneke,1,Duhh kaisikie Walibana,1,duhh kwa mbagala mama lazima awe supa,1,Fedha za maiti haziliwi bure,1,Fedha za watu kwa maendeleo ya watu,1,Fikira,14,filamu,320,Filamu ndio kielelezo cha ukuzi wa taifa,1,flamu,7,Gandamiza Kibara baba ake,1,haba,1,habar,3,Habari,7749,habari dodoma,41,habari. dodoma,32,habaria,1,hadithi,27,hakika tumeweka historia,1,hakuna noma jongwe,1,hapa kwetu inakuwaje vile,1,hasira hasara,1,hata maji,1,hataki masikhara na maisha yake,1,hatubonyezi kizenji,1,haya ndiyo mambo ya Ulaya,1,haya si yangu ni ya mdau mwenye hasira,1,haya wabongo na mambo kutoka nje,1,He he he wananikumbusha upishi wa shaba,1,Headline,1,Hii hurejesha uhai,1,Hii iko sawa kweli?,1,Hii imekaa vizuri,1,Hii inakaaje vile,1,Hii kweli noma,1,Hii maana yake Moro kuna uhaba wa chakula,1,Hii mexico,1,Hii mihasira mingine bwana,1,Hii ndio moro sio mpaka dar,1,hii ni hatari,1,Hii ni kiboko anayetaka kubisha ajibishie tu,1,Hii ni moja ya staili za kunyoa nywele,1,Hii si lukwangule,1,hii staili mpya,1,hili ni jengo pacha la malaysia ghorofa 88,1,Hivi ni ngoma tu,1,hivi nini siri za serikali,1,hivi sisi tunajua kama kuna vitu vya aina hii,1,hivi vitu bwana,1,Hiyo ndiyo gharama ya demokrasia,1,Hizi imani nyingine ni hatari,1,Hizi takwimu hizi mhh,1,Hongera bibie,1,Hongera dada etu kwa kutuletea kaka etu (shemeji) kwani mwenye dada hakosi shemeji,1,Hongera sana,1,huhitaji mifedha kuwa msafi,1,Huko Ulaya,1,Huu ndio ustaarabu,1,huu ujiko utakuwa mkubwa,1,imetosha,1,Inahitaji nidhamu fulani,1,inakuuma au...,1,Inakuwaje kama filamu yenyewe itahitaji busu la nguvu,1,Inaonekana watanzania hatukuwepo,1,Ipo kazi Maximo,1,Iringa,22,Isiwe mijineno tu manake mihela hubadili watu kweli,1,Itakuwa laki moja ya halali,1,jamani huu kama si ushamba kumbe nini,1,Jamani mbona Mungu anatupigania,1,Jamani watoto wanatakiwa kupendwa,1,jamani.. jamani ukiikosa Diamond usijutie,1,Je nyumbani hakuna vitu vya aina hii?Tuambie,1,je walikuwepo watu wa huduma ya kwanza,1,Je watanzania wanalipa kodi,1,jela kwa raha,1,Jolie,1,juhudi za lazima kuinua filamu,1,kama si kiwanda cha chumvi nani atawajua hawa,1,Kama kweli ndio kweli basi kila heri,1,Kama Mkristo naamini hilo hiyo si sahihi,1,kama unajua kuyarudi nenda Malta,1,kama wao wanaweza sisi je,1,Kamua baba waache wakanyagane,1,karibu nyumbani dada yote maisha tu,1,karibu Tatiii,1,KARIBUNI,1,Katavi,5,kaza buti hakuna kukata tamaa inalipa,1,kazi kwako mheshimiwa waziri wa madini,1,kazi na burudani,1,keep it up bloggers,1,kero ya usafiri sasa kwisha,1,Kila chenye roho na mwili kitaonja umauti,1,kila kitu kina vitu,1,Kila la Heri jamila,1,kila la heri kwani ni changamoto,1,Kipya,51,Kiuno bila mfupa,1,Kolelo mzimu ambao bado hai,1,KUBWA,1,Kudumisha urafiki wa dunia,1,Kuna dalili za wasomi kukubali Uafrika,1,kuna makala humu humu ndani ya blogu sijui mnasemaje,1,Kuu,113,kwa mara nyingine tena Tigo imewezesha,1,Kwa mchanganyiko huu muungano lazima udumu,1,Kwa mihasira hajambo,1,kweli,1,Kweli ina mkono mrefu tuone,1,Kweli duniani tunatofautiana,1,la maana ni kuwa na jiko au vipi,1,labda halitabadilika tena,1,lakini mwafaka lazima,1,lengo ni kutafakari,1,leteni vitu tuvione,1,lets us,1,Lucy wanakuelewa hawa...,1,Lukwangule nyumbani kwetu,2,M ungu bariki mikono ya madaktari wafanikiwe,1,MAARUFU,1,maendeleo ya soka siku zote yanahitaji fedha ili yapatikane,1,maisha ni vyema kuyaangalia,1,MAJIBU,1,makala,52,mama ni mama tu anapendeza,1,mambo mengine we angalia tu,1,mambo msimamo,1,mambo sasa mchanganyiko,1,Mara nyingine huona tunakotoka kwa kuona wenzetu,1,Mashabiki wa rhumba mpooooooooo,1,Masitaa,12,Maskani,1,MASOKO,3,Masupa staa mnaoinukia mpoo,1,Matamasha,6,mavazi ya kuogelea yanaposhindaniwa,1,Mbeya,11,Mchakamchaka anti Asmah,1,Mchanganyiko,81,MCHANYATO,1,mchezo,7,mengi wanayoyaita siri ni public information,1,mfumuko wa bei mpaka noma,1,Mhh sijui watu wa Sua ambao wako huko wanasemaje,1,Mhh ugua pole dada watu wanataka burudani,1,Michezo,778,Michezo maalum inatakiwa kupigiwa debe,1,miguu,1,miguu babu,1,Mikataba mingine ama hakika tuiangalie hata wakopeshaji nao wanatugeuza sakala,1,MIMI NI KISURA NAJITAMBUA,1,Mimi sijajua hasa kumetokea nini kwani ninavyojua hawa huwa na ungalizi wa hali ya juu,1,Mimi simo,1,mimi sisemi,1,miochezo,1,mkiwa chumvi basi mkoze,1,Mkiwa taa mulikeni,1,Mnaonaje je hii imekaa vyema,1,Mnaweza wakwetu hapa,1,Morogoro,51,mrithi wa mwanadada Whitney Houston,1,Mtwara,4,Mungu aiweke mahali pema roho yake,4,Mungu amrehemu,1,Mungu amweke pema peponi,1,Mungu awabariki sana,1,Mungu awe nao,1,Mungu ibariki Tanzania,1,Mungu tuepushe na imani hizi za kishirikina,1,mungu tufanye tuwe na upendo,1,Mungu twaomba utuhurumie,1,Muziki,376,muziki na fasheni,21,Mwanahabari,33,Mwanza,6,Mwendo mdundo dada,1,Mwenge huo utakimbizwa duniani kwa siku 130,1,Mwenge wa olimpiki ni ishara ya urafiki,1,Mzee wa Farasi nakupa saluti,1,Mzimbabwe huyu kutoka kwa mama mkali,1,N i dar mpaka Moro au bao tatu bila,1,Na sisi je,1,Naam kama haiwezekani hapa,1,Nairobi waanzisha tena utalii,1,namna bora ya kusaidia jamii,1,nani abebe hukumu na lawama,1,nani asiyejua utamu wa pipi,1,Nani kama baba,1,naona inafaa kuchangia mimi sitoi hoja,1,ndoa za mastaa huwa na mgogoro,1,nenda mwaya nenda,1,New Zanzibar Modern Taarab na wapenzi big up,1,news,5,Ni bikini kwa kwenda mbele,1,Ni Dar mpaka Moro au.. tatu bila,1,ni furaha za muungano,1,Ni kazi ngumu yenye kuhifadhi utamaduni,1,Ni kuchakarika kuonyesha urafiki na biashara pia,1,ni mfumuko wa bei au mfumuko wa nchi,1,Ni muhimu kutazama afya yako,1,ni muziki kwa kwenda mbele,1,Ni muziki mpaka China,1,Ni raha tupu,1,Ni Serengeti Premium Lager,1,Ni Tigo na mawasiliano ya kisasa,1,Ni wakati wa kuujadili utamaduni,1,Ni zaidi ya jazz,1,Nitasubiri and welcome home,1,nje je?,1,NUKUU YA LEO,1,nyie mnasemaje kuhusu hili,1,Ona Kolelo na sindikizwa na Wazee wa Gwasuma,1,ona vya dunia,1,One step ahead,1,patna mwingine mjamzito,1,Pengine anamuogopa Jada Pinkett manake kwa wivu..,1,picha,494,Pole Jamila hayo ndiyo mashindano,1,poleni sana,1,poleni sana wanyalukolo,1,Powa sana,1,Profesa jamaa wanakumaindi,1,Roho za marehemu zipate pumziko la milele,1,Ruvuma,9,sakata dansi mpaka kwenye kilele cha dunia,1,sasa kumebakia ugonjwa mmoja polisi kuendesha mashtaka,1,sasa mifedha kila mahali hongereni,1,Sasa ni mavuno,1,Sasa ni wakati wa kutafuta upenyo ndani ya IDOLS,1,SAYANSI,10,SAYANSI ANGA,16,See Uluguru Montains,1,serikali inataka kujihami kwanini,1,Show of support Big Up Madame,1,Si kitu kidogo hata kidogo,1,si unajua tena namie naimwaga hivyo hivyo,1,Siasa,346,siasa habari,2,Sijui kama City wanajua Mbagala noma,1,Sijui tunaishi karne gani yailahi,1,Sinema,17,sio advencha....kaaa ...niko kibaruani,1,Sisi ndio tunaanza vitongoji,1,Sisi yetu macho na masikio,1,Slow slow jamani,1,sto,1,tabasamu kali la mwenge wa olimpiki,1,Tabora,1,Tazama Waziri Mkuu Pinda wasije wakapindisha maamuzi yako,1,TEKNOLOJIA,1,Thats big man game,1,This is crazy Africa,1,This is Mgeta,1,Tibet wamegeuza Olimpiki jukwaa la siasa,1,Titbits collection,1,Tubadili tamaduni,1,Tuchangie mambo yaive,1,tuendeleze sanaa,1,tuienzi na sisi mbona wizara haituambii,1,Tuipeleke kaskazini,1,Tuisaidie serikali shida ya Mererani,1,tujue namna ya kupumzika,1,Tulienda kustarehe au kufanya fujo,1,Tumsaidie mtototo huyu kurejea katika hali ya kawaida,1,tunahitaji haya,1,Tunajifunza kweli kutoka kwao,1,Tunapandisha chati tu,1,Tunasubiri,1,tunazidi kuhesabu siku,1,TUNAZISUBIRI ZA VINARA ADAR,1,Tuombe nafuu kwa wagonjwa,1,Tuombe rehema kwa mungu,1,Tuone yatufae,1,Tusingoje wengine watusemee,1,tutampa tafu kubwa Prof,1,tuuenzi utamaduni au vipi,1,Tuukuze na kuulinda,1,tuvipende,1,tuwalinde maalbino,1,Tuwe kweli wakweli,1,ubunifu siku zote hulipa,1,uchumi huzunguka kwa kuwawezesha wasukaji,1,udumu muungano,1,Ugonjwa huu wa sasa ni kitendawili,1,Ukiiona kolelo utaipenda,1,Ukirejea salama kila mtu anafurahi,1,Umelenga Mkuchika utamaduni unakufa,1,unaposaka uwakilishi wa dunia,1,urafiki,1,urembo,1,Usisahau wazee wa Ngwasuma,1,UTALII,1,UTAMADUNI,4,Video,2,Vionjo vipya ndani ya Gwasuma,1,Vita dhidi ya ufisadi,1,vitongoji Miss Tanzania navyo vimeanza,1,Vitu vikali vyazidi kuingia Dar,1,Vituko,77,Vituo vya polisi Tanga vyatelekezwa,1,VIVALO,1,Wacha tujifue,2,Wadau ilitolewa kiingereza,1,wakali wa ubunifu,1,wala usibabaike mwakwetu hii noma,1,wanadamu wanapotaka kujua zaidi,1,wanasema mpaka kieleweke,1,Wanataka kujua mali za JK na wengine,1,Wanawake wenye mvuto: Monroe,1,Wapo mabinti wa matawi ya juu,1,watu wanapofanya weli kwenye sanaa,1,waweza kurejea enzi ya Moro jazz na Cuban malimba,1,Wazee tupo kusindikiza,1,waziri,1,welcome dar baby,1,Wenzetu wameona sisi tunangoja nini kuangalia,1,wewe unasemaje,1,wigo mpana wa utamaduni,1,wilaya ya 'Mbagala' mlie tu,1,Yaaani sijui itawezekana,1,Yaani wakati mwingine hata huelewi prioty over priority,1,yeye mbele sisi nyuma,1,Yote maisha dada,1,ZA MOTOMOTO,1,Zanzibar,79,zawadi zinatakiwa ziende shule,1,ZILIZOTIA FORA,1,zitachangia kupunguza makali ya bei za umeme,1,
ltr
item
Lukwangule Entertainment: MAKAMU WA RAIS ATOA MIEZI SITA KWA WIZARA YA BIASHARA KUJA NA SERA MAHUSUSI KWA STARTUPS
MAKAMU WA RAIS ATOA MIEZI SITA KWA WIZARA YA BIASHARA KUJA NA SERA MAHUSUSI KWA STARTUPS
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiPXnmhK8yeGGLiONfpT5konszBzw6O0eb3KkGEw2mJ3cVud-knLST2aHxQrU9s77npKm60yjIGcCHj8xZkUd6qMz92HaWt9UETmlt60-0s0pL-GcnqYyRRS0q0kYQf_04WI66jylbkO2Q7PokWats8P8esfxB-mhhbI_Uq2awQscAeZ2FTKq8zSq_RjJ77/s320/A00005.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiPXnmhK8yeGGLiONfpT5konszBzw6O0eb3KkGEw2mJ3cVud-knLST2aHxQrU9s77npKm60yjIGcCHj8xZkUd6qMz92HaWt9UETmlt60-0s0pL-GcnqYyRRS0q0kYQf_04WI66jylbkO2Q7PokWats8P8esfxB-mhhbI_Uq2awQscAeZ2FTKq8zSq_RjJ77/s72-c/A00005.JPG
Lukwangule Entertainment
https://lukwangule.blogspot.com/2026/10/makamu-wa-rais-atoa-miezi-sita-kwa.html
https://lukwangule.blogspot.com/
http://lukwangule.blogspot.com/
http://lukwangule.blogspot.com/2026/10/makamu-wa-rais-atoa-miezi-sita-kwa.html
true
934549962738256429
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy