MASWALI NA MAJIBU YA SERIKALI BUNGENI OKT 30: TEKNOLOJIA, ELIMU NA AFYA

    KUIMARISHA SEKTA YA AFYA - GEITA MJINI MHESHIMIWA ENG. CHACHA MWITA WAMBURA (GEITA MJINI) Atauliza:- Je, Serikali ina mpango gan...

 



 

KUIMARISHA SEKTA YA AFYA - GEITA MJINI

MHESHIMIWA ENG. CHACHA MWITA WAMBURA (GEITA MJINI) Atauliza:-

Je, Serikali ina mpango gani wa kuimarisha sekta ya Afya kwa kuongeza Vituo vya Afya, Madaktari, Wauguzi na Vifaa tiba - Geita Mjini.

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU (TAMISEMI) Atajibu:-

Mheshimiwa Spika, Serikali imeendeleta kuimalisha huduma za afya hususani Ngazi ya Afya ya Msingi kwa kujenga/kukarabati miundombinu ya afya, kuajiri watumishi wa Kada za Afya pamoja na kutenga fedha kwa ajili ya ununuzi wa dawa na Vifaa Tiba.

Mheshimiwa Spika, Katika mwaka wa fedha 2024/25 na 2025/26 Serikali imeajiri jumla ya watumishi wa Kada ya Afya 11,198 ambapo watumishi wa Kada ya Uuguzi walioajiriwa walikuwa 6,450 na Halmashauri ya Mji wa Geita ilipangiwa jumla ya watumishi wa afya 109.

Mheshimiwa Spika, Katika mwaka wa fedha 2026/27 Serikali imetenga shilingi bilioni 56.25 kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa Hospitali na shilingi bilioni 23.37 kwa ajili ya ukamilishaji wa vituo vya afya 111 kote nchini. Aidha, halmashauri ya Mji wa Geita imetengewa shilingi milioni 170 kwa ajili ya ukamilishaji wa vituo vya Afya.

Mheshimiwa Spika, Kwa mwaka wa fedha 2026/27 Serikali imetenga jumla ya shilingi bilioni 405 kwa ajili ya ununuzi wa dawa na vifaa tiba, ambapo Mkoa wa Geita umetengewa shilingi bilioni 7.28 na Manispaa ya Geita imetengewa kiasi cha shilingi bilioni 1.09.

UHITAJI WA WODI YA WATOTO KITUO CHA AFYA CHA MJIMWEMA SONGEA

MHESHIMIWA MARIAMU MADALU NYOKA (VITI MAALUM) Atauliza:-

Je, lini Serikali itajenga Wodi ya Watoto katika Kituo cha Afya cha Mjimwema kilichopo Manispaa ya Songea.

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU (TAMISEMI) Atajibu:-

Mheshimiwa Spika, Kituo cha Afya Mjimwema kimejengwa mwaka 2001. Kituo hiki kinaupungufu wa miundombinu ya jengo la Maabara, jengo la Mionzi, wodi za kulaza wagonjwa na wodi ya wazazi.

Mheshimiwa Spika, Kituo cha Afya Mjimwema ni miongoni mwa vituo vya afya Kongwe 358 vilivyofanyiwa tathmini ambavyo vinahitaji kufanyiwa ukarabati pamoja na kuongezewa miundombinu ya msingi ili viweze kutoa huduma stahiki ngazi ya Kituo cha Afya.

Mheshimiwa Spika, Serikali inaendelea kutenga bajeti kwa ajili ya ukarabati wa vituo vya afya Kongwe kote Nchini ambapo jumla ya shilingi bilioni 164.86 zinahitajika. Aidha, katika mwaka wa fedha 2026/27 Serikali kupitia fedha za mapato ya ndani ya Halmashauri ya Manispaa ya Songea imetenga shilingi milioni 31 kwa ajili ya ujenzi wa Jengo la maabara katika Kituo cha afya Mjimwema.

UHITAJI WA KIDATO CHA TANO NA SITA SHULE YA SEKONDARI NGARA MJINI

MHESHIMIWA DOTTO JASSON BAHEMU (NGARA) Atauliza:-

Je, lini Serikali itaanzisha Kidato cha Tano na Sita katika Shule ya Sekondari Ngara Mjini.

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU (TAMISEMI) Atajibu:-

Mheshimiwa Spika, Serikali imekuwa ikijenga shule mpya za kidato cha tano na sita au kuongeza miundombinu katika shule za sekondari zilizopo ili kuzipandisha hadhi kupokea wanafunzi wa kidato cha tano na sita.

Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha Mwaka wa fedha 2024/25 - 2025/26, Serikali imepeleka shilingi bilioni 2.08 katika halmashauri ya Ngara kwa ajili ya kuongeza miundombinu katika shule saba za sekondari za Rusumo, Kabanga, Lukole, Muyenzi, Murugamba, Ndomba na Ngara High School na kuzipandisha hadhi ambapo kwa sasa zina jumla ya wanafunzi 6,881 wa kidato cha tano na sita.

Mheshimiwa Spika, kwa sasa shule ya Sekondari Ngara Mjini haina mahitaji makubwa ya kupokea wanafunzi wa kidato cha tano na sita. Shule ya Sekondari Ngara Mjini ipo tarafa ya Nyamiaga yenye shule za tatu za Kidato cha Tano na Sita (Rusumo, Lukole na Ngara High) zenye jumla ya wanafunzi 2,915. Aidha, Serikali itaendelea kutenga fedha za ujenzi wa miundombinu ya kupokea wanafunzi wa kidato cha tano na sita kwa kuzingatia tathmini ya mahitaji.

UJENZI WA SOKO LA KISASA HALMASHAURI YA MJI WA MBULU

MHESHIMIWA YUSTINA ARCADIUS RAHHI (VITI MAALUM) Atauliza:-

Je, lini Serikali itajenga Soko la Kisasa katika Halmashauri ya Mji wa Mbulu.

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU (TAMISEMI) Atajibu:-

Mheshimiwa Spika, Serikali inatambua umuhimu wa kuwa na soko la kisasa katika Mji wa Mbulu. Kwa kuzingatia umuhimu huo, mrati huu ni miongoni mwa miradi inayotarajiwa kutekelezwa kupitia mradi wa uoreshaji wa miundombinu ya Mji na Halmashauri nchini (TACTIC) awamu ya tatu.

Mheshimiwa Spika, Hatua zilizofiwa katika utekelezaji wa mradi huu ni pamoja na , Halmashauri ya Mji wa Mbulu kutenga eneo la ujenzi na taratibu zote za umiliki wa ardhi kwa ajili ya mradi huo. Aidha, tayari upembuzi yakinifu, usanifu wa kina wa majengo na gharama za mradi zimejulikana.

Mheshimiwa Spika, Serikali itaanza ujenzi pindi taratibu za kibajeti zitakapo kamilika na Zabuni kutangazwa kuwapata wakandarasi na Washauri elekezi.

UJENZI WA BARABARA YA MUGOMBE-KAGERANKANDA

MHESHIMIWA EDIBILY KINYOMA KAZALA (KASULU VIJIJINI) Atauliza:-

Je, lini Serikali itaanza ujenzi wa Barabara ya Mugombe-Kagerankanda,ambayo ni ahadi za Mheshimiwa Rais.

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU-TAMISEMI Atajibu:-

Mheshimiwa Spika, Katika mwaka wa fedha 2026/2027, Serikali imetenga kiasi cha shilingi Milioni 89.4 kwa ajili kufanya matengenezo ya kawaida na usanifu wa ujenzi wa barabara ya Mugombe-Kagerankanda kilomita 37 ili kupata gharama halisi za ujenzi wake ambapo baada ya kubaini gharama hizo, Serikali itatafuta fedha kwa ajili ya kutekeleza kazi hiyo.

Mheshimiwa Spika, Aidha katika mwaka wa fedha 2025/2026 barabara hiyo ilifanyiwa matengenezo ya urefu wa kilomita 19 kwa kiwango cha changarawe kwa gharama ya Shilingi milioni 534.26.

Mheshimiwa Spika, Serikali itaendelea kuiboresha Barabara hii kwa tabaka la changarawe ili iweze kupitika misimu yote wakati maandalizi ya usanifu wa barabara hiyo yakiendelea.

UKUZAJI WA SEKTA BINAFSI ILI KUONGEZA AJIRA

MHESHIMIWA DKT. REGINA CHRISTOPHER MALIMA (VITI MAALUM) Atauliza:-

Je, Serikali inajipangeje kuhakikisha inaimarisha mazingira ya uzalishaji na ukuaji wa sekta binafsi inayobeba ajira nyingi kwa vijana.

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS (MIPANGO NA UWEKEZAJI) Atajibu:-

Mheshimiwa Spika, Serikali inatambua umuhimu wa sekta binafsi katika kuongeza uzalishaji, uwekezaji na ajira kwa vijana. Katika kutekeleza Dira 2050, Serikali imeandaa Mkakati wa Taifa wa Kuimarisha Mazingira ya Biashara na Uwekezaji (MKUMBI II), unaolenga kupunguza gharama za kufanya biashara, kurahisisha taratibu za uwekezaji na kuimarisha mazingira ya uzalishaji na utoaji wa huduma. Pia Serikali imesaini azimio la pamoja ya Sekta Binafsi na Sekta ya Umma la 2026.

Mheshimiwa Spika, Tathmini ya Utekelezaji wa MKUMBI I ya mwaka 2024, Tathmini ya Sekta Binafsi ya mwaka 2024 na Taarifa ya Hali ya Sekta Binafsi Tanzania ya mwaka 2026 zimebainisha mwenendo, changamoto na fursa za sekta binafsi nchini. Kwa kuzingatia matokeo na mapendekezo ya taarifa hizo, Serikali imeanza maandalizi ya kuandaa Sheria ya Maendeleo ya Sekta Binafsi, inayoleta kuimarisha uratibu wa taasisi za sekta binafsi, ushirikiano kati ya Serikali na sekta binafsi, pamoja na utawala bora ndani ya taasisi za sekta binafsi. Aidha, itaweka mfumo wa kushughulikia changamoto zinazoathiri uzalishaji, uwekezaji na ukuaji wa biashara kuanzia ngazi ya Kitaifa hadi mamlaka za Serikali za Mitaa.

Mheshimiwa Spika, Serikali pia inaendelea kuimarisha majukwaa ya majadiliano na sekta binafsi pamoja na Idara za Viwanda, Biashara na Uwekezaji katika ngazi za mikoa na wilaya. Aidha, imeandaa Kipimo cha Ushindani wa Mamlaka za Serikali za Mitaa kuboresha Mazingira ya Biashara na Uwekezaji (LGA Business and Investment Competitiveness Index) ili kuchochea utoaji huduma kwa wafanyabiashara na wawekezaji. Hatua hizi zinalenga kuongeza uzalishaji, ushindani wa biashara za ndani na uwekezaji unaopanua fursa za ujasiriamali na ajira zenye tija kwa vijana.

KUWEZESHA VIJANA NCHINI

MHESHIMIWA LATIFA KHAMIS JUWAKALI (VITI MAALUM) Atauliza:-

Je, Serikali haioni haja ya kuweka 4% au 10% kwa kila Wizara ya Kisekta kwa ajili ya kuwawezesha Vijana.

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS – MAENDELEO YA VIJANA Atajibu:

Mheshimiwa Spika, Serikali inatambua kuwa uwezeshaji wa vijana ni jukumu mtambuka linalohitaji ushiriki wa Wizara zote za Kisekta kulingana na majukumu na fursa zilizopo katika sekta husika. Katika mwaka wa fedha 2025/26, Serikali kupitia Wizara mbalimbali imetumia kiasi cha Shilingi bilioni 966.8 kwa ajili ya programu na shughuli za uwezeshaji vijana, zilizowafikia vijana 6,933,835. Aidha, katika mwaka wa fedha 2026/27, Serikali imepanga kutumia takriban Shilingi trilioni 1.853 kwa ajili ya kuwawezesha vijana 18,644,433. Hatua hizi zinaonesha dhamira ya Serikali ya kuendelea kutenga rasilimali kwa ajili ya maendeleo na uwezeshaji vijana kupitia sekta mbalimbali.

Mheshimiwa Spika, Serikali inapokea pendekezo la kutenga asilimia nne (4%) au kumi (10%) ya bajeti ya kila Wizara ya Kisekta kwa ajili ya uwezeshaji vijana, na italitathmini katika muktadha wa maandalizi ya mipango na bajeti za Serikali, kwa kuzingatia vipaumbele vya kitaifa, majukumu ya kisekta na upatikanaji wa rasilimali. Lengo ni kuhakikisha vijana wanapata fursa stahiki na kunufaika na programu za Serikali kwa kuzingatia vigezo na taratibu zilizowekwa.

KUCHOCHEA MAPINDUZI YA KIDIjJITALI KATIKA SHUGHULI ZA KIUCHUMI NA KIJAMII

MHESHIMIWA ESTHER EDWIN MALLEKO (VITI MAALUM) Atauliza:-

Je, Serikali ina Mkakati gani katika kuchochea mapinduzi ya Kidijitali katika Shughuli za Kiuchumi na Kijamii.

WAZIRI WA MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI Atajibu:-

Mheshimiwa Spika, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaendelea na utekelezaji wa Mkakati wa Uchumi wa Kidijitali katika Tanzania ya Mwaka 2024 - 2034 (Tanzania Digital Economy Strategic Framework 2024 - 2034) unaoweka mwelekeo wa maendeleo ya Uchumi wa Kidijitali hapa Nchini.

Mheshimiwa Spika, Utekelezaji wa Mkakati huu unalenga kuongeza mchango wa Uchumi wa Kidijitali katika Pato la Taifa, kuimarisha tija na ufanisi katika shughuli za Kiuchumi na Kijamii, kupanua fursa za ajira na biashara, kuchochea ubunifu na uwekezaji pamoja na kuboresha ubora na upatikanaji wa huduma za Umma. Hatua hizi ni sehemu muhimu ya jitihada za Serikali za kujenga Jamii ya Kidijitali na zinaunga mkono utekelezaji wa Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050.

UJENZI WA BARABARA YA MTAMA – NEWALA

MHESHIMIWA YAHAYA ESMAIL NAWANDA (NEWALA VIJIJINI) Atauliza:-

Je, lini Barabara ya Mtama hadi Newala itajengwa kwa kiwango cha lami.

WAZIRI WA UJENZI Atajibu:-

Mheshimiwa Spika, Kazi za Upembuzi Yakinifu na Usanifu wa Kina wa barabara ya Mtama – Mkwiti – Newala yenye urefu wa kilometa 74 kwa ajili ya ujenzi kwa kiwango cha lami zinaendelea na ziko katika hatua za mwisho. Baada ya kukamilika kwa hatua hii Serikali itatenga bajeti kwa ajili ya ujenzi wa barabara hiyo.

 

COMMENTS

Name

Anga,12,Arusha,27,batiki,1,Burudani,477,burundani,2,come rain,1,come sun,1,Crazy in Love kama wimbo kama wao wenyewe,1,dahh sijui kweli mbona shida,1,Dar utakuja je tumejiandaa,1,daraja sahau nini,1,demokrasia ya upanga,1,Dodoma,78,Dole tupu vijana wa zamani,1,Duhh bibie endeleza libeneke,1,Duhh kaisikie Walibana,1,duhh kwa mbagala mama lazima awe supa,1,Fedha za maiti haziliwi bure,1,Fedha za watu kwa maendeleo ya watu,1,Fikira,14,filamu,322,Filamu ndio kielelezo cha ukuzi wa taifa,1,flamu,7,Gandamiza Kibara baba ake,1,haba,1,habar,3,Habari,7815,habari dodoma,41,habari. dodoma,32,habaria,1,hadithi,27,hakika tumeweka historia,1,hakuna noma jongwe,1,hapa kwetu inakuwaje vile,1,hasira hasara,1,hata maji,1,hataki masikhara na maisha yake,1,hatubonyezi kizenji,1,haya ndiyo mambo ya Ulaya,1,haya si yangu ni ya mdau mwenye hasira,1,haya wabongo na mambo kutoka nje,1,He he he wananikumbusha upishi wa shaba,1,Headline,1,Hii hurejesha uhai,1,Hii iko sawa kweli?,1,Hii imekaa vizuri,1,Hii inakaaje vile,1,Hii kweli noma,1,Hii maana yake Moro kuna uhaba wa chakula,1,Hii mexico,1,Hii mihasira mingine bwana,1,Hii ndio moro sio mpaka dar,1,hii ni hatari,1,Hii ni kiboko anayetaka kubisha ajibishie tu,1,Hii ni moja ya staili za kunyoa nywele,1,Hii si lukwangule,1,hii staili mpya,1,hili ni jengo pacha la malaysia ghorofa 88,1,Hivi ni ngoma tu,1,hivi nini siri za serikali,1,hivi sisi tunajua kama kuna vitu vya aina hii,1,hivi vitu bwana,1,Hiyo ndiyo gharama ya demokrasia,1,Hizi imani nyingine ni hatari,1,Hizi takwimu hizi mhh,1,Hongera bibie,1,Hongera dada etu kwa kutuletea kaka etu (shemeji) kwani mwenye dada hakosi shemeji,1,Hongera sana,1,huhitaji mifedha kuwa msafi,1,Huko Ulaya,1,Huu ndio ustaarabu,1,huu ujiko utakuwa mkubwa,1,imetosha,1,Inahitaji nidhamu fulani,1,inakuuma au...,1,Inakuwaje kama filamu yenyewe itahitaji busu la nguvu,1,Inaonekana watanzania hatukuwepo,1,Ipo kazi Maximo,1,Iringa,22,Isiwe mijineno tu manake mihela hubadili watu kweli,1,Itakuwa laki moja ya halali,1,jamani huu kama si ushamba kumbe nini,1,Jamani mbona Mungu anatupigania,1,Jamani watoto wanatakiwa kupendwa,1,jamani.. jamani ukiikosa Diamond usijutie,1,Je nyumbani hakuna vitu vya aina hii?Tuambie,1,je walikuwepo watu wa huduma ya kwanza,1,Je watanzania wanalipa kodi,1,jela kwa raha,1,Jolie,1,juhudi za lazima kuinua filamu,1,kama si kiwanda cha chumvi nani atawajua hawa,1,Kama kweli ndio kweli basi kila heri,1,Kama Mkristo naamini hilo hiyo si sahihi,1,kama unajua kuyarudi nenda Malta,1,kama wao wanaweza sisi je,1,Kamua baba waache wakanyagane,1,karibu nyumbani dada yote maisha tu,1,karibu Tatiii,1,KARIBUNI,1,Katavi,5,kaza buti hakuna kukata tamaa inalipa,1,kazi kwako mheshimiwa waziri wa madini,1,kazi na burudani,1,keep it up bloggers,1,kero ya usafiri sasa kwisha,1,Kila chenye roho na mwili kitaonja umauti,1,kila kitu kina vitu,1,Kila la Heri jamila,1,kila la heri kwani ni changamoto,1,Kipya,51,Kiuno bila mfupa,1,Kolelo mzimu ambao bado hai,1,KUBWA,1,Kudumisha urafiki wa dunia,1,Kuna dalili za wasomi kukubali Uafrika,1,kuna makala humu humu ndani ya blogu sijui mnasemaje,1,Kuu,113,kwa mara nyingine tena Tigo imewezesha,1,Kwa mchanganyiko huu muungano lazima udumu,1,Kwa mihasira hajambo,1,kweli,1,Kweli ina mkono mrefu tuone,1,Kweli duniani tunatofautiana,1,la maana ni kuwa na jiko au vipi,1,labda halitabadilika tena,1,lakini mwafaka lazima,1,lengo ni kutafakari,1,leteni vitu tuvione,1,lets us,1,Lucy wanakuelewa hawa...,1,Lukwangule nyumbani kwetu,2,M ungu bariki mikono ya madaktari wafanikiwe,1,MAARUFU,1,maendeleo ya soka siku zote yanahitaji fedha ili yapatikane,1,maisha ni vyema kuyaangalia,1,MAJIBU,1,makala,52,mama ni mama tu anapendeza,1,mambo mengine we angalia tu,1,mambo msimamo,1,mambo sasa mchanganyiko,1,Mara nyingine huona tunakotoka kwa kuona wenzetu,1,Mashabiki wa rhumba mpooooooooo,1,Masitaa,12,Maskani,1,MASOKO,3,Masupa staa mnaoinukia mpoo,1,Matamasha,6,mavazi ya kuogelea yanaposhindaniwa,1,Mbeya,11,Mchakamchaka anti Asmah,1,Mchanganyiko,81,MCHANYATO,1,mchezo,7,mengi wanayoyaita siri ni public information,1,mfumuko wa bei mpaka noma,1,Mhh sijui watu wa Sua ambao wako huko wanasemaje,1,Mhh ugua pole dada watu wanataka burudani,1,Michezo,779,Michezo maalum inatakiwa kupigiwa debe,1,miguu,1,miguu babu,1,Mikataba mingine ama hakika tuiangalie hata wakopeshaji nao wanatugeuza sakala,1,MIMI NI KISURA NAJITAMBUA,1,Mimi sijajua hasa kumetokea nini kwani ninavyojua hawa huwa na ungalizi wa hali ya juu,1,Mimi simo,1,mimi sisemi,1,miochezo,1,mkiwa chumvi basi mkoze,1,Mkiwa taa mulikeni,1,Mnaonaje je hii imekaa vyema,1,Mnaweza wakwetu hapa,1,Morogoro,51,mrithi wa mwanadada Whitney Houston,1,Mtwara,4,Mungu aiweke mahali pema roho yake,4,Mungu amrehemu,1,Mungu amweke pema peponi,1,Mungu awabariki sana,1,Mungu awe nao,1,Mungu ibariki Tanzania,1,Mungu tuepushe na imani hizi za kishirikina,1,mungu tufanye tuwe na upendo,1,Mungu twaomba utuhurumie,1,Muziki,376,muziki na fasheni,21,Mwanahabari,33,Mwanza,6,Mwendo mdundo dada,1,Mwenge huo utakimbizwa duniani kwa siku 130,1,Mwenge wa olimpiki ni ishara ya urafiki,1,Mzee wa Farasi nakupa saluti,1,Mzimbabwe huyu kutoka kwa mama mkali,1,N i dar mpaka Moro au bao tatu bila,1,Na sisi je,1,Naam kama haiwezekani hapa,1,Nairobi waanzisha tena utalii,1,namna bora ya kusaidia jamii,1,nani abebe hukumu na lawama,1,nani asiyejua utamu wa pipi,1,Nani kama baba,1,naona inafaa kuchangia mimi sitoi hoja,1,ndoa za mastaa huwa na mgogoro,1,nenda mwaya nenda,1,New Zanzibar Modern Taarab na wapenzi big up,1,news,5,Ni bikini kwa kwenda mbele,1,Ni Dar mpaka Moro au.. tatu bila,1,ni furaha za muungano,1,Ni kazi ngumu yenye kuhifadhi utamaduni,1,Ni kuchakarika kuonyesha urafiki na biashara pia,1,ni mfumuko wa bei au mfumuko wa nchi,1,Ni muhimu kutazama afya yako,1,ni muziki kwa kwenda mbele,1,Ni muziki mpaka China,1,Ni raha tupu,1,Ni Serengeti Premium Lager,1,Ni Tigo na mawasiliano ya kisasa,1,Ni wakati wa kuujadili utamaduni,1,Ni zaidi ya jazz,1,Nitasubiri and welcome home,1,nje je?,1,NUKUU YA LEO,1,nyie mnasemaje kuhusu hili,1,Ona Kolelo na sindikizwa na Wazee wa Gwasuma,1,ona vya dunia,1,One step ahead,1,patna mwingine mjamzito,1,Pengine anamuogopa Jada Pinkett manake kwa wivu..,1,picha,494,Pole Jamila hayo ndiyo mashindano,1,poleni sana,1,poleni sana wanyalukolo,1,Powa sana,1,Profesa jamaa wanakumaindi,1,Roho za marehemu zipate pumziko la milele,1,Ruvuma,9,sakata dansi mpaka kwenye kilele cha dunia,1,sasa kumebakia ugonjwa mmoja polisi kuendesha mashtaka,1,sasa mifedha kila mahali hongereni,1,Sasa ni mavuno,1,Sasa ni wakati wa kutafuta upenyo ndani ya IDOLS,1,SAYANSI,10,SAYANSI ANGA,16,See Uluguru Montains,1,serikali inataka kujihami kwanini,1,Show of support Big Up Madame,1,Si kitu kidogo hata kidogo,1,si unajua tena namie naimwaga hivyo hivyo,1,Siasa,346,siasa habari,2,Sijui kama City wanajua Mbagala noma,1,Sijui tunaishi karne gani yailahi,1,Sinema,17,sio advencha....kaaa ...niko kibaruani,1,Sisi ndio tunaanza vitongoji,1,Sisi yetu macho na masikio,1,Slow slow jamani,1,sto,1,tabasamu kali la mwenge wa olimpiki,1,Tabora,1,Tazama Waziri Mkuu Pinda wasije wakapindisha maamuzi yako,1,TEKNOLOJIA,1,Thats big man game,1,This is crazy Africa,1,This is Mgeta,1,Tibet wamegeuza Olimpiki jukwaa la siasa,1,Titbits collection,1,Tubadili tamaduni,1,Tuchangie mambo yaive,1,tuendeleze sanaa,1,tuienzi na sisi mbona wizara haituambii,1,Tuipeleke kaskazini,1,Tuisaidie serikali shida ya Mererani,1,tujue namna ya kupumzika,1,Tulienda kustarehe au kufanya fujo,1,Tumsaidie mtototo huyu kurejea katika hali ya kawaida,1,tunahitaji haya,1,Tunajifunza kweli kutoka kwao,1,Tunapandisha chati tu,1,Tunasubiri,1,tunazidi kuhesabu siku,1,TUNAZISUBIRI ZA VINARA ADAR,1,Tuombe nafuu kwa wagonjwa,1,Tuombe rehema kwa mungu,1,Tuone yatufae,1,Tusingoje wengine watusemee,1,tutampa tafu kubwa Prof,1,tuuenzi utamaduni au vipi,1,Tuukuze na kuulinda,1,tuvipende,1,tuwalinde maalbino,1,Tuwe kweli wakweli,1,ubunifu siku zote hulipa,1,uchumi huzunguka kwa kuwawezesha wasukaji,1,udumu muungano,1,Ugonjwa huu wa sasa ni kitendawili,1,Ukiiona kolelo utaipenda,1,Ukirejea salama kila mtu anafurahi,1,Umelenga Mkuchika utamaduni unakufa,1,unaposaka uwakilishi wa dunia,1,urafiki,1,urembo,1,Usisahau wazee wa Ngwasuma,1,UTALII,1,UTAMADUNI,4,Video,2,Vionjo vipya ndani ya Gwasuma,1,Vita dhidi ya ufisadi,1,vitongoji Miss Tanzania navyo vimeanza,1,Vitu vikali vyazidi kuingia Dar,1,Vituko,77,Vituo vya polisi Tanga vyatelekezwa,1,VIVALO,1,Wacha tujifue,2,Wadau ilitolewa kiingereza,1,wakali wa ubunifu,1,wala usibabaike mwakwetu hii noma,1,wanadamu wanapotaka kujua zaidi,1,wanasema mpaka kieleweke,1,Wanataka kujua mali za JK na wengine,1,Wanawake wenye mvuto: Monroe,1,Wapo mabinti wa matawi ya juu,1,watu wanapofanya weli kwenye sanaa,1,waweza kurejea enzi ya Moro jazz na Cuban malimba,1,Wazee tupo kusindikiza,1,waziri,1,welcome dar baby,1,Wenzetu wameona sisi tunangoja nini kuangalia,1,wewe unasemaje,1,wigo mpana wa utamaduni,1,wilaya ya 'Mbagala' mlie tu,1,Yaaani sijui itawezekana,1,Yaani wakati mwingine hata huelewi prioty over priority,1,yeye mbele sisi nyuma,1,Yote maisha dada,1,ZA MOTOMOTO,1,Zanzibar,79,zawadi zinatakiwa ziende shule,1,ZILIZOTIA FORA,1,zitachangia kupunguza makali ya bei za umeme,1,
ltr
item
Lukwangule Entertainment: MASWALI NA MAJIBU YA SERIKALI BUNGENI OKT 30: TEKNOLOJIA, ELIMU NA AFYA
MASWALI NA MAJIBU YA SERIKALI BUNGENI OKT 30: TEKNOLOJIA, ELIMU NA AFYA
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiu8PWGKXLPaUcYLAMox0zV745kg3TLSo3QjTbbricTCqLbC1lNGYn6CfiMriQesH1ZkQ02ZpGaqCc206KlhCZg9TKDob8DBPc5Ocs4k0DxvQWzz8qvvLgHQVPqyUN62EOD0E55VRzUBKU24Ja1Kr_axbyLtRCy_BoiPE9glAV0UK8EyH7tzZmCAno5tUYA/s320/BUNGE.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiu8PWGKXLPaUcYLAMox0zV745kg3TLSo3QjTbbricTCqLbC1lNGYn6CfiMriQesH1ZkQ02ZpGaqCc206KlhCZg9TKDob8DBPc5Ocs4k0DxvQWzz8qvvLgHQVPqyUN62EOD0E55VRzUBKU24Ja1Kr_axbyLtRCy_BoiPE9glAV0UK8EyH7tzZmCAno5tUYA/s72-c/BUNGE.jpg
Lukwangule Entertainment
https://lukwangule.blogspot.com/2026/10/maswali-na-majibu-ya-serikali-bungeni_01160685493.html
https://lukwangule.blogspot.com/
http://lukwangule.blogspot.com/
http://lukwangule.blogspot.com/2026/10/maswali-na-majibu-ya-serikali-bungeni_01160685493.html
true
934549962738256429
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy