TANZANIA NA MAREKANI ZAIMARISHA UHUSIANO

*Mahusiano ya Miji Dada na viwanja vya ndege yang’ara   BALOZI wa Tanzania wa Washington, Marekani, Dkt. Elsie Kanza amesema mahusiano ya Ta...



*Mahusiano ya Miji Dada na viwanja vya ndege yang’ara

 

BALOZI wa Tanzania wa Washington, Marekani, Dkt. Elsie Kanza amesema mahusiano ya Tanzania na Marekani yamezidi kuimarika na kuibua fursa kwenye sekta mbalimbali kama vile uchukuzi, utalii na mahusiano ya miji dada.

 

Akitoa taarifa kwa Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba, Balozi Dkt. Elsie Kanza alisema Tanzania imeendelea kushirikiana na nchi hiyo kwenye sekta mbalimbali ikiwemo afya, usafiri, nishati, elimu na mafunzo.

 

“Julai mwaka huu, Tanzania na Marekani zilisaini Hati ya Makubaliano ya Ushirikiano (MoU) ya miaka mitano katika sekta ya afya yenye thamani ya dola za Marekani bilioni 3.1,” alisema Balozi Kanza na kuongeza kuwa wapo katika hatua za mwisho za kuanzisha uhusiano baina ya viwanja vya ndege na bandari kati ya Tanzania na Marekani.

 

“Tupo katika hatua za mwisho za kuanzisha uhusiano baina ya viwanja vya ndege (sister airports) kati ya Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Hartsfield-Jackson Atlanta, ambao unaongoza kwa kuhudumia abiria wengi zaidi duniani. Pia, tunaendelea na mazungumzo na Bandari ya Philadelphia ili kuanzisha uhusiano na bandari ya Dar es Salaam,” alisema.

 

Takwimu za mwaka 2025 zinaonesha kuwa uwanja wa Hartsfield-Jackson Atlanta unahudumia abiria milioni 106.3 kwa mwaka hali inayouweka kuwa uwanja wenye wasafiri wengi duniani, ikifuatiwa na viwanja vya Dubai (UAE) na Tokyo (Japan). Wastani wa abiria kwa siku ni 291,000.

 

Akitoa ufafanuzi kuhusu uhusiano wa Miji Dada, Balozi Dkt. Kanza alisema dhana ya miji dada ni muhimu kwani miji husika hushirikiana kwenye masuala mbalimbali ya kibiashara, kijamii, kitamaduni na kiuchumi.

 

“Miji na majiji ya Tanzania na Marekani imeendelea kuanzisha uhusiano wa miji dada (sister cities) na hadi sasa majiji 10 ya Tanzania na Marekani yana uhusiano wa miji dada. Mara ya mwisho kuingia makubaliano hayo ni mwaka 2025, ambapo majiji ya Mwanza na Tulsa, Oklahoma na majiji ya Dar es Salaam na Dallas, Texas, yalianzisha uhusiano huo.”

 

“Kwa sasa, mazungumzo yanaendelea ili kuanzisha uhusiano wa miji dada kati ya Jiji la New Orleans, Louisiana na Jiji la Zanzibar; Mbeya na Omaha, Nebraska; Morogoro na Oregon; Dodoma na Phoenix, Arkansas; pamoja na Dar es Salaam na Philadelphia, Pennsylvania,” alisema.

 

Miji dada mingine ambayo tayari imepata washirika ni Arusha na Durham, North Carolina; Tanga na Toledo, Ohio; Moshi na DelRay Beach, Florida; Bagamoyo na Vallejo, Califonia; Arusha na Kansas City, Missouri; Tarime na Milwaukee, Wisconsin; na Dar Es Salaam na Lansing, Michigan.

 

Akielezea kuhusu ukuaji wa biashara kati ya Tanzania na Marekani, Balozi huyo alisema kwamba jitihada za ubalozi zinaendelea kuzaa matunda ambapo mwaka 2025, thamani ya mauzo ya bidhaa za Tanzania nchini Marekani ziliongezeka kwa asilimia 18, Tanzania ikiwa imerekodi ziada ya biashara (trade surplus) ya takribani dola za Marekani milioni 120 dhidi ya Marekani.

 

Alisema mwaka 2024, biashara kati ya Tanzania na Marekani ilifikia dola za Marekani bilioni 1.4 ambacho ni kiwango cha juu zaidi kuwahi kufikiwa katika historia ya uhusiano baina ya nchi hizo mbili.

 

Kuhusu ufanyaji biashara chini ya Mpango wa AGOA, Balozi Dkt. Kanza alisema programu hiyo iliyodumu kwa miaka 25 ambayo awali ilifikia ukomo Septemba 30, mwaka jana, hivi sasa imeongezewa muda hadi Desemba, 2028. “Programu hiyo inasaidia baadhi ya bidhaa za Tanzania kuuzwa hapa Marekani kwa bei ya ushindani. Asilimia 42.85 ya mauzo yote ya bidhaa za Tanzania nchini Marekani kwa mwaka 2024, yalifanyika chini ya AGOA,” alisema.

 

Katika kuendelea kuvutia biashara na uwekezaji baina ya Tanzania na Marekani, Balozi huyo alisema wameendelea kuandaa makongamano ya biashara na uwekezaji pamoja na ziara za kibiashara (trade missions) baina ya nchi hizo. “Kwa mfano, Juni 2026 tulishirikiana na taasisi ya Virginia Economic Development Partnership (VEDP) kupeleka kampuni tisa za kibiashara nchini Tanzania ambazo zilitembelea Tanzania Bara na Zanzibar kuangalia fursa mbalimbali za biashara na uwekezaji.”

 

“Kwa sasa, tunashirikiana na Jiji la Chicago, Illinois kupeleka ziara ya wafanyabiashara Tanzania ifikapo Desemba 2026, kwa ajili ya kuangalia fursa zilizopo na kuwahamasisha kuzichangamkia. Kwa mwaka 2027, tayari tumeanza kushirikiana na majimbo ya Arizona na Pennsylvania kuandaa ziara za kibiashara kwenda Tanzania,” alisema.

 

COMMENTS

Name

Anga,12,Arusha,27,batiki,1,Burudani,476,burundani,2,come rain,1,come sun,1,Crazy in Love kama wimbo kama wao wenyewe,1,dahh sijui kweli mbona shida,1,Dar utakuja je tumejiandaa,1,daraja sahau nini,1,demokrasia ya upanga,1,Dodoma,78,Dole tupu vijana wa zamani,1,Duhh bibie endeleza libeneke,1,Duhh kaisikie Walibana,1,duhh kwa mbagala mama lazima awe supa,1,Fedha za maiti haziliwi bure,1,Fedha za watu kwa maendeleo ya watu,1,Fikira,14,filamu,320,Filamu ndio kielelezo cha ukuzi wa taifa,1,flamu,7,Gandamiza Kibara baba ake,1,haba,1,habar,3,Habari,7772,habari dodoma,41,habari. dodoma,32,habaria,1,hadithi,27,hakika tumeweka historia,1,hakuna noma jongwe,1,hapa kwetu inakuwaje vile,1,hasira hasara,1,hata maji,1,hataki masikhara na maisha yake,1,hatubonyezi kizenji,1,haya ndiyo mambo ya Ulaya,1,haya si yangu ni ya mdau mwenye hasira,1,haya wabongo na mambo kutoka nje,1,He he he wananikumbusha upishi wa shaba,1,Headline,1,Hii hurejesha uhai,1,Hii iko sawa kweli?,1,Hii imekaa vizuri,1,Hii inakaaje vile,1,Hii kweli noma,1,Hii maana yake Moro kuna uhaba wa chakula,1,Hii mexico,1,Hii mihasira mingine bwana,1,Hii ndio moro sio mpaka dar,1,hii ni hatari,1,Hii ni kiboko anayetaka kubisha ajibishie tu,1,Hii ni moja ya staili za kunyoa nywele,1,Hii si lukwangule,1,hii staili mpya,1,hili ni jengo pacha la malaysia ghorofa 88,1,Hivi ni ngoma tu,1,hivi nini siri za serikali,1,hivi sisi tunajua kama kuna vitu vya aina hii,1,hivi vitu bwana,1,Hiyo ndiyo gharama ya demokrasia,1,Hizi imani nyingine ni hatari,1,Hizi takwimu hizi mhh,1,Hongera bibie,1,Hongera dada etu kwa kutuletea kaka etu (shemeji) kwani mwenye dada hakosi shemeji,1,Hongera sana,1,huhitaji mifedha kuwa msafi,1,Huko Ulaya,1,Huu ndio ustaarabu,1,huu ujiko utakuwa mkubwa,1,imetosha,1,Inahitaji nidhamu fulani,1,inakuuma au...,1,Inakuwaje kama filamu yenyewe itahitaji busu la nguvu,1,Inaonekana watanzania hatukuwepo,1,Ipo kazi Maximo,1,Iringa,22,Isiwe mijineno tu manake mihela hubadili watu kweli,1,Itakuwa laki moja ya halali,1,jamani huu kama si ushamba kumbe nini,1,Jamani mbona Mungu anatupigania,1,Jamani watoto wanatakiwa kupendwa,1,jamani.. jamani ukiikosa Diamond usijutie,1,Je nyumbani hakuna vitu vya aina hii?Tuambie,1,je walikuwepo watu wa huduma ya kwanza,1,Je watanzania wanalipa kodi,1,jela kwa raha,1,Jolie,1,juhudi za lazima kuinua filamu,1,kama si kiwanda cha chumvi nani atawajua hawa,1,Kama kweli ndio kweli basi kila heri,1,Kama Mkristo naamini hilo hiyo si sahihi,1,kama unajua kuyarudi nenda Malta,1,kama wao wanaweza sisi je,1,Kamua baba waache wakanyagane,1,karibu nyumbani dada yote maisha tu,1,karibu Tatiii,1,KARIBUNI,1,Katavi,5,kaza buti hakuna kukata tamaa inalipa,1,kazi kwako mheshimiwa waziri wa madini,1,kazi na burudani,1,keep it up bloggers,1,kero ya usafiri sasa kwisha,1,Kila chenye roho na mwili kitaonja umauti,1,kila kitu kina vitu,1,Kila la Heri jamila,1,kila la heri kwani ni changamoto,1,Kipya,51,Kiuno bila mfupa,1,Kolelo mzimu ambao bado hai,1,KUBWA,1,Kudumisha urafiki wa dunia,1,Kuna dalili za wasomi kukubali Uafrika,1,kuna makala humu humu ndani ya blogu sijui mnasemaje,1,Kuu,113,kwa mara nyingine tena Tigo imewezesha,1,Kwa mchanganyiko huu muungano lazima udumu,1,Kwa mihasira hajambo,1,kweli,1,Kweli ina mkono mrefu tuone,1,Kweli duniani tunatofautiana,1,la maana ni kuwa na jiko au vipi,1,labda halitabadilika tena,1,lakini mwafaka lazima,1,lengo ni kutafakari,1,leteni vitu tuvione,1,lets us,1,Lucy wanakuelewa hawa...,1,Lukwangule nyumbani kwetu,2,M ungu bariki mikono ya madaktari wafanikiwe,1,MAARUFU,1,maendeleo ya soka siku zote yanahitaji fedha ili yapatikane,1,maisha ni vyema kuyaangalia,1,MAJIBU,1,makala,52,mama ni mama tu anapendeza,1,mambo mengine we angalia tu,1,mambo msimamo,1,mambo sasa mchanganyiko,1,Mara nyingine huona tunakotoka kwa kuona wenzetu,1,Mashabiki wa rhumba mpooooooooo,1,Masitaa,12,Maskani,1,MASOKO,3,Masupa staa mnaoinukia mpoo,1,Matamasha,6,mavazi ya kuogelea yanaposhindaniwa,1,Mbeya,11,Mchakamchaka anti Asmah,1,Mchanganyiko,81,MCHANYATO,1,mchezo,7,mengi wanayoyaita siri ni public information,1,mfumuko wa bei mpaka noma,1,Mhh sijui watu wa Sua ambao wako huko wanasemaje,1,Mhh ugua pole dada watu wanataka burudani,1,Michezo,779,Michezo maalum inatakiwa kupigiwa debe,1,miguu,1,miguu babu,1,Mikataba mingine ama hakika tuiangalie hata wakopeshaji nao wanatugeuza sakala,1,MIMI NI KISURA NAJITAMBUA,1,Mimi sijajua hasa kumetokea nini kwani ninavyojua hawa huwa na ungalizi wa hali ya juu,1,Mimi simo,1,mimi sisemi,1,miochezo,1,mkiwa chumvi basi mkoze,1,Mkiwa taa mulikeni,1,Mnaonaje je hii imekaa vyema,1,Mnaweza wakwetu hapa,1,Morogoro,51,mrithi wa mwanadada Whitney Houston,1,Mtwara,4,Mungu aiweke mahali pema roho yake,4,Mungu amrehemu,1,Mungu amweke pema peponi,1,Mungu awabariki sana,1,Mungu awe nao,1,Mungu ibariki Tanzania,1,Mungu tuepushe na imani hizi za kishirikina,1,mungu tufanye tuwe na upendo,1,Mungu twaomba utuhurumie,1,Muziki,376,muziki na fasheni,21,Mwanahabari,33,Mwanza,6,Mwendo mdundo dada,1,Mwenge huo utakimbizwa duniani kwa siku 130,1,Mwenge wa olimpiki ni ishara ya urafiki,1,Mzee wa Farasi nakupa saluti,1,Mzimbabwe huyu kutoka kwa mama mkali,1,N i dar mpaka Moro au bao tatu bila,1,Na sisi je,1,Naam kama haiwezekani hapa,1,Nairobi waanzisha tena utalii,1,namna bora ya kusaidia jamii,1,nani abebe hukumu na lawama,1,nani asiyejua utamu wa pipi,1,Nani kama baba,1,naona inafaa kuchangia mimi sitoi hoja,1,ndoa za mastaa huwa na mgogoro,1,nenda mwaya nenda,1,New Zanzibar Modern Taarab na wapenzi big up,1,news,5,Ni bikini kwa kwenda mbele,1,Ni Dar mpaka Moro au.. tatu bila,1,ni furaha za muungano,1,Ni kazi ngumu yenye kuhifadhi utamaduni,1,Ni kuchakarika kuonyesha urafiki na biashara pia,1,ni mfumuko wa bei au mfumuko wa nchi,1,Ni muhimu kutazama afya yako,1,ni muziki kwa kwenda mbele,1,Ni muziki mpaka China,1,Ni raha tupu,1,Ni Serengeti Premium Lager,1,Ni Tigo na mawasiliano ya kisasa,1,Ni wakati wa kuujadili utamaduni,1,Ni zaidi ya jazz,1,Nitasubiri and welcome home,1,nje je?,1,NUKUU YA LEO,1,nyie mnasemaje kuhusu hili,1,Ona Kolelo na sindikizwa na Wazee wa Gwasuma,1,ona vya dunia,1,One step ahead,1,patna mwingine mjamzito,1,Pengine anamuogopa Jada Pinkett manake kwa wivu..,1,picha,494,Pole Jamila hayo ndiyo mashindano,1,poleni sana,1,poleni sana wanyalukolo,1,Powa sana,1,Profesa jamaa wanakumaindi,1,Roho za marehemu zipate pumziko la milele,1,Ruvuma,9,sakata dansi mpaka kwenye kilele cha dunia,1,sasa kumebakia ugonjwa mmoja polisi kuendesha mashtaka,1,sasa mifedha kila mahali hongereni,1,Sasa ni mavuno,1,Sasa ni wakati wa kutafuta upenyo ndani ya IDOLS,1,SAYANSI,10,SAYANSI ANGA,16,See Uluguru Montains,1,serikali inataka kujihami kwanini,1,Show of support Big Up Madame,1,Si kitu kidogo hata kidogo,1,si unajua tena namie naimwaga hivyo hivyo,1,Siasa,346,siasa habari,2,Sijui kama City wanajua Mbagala noma,1,Sijui tunaishi karne gani yailahi,1,Sinema,17,sio advencha....kaaa ...niko kibaruani,1,Sisi ndio tunaanza vitongoji,1,Sisi yetu macho na masikio,1,Slow slow jamani,1,sto,1,tabasamu kali la mwenge wa olimpiki,1,Tabora,1,Tazama Waziri Mkuu Pinda wasije wakapindisha maamuzi yako,1,TEKNOLOJIA,1,Thats big man game,1,This is crazy Africa,1,This is Mgeta,1,Tibet wamegeuza Olimpiki jukwaa la siasa,1,Titbits collection,1,Tubadili tamaduni,1,Tuchangie mambo yaive,1,tuendeleze sanaa,1,tuienzi na sisi mbona wizara haituambii,1,Tuipeleke kaskazini,1,Tuisaidie serikali shida ya Mererani,1,tujue namna ya kupumzika,1,Tulienda kustarehe au kufanya fujo,1,Tumsaidie mtototo huyu kurejea katika hali ya kawaida,1,tunahitaji haya,1,Tunajifunza kweli kutoka kwao,1,Tunapandisha chati tu,1,Tunasubiri,1,tunazidi kuhesabu siku,1,TUNAZISUBIRI ZA VINARA ADAR,1,Tuombe nafuu kwa wagonjwa,1,Tuombe rehema kwa mungu,1,Tuone yatufae,1,Tusingoje wengine watusemee,1,tutampa tafu kubwa Prof,1,tuuenzi utamaduni au vipi,1,Tuukuze na kuulinda,1,tuvipende,1,tuwalinde maalbino,1,Tuwe kweli wakweli,1,ubunifu siku zote hulipa,1,uchumi huzunguka kwa kuwawezesha wasukaji,1,udumu muungano,1,Ugonjwa huu wa sasa ni kitendawili,1,Ukiiona kolelo utaipenda,1,Ukirejea salama kila mtu anafurahi,1,Umelenga Mkuchika utamaduni unakufa,1,unaposaka uwakilishi wa dunia,1,urafiki,1,urembo,1,Usisahau wazee wa Ngwasuma,1,UTALII,1,UTAMADUNI,4,Video,2,Vionjo vipya ndani ya Gwasuma,1,Vita dhidi ya ufisadi,1,vitongoji Miss Tanzania navyo vimeanza,1,Vitu vikali vyazidi kuingia Dar,1,Vituko,77,Vituo vya polisi Tanga vyatelekezwa,1,VIVALO,1,Wacha tujifue,2,Wadau ilitolewa kiingereza,1,wakali wa ubunifu,1,wala usibabaike mwakwetu hii noma,1,wanadamu wanapotaka kujua zaidi,1,wanasema mpaka kieleweke,1,Wanataka kujua mali za JK na wengine,1,Wanawake wenye mvuto: Monroe,1,Wapo mabinti wa matawi ya juu,1,watu wanapofanya weli kwenye sanaa,1,waweza kurejea enzi ya Moro jazz na Cuban malimba,1,Wazee tupo kusindikiza,1,waziri,1,welcome dar baby,1,Wenzetu wameona sisi tunangoja nini kuangalia,1,wewe unasemaje,1,wigo mpana wa utamaduni,1,wilaya ya 'Mbagala' mlie tu,1,Yaaani sijui itawezekana,1,Yaani wakati mwingine hata huelewi prioty over priority,1,yeye mbele sisi nyuma,1,Yote maisha dada,1,ZA MOTOMOTO,1,Zanzibar,79,zawadi zinatakiwa ziende shule,1,ZILIZOTIA FORA,1,zitachangia kupunguza makali ya bei za umeme,1,
ltr
item
Lukwangule Entertainment: TANZANIA NA MAREKANI ZAIMARISHA UHUSIANO
TANZANIA NA MAREKANI ZAIMARISHA UHUSIANO
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEijsqBO6N2uNAmHNR3dqh18L8qSP5kbRqI2BK5SEcFehf94MxzZpr48bQ1esy9BPm3OoHCKGvUj_sVp9egLsPOxS7Y14rYP-WHcA4RmU1NMuS-SZHQ_060ygy2zE8WdnnU0VQffvANwgFo0fRlME4LhP3fcIlNU2Ui2tLwofmdW7TBaw65ssibcsYpRssYy/s320/waziri%20mkuu.jfif
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEijsqBO6N2uNAmHNR3dqh18L8qSP5kbRqI2BK5SEcFehf94MxzZpr48bQ1esy9BPm3OoHCKGvUj_sVp9egLsPOxS7Y14rYP-WHcA4RmU1NMuS-SZHQ_060ygy2zE8WdnnU0VQffvANwgFo0fRlME4LhP3fcIlNU2Ui2tLwofmdW7TBaw65ssibcsYpRssYy/s72-c/waziri%20mkuu.jfif
Lukwangule Entertainment
https://lukwangule.blogspot.com/2026/10/tanzania-na-marekani-zaimarisha-uhusiano.html
https://lukwangule.blogspot.com/
http://lukwangule.blogspot.com/
http://lukwangule.blogspot.com/2026/10/tanzania-na-marekani-zaimarisha-uhusiano.html
true
934549962738256429
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy