LINDI, MTWARA ZAHITAJI PEMBEJEO ZA RUZUKU - PINDA *Ambana Mkurugenzi wa Lindi Vijijini kuhusu power-tillers *Asema anakerwa na lawama za wan...
LINDI, MTWARA ZAHITAJI PEMBEJEO ZA RUZUKU - PINDA
*Ambana Mkurugenzi wa Lindi Vijijini kuhusu power-tillers
*Asema anakerwa na lawama za wananchi kudaiwa kutoibua miradi
WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amesema mikoa ya Lindi na Mtwara inastahili kuingizwa kwenye mpango wa ruzuku za pembejeo ili iweze kukuza kilimo chamao ya chakula na biashara.
Pia amemtaka Mkurugenzi wa Halmashauri ya Lindi, Bw. Hijob Shenkalwa afanye juu chini kuhakikisha kuwa anapata fedha za kununulia power-tillers za kutosha kwa ajili ya halmashauri hiyo la sivyo hamtamsamehe kwa kupuuza agizo lake.
Waziri Mkuu alitoa kauli hiyo jana mchana (Jumanne, Novemba 17, 2009) katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye kijiji cha Mtama, wilayani Lindi mara baada ya kupokea taarifa ya wilaya hiyo akitokea wilayani Ruangwa.
“Mikoa ya Lindi na Mtwara tumekuwa tukiichukulia kuwa ni mikoa ya kilimo cha korosho tu, lakini katika ziara hii nimebaini kuwa ipo haja ya kuiingiza kwenye mpango wa ruzuku ya mbolea na mbegu ili waweze kuzalisha kwa wingi mazao ya chakula na biashara,” alisema Waziri Mkuu huku akishangiliwa.
Alisema atafuatilia suala hilo na kuhakikisha linaingizwa kwenye bajeti ya mwakani ili zoezi la kuwapa pembejeo na mbolea lianze mara moja. “Nimeona jinsi ardhi yenu ilivyo nzuri, kuna pori jingi tu… mnahitaji kuongeza eneo la kilimo ili kuzalisha zaidi,” alisema.
Akifafanua kuhusu matumizi ya zana bora za kilimo, Waziri Mkuu alisema wilaya hiyo ina hekta zaidi ya 500,000 lakini zinazotumika hivi sasa ni hekta 100,000 tu na kwamba hakuna njia ya mkato isipokuwa kuachana na jembe la mkono na kuhamia kwenye zana za kisasa.
“Mkurugenzi umenunua powertillers tisa tu, maagizo yalikuwa ni Halmashauri kuagiza power-tillers 50 katika mwaka wa kwanza na kuzisambaza katika vijiji ili wananchi waanze kuona umuhimu wa matumizi yake ikiwa na njia ya utekelezaji wa kaulimbiu ya Kilimo Kwanza,” alisema.
“Itabidi uongeze la sivyo sitakusamehe kwa kupuuza kununua zana za kilimo za kumsadia mkulima kuondokana na kilimo cha kizamani… wewe unatafuta ushuru, unataka hawa watu wachangie maendeleo… watatoa wapi hizo fedha kama hawalimi vya kutosha?”
“Nyie mnakaa ofisini mnasubiri baba au mama wa Kimwera watumie ‘chingondola’ (jembe la asili) kuleta Mapinduzi ya Kilimo, hapana! Haiwezekani! Kuanzia sasa mipango yako ya kilimo iwe ni kuondoa ‘chingondola’ kwa silaha nyingine kama wanyamakazi au powertiller.”
Alisema anakerwa na tabia za watendaji wa Halmashauri kuwabebesha lawama wananchi kwamba hawaibui miradi ndiyo maana wanashindwa kuingiza miradi kwenye mipango yao .
“Tusiwabebeshe watu wetu lawama kuwa hawaibui miradi… Wananchi hawaambiwi kuna fedha za miradi, mkiulizwa mnadai hawajaibua miradi. Acheni hii lugha! Je wataibuaje miradi kama hawajaambiwa?” alihoji na kuongeza: “Kwa vile hawapewi taarifa wanaishia kuibua miradi ya ufugaji kuku, mbuzi au ng’ombe badala ya power-tiller, kilimo cha umwagiliaji au vifaa vya usindikaji,” alisema na kushangiliwa.
Waziri Mkuu alisema: “DC na Halmashauri nzima ni lazima mjipange upya, msiache watu wetu wafe na njaa wakati ardhi ipo tena ya kutosha, msikae kusema ni wavivu wakati sababu inayowakwamisha kulima ni zana duni za kilimo,” alisema.
Leo Waziri Mkuu anamalizia ziara yake ya siku sita katika mkoa wa Lindi kwa kuzindua kisima cha maji katika shule ya msingi Mtanda na kuzindua uchimbaji wa visima virefu 100 kwenye Halmashauri ya Lindi Mjini. Pia atatembelea Hospitali ya Sokoine na kuweka jiwe la msingi katika jengo la maabara kisha atakabidhi Bajaj kwa mtumishi wa ofisi ya Katibu Tawala wa Mkoa huo kabla ya kufanya majumuisho ya ziara yake katika mkoa huu.
Alasiri ataelekea wilaya ya Masasi mkoani Mtwara kuanza ziara ya kikazi ya siku sita.
(mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMATANO, NOVEMBA 18, 2009.
ANGALIZO:
Bosi nilikuwapo Lindi na Mtwara sometime hivi duhh... je unajua vijitabia vya watu wa huko he he he hizo mbolea na ruzuku ziangalie unaweza ..... sijui niseme kuchemsha au kujutia.....

COMMENTS