KOCHA Mkuu wa timu ya Soka ya Ruvu Shooting , Fred Felix Minziro, amesema hatishiki na Yanga ,licha ya kunolewa na Kocha wa kigeni, Kostadin...
KOCHA Mkuu wa timu ya Soka ya Ruvu Shooting , Fred Felix Minziro, amesema hatishiki na Yanga ,licha ya kunolewa na Kocha wa kigeni, Kostadin Papic , na kudai kuwa hakuna jambo jipya katika timu hiyo litakalomzuia kuibuka na ushindi katika mchezo huo wa leo utakaofanyika kwenye uwanja wa Jamhuri wa Mjini hapa.
Minziro, Beki na Kocha wa zamani wa Yanga, ambaye sasa ni Kocha Mkuu wa Ruvu Shooting, alisema hayo hivi karibuni mjini hapa, wakati timu yake ilipofanikiwa kuwafunga wababe wa Simba msimu huu, timu ya Polisi Dodoma bao 2-0 , katika mchezo uliofanyika wiki iliyopita mjini hapa.
“ bado makocha wa kigeni hawajaonyesha kilichotarajiwa ..hivyo inanipa matumaini kuweza kufanya vyema katika mchezo wangu na Yanga …” alisema Kocha Mkuu huyo wa Ruvu Shooting.
Hata hivyo aliongeza kusenma “ hata wapenzi wa timu hizi zinazofundishwa na makocha hawa wa kigeni , hakuna hata mmoja aliyeonesha uwezo wa timu yake kwa wachezaji kupachika mabao mengi kama matarajio ya wengi” alisema Minziro.
“ tulitengemea timu yenye makocha wakineni zingepata idadi kubwa ya mabao kuonyesha kuwa wao ni kweli ni walimu wa kigeni …tungeona mambo mapya kila mchezo . lakini hili halipo…nimeiona Simba inavyocheza …kwa Yanga ndiyo nitaiona leo” aliongeza kusema Mchezaji huo wa zamani wa Yanga
Hata hivyo Minziro alisema, amewaandaa vyema vijana wake katika mchezo wao dhidi ya Yanga , licha ya ugumu alioanza kujitokeza kwa kila timu kijizatiti vilivyo kucheza kiushindani ,jambo ambapo linalojidhihirisha na idadi ndogo ya mabao yanapatikana kwenye michezo ya ligi kuu hiyo.
“ ligi sasa inaenda pazuri…kila timu inacheza mpira unaoonekena na mabadiriko yanajitokeza kila mchezo …lakini kwa Ruvu Shooting , tunawaomba wapenzi wa Morogoro watuunge mkono kila tunapocheza ili tupate ushindi wa pointi tatu ukuwemo na nchezo wa Yanga” alisema Minziro
Kwa upande wa Yanga , inaingia uwanjani ikiwa na lengo moja la kutaka kuendeleza ubabe wake ambapo katika mchezo uliofanyika Septemba 23, mwaka huu kwenye uwanja wa Jamhuri wa Mjini hapa, iliweza kuifunga timu ya Kagera Sugar kwa bao 2-0.
Yanga tangu ihamie katika uwanja wa Jamhuri kama uwanjwa wao wa nyumbani ilitoka sare ya bao 1-1 na Mtibwa Sugar , ikashinda bao 1 -0 dhidi ya Maji Maji ya Songea pia na Kagera kwa bao 2-0.
Mchezo huo wa Kagera mara baada ya kumalizika kulizuka tafrani kati ya viongozi wa timu ya Kagera na Yanga pamoja na mashabiki wa pande hizo baada ya mmoja wa viongozi wa Kagera kudaiwa kumpiga Kocha Papic wa Yanga.
SOURCE:John Nditi Habarileo

COMMENTS