Hizi ni baadhi ya picha tu za jinsi shughuli za kumuaga zilivyofanyika.Picha zimechukuliwa kwa namna ambavyo bloga aliona inastahili. rai...
Hizi ni baadhi ya picha tu za jinsi shughuli za kumuaga zilivyofanyika.Picha zimechukuliwa kwa namna ambavyo bloga aliona inastahili.
rais akitoa pole kwa familia
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo, Agosti 10, 2011, ameongoza mamia ya wananchi kuuga mwili wa Ofisa wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Luteni Jenerali (Mst) Silas Peter Mayunga katika shughuli iliyofanyika kwenye Viwanja vya Hospitali ya JWTZ ya Lugalo, mjini Dar Es Salaam.
Jenerali Mayunga alifariki dunia mwishoni mwa wiki katika Hospitali ya Apollo, iliyoko mjini New Delhi, India. Alikuwa na umri wa miaka 71.
Mara baada ya kuwasili kwenye viwanja hivyo, Rais Kikwete alikwenda moja kwa moja kutia saini kitabu cha rambirambi na baada ya kumaliza kutia saini, jeneza lililobeba mwili wa Jenerali Mayunga likiwa limebebwa na mameja waliosindikizwa na makanali wa JWTZ lililetwa kwenye viwanja vya hospitali hiyo.
Rais Kikwete akifuatana na Mama Salma Kikwete alikuwa wa kwanza kutoa heshima zake za mwisho kwa mwili wa Jenerali Mayunga akifuatiwa na Makamu wa Rais, Mheshimiwa Dkt. Mohamed Gharib Bilal na Rais Mstaafu Mheshimiwa Benjamin William Mkapa.
Viongozi wengine walioaga mwili wa Jenerali Mayunga walikuwa ni pamoja na mawaziri wakuu wastaafu Mheshimiwa Salim Ahmed Salim na Mheshimiwa Joseph Sinde Warioba, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Davis Mwamunyange, Waziri wa Ulinzi, Mheshimiwa Hussein Mwinyi na Mnadhimu Mkuu wa JWTZ, Jenerali Shimbo ambao walifuatiwa na maofisa wengine wa jeshi na wananchi.
Kwa mujibu wa mipango ya mazishi, mwili wa Jenerali Mayunga utasafirishwa kesho, Alhamisi, Agosti 11, 2011 kwenda kwao Maswa, mkoani Shinyanga ambako imepangwa kuwa utazikwa keshokutwa.
Luteni Jenerali Silas Peter Mayunga alizaliwa Maswa, Shinyanga mwaka 1940. Alijiunga na Jeshi la Tanganyika Rifles Januari 10, mwaka 1963, baada ya kumaliza elimu ya sekondari katika Shule ya Sekondari ya Bwiru, Mwanza.
Alihitimu kozi ya Uofisa wa Jeshi Julai 26, 1963, nchini Israel, akahitimu kozi ya Unadhimu na Ukamanda wa Jeshi mwaka 1973 nchini Canada na kuhitimu kozi ya Ukamanda wa Juu wa Jeshi mwaka 1974 hapa nchini.
Alipandishwa cheo na kuwa Luteni Jenerali Juni 21, mwaka 1995 na kabla ya kustaafu jeshini Desemba 31, 1995, alipata kuwa Mkurugenzi wa Mafunzo katika Makao Makuu ya Jeshi, Mkurugenzi wa Tawi la Mafunzo Makao Makuu ya Jeshi, Kamanda wa Brigedi ya 202 ya Tabora, na Kamanda wa Divisheni za 20 na 30 za Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).
Jenerali Mayunga alishiriki kikamilifu Vita Dhidi ya Iddi Amin katika Operesheni Chakaza ambako alikuwa Kamanda wa Brigedi ya 206 na baada ya hapo kuwa Kamanda wa Kikosi Maalum cha JWTZ nchini Uganda kati ya 1979 na 1980.
Mbali na jeshi, Jenerali Mayunga alitumikia umma kama Mkuu wa Mkoa wa Singida mwaka 1977 – 1978, Katibu wa Chama wa Mkoa wa Kilimanjaro 1983-1988, Balozi wa Tanzania katika Nigeria kati ya 1989 hadi 1998 na Balozi wa Tanzania katika DRC kati ya 1998 na 2002 alipostaafu utumishi wa umma.
Viongozi wa sasa na wa zamani kwa jinsi walivyoweza kupatikana wakisubiri utaratibu.
Mkuu wa majeshi akitoa saluti
Rais mstaafu, mzee wa displini,Benjamin Mkapa akitoa salamu za mwisho

COMMENTS