MKOA wa Rukwa unakabiliwa na changamoto ya kukamilisha agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr Jakaya Kikwete juu ya ujenzi wa...
MKOA wa Rukwa unakabiliwa na changamoto ya kukamilisha agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr Jakaya Kikwete juu ya ujenzi wa maabara katika shule za sekondari nchini baada ya kubainika kuwa ni shule zilizokamilisha ujenzi wa maabara ni asilimia 10.6 ya shule zilizopo mkoani humo.
Akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa agizo la Mhe Rais juu ya ujenzi wa maabara katika shule za sekondari mkoani Rukwa mbele ya kamati ya siasa ya CCM ya mkoa na madiwani wa mkoa huo, Afisa elimu wa mkoa wa Rukwa Stephen Mgina alisema mkoa una maabara zilizokamilika 22 tu kati ya mahitaji ya maabara 207 sawa na asilimia 10.6
Mgina alisema mkoa una jumla ya shule za sekondari 69 zenye mahitaji ya maabara 207 kati ya hizo maabara zinazojengwa na ziko katika hatua ya umaliziaji ni maabara 8, lenta ni maabara 27, katika hatua ya msingi ni 56 na maabara 94 hazijaanza kujengwa kabisa sawa na asilimia 45.4
Akizungumza katika kikao hicho mwenyekiti wa CCM mkoa wa Rukwa Hypotus Matete alisema agizo la Mhe Rais siyo la kubeza ni lazima kila mmoja awajibike nal na wala hakuna haja ya kutengeneza sababu kwani ni agizo la mkuu wa nchi ambaye hawezi kutania katika maagizo.
Alisema madiwani wasibweteke na kuona kuwa agizo hilo ni la wataalamu peke yao kwani hakuna asiyekuwa na jukumu katika agizo la Mhe Rais ambalo lina lengo la kuongeza wigo wa ajira kwa vijana wa Tanzania kutokana na ukweli kuwa nchi kama China wamepiga hatua kimaendeleo kutokana na kuwekeza vya kutosha katika teknolojia na vyuo vya sayansi vya VETA.
Wakizungumza katika kikao hicho baadhi ya madiwani walilalamikia kitendo cha baadhi ya watumishi wa serikali kukataa kuchangia michango ya ujenzi wa maabara katika maeneo yao na kuomba serikali ya mkoa kutoa tamko litakaloelekeza kama ni halali kwa mtumishi kukataa kuchangia maendeleo katika eneo analoishi au la.
Akitoa tamko kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Rukwa, Mkuu wa wilaya ya Sumbawanga, Mathew Sedoyeka alisema ni lazima mtumishi yeyote kuchangia michango ya maendeleo na ya kijamii katika eneo analoishi na akibainika kuwapo mtumishi anayegomea michango hiyo serikali itamchukulia hatua za kinidhamu.
Baada ya kikao kila diwani alitoa ahadi ya kukamilisha ujenzi wa maabara katika shule yake ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Mhe Rais kabla ya muda uliopangwa ambapo mkoa uliagiza kukabidhiwa maabara hizo kabla ya tarehe 15 Novemba ili kuandaa taarifa ya kumkabidhi Rais kabla ya muda alioagiza.
Hata hivyo baadhi ya wananchi walionesha mashaka ya kukamilisha kiukweli ujenzi wa maabara hizo na ubora wake kwani muda uliobaki ni siku sitini tu za kukamilisha ujenzi huo.
Source:Na Willy Sumia, Sumbawanga

COMMENTS