LELETI Khumalo ni mmoja wa wadada walioleta heshima kubwa katika tasnia ya filamu kutokana na uwezo wake wa kuigiza ambao aliuonesha kati...
LELETI Khumalo ni mmoja wa wadada walioleta heshima kubwa katika tasnia ya filamu kutokana na uwezo wake wa kuigiza ambao aliuonesha katika sinema inayoelezea historia na dhamira ya mapambano ya kudai haki, sinema ya Sarafina iliyochezwa mwaka 1992.
Binti huyu aliyezaliwa mwaka 1970 kutoka kabila la Wazulu nchini Afrika Kusini ameshacheza sinema nyingine nane maarufu ambazo zimempa heshima kubwa na ni kutokana na heshima hiyo Tamasha la Filamu la Zanzibar (ZIFF) wamemwalika na kwa mujibu wa Meneja wa Tamasha hilo Daniel Nyalusi kila kitu kiko sawa kwa Watanzania kumuona binti huyu wa Afrika Kusini ambaye ameleta utamu mkubwa katika sinema za mapambano dhidi ya ugandamizaji.
Binti huyu ambaye pia ameshacheza filamu hizo Uzalo (2015 -) ,Winnie Mandela (2011), Invictus (2009), Faith's Corner (2005), Hotel Rwanda (2004), Yesterday (2004), Cry, the Beloved Country (1995), Sarafina! (1992) na Voices of Sarafina! (1988).
Wakati nazungumza na Daniel Nyalusi kuhusu ugeni mzito katika tamasha la nchi za jahazi (ZIFF) Julai mwaka huu alisema kwamba pamoja na Leleti khumalo atakuja pia Mtengeneza sinema ya Selma, Ava Duvernay Director.
Leleti Khumalo ambaye amepata sifa si tu katika Sarafina bali pia katika sinema ya Hotel Rwanda na Yesterday alizaliwa Machi 30, 1970, eneo la KwaMashu, kaskazini mwa Durban, Afrika Kusini na kuwa katika safari ndefu ya sanaa kuanzia alipokuwa na umri mdogo.
Alianza kujihusisha na sanaa kwa kujiunga na kundi la Amajika, lililokuwa likiongozwa na Tu Nokwe.
Mwaka 1985, aliwania nafasi katika kazi ya Mbongeni Ngema ya Sarafina!, Ngema aliandika mitiririko ya aya za Sarafina kwa ajili ya Khumalo. Khumalo alifanya mchezo huu kwanza jukwani na mwaka 1988 alitajwa kuwania Tuzo ya Tony. Baadaye mchezo huo ulipelekwa duniani kote na mwaka 1987 Khumalo alipokea tuzo ya NAACP ya muigizaji bora wa kike katika jukwaa.
Mwaka 1992, aliigiza pamoja na Whoopi Goldberg, Miriam Makeba na John Kani katika filamu ya Darrell James Roodt ya Sarafina!. Filamu hii ilipata sifa kubwa sana, sifa ya kumpatia nafasi ya kuchaguliwa tuzo ya Image sanjari na akina Angela Bassett, Whoopi Goldberg na Janet Jackson.
Sarafina ambayo imejijenga kwa kuangalia machafuko ya Soweto ya mwaka 1976 inaelezea habari za msichana mmoja wa shule ambaye alikuwa na moyo wa ujasiri kiasi cha kupeleka ushawishi kwa wanafunzi wenzake kufanya uasi hasa baada ya mwalimu wake Mary Masombuka (Goldberg) kutiwa jela.
Filamu hii ilifanyiwa toleo la pili Juni 16 ,2006 kuadhimisha miaka 30 ya machafuko ya Soweto.
Khumalo si tu muigizaji bali pia ni mwimbaji na alishiriki kitu kingine cha Mbongeni Ngema cha Magic at 4 AM rasmi kwa ajili ya Muhammad Ali , kisha Mama (1996), iliyomwezesha kutembelea Ulaya na Australia. Na mwaka 1997, aliigiza Sarafina 2.
Mwaka 2004 Khumalo aliigiza Hotel Rwanda na Yesterday, na kutajwa katika tuzo za Oscar za 2005 kategori ya "Best Foreign Language Film". Yesterday ilipata tuzo ya sinema bora ya tamasha la Pune International la India na kupata heshima kubwa katika matamsha ya sinema ya Venice na Toronto .
Khumalo si tu anaigiza katika sinema lakini kwa wale wanaopenda kuangalia tamthiliya wanaweza kumkuta katika Generations mwaka 2005 hadi 2007 kama Busiswe (Busi) Dlomo, mama asiyetaka masikhara akiendesha kampuni yake ya uchapishaji huko Cape Town.
Leleti Khumalo ambaye unaweza kusema kwamba ni muigizaji wa mfano nchini Afrika Kusini aliwahi kuolewa na Mbongeni Ngema kuanzia mwaka 1992 na walitengana mwaka 2005.
Binti huyu ambaye kwa sasa anaishi na Skhuthazo ambaye ni mdogo kwake kwa miaka miwili Novemba 2012 alijifungua pacha wawili. Alikutana na mwanamume huyu wakati akifanya kazi katika shirika la ndege la Afrika Kusini SAA. Aidha amekuwa mtangazaji katika stesheni ya Vuma FM.
Binti huyu ambaye atakuja Tanzania ameonesha umahiri wake katika michezo ya kuigiza, uwasilishaji wa vipindi na hata kwenye sinema.
Wengi wetu pengine hatujaona sinema ya Yesterday ambapo suala la Ukimwi limezungumzwa sana na huenda kuja kwake tutazidi kumtambua zaidi.
mwisho/FM

Leleti na mumewe wa sasa Skhuthazo Kanyile |

COMMENTS