Mwalimu wa Yoga wa kimataifa,Sensei Rumadha Fundi (PICHANI) katika akitafakari kwa njia ya sanaa ya Yoga. Meditation &am...
Mwalimu wa Yoga wa kimataifa,Sensei Rumadha Fundi (PICHANI) katika akitafakari
kwa njia ya sanaa ya Yoga.
Meditation
& Mantra
Mara nyingi neno”Meditation”
au kutafakari huchanganywa na kufikiri ni kukaa kimya kufumba macho
kiufanisi au kuwaza jambo fulani. Pia, wengine huchanganya hili neno na kuwa
umekaa kimya na kujaribu kutofikiria lolote, ama pia kuivuta au kuisukuma akili
yako na kutoku fikiria kitu cha iana yeyote ile muda wote wa kutafakari na
kuamini kwamba hiyo ni “Meditation” au Tafakari. Kamwe, hamna hata moja
ya mifano hii inaweza kuifikia maana yake halisi katika mfumo kisayansi na
filosofia ya “Yogic”.
Kisayansi ya Yoga, “Meditation”
inaitwa “Mtiririko wa akili”( Flow of the mind).” Kuiongoza akili au
mawazo ya mtu kupia Meditation, inahitaji pointi au sehemu muhimu katika
maungo yako unayo kuwa unatumia kama vile mfano wa mionzi ya akili kuirushia na
kuelekeza katika sehemu moja tu. Hivyo kwa kutumia msaada wa sauti maalum
itwayo “Mantra”, hiyo ndio chombo hutumika kupitia mkufunzi aliye hitimu
Sanaa ya Yoga na kufundisha kutokana na mazingira tofauti kati ya tofauti
za watu zilivyo.
Kama jinsi inavyoelezwa katika
filosofia ya Yoga kwamba, akili ya mwana adam, kamwe haitulii, wakati
wote ipo mbio na inatafuta cha kufikiri, hivyo basi huwa ni kazi ngumu sana kwa
mtu hata kuanza tu somo la kwanza (First lesson), kwa mistuko ya
mchanganyiko wa mawazo ya mwana adam. Hivyo huwa taabu sana kukusanya mawazo
yako binafsi na kufanya meditation bila muongozo wa kiutaam.
Napenda kuongelea vitu vichache
hapa. Kuna vitu, au pointi tano tofauti zilizo muhimu na utumika katika mbinu
za kutafakari kwa jina la “Sense withdrawal”, ambayo huitajika
ili uweze kushawishi akili yako na mawazo kwamba utaweza kutafakari bila
vikwazo vya mawzo yoyote au kuwa na utata katika mfomo mzima wa kutafakari.
Ufuatao ni muktasari tu wa jinsi gani wana-Yoga wana tafakari kwa masaa mengi
bila mgongano au (interraption) kupitia njia hii:
1.
Asana (Mkao wa mazoezi ya Yoga): “Lotus posture” kukunja miguu. Faida
zake; kuweza kumiliki viungo vya mwili wakati wa kutafakari. Ndipo jinsi
unaweza kumiliki viungo vya mwili wako vinavyokuwezasha kuona vitu “Sensory
organs”. Kufumba macho, kutokuona kinachoendelea nje ya upeo wa macho ili
kuweza kuelekeza mionzi ya fikra zako (Focus) sehemu moja tu. Kukunja
ulimi zidi ya dari ya mdomo “Roof of the mouth” (Palate) wako ili
kuweza miliki hamu ya kuonja radha au haja ya chakula chochote kile (Control
taste). Kukunja mikono na vidole kuweza kumiliki hamu ya kushika kitu
(Control sense of touch). Kitu kisicho wezekana kukimiliki ni harufu ( Sense
of smell), na ndio maana “Meditation” hufanywa katika
mazingira safi bila moshi wala harufu mbaya kuepuka mkatiko wa mtiririko
wa mawazo waka wa kutafakari.
2. Kutoka
katika mazingira ya mzumguuko wako wa kila siku (Withdrawl from external
world) “Bhuta Shuddhi”. Kujitoa kimawazo kiuwoga wa matatizo ya kila siku
kimaisha, kuwa umetulia mwili wako wakati wa kutafakari (Relaxation).
3. Kujitoa
kimawazo katika mwili wako mwenyewe (Withdrawal from the body) “Asana
Shuddhi”. Kutowaza lolote kuhusu mwili wako na hali yake nzima au
kutokuambatanisha fikra zako katika maumbile ya mwili wako ( Withdrawal from
each parts of your body; concentrate in one singular point) “Ista Chakra”.
4. Kujitoa
kabisa kimawazo (Withdrawal from thoughts of interruption) “Citta
Shuddhi”, hapa katika hatua hii, mraba wa akili unakuwa unaelea kimawazo
sambamba katika anga za ulimwengu (Total suspension of mind in cosmic space;
Consciousness)
5. Mtiririko
wa mawazo na Mantra ( Flow of mind) “Dhyana” hii ndio njia nzima ya
utaratibu wa kufanya Meditation, au kwa namna nyingine ni mwanzo
wa Kutafakari (Process to start meditating). Hapa ndipo sasa mkufunzi wa
taaluma ya Yoga anakuwa anarudia kimoyo moyo Mantra aliyoisoma, sasa
hapa ndipo mwanzo wa kile tunaita “Tafakari”. (Meditation).
zipo njia nyingi
zaidi za kufanya “Meditation” au kutafakari ngazi ya juu zaidi
kupitia njia ya pumzi au “Prana Yama”(Vital Breathing). Hivyo, huu hapa
ni muktasari tu wa jinsi na namna gani tunaitafsiri “Meditation ” au
kutafakari kupitia mafunzo ya Yoga. Hayo pia ni machache naona vizuri
kushirikiana na kumulika mwanga kidogo kwa wale wasio fahamu nini hasa maana ya
Meditation kupitia Sanaa ya Yoga.
Imeandikwa na
mkufunzi wa Sanaa ya Yoga, Rumadha Fundi, mwenye uzoefu mkubwa na diploma
ya somo la Yoga toka “ College of Neo-humanists Studies, Gullringen, Vimmerby,
Sweden, aliyopa mwaka 1986 na hatimae baadae mwaka 1987 kwenda Tiljala,
Culcutta, India, na kupata shahada ya juu kabisa ya Yoga duniani ijulikanayo
kwa jina la “Avadhuta”.
COMMENTS