Ana tuzo 6 kimataifa ikiwemo ya anga za juu Ndiye anayesimamia urushaji wa satelaiti ya Tanzania Na Rahel Pallangyo TANZANIA...
Ana tuzo 6 kimataifa
ikiwemo ya anga za juu
Ndiye anayesimamia urushaji wa satelaiti ya Tanzania
Na Rahel Pallangyo
TANZANIA inapoende lea kujitangaza katika ulimwengu wa
teknolojia ya anga, ikitengeneza mradi wa kurusha satelaiti yake angani hivi
karibuni, jina moja linalo simama kidete kama kinara wa juhudi hizo ni Dk Sisti
Cariah.
Zao la Chuo Kikuu cha Riga (RAI), taasisi inayotambulika
hasa katika eneo la Baltic na Ulaya, kwa kutoa mafunzo ya uhandisi wa ndege za
abiria, usafiri wa anga za juu. Dk Sisti ni mtaalamu mbobezi katika masuala
nyeti ya anga za juu ikiwamo usafiri na uhandisi wa anga.
Katika mazungumzo na Dk Ca riah, anaonesha tuzo za utambuzi
tisa tofauti ambazo ni pamoja na ya mashindano ya kurusha satelaiti ndogo
kupitia programu ya Kibo Cube ya Japan. Ana machapisho 10 yanayohusu nyanja
mbalimbali kama uhandisi wa uramba zajI wa ndege na vifaa vya angani,
usindikaji wa ishara na hisabati.
Katika maendeleo ya
teknolojia na sayansi ya anga za juu nchini Tan zania, Dk Sisti anasimama kama
nguzo kuu yamaendeleo akiwa ni mhandisi wa mifumo tata na uhandisi wa anga
aliyesajiliwa na Bodi ya Usajili ya Wahandisi (ERB).
Sifa hizo zinamfanya Dk Sisti kuwa kinara wa mradi wa kihistoria
wa Tanzania wa kurusha satelaiti ya kwanza, TanzaniteSat-1, unaoratibiwa na
Taasisi ya Teknolo jia Dar es Salaam (DIT). Uongozi wake katika mradi huu
umepata baraka kutoka kwa Umoja wa Mataifa wa Masuala ya Anga za Juu (UNOOSA)
na Shirika la Utafiti wa Anga la Japani (JAXA). Vyombo hivi viwili vimemtambua
kama mta fiti mkuu wa kimataifa.
Asili na safari ya kielemu
Dk Sisti amezaliwa Kata ya Kaloleni, Wilaya ya Arusha na
baba yake alikuwa askari polisi katika kikosi cha mawasiliano na alitamani
watoto wake wawe wata alamu wa mawasiliano angani. Baba yake alipata uhamisho
wa kikazi na kuhamia Moshi. Huko ndiko alikoanza elimu katika Shule ya Msingi
Kibo (sasa Nyerere).
“Shule ya awali
nilisoma siku moja kwa kuwa nilikuwa najua kusoma na kuandika, pia kuhesabu na
vyote nilijifundisha mwenyewe. Siku ya pili nilianza darasa la kwanza, baada ya
walimu kurid hika siyo tu kusoma na kuandika na hesabu zinazozidi kiwango cha
darasa la kwanza hadi la nne,” anasema Dk Sisti.
Anasema baadaye alifaulu kwenda Shule ya Sekondari Mawenzi
na kidato cha sita alisoma Satelaiti Shule ya Sekondari na Ufundi Tanga ambapo
alichukua masomo ya Fizikia, Kemia na Hesabu (PCM). Alianza masomo ya Chuo
Kikuu cha Anga cha Riga nchini Latvia akibobea katika mifumo ya uhandisi wa
anga mojawapo ya fani kongwe na ya kimka kati katika nyanja za sayansi na
teknolojia.
Kwa mujibu wa maelezo yake, fani hiyo inakusanya utaalamu
kutoka maeneo mbalimbali; uhandisi wa kompyuta, uhandisi wa umeme, mawasiliano
ya simu, uhandisi wa ndege, mifumo ya satelaiti na mitandao.
“Fani hii ilitolewa kwa wazawa pekee na si kwa wanafunzi
kama sisi kutoka nje ya nchi. Niliomba na kwa kuwa nilikuwa na bidii sana
kimasomo nilikubaliwa. Niliweka bidii kubwa, nikaendelea na masomo hayo hadi
kufaniki sha kupata Shahada ya Uzamivu katika fani hiyo,” anasema Dk Sisti.
Anasema pamoja na ugumu wa masomo, anaishukuru sana familia yake.
“Familia yangu imekuwa na mchango mkubwa hususani kaka yangu
Wilhelm Karia ambaye alini hamashisha kupenda uhandisi. Wengine walinitia sana
moyo,” anasema Dk Sisti.
Safari ya utaalamu wa kina
Safari ya elimu ya Dk Sisti ni ushahidi wa jitihada na
umahiri wake. Alipata Shahada ya Kwanza katika Uhandisi wa mifumo kutoka Chuo
Kikuu cha Anga cha Riga kati ya mwaka 1988 na 1994, ambapo alitambuliwa kwa
utendaji bora katika kubuni mfumo wa kupima viashiria vya ndege. Katika kipindi
hicho hicho, alihitimu Shahada ya Uzamili katika Sayansi ya Kompyuta,
akizingatia hasa uchakataji na uchujaji wa taarifa za satelaiti.
Kati ya mwaka 1994 na 1997, alipata Shahada ya Udaktari wa
Sayansi ya Uhandisi kutoka Chuo Kikuu cha Anga cha Riga, ambapo tasnifu yake
ilihusu mifumo na vifaa vya kielektroniki vya redio kwa ajili ya ndege na
satelaiti.
Mafunzo yake mengine ni pamoja na utafiti mwingi wa kiteknolojia
na kozi fupi mbalimbali. Hizi ni pamoja na Cheti cha Hisia-Anga na akili unde
kutoka Chuo Kikuu cha RUDN, Moscow (2024) na kozi fupi za GIS na Hisia Anga
(2024).
Vilevile, alipata mafunzo ya kubuni, kujaribu na kurusha
satelaiti ndogo kutoka KiboCUBE Academy nchini Japan (2023) na mafunzo ya
teknolojia ya makombora na magari ya kurushia satelaiti nchini Uingereza
(2022). Pia, amepata mafunzo ya ukuzaji wa uwezo wa anga nchini Marekani (2021)
na ya matumizi ya satelaiti ya hisia-anga nchini China (2022). Hivi karibuni,
amepata mafunzo ya teknolojia ya msingi ya anga nchini Misri (2025).
Uzoefu na michango yake katika sayansi Katika utaalamu wake,
Dk Sisti amefanya kazi nyingi za kimataifa zenye faida kubwa. Mwaka 1997,
alibuni mfumo wa urambazaji wa ndege unaowezesha ndege kuruka katika njia
yoyote, wakati wowote. Pia, aligundua Confluence Kalman Filtration, mfumo wa
kipekee wa uchujaji wa taarifa za satelaiti unaoboresha usahihi wa vifaa vya
urambazaji wa satelaiti.
Miaka ya 1993 na 1994, alibuni mfumo wa kompyuta wa kukagua vifaa vya ndege kwa ajili ya kubaini vifaa vinavyoweza kuharibika ndege ikiwa angani, ambapo ndiyo iliyopelekea kut ambuliwa kama mwanafunzi bora katika Nchi ya Latvia mwaka huo.
Pia, kipindi hicho
hicho alitengeneza programu ya kuangalia ubora na kushauri matengenezo ya
helikopta kwenye kompyuta katika sehemu ya helikopta ya Shirika la Ndege la
AVIANCA nchini Colom bia, ulioboresha usimamizi katika sehemu ya helikopta.
Mchango wake kwa Tanzania ni muhimu zaidi, hasa katika
Teknolojia ya Habari na Maende leo (TEHAMA) na usimamizi wake. Kuanzia mwaka
2004 hadi 2015, aliratibu miradi mbalim bali iliyofadhiliwa na Shirika la Umoja
wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo (UNDP) ndani ya Tume Huru ya Taifa ya
Uchaguzi (INEC), na alisimamia uanzishwaji wa Daftari la Kudumu la Taifa la
Wapigakura. Mwaka 2014, alibuni mfumo wa kisasa wa usajili wa alama za vidole
ambao ulifanya vizuri zaidi duniani na alipanga na kusimamia kampeni ya nchi
nzima ya usajili wa wapigakura kwa kutumia alama za vidole (BVR) mwaka 2015,
akisajili wapigakura milioni 23.6 ndani ya miezi mitano.
Mafanikio haya yalisababisha kupata Tuzo za Kimataifa za APS
CA Radiant. Dk Sisti pia alihusika katika uboreshaji wa mifumo ya ramani (GIS)
ya Jeshi la Wananchi na mawasiliano ya radio ya Jeshila Polisi Tanzania.
Kati ya mwaka 2016 na 2018, alihudumu katika Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.
Tuzo, uanachama na machapisho
Umaarufu na utaalamu wa Dk Sisti umetambuliwa kimataifa
kupitia tuzo na uanachama mbalimbali. Mwaka 1996, alishinda tuzo ya kimataifa
ya Mwanasayansi Chipukizi kwa kazi yake ya utafiti katika uchakataji wa taarifa
za anga.
Sisti anajulikana kwa machapisho kadhaa, ikiwemo kitabu cha
Hisabati ya Anga kinachotara jiwa kutangazwa mwaka huu wa 2025. Ni mwanachama
wa Taasisi ya Wahandisi wa Elektroniki na Umeme (IEEE) katika eneo la anga
Marekani tangu mwaka 1997 na amesajiliwa na ERB kama Mhandi si Mshauri (230) na
Mhandisi Mtaalamu (2389)
Mradi wa Satelite wa Tanzanite Sat-1
Akizungumzia Mradi wa TanzaniteSat-1, Dk Sisti anasema ni
mradi wa kimkakati ukilenga kuandaa wataalamu wengi wa anga za juu, ili
Tanzania iwe na nguvukazi yenye uwezo wa kush iriki kikamilifu katika mapinduzi
ya kiteknolojia ya anga.
DIT imejipanga kupitia programu maalumu ya kuandaa wataalamu
wa anga za juu kwa kutumia dhana yake ya ufundish aji ya mafunzo viwandani.
Kupitia dhana hiyo, wanafunzi na watafiti wanashirikishwa moja kwa moja katika
kusanifu, kujenga, kurusha na kutumia satelaiti, huku wakiji funza matumizi
yake katika sekta mbalimbali za maendeleo ya taifa.
Sekta zote za kiuchumi zinahi taji kuwezeshwa na satelaiti,
jambo linalothibitisha kuwa teknolojia ya anga siyo anasa, bali ni nyenzo ya
msingi ya maendeleo. Hii pia ime ainishwa wazi katika Agenda 2063 (The Africa
We Want) na ndiyo dira ya Rais Samia Suluhu Hassan ya kuifanya Tanzania kuwa
kinara katika matumizi ya teknolojia za kisasa kwa maendeleo ya wanan chi wake.
“Katika utekelezaji
wa pro gramu hiyo, DIT imepanga kuru sha angalau satelaiti tatu na tayari
imeanza kuandaa algorithms za kimkakati zitakazotumika kusaidia sekta
mbalimbali nchini,” anasema Dk Sisti.
Dira ya baadaye
Dk Sisti anawaambia Watanza nia teknolojia ya anga za juu ni
nyenzo muhimu na mkombozi wa maendeleo katika sekta zote. Hii siyo tu sayansi
ya uchunguzi wa nyota na satelaiti, bali ni injini ya mageuzi ya kiuchumi na
kijamii.
Anasema sekta ya anga za juu ni chanzo kipya cha mapato,
chenye uwezo wa kuzalisha fedha nyingi na wakati huo huo kusaidia sekta
nyingine hususani kilimo, uvuvi, afya, elimu, mazingira, nishati, usalama na
miundombinu kuongeza tija na mapato kwa kiwango kikubwa.
CHANZO: Rahel pallangyo, HabariLeo
COMMENTS