Mwanadamu arejea mwezini:Ratiba ya Kila Siku ya Wanaanga wa Artemis kuuzunguka

  Safari ya siku 10 ya Artemis 2 ya NASA inajawa na tafiti za kisayansi, majaribio ya chombo, uchunguzi wa afya, mafunzo ya kujiokoa na me...

 


Safari ya siku 10 ya Artemis 2 ya NASA inajawa na tafiti za kisayansi, majaribio ya chombo, uchunguzi wa afya, mafunzo ya kujiokoa na mengine mengi.

Artemis 2 ya NASA inasafirisha wanaanga wanne katika safari ya siku 10 kuzunguka mwezi.

Wafanyakazi hao watakuwa ndani ya chombo cha Orion, wakitekeleza malengo mengi yakiwemo safari ya kwanza ya binadamu kupita karibu na mwezi katika kipindi cha zaidi ya nusu karne.

Wanaanga hao watatumia takriban saa tatu katika eneo la karibu zaidi na mwezi, na kila dakika ya safari yao imepangwa kwa umakini.

Wanaanga hao Reid Wiseman, Victor Glover, na Christina Koch (NASA), pamoja na Jeremy Hansen (Shirika la Anga la Kanada) wanatarajia kuleta utaalamu mpya kuhusiana na mwenendo wa safai na jinsi mwezi unavyoonekana.



Mchanganuo wa ratiba yao ya kila siku uko hivi:

Siku ya Urushaji Aprili 2(Launch Day)

Dakika nane za kwanza ni muhimu zaidi. Wanaanga watarushwa na roketi ya Space Launch System (SLS). Baada ya kufika angani, chombo cha Orion kitatengana na roketi na kuanza mfululizo wa majaribio.

Majaribio ya Ukaribu (Proximity Operations): Wanaanga wataendesha Orion kuzunguka sehemu ya roketi iliyotumika (ICPS) ili kudhihirisha uwezo wa Orion wa kuruka karibu na vitu vingine angani. Baada ya hapo, wataanza ukaguzi wa mifumo, kuvua suti zao za anga na kuvaa nguo za kawaida kabla ya kulala kwa saa 8.5.

Siku ya 2: Mazoezi

NASA imeweka vifaa vya mazoezi ndani ya Orion ili kupunguza athari za hali ya kutokuwa na uzito (microgravity) mwilini.

Translunar Injection (TLI): Saa sita baada ya kuamka, wanaanga watafanya manuva ya TLI. Huu ni muungurumo wa injini kwa dakika 30 utakaokisukuma chombo kuelekea mwezini. Bila hatua hii, chombo kitabaki kuzunguka dunia pekee.

Siku ya 3: Mapigo ya Moyo na Uchunguzi wa Mwezi

Wakiwa njiani kuelekea mwezini, wanaanga watatumia siku hii ya tatu kufanyia mazoezi kazi watakazozifanya watakapofika karibu na mwezi. Ni muhimu kuzoea kufanya kazi hizi katika hali ya kutokuwa na uzito. Pia, watafanya mazoezi ya usalama, ikiwemo huduma ya kwanza ya mapigo ya moyo (CPR) angani.

Siku ya 4: Picha za Dunia na Mwezi

Siku ya nne Orion itafanya marekebisho madogo ya njia. Wanaanga watatumia muda mwingi kuwasiliana na kituo cha udhibiti duniani na kufanya mazoezi ya kutumia darubini. Dakika 20 zimetengwa mahususi kwa ajili ya kupiga picha za Dunia na Mwezi wakiwa katikati ya safari.

Siku ya 5: Kuingia Katika Eneo la Mwezi

Hii ndiyo siku ambayo nguvu ya mvutano ya mwezi inakuwa na nguvu zaidi kuliko ya Dunia kwa chombo cha Orion.

Wanaanga watafanya majaribio ya kuvaa suti zao za anga kwa haraka (donning test) ili kujiandaa na dharura yoyote ya kupotea kwa hewa ndani ya chombo.


Siku ya 6: Kupita Karibu na Mwezi (Lunar Flyby)

Hii ndiyo siku kuu ya shughuli yenyewe! Wanaanga watapita umbali wa maili 4,000 hadi 6,000 (kilomita 6,440 - 9,650) juu ya uso wa mwezi. Kwa wanaanga hao, mwezi utaonekana mkubwa kama mpira wa kikapu ulio karibu. Watatumia saa tatu kuchukua data, kupiga picha, na kuchunguza maumbo ya kijiolojia.

Siku ya 7: Kurudi Duniani na Mawasiliano na ISS

Siku ya saba ya safari Orion itaanza taratibu za kurejea duniani. Wanaanga watatuma data kwa wanasayansi duniani kuhusu utendaji wa chombo na hali zao za kisaikolojia.

 Pia, kutakuwa na tukio la kihistoria: mazungumzo ya sauti kati ya wanaanga wa Orion na wale waliopo kwenye Kituo cha Kimataifa cha Anga za Juu (ISS).

Siku ya 8: Kinga dhidi ya Mionzi na Manuva

Kinga ya Mionzi: Ili kujilinda na mionzi ya jua, wanaanga watatumia matangi ya maji ya chombo hicho kama ngao ya kujikinga na mionzi upande mmoja.

Udhibiti wa Mkao (Attitude Control): Watafanya majaribio ya uendeshaji wa chombo kwa kutumia mifumo tofauti ya injini ili kuona jinsi chombo kinavyoweza kugeuka bila kupoteza njia yake.

Siku ya 9: Maandalizi ya Mwisho

Wanaanga wataanza kufunga kila kitu na kujiandaa kwa ajili ya kutua. Watavaa nguo maalum za kubana (compression garments) zinazosaidia mwili kuhimili mabadiliko ya shinikizo utakapofika duniani baada ya kukaa muda mrefu bila uzito.

Siku ya 10: Kuingia Kwenye Anga la Dunia na Kutua Baharini

Hii ndiyo hatua ya mwisho yenye joto kali. Orion itatenganisha sehemu yake ya huduma (service module) na kuelekeza ngao ya joto kuelekea mbele. Ngao hiyo itawalinda na joto la nyuzi joto 1,650 Celsius wakati wakipita kwenye anga la Dunia.

Miamvuli mitatu itafunguka ili kupunguza kasi, na chombo kitatua kwenye Bahari ya Pasifiki, karibu na pwani ya San Francisco, ambapo meli ya Jeshi la Majini la Marekani itawapokea na kuhitimisha safari hiyo.

 

COMMENTS

Name

Anga,11,Arusha,27,batiki,1,Burudani,420,burundani,2,come rain,1,come sun,1,Crazy in Love kama wimbo kama wao wenyewe,1,dahh sijui kweli mbona shida,1,Dar utakuja je tumejiandaa,1,daraja sahau nini,1,demokrasia ya upanga,1,Dodoma,78,Dole tupu vijana wa zamani,1,Duhh bibie endeleza libeneke,1,Duhh kaisikie Walibana,1,duhh kwa mbagala mama lazima awe supa,1,Fedha za maiti haziliwi bure,1,Fedha za watu kwa maendeleo ya watu,1,Fikira,14,filamu,277,Filamu ndio kielelezo cha ukuzi wa taifa,1,flamu,7,Gandamiza Kibara baba ake,1,haba,1,habar,2,Habari,6674,habari dodoma,38,habari. dodoma,32,habaria,1,hadithi,23,hakika tumeweka historia,1,hakuna noma jongwe,1,hapa kwetu inakuwaje vile,1,hasira hasara,1,hata maji,1,hataki masikhara na maisha yake,1,hatubonyezi kizenji,1,haya ndiyo mambo ya Ulaya,1,haya si yangu ni ya mdau mwenye hasira,1,haya wabongo na mambo kutoka nje,1,He he he wananikumbusha upishi wa shaba,1,Headline,1,Hii hurejesha uhai,1,Hii iko sawa kweli?,1,Hii imekaa vizuri,1,Hii inakaaje vile,1,Hii kweli noma,1,Hii maana yake Moro kuna uhaba wa chakula,1,Hii mexico,1,Hii mihasira mingine bwana,1,Hii ndio moro sio mpaka dar,1,hii ni hatari,1,Hii ni kiboko anayetaka kubisha ajibishie tu,1,Hii ni moja ya staili za kunyoa nywele,1,Hii si lukwangule,1,hii staili mpya,1,hili ni jengo pacha la malaysia ghorofa 88,1,Hivi ni ngoma tu,1,hivi nini siri za serikali,1,hivi sisi tunajua kama kuna vitu vya aina hii,1,hivi vitu bwana,1,Hiyo ndiyo gharama ya demokrasia,1,Hizi imani nyingine ni hatari,1,Hizi takwimu hizi mhh,1,Hongera bibie,1,Hongera dada etu kwa kutuletea kaka etu (shemeji) kwani mwenye dada hakosi shemeji,1,Hongera sana,1,huhitaji mifedha kuwa msafi,1,Huko Ulaya,1,Huu ndio ustaarabu,1,huu ujiko utakuwa mkubwa,1,imetosha,1,Inahitaji nidhamu fulani,1,inakuuma au...,1,Inakuwaje kama filamu yenyewe itahitaji busu la nguvu,1,Inaonekana watanzania hatukuwepo,1,Ipo kazi Maximo,1,Iringa,22,Isiwe mijineno tu manake mihela hubadili watu kweli,1,Itakuwa laki moja ya halali,1,jamani huu kama si ushamba kumbe nini,1,Jamani mbona Mungu anatupigania,1,Jamani watoto wanatakiwa kupendwa,1,jamani.. jamani ukiikosa Diamond usijutie,1,Je nyumbani hakuna vitu vya aina hii?Tuambie,1,je walikuwepo watu wa huduma ya kwanza,1,Je watanzania wanalipa kodi,1,jela kwa raha,1,Jolie,1,juhudi za lazima kuinua filamu,1,kama si kiwanda cha chumvi nani atawajua hawa,1,Kama kweli ndio kweli basi kila heri,1,Kama Mkristo naamini hilo hiyo si sahihi,1,kama unajua kuyarudi nenda Malta,1,kama wao wanaweza sisi je,1,Kamua baba waache wakanyagane,1,karibu nyumbani dada yote maisha tu,1,karibu Tatiii,1,KARIBUNI,1,Katavi,5,kaza buti hakuna kukata tamaa inalipa,1,kazi kwako mheshimiwa waziri wa madini,1,kazi na burudani,1,keep it up bloggers,1,kero ya usafiri sasa kwisha,1,Kila chenye roho na mwili kitaonja umauti,1,kila kitu kina vitu,1,Kila la Heri jamila,1,kila la heri kwani ni changamoto,1,Kipya,51,Kiuno bila mfupa,1,Kolelo mzimu ambao bado hai,1,KUBWA,1,Kudumisha urafiki wa dunia,1,Kuna dalili za wasomi kukubali Uafrika,1,kuna makala humu humu ndani ya blogu sijui mnasemaje,1,Kuu,113,kwa mara nyingine tena Tigo imewezesha,1,Kwa mchanganyiko huu muungano lazima udumu,1,Kwa mihasira hajambo,1,kweli,1,Kweli ina mkono mrefu tuone,1,Kweli duniani tunatofautiana,1,la maana ni kuwa na jiko au vipi,1,labda halitabadilika tena,1,lakini mwafaka lazima,1,lengo ni kutafakari,1,leteni vitu tuvione,1,lets us,1,Lucy wanakuelewa hawa...,1,Lukwangule nyumbani kwetu,2,M ungu bariki mikono ya madaktari wafanikiwe,1,MAARUFU,1,maendeleo ya soka siku zote yanahitaji fedha ili yapatikane,1,maisha ni vyema kuyaangalia,1,MAJIBU,1,makala,52,mama ni mama tu anapendeza,1,mambo mengine we angalia tu,1,mambo msimamo,1,mambo sasa mchanganyiko,1,Mara nyingine huona tunakotoka kwa kuona wenzetu,1,Mashabiki wa rhumba mpooooooooo,1,Masitaa,12,Maskani,1,MASOKO,3,Masupa staa mnaoinukia mpoo,1,Matamasha,6,mavazi ya kuogelea yanaposhindaniwa,1,Mbeya,11,Mchakamchaka anti Asmah,1,Mchanganyiko,81,MCHANYATO,1,mchezo,6,mengi wanayoyaita siri ni public information,1,mfumuko wa bei mpaka noma,1,Mhh sijui watu wa Sua ambao wako huko wanasemaje,1,Mhh ugua pole dada watu wanataka burudani,1,Michezo,695,Michezo maalum inatakiwa kupigiwa debe,1,miguu,1,miguu babu,1,Mikataba mingine ama hakika tuiangalie hata wakopeshaji nao wanatugeuza sakala,1,MIMI NI KISURA NAJITAMBUA,1,Mimi sijajua hasa kumetokea nini kwani ninavyojua hawa huwa na ungalizi wa hali ya juu,1,Mimi simo,1,mimi sisemi,1,miochezo,1,mkiwa chumvi basi mkoze,1,Mkiwa taa mulikeni,1,Mnaonaje je hii imekaa vyema,1,Mnaweza wakwetu hapa,1,Morogoro,51,mrithi wa mwanadada Whitney Houston,1,Mtwara,4,Mungu aiweke mahali pema roho yake,4,Mungu amrehemu,1,Mungu amweke pema peponi,1,Mungu awabariki sana,1,Mungu awe nao,1,Mungu ibariki Tanzania,1,Mungu tuepushe na imani hizi za kishirikina,1,mungu tufanye tuwe na upendo,1,Mungu twaomba utuhurumie,1,Muziki,370,muziki na fasheni,20,Mwanahabari,33,Mwanza,6,Mwendo mdundo dada,1,Mwenge huo utakimbizwa duniani kwa siku 130,1,Mwenge wa olimpiki ni ishara ya urafiki,1,Mzee wa Farasi nakupa saluti,1,Mzimbabwe huyu kutoka kwa mama mkali,1,N i dar mpaka Moro au bao tatu bila,1,Na sisi je,1,Naam kama haiwezekani hapa,1,Nairobi waanzisha tena utalii,1,namna bora ya kusaidia jamii,1,nani abebe hukumu na lawama,1,nani asiyejua utamu wa pipi,1,Nani kama baba,1,naona inafaa kuchangia mimi sitoi hoja,1,ndoa za mastaa huwa na mgogoro,1,nenda mwaya nenda,1,New Zanzibar Modern Taarab na wapenzi big up,1,news,5,Ni bikini kwa kwenda mbele,1,Ni Dar mpaka Moro au.. tatu bila,1,ni furaha za muungano,1,Ni kazi ngumu yenye kuhifadhi utamaduni,1,Ni kuchakarika kuonyesha urafiki na biashara pia,1,ni mfumuko wa bei au mfumuko wa nchi,1,Ni muhimu kutazama afya yako,1,ni muziki kwa kwenda mbele,1,Ni muziki mpaka China,1,Ni raha tupu,1,Ni Serengeti Premium Lager,1,Ni Tigo na mawasiliano ya kisasa,1,Ni wakati wa kuujadili utamaduni,1,Ni zaidi ya jazz,1,Nitasubiri and welcome home,1,nje je?,1,NUKUU YA LEO,1,nyie mnasemaje kuhusu hili,1,Ona Kolelo na sindikizwa na Wazee wa Gwasuma,1,ona vya dunia,1,One step ahead,1,patna mwingine mjamzito,1,Pengine anamuogopa Jada Pinkett manake kwa wivu..,1,picha,494,Pole Jamila hayo ndiyo mashindano,1,poleni sana,1,poleni sana wanyalukolo,1,Powa sana,1,Profesa jamaa wanakumaindi,1,Roho za marehemu zipate pumziko la milele,1,Ruvuma,9,sakata dansi mpaka kwenye kilele cha dunia,1,sasa kumebakia ugonjwa mmoja polisi kuendesha mashtaka,1,sasa mifedha kila mahali hongereni,1,Sasa ni mavuno,1,Sasa ni wakati wa kutafuta upenyo ndani ya IDOLS,1,SAYANSI,7,SAYANSI ANGA,8,See Uluguru Montains,1,serikali inataka kujihami kwanini,1,Show of support Big Up Madame,1,Si kitu kidogo hata kidogo,1,si unajua tena namie naimwaga hivyo hivyo,1,Siasa,346,siasa habari,2,Sijui kama City wanajua Mbagala noma,1,Sijui tunaishi karne gani yailahi,1,Sinema,17,sio advencha....kaaa ...niko kibaruani,1,Sisi ndio tunaanza vitongoji,1,Sisi yetu macho na masikio,1,Slow slow jamani,1,sto,1,tabasamu kali la mwenge wa olimpiki,1,Tabora,1,Tazama Waziri Mkuu Pinda wasije wakapindisha maamuzi yako,1,TEKNOLOJIA,1,Thats big man game,1,This is crazy Africa,1,This is Mgeta,1,Tibet wamegeuza Olimpiki jukwaa la siasa,1,Titbits collection,1,Tubadili tamaduni,1,Tuchangie mambo yaive,1,tuendeleze sanaa,1,tuienzi na sisi mbona wizara haituambii,1,Tuipeleke kaskazini,1,Tuisaidie serikali shida ya Mererani,1,tujue namna ya kupumzika,1,Tulienda kustarehe au kufanya fujo,1,Tumsaidie mtototo huyu kurejea katika hali ya kawaida,1,tunahitaji haya,1,Tunajifunza kweli kutoka kwao,1,Tunapandisha chati tu,1,Tunasubiri,1,tunazidi kuhesabu siku,1,TUNAZISUBIRI ZA VINARA ADAR,1,Tuombe nafuu kwa wagonjwa,1,Tuombe rehema kwa mungu,1,Tuone yatufae,1,Tusingoje wengine watusemee,1,tutampa tafu kubwa Prof,1,tuuenzi utamaduni au vipi,1,Tuukuze na kuulinda,1,tuvipende,1,tuwalinde maalbino,1,Tuwe kweli wakweli,1,ubunifu siku zote hulipa,1,uchumi huzunguka kwa kuwawezesha wasukaji,1,udumu muungano,1,Ugonjwa huu wa sasa ni kitendawili,1,Ukiiona kolelo utaipenda,1,Ukirejea salama kila mtu anafurahi,1,Umelenga Mkuchika utamaduni unakufa,1,unaposaka uwakilishi wa dunia,1,urafiki,1,urembo,1,Usisahau wazee wa Ngwasuma,1,UTALII,1,UTAMADUNI,4,Video,2,Vionjo vipya ndani ya Gwasuma,1,Vita dhidi ya ufisadi,1,vitongoji Miss Tanzania navyo vimeanza,1,Vitu vikali vyazidi kuingia Dar,1,Vituko,77,Vituo vya polisi Tanga vyatelekezwa,1,VIVALO,1,Wacha tujifue,2,Wadau ilitolewa kiingereza,1,wakali wa ubunifu,1,wala usibabaike mwakwetu hii noma,1,wanadamu wanapotaka kujua zaidi,1,wanasema mpaka kieleweke,1,Wanataka kujua mali za JK na wengine,1,Wanawake wenye mvuto: Monroe,1,Wapo mabinti wa matawi ya juu,1,watu wanapofanya weli kwenye sanaa,1,waweza kurejea enzi ya Moro jazz na Cuban malimba,1,Wazee tupo kusindikiza,1,waziri,1,welcome dar baby,1,Wenzetu wameona sisi tunangoja nini kuangalia,1,wewe unasemaje,1,wigo mpana wa utamaduni,1,wilaya ya 'Mbagala' mlie tu,1,Yaaani sijui itawezekana,1,Yaani wakati mwingine hata huelewi prioty over priority,1,yeye mbele sisi nyuma,1,Yote maisha dada,1,ZA MOTOMOTO,1,Zanzibar,79,zawadi zinatakiwa ziende shule,1,ZILIZOTIA FORA,1,zitachangia kupunguza makali ya bei za umeme,1,
ltr
item
Lukwangule Entertainment: Mwanadamu arejea mwezini:Ratiba ya Kila Siku ya Wanaanga wa Artemis kuuzunguka
Mwanadamu arejea mwezini:Ratiba ya Kila Siku ya Wanaanga wa Artemis kuuzunguka
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjE53miBClNfjI8-9oiuAQMnn6uw3DQ4JYl4yUV_naQxJrcXiOWNDhDVodq4Iz4ZQV5yClO8NP_O9GN8_mh8NLye-3wsuDLyZ53WoSKzpUYcQZipCXyApckRuZstZJSnpi5SvG1-IkCHanMHeQ2jplStFJ15KwKIZsoJ58gm9f2BalATxcN6s1PT5UPBasq/s320/wanaanga%20inafaa.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjE53miBClNfjI8-9oiuAQMnn6uw3DQ4JYl4yUV_naQxJrcXiOWNDhDVodq4Iz4ZQV5yClO8NP_O9GN8_mh8NLye-3wsuDLyZ53WoSKzpUYcQZipCXyApckRuZstZJSnpi5SvG1-IkCHanMHeQ2jplStFJ15KwKIZsoJ58gm9f2BalATxcN6s1PT5UPBasq/s72-c/wanaanga%20inafaa.jpg
Lukwangule Entertainment
https://lukwangule.blogspot.com/2026/04/mwanadamu-arejea-mweziniratiba-ya-kila.html
https://lukwangule.blogspot.com/
http://lukwangule.blogspot.com/
http://lukwangule.blogspot.com/2026/04/mwanadamu-arejea-mweziniratiba-ya-kila.html
true
934549962738256429
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy