POLISI wa Temeke leo alfajiri walilazimika kutumia tishio la bunduki kutawanya kundi la watu waliokuwa wanapora bia baada ya kutokea gari li...

POLISI wa Temeke leo alfajiri walilazimika kutumia tishio la bunduki kutawanya kundi la watu waliokuwa wanapora bia baada ya kutokea gari lililohusisha lori lililokuwa na shehena ya bia, daladala, pick up na pikipiki maeneo ya mtoni Kizinga, mara tu unapoacha daraja la juu la Reli ya TAZARA.
Katika ajali hiyo ambapo mtu mmoja inaaminika alikufa wimbi la vijana lilivamia eneo hilo na kuanza kuondoka na masanduku ya bia hali ambayo ilianza kuhatarisha usalama wao katika eneo hilo ambalo nyakati za asubuhi linapilikapilika kubwa za magari yakifukuzana kuelekea mjini huku wakiwa na njia finyu kutokana na ujenzi wa barabara unaoendelea ambao umeweka njia ya mchepuo jirani sana na eneo la ajali.
Katika vurumai la ajali nguzo ya umeme mkubwa iligongwa na kukatika.
Ajali hiyo ya asubuhi ilisababisha watu walioondoka Mbagala Rangi tatu saa moja asubuhi wafike mjini Posta saa nne asubuhi hali ambayo ilisababisha mtafaruku mkubwa kwao na wateja wao.mamia waliamua kutembea kwa miguu kutoka Mbagala baada ya kugundua kwamba hawana jinsi na hawajui kumetokea nini mbele yao.
Hali ya asubuhi ambayo ni kawaida kama kukitokea ajali kubwa katika barabara hiyo ilishughulikiwa haraka na polisi ili kupisha magari kuendelea na safari lakini si kabla ya kupita saa nne.
Chanzo cha ajali hiyo ni fuso T368 ABX ambalo liligonga kipanya T490 AJW. Fuso lilikuwa linatoka mjini kwenda mbagala.
Huku likiendelea kuyumba gari hilo ambalo lilionekana limekosa mwelekeo liliwafanya wenye magari ambao walikuwa katika foleni kuanza kuhaha kulikwepa ndipo Pick up moja STJ 9472 lilipovaa mtaro.
Baadaye Fuso liligonga pikipiki T219 AQT ikiwa inaaendeshwa na mtu aliyevaa kiaskari na abiria aliyepakiwa inasadikiwa alikufa palepale.
Kutoka hapo gari hilo lilivamia nguzo ya umeme wa msongo wa kati na kuirarua vibaya.
Doria PT 0966 lililokuwa katika barabara hiyo ya Kilwa iliwahi kufika hapo na kukuta tafarani hiyo.
Vijana , wazee kwa watoto walishazingira ajali hiyo na kuanza kujichukulia vitu kw aghasia hali ambayo ilisababisha watishie kw abunduki ili kuwatawanya watu hao.
hata hivyo walikuwa wamechelewa kwani vilaji vilitoweka kwa kasi katika eneo hilo maarufu kama uwanja wa vita kwa jinsi wanavyopamia vitu kunapotokea kasoro na kuhamisha kama tai.
Matumizi ya bunduki kutishia yalikuwa lazima kwani kulikuwa na kila dalili ya kutokea kwa vurumai katika eneo hilo.
Watu wengi kutoka Mbagala akiwemo mdau wa blogu hii leo walijikuta wakikaa katika foleni kwa saa kadhaa na kuingia mjini saa nne tayari kukabiliana na matusi kutoka kwa mabosi wao.

Picha hizi mbili zimetoka Dar leo
COMMENTS