Taarifa ya Waziri Mkuu kuhusu Richmond aliyoitoa leo Bungeni

Wasomaji hii ndiyo taarifa ambayo Waziri Mkuu Mizengo Pinda ameiwakilisha bungeni. Imechapwa kwa mkono sikuwa na muda wa kuhakiki taipografi...


Wasomaji hii ndiyo taarifa ambayo Waziri Mkuu Mizengo Pinda ameiwakilisha bungeni. Imechapwa kwa mkono sikuwa na muda wa kuhakiki taipografiki eras. lakini nimetekeleza ahadi yangu ya kwamba tutaleta kinachowezekana. Hatuna nyongeza.

Msimbe lukwangule




TAARIFA YA WAZIRI MKUU, MH. MIZENGO P PINDA,(MB),
KUHUSU UTEKELEZAJI WA MAAZIMIO YA BUNGE
YA MKATABA BAINA YA TANESCO NA RICHMOND
DEVELOPMENT COMPANY LLC
28 AGOSTI 2008

UTANGULIZI:

Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa kifungu cha 37 cha kanuni za kudumu za Bunge(Toleo la 2007), naomba kuwasilisha Taarifa ya Serikali kuhusu utekelezaji wa Maazimio ya Bunge ya Mkataba baina ya Tanesco na kampuni ya Richmond Development Company LLC.

Mheshimiwa Spika, katika Mkutano wa Kumi wa Bunge tarehe 15 Februari 2008, Bunge lako tukufu lilipitisha Maazimio 23 baada ya mjuadala wa taarifa ya kamati Teule ya Bunge iliyoundwa mwezi Novemba 2007 ili kuchunguza mchakato wa Zabuni ulioipa ushindi Kampuni ya Richmond Development Company LLC wa kuzalisha umeme wa dharura nchini mwaka 2006. Kwa kuzingatia uzito wa suala hili, wakati nilipotoa hotuba yangu ya kuahirisha Mkutano wa Kumi wa Bunge nilieleza kuwa serikali itaunda timu ndogo ya wataalamu ili kuchambua kwa makini na kupendekeza namna ya kutekeleza maazimio hayo 23 yaliyopitishwa na Bunge. Vilevile niliahidi kuwa kamati hiyo itazingatia mambo yote muhimu yaliyomo kwenye Taarifa ya kamati Teule ya Bunge na Taarifa za majadiliano zilizoingizwa kwenye kumbukumbu za Bunge(HANSARD).

Mheshimiwa Spika, tarehe 25 Aprili 2008 wakati nikitoa Hotuba yangu ya kuahirisha Mkutano wa kumi na moja wa Bunge lako tukufu , niliwasilisha taarifa ya Awali ya hatua zilizochukuliwa na serikali katika utekelezaji wa maazimio hayo.

Aidha , niliahidi pia kuwa serikali itajitahidi kuharakisha utekelezaji wa Maazimio hayo kwa kadri itakavyowezekana na Taarifa rasmi itawasilishwa katika Mkutano huu wa Kumi na mbili wa Bunge jambo ambalo linafanyika leo.

4. Mheshimiwa Spika, mwezi februari 2008 Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, alikubali kujiuzulu kwa aliyekuwa Waziri Mkuu Mheshimiwa Edward Lowassa(Mb). Aidh , Mawaziri wawili, Mheshimiwa Dkt. Ibrahim Msabaha(Mb), na Mheshimiwa Nazir Karamagi(Mb), nao kwa wakati mmoja walijiuzulu kw akuwajibika kwao kisiasa kwa maslahi ya Taifa. Kutokana na uamuzi wa aliyekuwa Waziri Mkuu kujiuzulu, kikatiba kulisababisha Baraza zima la Mawaziri kuvunjwa, jambo ambalo lilikuwa ni uamuzi mkubwa kwa serikali. Hatua hii inaonyesha kiwango kikubwa cha usikivu wa serikali yetu hasa kwa kuzingatia kwamba hatua hii ilichukuliwa mapema mara tu baada ya Taarifa ya Kamati Teule kuwasilishwa katika Bunge lako Tukufu.


Mheshimiwa Spika, pamoja na hatua hiyo, napenda kueleza hatua nyingine muhimu zilizochukuliwa na serikali hadi hivi sasa:-

Kwanza, Serikali imekwishapeleka maelekezo kwa kila Wizara na Taasisi zinazohusika na utekelezaji wa Maazimio haya na hatua za utekelezaji zinaendelea kuchukuliwa na vyombo hivyo.

Pili, Kufuatia utata uliojitokeza kuhusu uhalali wa Mkataba baina ya Tanesco na Richmond development Company LLC uliorithiwa na Dowans S.A , Serikali imechukua hatua ya kusitisha Mkataba huo kuanzia tarehe 1 Agosti 2008.

Tatu, Serikali imesitisha malipo yote ya fedha zinazohusiana na Mkataba baina ya Tanesco na Richmond Development Company LLC uliorithiwa na Kampuni ya Dowans S.A.

Nne, Watumishi wote wa Umma waliohusika katika mchakato wa kuandaa na kutoa Zabuni ya Mkataba baina ya TANESCO na RICHMOND wameandikiwa barua za kujieleza kama hatua za awali za kinidhamu kwa kuzingatia Sheria, taratibu na kanuni za Utumishi wa Umma, Aidha kwa wale watakaoonekana kuwa wamefanya makosa ya jinai hatua stahiki za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.

Mheshimiwa Spika, baada ya utangulizi huo sasa ningependa kueleza kipengele kwa kipengele kuhusu hatua za utekelezaji wa Maazimio yote kama yalivyorekebishwa tarehe 15 Februari 2008 na mtoa Hoja wakati akihitimisha hoja yake.

AZIMIO NAMBA 1.

“Sheria ya manunuzi ya Umma ya Mwaka 2004(Public procurement Act, 2004) haina nguvu ya kutosha. Sheria ipitiwe upya ili kuiboresha kwa kuipa mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma(PPRA) nguvu zaidi za udhibiti na uwezo wa kuchukua hatua pale Sheria na Kanuni zinapokiukwa, badala ya kutoa ushauri tu kama ilivyo sasa.”

HATUA ZILIZOCHUKULIWA:

Wizara ya Fedha na Uchumi ikishirikiana na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali pamoja na Mamlaka ya Udhibiti wa manunuzi ya Umma(PPRA), wamekwishaainisha maeneo yote yenye mapungufu na yanayohitaji marekebisho kwenye Sheria ya Manunuzi ya Umma ya mwaka 2004.

Baada ya zoezi hilo kufanyika , Serikali itawasilisha katika Mkutano wa Kumi na Tatu wa Bunge lako Tukufu, mapendekezo ya kufanya Marekebisho katika Sheria hiyo, maeneo yatakayozingatiwa ni yafuatayo:

(i) Kuipa uwezo PPRA kusitisha Zabuni yoyote pale itakapobainika kuwepo kwa ukiukwaji wa Sheria na Kanuni zinazosimamia Manunuzi ya Umma.
(ii) Kuipa nguvu PPRA kutoa maelekezo kwa Mamlaka zinazohusika na ununuzi(yaani Procuring Entities)kuchukua hatua kwa watakaokiuka Sheria ya manunuzi ya Umma.
(iii) Kuifanya PPRA kuwa Taasisi Huru inayojitegemea ikiwa na Muundo sawa na ule wa Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Serikali(CAG).
(iv) Kufanya marekebisho yatakayowezesha Sheria kutoa adhabu kali kwa Viongozi na Watumishi wa Umma watakaobainika kujihusisha na ukiukwaji wa Sheria na Kanuni za Manunuzi ya Umma.
(v) KUfanya marekebisho ya kuzitaka Mamlaka zenye dhamana zitakazopokea hoja za ukiukwaji wa Sheria ya Manunuzi ya Umma kutoka PPRA, kutoa taarifa kuhusu hoja hizo katika kipindi maalum na ikibidi kuchukua hatua zaidi kwa Taasisi au Mtu atakayekiuka Sheria na Kanuni za Manunuzi ya Umma.
(vi) Kuweka utaratibu mzuri wa namna ya kushughulikia masuala ya Ununuzi wa Dharura yanapotokea.
(vii) Kuweka utaratibu wa kuwezesha kufanyika uchunguzi wa kina(due diligence) kwa wazabuni wa ndani na nje ya Nchi wanaoomba kuingia mikataba na Serikali.
(viii) Kuweka utaratibu wa kutumia kamati Huru ya wataalamu itakayofanya uchunguzi wa kina pale itakapobidi.


AZIMIO NAMBA 2:

“Mamlaka ya Udhibiti wa ununuzi wa Umma(PPRA) isiwajibike Wizara ya Fedha ambayo nayp ni Taassi ya Ununuzi(procuring Entity) badala yake iwe chombo huru kinachowajibika ofisi ya Rais na Taarifa zake kuwasilishwa Bungeni.”

HATUA ZILIZOCHUKULIWA:

(i) Kulingana na Sheria ilivyo hivi sasa, PPRA ni Taasisi Huru inayojitegemea nje ya Muundo wa Wizara ya Fedha na uchumi, Aidha PPRA ina Bajeti yake inayojitegemea na pia ina chombo chake maalum cha usimamizi yaani Bodi ya wakurugenzi. Hata hivyo, katika Marekebisho ya Sheria yanayotarajiwa kufanyika. Serikali inakusudia kuwasilisha pendekezo la kufanya PPRA iwe na Muundo sawa nma ule wa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ambapo utatoa uhuru kwa Chombo hicho kutoa maamuzi ya kila siku bila kuingiliwa na Chombo chochote, ingawa kisera itaendelea kuwa chini ya usimamizi wa HAZINA kama ilivyo kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali.

(ii) Kuhusu Taarifa za mwaka za PPRA kuwasilishwa Bungeni, suala hili limezingatiwa katika Kifungu cha 26 (2) cha Sheria ya Manunuzi ya Umma ya mwaka 2004, inayotumika hivi sasa. Chini ya sheria hiyo, Waziri wa Fedha na Uchumi huwasilisha bungeni taarifa ya kila mwaka ya utendaji wa PPRA.

AZIMIO NAMBA 3:

“Mikataba kati ya TANESCO na Richmond Development Company LLC (uliorithiwa Dowans Holdings S.A) na ile kati ya TANESCO na IPTL, SONGAS, AGGREKO na Alstom Power Rentals ipitiwe upya mapema iwezekanavyo kama ambavyo Mikataba ya Madini ilivyopitiwa upya na Serikali. Bila kufanya hivyo, mzigo mkubwa wa gharama za umeme utawaelemea wananchi na kushindwa kufikia azma ya serikali ya maisha bora kw akila Mtanzania.”

HATUA ZILIZOCHUKULIWA:

Pamoja na kutoa taarifa ya utekelezaji wa Azimio hili, napenda kueleza kuhusu hali ilivyo sasa kwa Mikataba baina ya TANESCO na IPTL, SONGAS, AGGREKO na Power Rental.

(i) Mkataba baina ya TANESCO na IPTL

Mgogoro uliopo sas akati ya TANESCO na IPTL unatokana na kutokubaliana kwa pande zote mbili kuhusu kiwango cha capacity charge kinachotozwa na IPTL.

Kwa mujibu wa Mkataba wa kuuziana umeme kati ya IPTL na TANESCO, capacity charge inapaswa kukokotolewa kwa kuzingatia mtaji (eguity) wa asilimia 30 na faida ya asilimia 22.31 uliopaswa kuwa umewekezwa (ambao ni US $ 36.54 milioni) wakati IPTL wanaanza kuzalisha umeme na kuiuzia TANESCO tarehe 15 Januari, 2002. hata hivyo kufuatia uchunguzi uliofanywa na TANESCO imegundulika kwamba mtaji halisi wakati IPTL inaanza kuzalisha umeme ulikuwa shilingi hamsini elfu tu (50,000/=). Hivyo, mtaji huu ndiyo unaostahili kutumika kukokotoa capacity charge ambacho hakikustahili kulipwa kwa IPTL.

Kwa mantiki hiyo, madai ya TANESCO na Serikali katika mradi huu ni kuwa capacity charge inayotozwa na IPTL izingatie kiwango halisi cha mtaji (equity) uliowekezwa na IPTL na si zaidi ya hapo. Aidha serikali na TANESCO inadai kutoka IPTL kiasi chote cha malipo kilichofanywa kimakosa kama capacity charge ambacho hakikustahili kulipwa kwa IPTL.

Kutokana na Serikali kutoridhika na kiwango cha malipo ya capacity charge chini ya mradi huu wa IPTL, ilisitisha malipo kwa IPTL; jambo ambalo lilipelekea IPTL kufungua Sauri la Madai dhidi ya TANESCO kwenye Mahakama ya New Cork Nchini Marekani mwezi Novemba 2007. mnamo mwezi Aprili 2008 Serikali ilishinda Sauri hilo baada ya Mahakama hiyo kutupilia Mbale Sauri hilo na kuelekeza kwamba mgogoro huo uwasilishwe kwenye Baraza la Usuluhishi (Arbitration) kama Mkataba baina ya pande mbili unavyoelekeza.

Tarehe 9 Julai, 2008 IPTL iliwasilisha mgogoro huu kwenye Internacional Centre for Settlement of Investment Disputes (ICSID). Kwa sasa shauri hili bado halijatolewa uamuzi.

Hata hivyo, serikali imejiandaa ipasavyo kutetea na kulinda haki zake chini ya Kamati Maalum ya Serikali iliyoundwa kushughulikia mgogoro huu. Mmoja wa Wajumbe wa Kamati hiyo maalum ni Wakili wa Kujitegemea, Mheshimiwa Nimrod Elirehema Mkono, Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini.

Hivyo, Mkakaba huu tayari umekwishapitiwa na Kamati husika na mapungufu yake yaliyobainika ndiyo yamepelekea kuwepo kwa shauri hili.

(ii) Mkataba baina ya TANESCO na RICHMOND (ulioridhiwa na DOWANS)

Kutokana na utata uliojitokeza katika mchakato mzima kuhusu Mkataba baina ya TANESCO na RICHMOND uliotiwa saini tarehe 23 Juni 2006, Serikali kupitia TANESCO iliamua kufanyike mapitio ya Mkataba huo na kupata ushauri wa kitaalam kutoka kwa Wanasheria waliobobea katika masuala ya Mikataba ya Kimataifa wa Kampuni ya REX ATTORNEYS. Uchunguzi wa REX ATTORNEYS ulibaini pamoja na mambo mengine kwamba;

(a) Utaratibu mzima wa manunuzi ya huduma ya umeme na kuingia Mkataba na Richmond Development Company LLC ulikiuka Sheria ya manunuzi ya Umma ya mwaka 2004;

(b) Kutokana na ukiukwaji huo, Mkataba baina ya TANESCO na Richmond Development Company LLC, haukuwa halali na hauna nguvu kisheria; na,

(c) Vilevile, hata kama Mkataba husika ungekuwa halali, uhamishaji (assignment) wa mkataba huo kutoka RDEVCO badala ya Richmond Development Company LLC kwenda DOWANS HOLDINGS S.A. na hatimaye Dowans Tanzania Limited haukuwa halali.

Kwa kuzingatia mapungufu hayo yaliobainishwa katika Mkataba huo serikali iliamua kusitisha huduma za Dowans Tanznaia Limited kuanzia tarehe 1 Agosti 2008.

(iii) Mkataba baina ya Tanesco na Aistom Power Rentals (APR)

Kama nilivyoelezwa na WAziri wa Nishati na Madini William Ngeleja wakati akiwaslisha hotuba yake hapa bungeni tarehe 8 Julai 2008, katika mkutano huu wa Bunge lako tukufu alifafanua kuwa mitambo ya Alstom Power Rentals ilikodishwa na Tanesco kwa kipindi cha miezi 12 kuanzia tarehe 20 Machi 2007 hadi tarehe 19 machi 2008. baada ya ya muda wa mkataba huo kumalizika serikali haikuhuisha mkataba huo licha ya jitihada za wahusika kutaka uhuishwe.


iv) Mkataba baina ya Tanesco ya AGGREKO

Mkataba baina ya Tanesco na Aggreko ulianza kutekelezwa mwezi Desemba 2006 na unatarajiwa kumalizika mwezi Novemba 2008. Kamati ya Serikali ya Wataalam inapitia mkataba huu ili kujiridhisha kama upo kwa maslahi ya taifa na kuchukua hatua kadri itakavyoonekana inafaa.

v)Mkataba baina ya Tanesco na SONGAS

Kwa sasa mkataba mkubwa wa Sekta ya Nishati ambao unapawa kupitiwa upya ni baina ya Tanesco na Songas. Mkataba wa Songas unahusisha wadau wengi na unajumuisha mikaaba midogo mbalibmali ipatayo ishirini na moja inayohusu masuala ya utafutaji, usambazaji, ununuzi na mikopo ya uendelezaji wa gesi asilia na hivyo kuwa na uzito wa aina yake (Complex). Ili kuwa na tija katika mapitio ya mikataba hiyo na kupata ushauri mzuri, serikali inaendelea kushauriana na wataaalam washauri waliobobea katika sekta hiyo ya gaesi asilia wakiwemo wanasheria ambao wataweza kushauri ipasavyo iwapo kuna mapungufu yoyote yanayostahili kufanyiwa marekebisho kwa maslahi ya taifa.

AZIMIO NAMBA 4:
“Serikali itathmini uya uhalali wa kuwepo Mkataba kati ya Tanesco na Richmond Development Company LLC (Sasa Dowans Holdings S.A) kwa lengo la kusitisha mlipo kwa Dowans Holdings S.A na kuvunja mkataba huo haraka iwezekanavyo.

HATUA ZILIZOCHUKULIWA:
Kama nilivyoeleza awali kufuatia utata uliojitokeza kuhusu uhalali wa mkataba baina ya Tanesco na Richmond uliorithiwa na Dowans , Serikali imesitisha mkataba huo kuanzia tarehe 1 Agosti 2008. vile vile Serikali imesitisha malipo yote ya fedha zinazohusiana na mkataba huo.

AZIMIO NAMB 5:
“Kwa kuwa mkataba kati ya Tanesco na Richmond Development Company LLS (Sasa Dowans Holding S.A) umesheheni makosa mengi ya kisheria yanayoashiria udhaifu mkubwa wa kitaalam katika ofisi ya mwanasheria mkuu wa Serikali au ukosefu wa umakini katika kuiwakilisha serikali; Mwanasheria Mkuu wa Serikali na wakili wa serikali Donald Chidowu ambaye ushiriki wake katika GNT haukuwa na tija yoyote, wawajibishwe na mamlaka juu ya nchi kwa kuchangia kuiingiza nchi katika mkataba wa aibu.”


HATUA ZILIZOCHUKULIWA:
I) Kikatiba Mwanasheria Mkuu wa Serikali ndiye mshauri mkuu wa Serikali katika masuala yote ya sheria za nchi. Hivyo ana wajibu mkubwa wa kuishauri serikali katika maeneo ambayo anaona yanakiuka Sheria, taratibu na kanuni za nchi.

Kutokana na nafasi yake kikatiba, mamlaka yake ya nidhamu ni mheshimiwa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kwa hiyo mwanasheria mkuu wa Serikali ambaye alikuwa miongoni mwa watendaji wakuu watatu waliokuwa wanaishauri Serikali suala lake la kuhusishwa kwake katika mchakato mzima wa mkataba hao linashughulikiwa na ofisi ya Rais Ikulu

Kuhusu Wakili wa Serikali Donald Chidowu ambaye aliukwa ni miongoni mwa wajumbe wa kamati ya majadiliano (GNT) akimwakilisha mwanasheria mkuu wa Serikali, amepelekwa barua ya kutakiwa ajieleze kwa kuzingatia misingi ya kanuni asilia ya haki ya kusikilizwa kwanza (natural justice) na kuzingatia Sheria za Utumishi wa umma.

Mtumishi huyu amewasilisha utetezi wake kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Sheria ya sheria na katiba ambaye ndiye Mamlaka yake ya nidhamu katika muda wa siku 14 zilizotakiwa. Hivi sasa maelezo ya utetezi wake yanafanyiwa uchambuzi wa mamlaka yake ya nidhamu ili hatimaye maamuzi yatolewe kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za utumishi wa umma.

AZIMIO NAMBA 6:

“Katika kushughulikia mikataba yote na makampuni ya nje, Serikali ihakikishe kuwa wakala wa usajili wa biashara na Leseni (Brela) inatumika kikamilifu kupat aaarifa kamili za makampuni haya. Aidha ofisi zetu za ubalozi zilizo sehemu mbalimbali duniani zihusishwe katika majadiliano na makampuni yanayotoka nje ya nchi na vile vile katika kuyachunguza makampuni hayo kwa lengo la kupata taarifa zao za msingi na kuboresha nguvu ya hoja ya Serikali, kabla ya kuingia mikataba husika.”


HATUA ZILIZOCHUKULIWA:

Serikali imetafakari na kuzingatia kwa makini pendekezo hili. Hatua zilizoanza kuchukuliwa ni pamoja na zifuatazo:

i) Kuanzia sasa balozi zetu zote za nje zitakuwa zinashirikishwa kikamilifu katika kufanya uchunguzi wa kina (due diligence) kwa makampuni ya nje ambayo Serikali inatarajia kuingai nayo mikataba katika manunuzi ai katika miradi mikubwa. Serikali imeshato amaelekzo haya kwenye wizara zote. Aidha wizara ya mambo ya nje na ushirikiano wa kimataif anayo imetoa maelekezo kwa balozi zetu zote ili zizingatie uamuzi huu.

ii) kama ilivyoelezwa katika Azimio namba moja, serikali itawasilisha mapendekezo kuhusu marekebisho ya sheria ya manunuzi ya umma ili kuongeza kifungu kinachohusu kufanya uchunguzi wa kina wa wazabuni wa ndani na nje ya nchi wanaoomba kuingia mikataba na Serikali. Miongoni mwa mapendekezo haya ni pamoja na kuwa na kamati huru ya awataalam itakayofanya uchunguzi huu wa kina pale itakapobidi.

iii) katika kuhakikisha kuwa teknolojia ya habari na mawasiliano inatumika ipasavyo katika masual ya manunuzi ya umma PPRA tayari imeanzisha mfumo wa habari na mawasiliano katika manunuzi ya umma ujulikanao kama procurement information system. Ni matumaini ya Serikali kuwa mfumo huu utatumika kurahisisha upatikanaji wa taarifa mbalimbali za manunuzi kati ya mamala yaani PPRA na taasisi za ununuzi.


AZIMIO NAMBA 7;

Wajumbe wote wa kamati ya Serikali ya majadiliano (Government Negotiation Team-GNT) ambao ni maafisa waandamizi wa Serikali wawajibishwe kwa manufaa ya umma kwa kulitia hasara taifa kutokana na kushindwa kutumia elimu na ujuzi wao kulinda maslahi ya taifa.

HATUA ZILIZOCHUKULIWA:
Katika kushughulikia suala hili (yaani katika mchakato mzima wa zabuni pamoja na majadiliano ya mkataba baina ya Tanesco na Richmond kulikuwa na kamati za aina tatu.

Kwanza ni kamati iliyokuwa inaundwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mheshimiwa Johnson Mwanyika (mb) katibu Mkuu wa wizara ya nishati na madini Arthur Mwakapugi pamoja na akatibu mkuu wizara ya fedha na uchumi Gray Mgonja. Kamati hii ilikuwa na jukumu la kutoa ushauri kwa Waziri wa Nishati na Madini na Serikali kwa ujumla

Kamati ya pili ilikuwa ni timu ya wataalamu (expert team) iliyokuwa na wajumbe na Taasisi zifuatazo:

1. Singi Madata –Fedha na Uchumi (Mwenyekiti)
2. Dk Lutengano Mwakahesya- Nishati na Madini (Mjumbe)
3. Theophilo Bwakea –Nishati na madini (mjumbe)
4. Stephen Mabada –Tanesco (mjumbe)
5. Athanas Mbawala –tanesco (mjumbe)
6. James Mwalilimo –Tanesco (Mjumbe)
7. Julius Sarota –Nishati na Madini (mjumbe)

Kamati hii ilikuwa na jukumu ya kutathmini wazabuni wote waliokuwa wameomba zabuni za mitambo ya kukodi ya dharura ya kufua umeme wa megawati 105.6.

Kamati ya tatu ni ile ya majadiliano ya Serikali na wawakilishi wa kampuni ya Richmond Development Company LLC. Wajumbe wa kamati hii ni:

1. Singi Madata –Fedha na Uchumi (Mwenyekiti)
2. Theophilo Bwakea –Nishati na madini(mjumbe)
3. Stephen Mabada –Tanesco (Mjumbe)
4. Godson Makia –Tanesco(Mjumbe)
5. Donald Chidowu –Ofisi ya Mwanasheria Mkuu (Mjumbe)
6. Dick Tewa –Benki Kuu (Mjumbe)
7. Gideon Nassari –CTI (Mjumbe)
8. Julius Sarota –Nishati na Madini (Sekretarieti)
9. Mwita Wangwe –Tanesco (Sekretariet)

Kamati mbili za wataalam (yaani kamati ya pili na ya tatu) zote zilikuwa zinaripoti na kutoa ushauri kwa kamati ya makatibu wakuu wawili wa Hazina, na Nishati na Madini pamoja na Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Kwa madhumuni ya utekelezaji wa Azimio hili, wajumbe wote wa kamati hizi tatu wamepelekewa barua za kutakiwa watoe maelezo kwa mujibu wa Sheria zinazohusu nidhamu katika utumishi wao.

Hatua hii inazingatia Misingi ya Kanuni Asili ya Haki ya Kusikilizwa Kwanza (Natural Justice), kabla ya hatua nyingine kuchukuliwa.

Miongoni mwa maeneo ambayo watumishi hawa wametakiwa kutoa maelezo ni jinsi walivyohusika katika mchakato mzima na kuingiza Serikali katika mkataba unaonekana kutokuwa na maslahi kwa Taifa.

Maeneo hayo ni pamoja na:

(i) Kutotumia utaalamu na uzoefu wao kikamilifu ili kutambua mapema kuwa Richmond Development Company LLC haikuwa na uwezo kitaalamu, kifedha na kuzoefu na hivyo kutokidhi matakwa ya zabuni.
(ii) Kutozingatia kikamilifu Sheria ya Manunuzi ya Umma, ya mwaka 2004 katika mchakato mzima wa kutoa zabuni.
(iii) Wajumbe kushindwa kuishauri Serikali kuhusu kuifanyia Kampuni ya Richmond Development LLC uchunguzi wa awali (Due Diligence) pamoja na ukaguzi baada ya tathmini ya zabuni (post qualification)
(iv) Kutokuwa makini na hivyo kushinddwa kutambua udanganyifu wa ubia/ uhusiano wa kibiashara kati ya Richmond Development Company LLC na Pratty & Whitney
Watumishi wote wameshawasilisha utetezi wao katkka muda wa siku 14 zilizopangwa. Aidha, hivi sasa utetezi wao unafanyiwa uchambuzi wa kina na Mamlaka zao za nidhamu ili hatua muafaka zichukuliwe kwa mujibu wa Sheria, Kanuni na Taratibu zinazotawala Utumishi wao.

Kwa upande wa watumishi wa Tanesco ambao ni Stephen Mabada, Athanas Mbawala James Mwalilimo, Godson Makia na Mwita Wangwe, Kamati Ndogo ya Nidhamu ya Bodi ya Tanesco tayari imekwisha pitia maelezo ya watumishi wao wote na mapendekezo ya kamati hiyo yamewasilishwa kwenye Bodi ya Wakurugenzi ya Tanesco ambayo itatoa maamuzi yake na kuishauri Serikali.

AZIMIA NAMBA 8:

“Waziri wa Nishati na Madini Mh. Nazir Karamagi (MB), aliyeshabikia sana uhaulishaji wa Mkataba kutoka kwa Richmond Development Company LLC kwenda kwa Dowans Holdings S.A awajibishwe,”

HATUA ZILIZOCHUKULIWA

Nazir Karamagi (MB) aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini alijiuzulu Februari 2008 kwa kuwajibika kutokana na suala hili. Hatahivyo, kwa lengo la Serikali kujiridhisha kuhusu ushiriki na ushauri wake katika suala hili, Vyombo vya Dola vinaendelea na uchunguzi wa kina kwa lengo la kutaka kujua kama kuna rushwa yeyote ambayo ilijitokeza katika mchakato huu inayomhusisha Mheshimiwa Nazir Karamagi (Mb), katika suala hili.

Taarifa ya uchunguzi huo itawezesha Serikali kuamua juu ya hatua zaidi zinazostahili kuchukuliwa dhidi yake.

AZIMIO NAMBA 9

“Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru awajibishwe kwa manufaa ya Umma na Maofisa wa Takukuru walioshiriki katika zoezi la uchunguzi kuandaa Taarifa ya Richmond Development Company LLC iliyoficha ukweli nao pia wawajibishwe kwa manufaa ya Umma”

HATUA ZILIZOCHUKULIWA

Zoezi la kufanya uchunguzi lililofanywa na Takukuru lilihusisha watumishi wafuatao:

(i) Mkurugenzi wa Takukuru, Edward Hosea akiwa ndiyo msimamizi mkuu wa Takukuru, iliyohusika na uchunguzi wa mchakato wa mzima wa zabuni ya umeme wa dharura, ulioipa ushindi kampuni ya Richmond Development Company LLC.
(ii) Mkurugenzi wa Upelelezi, Alex Mfungo ambaye ndiye alisimamia zoezi zima la uchunguzi na kuandaa ripoti ya uchunguzi ya Takukuru kuhusu suala hili.
(iii) Maofisa wanane wa Takukuru walioshiriki katika zoezi la uchunguzi na kuandaa taarifa katika maeneo yao ya utaalamu katika mchakato mzima wa Zabuni ya ununuzi wa mitambo ya umeme wa dharura ulioipa ushindi kampuni ya Richmond Development Company LLC
Ili kutekeleza azimio hili, Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru amepelekewa barua ya kutakiwa kujieleza na Mamlaka yake ya Nidhamu ambayo ni Katibu Mkuu Kiongozi. Vilevile wasaidizi walio chini yake walioshiriki katika zoezi hilo nao wametakiwa kutoa maelezo yao kwa Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru ambaye ndiye mamlaka yao ya Nidhamu. Hii ni kuzingatia Misingi ileile ya Kanuni Asilia ya Haki ya Kusikilizwa Kwanza (Natural Justice).

Hatahivyo kwa kuzingatia mazingira ya shauri hili, Katibu Mkuu Kiongozi ataamua juu ya utaratibu mzuri wa hatua za nidhamu dhidi ya wasaidizi wote wa Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru waliohusika katika suala hili.

Baadhi ya maeneo ambayo Mkurugenzi Mkuu na Wasaidizi wake wamepelekewa barua wajieleze ni yafuatayo:

(i) Kushindwa kuona kuwa taarifa ya uchunguzi iliyofanywa na Wataalamu wa Taasisi yake haikubainisha kuwepo kwa kasoro nyingi zilizokuwepo katika zabuni hiyo kama zilivyoainishwa katika Taarifa ya Kamati Teule ya Bunge.

Badala yake Takukuru iliona kwamba: Mchakato mzima ulizingatia Sheria, Kanuni na Taratibu za Serikali.



*Hayakuwepo mapungufu makubwa katika zabuni
*Hakukuwa na hasara kwa taifa kutokana na zabuni hii.

(ii)Kushindwa kuona kuwa ushauri uliotolewa na PPRA kwa TANESCO kuhusu muda wa kutangaza zabuni kimataifa ulipuuzwa na hivyo kuvunjwa kwa taratibu za Sheria ya Manunuzi ya mwaka 2004 na hivyo kutia shaka.

Hivi sasa watumishi wote tisa wameshawasilisha utetezi wao katika muda uliopangwa. Aidha kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na Utaratibu wa Utumishi wa Umma, Mamlaka yao na nidhamu inapitia utetezi wao ili kutoa uamuzi unaostahili.

AZIMIO NAMBA10

“Gavana wa Benki Kuu pamoja na Bodi ya Wakurugenzi wachunguze kwa makini uhalali wa malipo ya ziada)US$4,865,000) yaliyofanywa kwa Dowans Holdings A.S iliyorithi majukumu ya Richmond Development Company na kuwachukulia hatua waliohusika na uzembe huo.”

HATUA ZILIZOCHUKULIWA

Wizara ya Fedha na Uchumi na Benki Kuu ya Tanzania wamechunguza na kuona kuwa malipo ya US$4,865,000 yaliyolipwa kwa kampuni ya Dowans Holdings S.A iliyorithi majukumu ya Richmond Development Company LLC ni halali. Malipo hayo yalilipwa tarehe 2Februari 2007 ikiwa ni gharama za ndege za usfairishaji wa mitambo ya kukodi ya umeme wa dharura baada ya kupokea invoice Na.EFD786675.Uchunguzi unaonyesha kuwa, taratibu zote za malipo zilifuatwa na malipo yalifanywa baada ya kuhakikiwa na TANESCO, wizara ya Nishati na MAdini na HAZINA baada ya kupata ushauri wa kisheria kutoka kwa Mwanasheria Mkuu wa serikali kwamba yanawiana na mkataba husika.

UK. 17

AZIMIO NAMBA 11

“Shetia ya Maadili ya Viongozi wa Umma ya Mwaka 1995(The Public Leadership Code of Ethics Act) ifanyiwe marekebisho makubwa ili kudhibiti utaratibu unaonekana wa kawaida sasa wa viongozi waandamizi wenye dhamana ya kisiasa kuendelea na biashara zao binafsi wakiwa madarakan, jambo ambalo lina mgongano wa kimaslahi. Serikali ianze rasmi maandalizi ya majadiliano ya kina kuhusu suala hili ndani na nje ya BUnge kwa kuwashirikisha wadau mbalimbali.”

HATUA ZILIZOCHUKULIWA:

(i)Kama alivyoeleza Mheshimiwa Rais Jakaya Mrishi Kikwete katika Hotuba yake tarehe 21 Agosti 2008 wakati akilihutubia Bunge lako Tukufu kwamba, serikali inayo dhamira ya dhati ya kuangalia namna ya kutenganisha shughuli za biashara na uongozi katika Utumishi wa Umma katika ngazi za juu za viongozi na watendaji waandamizi. Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, imeanza mchakato wa kushughulikia suala hili na tayari wamewasilisha mapendekezo yao ya awali serikalini.

(ii)Hivi sasa serikali imeunda Timu inayojumuisha wajumbe kutoka sekretarieti ya maadili ya viongozi wa umma, Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Tume ya Uchunguzi, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na TAKUKURU ili kufanya uchambuzi zaidi wa mapendekezo hayo. Aidha, Timu hiyo itafanya uchambuzi wa Sheria za Nchi zilizofanikiwa kuweka utaratibu wa viongozi wa Umma kuweza kutenganisha shughuli za biashara zao na uongozi ili kuondoa mgongano wa kimaslahi.

(iii)Katika zoezi hili, wananchi na wadau mbalimbali watashirikishwa kikamilifu ili kupata maoni yao.

(IV) Baada ya hatua hizo serikali inatarajia kuwasilisha hapa bungeni marekebisho ya sheria ya maadili ya viongozi wa umma mwezi Aprili 2009.

UK18.

AZIMIO NAMBA 12
“Serikali ijiepushe kadri inavyowezekana na uataratibu wa kutumia mawakala katika ununuzi wa Umma na kuhakikisha kuwa Wizara zote zina taarifa za bei halisi za mahitaji yao kila wakati ili kujiepusha na mchezo wa kawaida wa mawakala kupandisha bei mara mbili au zaidi ya bei halisi.”

HATUA ZILIZOCHUKULIWA:

Katika utekelezaji wa Azimio hili, wizara zote, wakala na idara za serikali zinazojitegemea. Mikoa pamoja na mashirika ya umma zimeagizwa kuzingatia kikamilifu taratibu za manunuzi na ugavi kama zilivyoanishwa katika Sheria ya manunuzi ya umma ya mwaka 2004. Pamoja na maelekezo hayo hatua zifuatzo zitachukuliwa:

(i)Serikali imeamua kuwa kila inapowezekana taasisi za ununuzi zinunue vifaa moja kwa moja kutoka kwa watengenezaji wa bidhaa hizo, ikibidi kununua kutoka kwa wakala walioidhinishwa ni lazima taratibu za manunuzi ya umma zizingatiwe kikamilifu.

(ii)Katika hatua za awali, Wizara ya Fedha na Uchumi inaandaa utaratibu wa kufanya ununuzi wa pamoja wa bidhaa zinazoweza kutumika na taasisi zaidi ya moja(common use items). Utaratibu huo utakapokamilika utawezesha bidhaa hizo kuagizwa kwa pamoja kupitia wakala wa serikali wa huduma za ununuzi na endapo itabidi kununua moja kwa moja kutoka kwa watengenezaji kwa lengo la kupata unafuu wa bei.

(iii)Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma tangu mwezi Juni 2008, imempata mtaalamu mwelekezi wa kuandaa mfumo wa ununuzi wa pamoja na kupata takwimu za bei. Dira za bidhaa mbalimbali(indicative Price) kutoka kwa wazalishaji wa bidhaa na huduma. Kazi hiyo itakamilika mwezi Septemba 2008. takwimu hizo zitawekwa katika mtandao wa Mamlaka na kwenye matoleo ya Jarida la Masuala ya Ununuzi Tanzania ili ziweze kutumiwa na taasisi za ununuzi pamoja na Wazabuni. Bei hizo zitafanyiwa mapitio ya mara kwa mara na PPRA.

UK 19

AZIMIO NAMBA 13:
“Serikali izihusihe Kamati za Kudumu za Bunge kwenye hatua za awali za maandalizi ya Mikataba mikubwa ya kibiashara nay a muda mrefu ili kuondokana na utaratibu uliopitwa na wakati kwamba mikataba ya kibiashara ni siri, hata kwa walipa kodi wenyewe. Aidha, serikali ihakikishe kuwa Kamati zote za bunge zinapitia mikataba mikubwa ya kibiashara nay a muda mrefu chini ya sekta zao ili kuliondolea taifa mizigo isiyo na lazima.”

HATUA ZILIZOCHUKULIWA:
Tarehe 24 Aprili 2008, Ofisi ya Waziri Mkuu ilimwandikia narua Mheshimiwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kumfahamisha kuhusu utekelezaji wa awali wa baadhi ya maazimio ya Kamati Teule yaliyopitishwa na Bunge katika narua hiyo, utekelezaji wa maazimio Namba13, 15, 16, 21 na 23 yaliyotolewa taarifa. Hata hivyo, kwa madhumuni ya taariga hii ninapenda kurejea kwa muhtasari maelezo kuhusu utekelezaji wa maazimio hayo.

Kuhusu Azimio Na.13, serikali imechambua Azimio hili kwa kina na imekubali kimsingi kwamba, mikataba yote muhimu ya serikali itakuwa inawekwa kwenye maktaba maalum ya bunge ili kamati za Bunge lako Tukufu ziweze kupata nafasi ya kupitia mikataba mikubwa ya kibiashara nay a kuda mrefu chini ya sekta zao na kushauriana ipasavy.

Kuhusu kuzihusisha Kamati za kudumu za Bunge kwenye hatua za awali za maanalizi ya mikataba mikubwa ya kibiashara nay a muda mrefu, serikali imeanza kufanya tafiti katika mabunge ya nchi za Jumuiya ya Madola ili kupata uzoefu zaidi utakaosaidia katika utekelezaji wa suala hili.


“Waziri wa Nishati na Madini Dkt Ibrahimu Msabaha(MB) na Katibu Mkuu Ndugu Arthur Mwakapugi wachukuliwe hatua kali za kinidhamu kwa kuliingiza Taifa kw amakusudi kwenye mkataba wa Kampuni ya Mfukoni.

Aidha Kamishna wa Nishati nNdugu Bashir Mrindoko naye achukuliwe hatua za kinidhamu kwa kushindwa kumshauri katibu mikuu wake mpya kuhusu udhaifu wa Richmond Development Company (LLC) ambao ulijulikana dhahiri na Wizara mwaka 2004 kwenye mradi wa bomba la mafuta.

Ndugu Mrindoko ndie aliyeandika barua kampuni hiyo kusitisha mkataba wake na serikali mwezi mmoja tu kabla ya mchakato wa Zabuni ya umeme wa dharura haujaanza.

HATUA ZILIZOCHUKULIWA.

(a)Mheshimiwa Dkt Ibrahimu Msabaha(Mb) aliyekuwa Waziri wa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki alijuzulu mwezi Februali 2008 kwa kuwajibika kutokana na suala hili.

Hata hivyo kwa lengo la serikali kujidharisha zaidi kuhusu ushiriki na ushauri wake katika msual ahili, Vyombo vya dola vinaendelea kkuendesha uchunguzi wa kina.

Lengo ni kutaka kujua kama kuna rushwa yoyote inayomhusisha Mheshimiwa Dkt Ibrahim Msabaha(Mb) ambayo ilijitokeza katika mmachakato huu ili hatimae uamuzi stahiki dhidi yake uweze kuchukuliwa.

(b) Kuhusu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Bw Arhtur Mwakapugi ambae alikuwa miongoni mwa wajumbe watatu wa kamatio iliyoundwa na Katibu Mkuu Fedha na Uchumi, Nishati na Madini pamoja na Mwanasheria Mkuu wa Serikali naye amepewa barua ya kutakiw akujieleza katika maeneo ambayo kamati ya bunge ilibaini kuwa hakuyazingatia kwa maslahi ya taifa.

Hatua hiyo imechukuliwa kwa kuzingatia kuwa sheria na ikanuni za nidhamu katika utumishi wa ummaa na misingi ya kanuni Asilia ya haki ya kusikilizwa kwanza (Natural Justice)
Kabla ya hatua nyingine kuchukuliwa.

Badahi ya maeneo ambayo katibu mkuu ametakiwa kujieleza ni kama yafuatayo: (1) Kutozingatia maagizo ya baraza la Mawaziri kuhusian ana suala la ununuzi wa mitambo ya umeme wa dharura.

(11) Kutozingatia ushauri wa kitaalam ukliotolewa na PPRA kuhusu kufuata sheria ya manunizi ya Umma ya mwaka 2004 na kanuni zake za mwaka 2005.

(111) Kutoishauri Serikali ipasavyo kuhusu umuhimu kuifanyia uchunguzi zaidi kampuni ya Richmond Development Company (LLC) ili kujidhihirisha na uwezo wake kifedha kiutendaji, kiutaalamu na kiuzoefu ili kulinda maslahi ya Taifa.

Hivi sasa Mamlaka yake ya nidhamu ambaye ni Katibu Mkuu kiongozi inafanya uchambuzi wa maelezo yake aliyoyawisilisha ili hatiame maamuzi yatolewe kwa kuzingatia sheria kanuni na taratibu za utumishi.

Azimio Namba 15.
“Utaratibu wa kuteua Wakurugenzi wa Makamisha katika Wiazarta kuwa Wajumbe wa bodi za wakurugenzi wa Mashirika yaliyo chini ya Waizara zao unazua mgongano wa kimaslahi na kudhoofisha usimamzi pamoja na uwajibikaji, hivyo serikali iupige marufuku mara moja”

Hatua zilizochokuliwa.

Ni ukweli Kuwa huenda katika baadhi ya maeneo mfumo huu wa uteuzi wa Wakurugenzi au Makamishna kuwa wajumbe wa Bodi za Mashirika ya umma unaweza kuwa na matatizo.

Hata hivyo baada ya seriklai kuzingatia Azimio hili imeona pia kwamba zipo pia faida za baadhi ya Wakurugenzi au Makamishna kuwa wajumbe wa bodi hasa katika kusaidia kutoa msimamo na ufafanuzi wa sera na mipango mbalimbali ya serikali.

Kwa kuzingatia umuhimu huo seriklai ianona ni vyema utaratibu huo uendelee lakini kila bodi itaangaliwa kipekee pale itakapodhihirika kuwa ni maslahi ya taifa kuwateua baadhi ya Wakurugenzi au Makamishna kuwa wajumbe katika baadhi ya bodi serikali itafanya hivyo kwa maslahi ya taifa letu.

AZIMIO NAMBA 16.

“Kwa kuzingatia umuhimu wa nafasi aliyonayo Mheshimiwa Waziri Mkuu katika uendeshaji wa shughuli za serikali na uongozui wa Nchi kw aujumla, ni wajibu wake yey mwenyewe kupima uzito wa amtoeko ya uchunguiz huu na wajibu wake kikatiba ndani na nje ya Bunge, vilevile ni wajibu Ibara ya 51 ya katiba kuangalia kama matokeo ya uchunguzi huu hayataathiri hadhi na uzito wakle nadni ya Bunge”

HATUA ZILZIOCHUKULIWA.

Serikali imefanya uchunguzi juu ya usajili wa Kampuni ya Richmond Development Company(LLC) pamoja na Richmond development Company Tanzania (LLCT) ili kubaini uhalali wake na kutaka kujidhihirisha kama usajili wake uliofanywa na BRELA ulikuwa kinyume cha sheria za Nchi Uchunguzi huo umebaini yafuatayo.

(1) Kampuni ya Richmond Development Company (T) Limited ili kubaini uhaklali wake na kutaka kujidhihirisha kama usajili wake uliofanyw ana BRELA ulikuwa kinyume cha Sheria za nchi uchunguzi huo umebaini yafuatayo.
(2) Kampuni ya Richmond Development Company(T) Limited ni kampuni iliyosajiliwa na BRELA hapa Tanzania terehe 12 Julai 2006 na kupewa Certificate of Incorporation Namba 57014 ili kuiwezesha kupatiwa leseni ya biashara ya uzalishaji wa umeme na Masoko unaonyesha kuwa Richomond Debvelopemnt Company (LLC) haikuwa imesajiliwa na BRELA.


(ii) Hakuna taarifa ndani ya BRELA zinazoonyesha kuwa Richmond
Development Company LLC iliyoshinda zabuni husika, ilikasimu
jukumu lake la kuzalisha umeme wadharura kwa Richmond Development
Company (T) Limited ambayo ndiyo ilisajiliwa Nchini kwa kusudio hilo.

(iii) Kutokana na utata huo uliojitokeza , Mwanasheria Mkuu wa Serikali
ametoa ushauri juu ya Mamlaka ya BRELA Limited kwa kuzingatia
Sheria ya Makampuni (Sura ya 212) ,Hivyo kwa mujibu wa kifungu cha
215 cha Sheria hiyo, BRELA imekwishatoa motisi ya siku thelathini
kwa Kmapuni ya Richmond Development Company (T) Limited
kuwasilisha utetezi wake kabla ya hatua za kuifuta kampuni hiyo
kuchukuliwa .Taarifa hiyo ya notisi iliyotolewa na BRELA haijajibiwa.

AZIMIO NAMBA 18.
“Wamiliki wa Richmond Development Company LLC na Richmond Development Company (T) Ltd wafunguliwe kesi ya jinai mara moja kwa udanganyifu na ujanja wa kuiibia Serikali”.

HATUA ZILIZOCHUKULIWA:
Awali, Serikali ilimuagiza Mwanasheria Mkuu wa Serikali kupitia kwa makini Taarifa za Kamati Teule ya Bunge pamoja na kumbukumbu zote za Mjadala wa suala hili Bungeni ,ili kubaini maeneo yenye Makosa ya Jinai ambayo yangewezesha Serikali kuwafungulia mashtaka Wamiliki wa Kampuni ya Richmond Development Company LLC na Richomond Development Company (T) Ltd na Wawakilishi wao.

Baadhi ya maeneo ambayo yaliangaliwa ni pamoja na

(a) Kampuni ya Richmond Development Company LLC kuwasilisha taarifa za udanganyifu Serikalini kwamba wanauwezo wa kifedha,kiutendaji na utaalam katika kuzalisha umeme jambo ambalo halikuwa kweli.

(b) Kuwasilisha Hati na Vielelezo vya udanganyifu kwa Kamati ya Serikali na Mjadiliano kuwa Kampuni ya Richmond Development Company LLC ina Mkataba wa Ubia (Consortium Agreement )baina yake na Kampuni ya Pratt& whitney ambayo inajulikana kuwa na uwezo mkubwa Kimataifa

Baada ya zoezi hilo kufanyika, Mwanasheria Mkuu wa Serikali alishauri kuwa pamoja na mambo mengine ipo haja kwa Serikali

(i) Kufanya uchunguzi wa kina ili kuthibitisha kuwa Kampuni ya Richmond
Development Company LLc haina uhai wa kikampuni (Corporate
Peronality ) na hivyo kujiridhisha kuwa mambo yote yaliyofanywa kwa
jina la Kmapuni hii, yalikuwa batili.Hii ni kwa kuzingatia fungu la 320 la
sheria ya Makampuni (Sura ya 212).

(ii) Kufanya uchunguzu wa kina katika makosa yanayoonekana kuwa ya jinai kwa watu waliohusika katika uwasilishaji wa baadhi ya nyaraka na vielelezo vingine vya udanganyifu vilivyowezesha Kampuni ya RICHMOND kupata ushindi wa Zabuni hii.

(iii) Kwakuwa Makosa ya Jinai hupelelezwa na Polisi ,TAKUKURU , Mamlaka ya Mapato na Vyombo vingine ambavyo vimepewa Mamlaka hayo kisheria , serikali iagize Vyombo hivyo vya Dola vilivyopewa Mamlaka ya kufanya upelelezi na kukusanya ushahidi vifanye kazi hiyo.Hii ni kwa mujibu wa Sheria ya Mwenendo wa Mashtaka ya Jinai (The Criminal Procedure Act Cap.20.R.E 2002).

Lengo la zoezi hili ni kijiridhisha na kupata umweli na ushahidi wa kurtosha unaoweza kupokelewa na kukubalika Mahakamani kwa kuzingatia masharti ya sheria ya ushahidi (The Evidence Act cap 6.R.E.2002)

Hivyo hivi sasa Vyombo vya Dola ikiwemo Idara ya Polisi vimepewa kazi hiyo na vinaendelea kufanya upelelezi na uchunguzi wa kina wa nyaraka na hati mbalimbali zilizowasilishwa na wahusika kabla ya kuchukua hatua nyingine dhidi ya Wamiliki wa Kampuni ya Richmond Development Company LLC na Richmond Development Company (T) Ltd na Wawakilishi wao kwa kuzingatia Sheria , Kanuni na Taratibu zilizopo.

AZIMIO NAMBA 19:
“Serikali ichukue hatua za kuvinoresha na kuvitumia ipasavyo Vitengo vya Utabiri wa Hali ya Hewa na Kitengo cha Maji –TANESCO ili kuepusha Nchi na Maamuzi ya zimamoto, ambayo uzoefu unaonyesha yanaiingiza Nchi kwenye hasara kubwa”.

HATUA ZILIZOCHUKULIWA:
Hatua zifuatazo zinaendelea kuchukuliwa na Serikali kama mkakati wa utekelezaji wa Azimio hili:
(i) Serikali imeanza kuimarisha Wakala wa hali ya Hewa Nchini kwa kutoa mafunzo na kuwapatia vifaa vya kisasa kama kompyuta, vifaa vya kupimia mvua na ununuzi wa mitambo ya kisasa ya mawasiliano nay a kuchambua takwimu za hali ya hewa.mfano, hadi sasa Serikali imekwishanunua mitambo ya mawasiliano ya kisasa iitwayo Retin 4 na Snergie kwaajili ya kuimarisha Utabiri wa hali ya Hewa Nchini.

(ii) Kuhusu ushirikiano baina ya Kitengo cha Utabiri wa Hali ya Hewa na TANESCO pamoja na Mabonde ya Maji ni mzuri, kwani kila siku TANESCO inapokea Taarifa za utabiri wa hali ya mvua na kuziingiza katika Takwimu za Msingi9( Data base) zinazoonyesha Mfumo wa uzalishaji umeme wa kila siku.

(iii) Vilevile ,serikali kupitia Mradi wa Maendeleo sekta ya Maji (Water sector Development program) itaimarisha Ofisi za mabonde ya maji ili kuwezesha upatikana wa taarifa muhimu kwa Vitengo vya mai vya TANESCO>Hii ni pamoja na kutoa mafunzo kwa Watumishi na kukunua zana za kufanyia kazi kama vile magari na vifaa vya kupima kina cha maji, na wingi wa maji kwenye mito na mabwawa. Vifaa vingine ni vya kupimia mvua, maji nchini ya ardhu ,kupima ardhi na kuanzisha Mtandao wa Mawasiliano kwa njia ya Kompyuta

AZIMIO NAMBA 20:
“Serikali iendeshe uchunguzi maalumu ili kubaini ukweli kama Taarifa rasmi ya TAKUKURU iliyotoa matokeo ya uchunguzi kuhusu mchakato wa Richmond lilikataliwa na kuharibiwa na kutolewa nyingine na kama jalada halisi linalohusu Kampuni ya Richmond lililokuwa BRELA liliharibiwa na kuwekwa lingine kwa lengo la kuficha ukweli”

HATUA ZILIZOCHUKULIWA:
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwakushirikiana na Vyombo vingine vya dola wanaendelea na uchunguzi wa kina kuhusu suala hili.

AZIMIO NAMBA 21:
“Ofisi ya Bunge ianzishe Mktaba Maalum itakayohusika na utunzaji wa Mikataba yote uinayoingiwa na Serikali”.

HATUA ZILIZOCHUKULIWA:
Serikali inakubali utaratibu huo na itatoa ushirikiano ili kufanikisha utekelezaji wa Azimio hili kama nilivyoeleza katika Azimio Na.13.

AZIMIO NAMBA 22
“Miswada yote inayowasilishwa Bungeni hasa Miswada ya umeme na Mafuta, (The electricity Bill, 2007 na Petroleum Supply Bill, 2007) izingatie changamoto zilizoonekana wakati wa mjadala wa taarifa ya kamati Teule”

HATUA ZILIZOCHUKULIWA

Miswada ya Sheria ya Umeme na ule wa Sheria ya mafuta ilijadiliwa bungeni mwezi Aprili 2008 na kupitishwa. Wakati wa Mjadala huo, ushauri uliopo katika Azimio hili ulizingatiwa kikamilifu.

AZIMIO NAMBA 23:

“Serikali iyafanyie kazi mapendekezo ya kamati teule na kuliarifu Bunge kuhusu utekelezaji wake ndani ya miezi mitatu kuanzia tarehe 15/2?2008.”

HATUA ZILIZOCHUKULIWA:

Hali halisi inaonyesha kuwa, jitihada zimefanywa na Serikali kuhakikisha Maazimio ya Bunge yanatekelezwa ndani ya miezi mitatu kuanzia tarehe 15 februari 2008. Muda huo uliisha tarehe 14 Mei 2008. Hata hivyo, katika utekelezaji, imedhihirika kuwa baadhi ya Maazimio yanayohitaji muda mrefu kukamilisha mchakato wake wa utekelezaji hasa yale yanayohusu marekebisho ya Sheria na mifumo mbalimbali ndani ya serikali na pia yale yanayohitaji kufungua mashtaka ya jinai au mashtaka ya makosa ya nidhamu.

HATUA ZA NIDHAMU KWA WATUMISHI:

7. Mheshimiwa Spika, kabla ya kumalizia naomba kutoa angalizo kwamba , katika kushughulikia suala hili, kamati Teule ya Bunge katika baadhi ya Maazimio yake yanayohusiana na kuwachukulia hatua za kinidhamu baadhi ya watumishi wa Umma waliohusika katika mchakato mzima wa Mkataba baina ya TANESCO na RICHMOND, imetumia maneno mbalimbali kama ifuatavyo:

AZIMIO NAMBA 5:

“…Wawawajibishwe na Mamlaka ya juu ya Nchi kwa kuchangia kuiingiza Nchi katika Mkataba wa aibu.”

AZIMIO NAMBA 7:

“…Maofisa Waandamizi wa Serikali wawajibishwe kwa manufaa ya Umma…”.

AZIMIO NAMBA 9:

“… wawajibishwe kwa manufaa ya Umma.”

AZIMIO NAMBA 14:

“…Wachukuliwe hatua kali za kinidhamu kwa kuliingiza Taifa kwa makusudi kwenye Mkataba wa Kampuni ya Mfukoni,”

8. Mheshimiwa Spika, katika kutafsiri maana ya maelekezo haya, Serikali imeona kwamba yanaweza kuwa na maana ya kushtakiwa Mahakamani kwa Makosa ya Jinai; ama kutumia Mamlaka ya Rais ya kuwastaafisha kwa manufaa ya Umma; ama kuchukua hatua za kinidhamu kwa mujibu wa sheria ya utumishi wa Umma na kanuni zake.

Serikali baada ya kutafakari kwa kina suala hili, imeona kuwa katika mazingira ya suala hili, ni busara kutumia utaratibu wa hatua za mashtaka ya nidhamu chini ya sheria ya Utumishi wa Umma. Utaratibu hu ni mwepesi na unaweza kusimamiwa kwa haraka zaidi lakini bila ya kuathiri misingi ya Haki Asilia(Natural Justice) ya mtu kupewa haki ya kusikilizwa kwanza. Hii ni hatua muhimu sana kwani hata chini ya Mamlaka ya Rais ya kumstaafisha Mtumishi kwa manufaa ya umma, taratibu zinataka mtumishi apewe fursa ya kutoa maelezo ya kutetea kabla ya hatua yoyote kuchukuliwa. Hii inatuondolea hatari ya serikali kushtakiwa kwa kutofuata sheria, Kanuni na taratibu kama ilivyowahi kutokea huko nyuma ambapo baadhi ya viongozi na watendaji walistaafishwa kwa manufaa ya umma kimakosa, na baadaye serikali ikalazimika kuingia gharama kubwa ya kuwalipa fidia. Vilevile, hatua hii inaipa nafasi serikali kupitia utetezi utakaotolewa kuona ni watumishi gani wanaoweza kustahili kushtakiwa kwa makosa ya jinai kwa mujibu wa Sheria za Nchi.

HITIMISHO:

9. Mheshimiwa Spika, napenda kusema kuwa yapo mambo mengi ambayo sisi kama taifa tumejifunza kutokana na mapungufu yaliyojitokeza katika mchakato wa zabuni ya mkataba baina ya Tanesco na Richmond, lakini pia na mikataba mingine. Kwa kuzingatia hali hiyo, Serikali imeanza kulifanyia kazi suala la kuimarisha mfumo wa uwezo wetu wa ndani wa majadiliano ya mikataba hasa ile mikubwa ya kibiashara na kiuchumi na ya muda mrefu yenye maslahi makubwa kwa Taifa letu kwa kuchukua hatua mbalimbali. Ofisi yangu tayari imepata maoni ya wanasheria mbalimbali wakiwemo Mheshimiwa Andrew Chenge, Mbunge wa Bariadi Magharibi na Mwanasheria Mkuu wa Serikali staafu; Mheshimiwa Johnson Mwanyika-Mwanasheria Mkuu wa Serikali; na Mheshimiwa Nimrod Mkono Mbunge wa Musoma vijijini. Maoni yao yatatusaidia sana katika kuimarisha mfumo wa wetu wa majadiliano ya mikataba. Naomba nitumie nafasi hii kuwashukuru waheshimiwa wabunge hawa kwa maoni na ushauri wao mzuri sana.

Vilevile, nimepata nafasi ya kuzungumza na Mheshimiwa Dkt. Harrison Mwakyembe Mbunge wa Kyela, ambaye pia alinipa ushauri mzuri kuhusu namna mbalimbali za kui8marisha majadiliano katika mikataba baina serikali na vyombo vingine vya uwekezaji. Naomba kutumia fursa hii naye kumshukuru sana kwa mawazo yake.

Aidha, Ofisi yangu kwa kushirikiana na Wizara ya Sheria na Katiba kwa kushirikiana na Shirika la Mpango wa Maendeleo la Umoja wa Mataifa(UNDP), tunaendelea kulifanyia kazi jambo hili. Serikali inatarajia kwamba jitihada hizi zitatuwezesha kubaini kwa kina mapungufu yaliyopo na kushauri njia bora zaidi za kuimarisha majadiliano yanayohusu mikataba.

10. Mheshimiwa Spika, mwisho natoa wito kwa watumishi wote wa Umma kufanya kazi kwa uadilifu, bidii, uzalendo na kuwa makini katika kila kazi kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na Taratibu za Serikali. Kwa upande wake Serikali itajitahidi kuhakikisha kuwa viongozi na watendaji wote katika ngazi zote za Utumishi wa umma wanafanya kazi kwa umakini na kuwatumikia wananchi kwa kutanguliza mbele maslahi ya Taifa letu.

11. Mheshimiwa Spika, naomba kuwasilisha.

(tamati).

COMMENTS

BLOGGER: 1
Loading...
Name

Anga,12,Arusha,27,batiki,1,Burudani,447,burundani,2,come rain,1,come sun,1,Crazy in Love kama wimbo kama wao wenyewe,1,dahh sijui kweli mbona shida,1,Dar utakuja je tumejiandaa,1,daraja sahau nini,1,demokrasia ya upanga,1,Dodoma,78,Dole tupu vijana wa zamani,1,Duhh bibie endeleza libeneke,1,Duhh kaisikie Walibana,1,duhh kwa mbagala mama lazima awe supa,1,Fedha za maiti haziliwi bure,1,Fedha za watu kwa maendeleo ya watu,1,Fikira,14,filamu,287,Filamu ndio kielelezo cha ukuzi wa taifa,1,flamu,7,Gandamiza Kibara baba ake,1,haba,1,habar,3,Habari,7054,habari dodoma,39,habari. dodoma,32,habaria,1,hadithi,23,hakika tumeweka historia,1,hakuna noma jongwe,1,hapa kwetu inakuwaje vile,1,hasira hasara,1,hata maji,1,hataki masikhara na maisha yake,1,hatubonyezi kizenji,1,haya ndiyo mambo ya Ulaya,1,haya si yangu ni ya mdau mwenye hasira,1,haya wabongo na mambo kutoka nje,1,He he he wananikumbusha upishi wa shaba,1,Headline,1,Hii hurejesha uhai,1,Hii iko sawa kweli?,1,Hii imekaa vizuri,1,Hii inakaaje vile,1,Hii kweli noma,1,Hii maana yake Moro kuna uhaba wa chakula,1,Hii mexico,1,Hii mihasira mingine bwana,1,Hii ndio moro sio mpaka dar,1,hii ni hatari,1,Hii ni kiboko anayetaka kubisha ajibishie tu,1,Hii ni moja ya staili za kunyoa nywele,1,Hii si lukwangule,1,hii staili mpya,1,hili ni jengo pacha la malaysia ghorofa 88,1,Hivi ni ngoma tu,1,hivi nini siri za serikali,1,hivi sisi tunajua kama kuna vitu vya aina hii,1,hivi vitu bwana,1,Hiyo ndiyo gharama ya demokrasia,1,Hizi imani nyingine ni hatari,1,Hizi takwimu hizi mhh,1,Hongera bibie,1,Hongera dada etu kwa kutuletea kaka etu (shemeji) kwani mwenye dada hakosi shemeji,1,Hongera sana,1,huhitaji mifedha kuwa msafi,1,Huko Ulaya,1,Huu ndio ustaarabu,1,huu ujiko utakuwa mkubwa,1,imetosha,1,Inahitaji nidhamu fulani,1,inakuuma au...,1,Inakuwaje kama filamu yenyewe itahitaji busu la nguvu,1,Inaonekana watanzania hatukuwepo,1,Ipo kazi Maximo,1,Iringa,22,Isiwe mijineno tu manake mihela hubadili watu kweli,1,Itakuwa laki moja ya halali,1,jamani huu kama si ushamba kumbe nini,1,Jamani mbona Mungu anatupigania,1,Jamani watoto wanatakiwa kupendwa,1,jamani.. jamani ukiikosa Diamond usijutie,1,Je nyumbani hakuna vitu vya aina hii?Tuambie,1,je walikuwepo watu wa huduma ya kwanza,1,Je watanzania wanalipa kodi,1,jela kwa raha,1,Jolie,1,juhudi za lazima kuinua filamu,1,kama si kiwanda cha chumvi nani atawajua hawa,1,Kama kweli ndio kweli basi kila heri,1,Kama Mkristo naamini hilo hiyo si sahihi,1,kama unajua kuyarudi nenda Malta,1,kama wao wanaweza sisi je,1,Kamua baba waache wakanyagane,1,karibu nyumbani dada yote maisha tu,1,karibu Tatiii,1,KARIBUNI,1,Katavi,5,kaza buti hakuna kukata tamaa inalipa,1,kazi kwako mheshimiwa waziri wa madini,1,kazi na burudani,1,keep it up bloggers,1,kero ya usafiri sasa kwisha,1,Kila chenye roho na mwili kitaonja umauti,1,kila kitu kina vitu,1,Kila la Heri jamila,1,kila la heri kwani ni changamoto,1,Kipya,51,Kiuno bila mfupa,1,Kolelo mzimu ambao bado hai,1,KUBWA,1,Kudumisha urafiki wa dunia,1,Kuna dalili za wasomi kukubali Uafrika,1,kuna makala humu humu ndani ya blogu sijui mnasemaje,1,Kuu,113,kwa mara nyingine tena Tigo imewezesha,1,Kwa mchanganyiko huu muungano lazima udumu,1,Kwa mihasira hajambo,1,kweli,1,Kweli ina mkono mrefu tuone,1,Kweli duniani tunatofautiana,1,la maana ni kuwa na jiko au vipi,1,labda halitabadilika tena,1,lakini mwafaka lazima,1,lengo ni kutafakari,1,leteni vitu tuvione,1,lets us,1,Lucy wanakuelewa hawa...,1,Lukwangule nyumbani kwetu,2,M ungu bariki mikono ya madaktari wafanikiwe,1,MAARUFU,1,maendeleo ya soka siku zote yanahitaji fedha ili yapatikane,1,maisha ni vyema kuyaangalia,1,MAJIBU,1,makala,52,mama ni mama tu anapendeza,1,mambo mengine we angalia tu,1,mambo msimamo,1,mambo sasa mchanganyiko,1,Mara nyingine huona tunakotoka kwa kuona wenzetu,1,Mashabiki wa rhumba mpooooooooo,1,Masitaa,12,Maskani,1,MASOKO,3,Masupa staa mnaoinukia mpoo,1,Matamasha,6,mavazi ya kuogelea yanaposhindaniwa,1,Mbeya,11,Mchakamchaka anti Asmah,1,Mchanganyiko,81,MCHANYATO,1,mchezo,6,mengi wanayoyaita siri ni public information,1,mfumuko wa bei mpaka noma,1,Mhh sijui watu wa Sua ambao wako huko wanasemaje,1,Mhh ugua pole dada watu wanataka burudani,1,Michezo,739,Michezo maalum inatakiwa kupigiwa debe,1,miguu,1,miguu babu,1,Mikataba mingine ama hakika tuiangalie hata wakopeshaji nao wanatugeuza sakala,1,MIMI NI KISURA NAJITAMBUA,1,Mimi sijajua hasa kumetokea nini kwani ninavyojua hawa huwa na ungalizi wa hali ya juu,1,Mimi simo,1,mimi sisemi,1,miochezo,1,mkiwa chumvi basi mkoze,1,Mkiwa taa mulikeni,1,Mnaonaje je hii imekaa vyema,1,Mnaweza wakwetu hapa,1,Morogoro,51,mrithi wa mwanadada Whitney Houston,1,Mtwara,4,Mungu aiweke mahali pema roho yake,4,Mungu amrehemu,1,Mungu amweke pema peponi,1,Mungu awabariki sana,1,Mungu awe nao,1,Mungu ibariki Tanzania,1,Mungu tuepushe na imani hizi za kishirikina,1,mungu tufanye tuwe na upendo,1,Mungu twaomba utuhurumie,1,Muziki,376,muziki na fasheni,20,Mwanahabari,33,Mwanza,6,Mwendo mdundo dada,1,Mwenge huo utakimbizwa duniani kwa siku 130,1,Mwenge wa olimpiki ni ishara ya urafiki,1,Mzee wa Farasi nakupa saluti,1,Mzimbabwe huyu kutoka kwa mama mkali,1,N i dar mpaka Moro au bao tatu bila,1,Na sisi je,1,Naam kama haiwezekani hapa,1,Nairobi waanzisha tena utalii,1,namna bora ya kusaidia jamii,1,nani abebe hukumu na lawama,1,nani asiyejua utamu wa pipi,1,Nani kama baba,1,naona inafaa kuchangia mimi sitoi hoja,1,ndoa za mastaa huwa na mgogoro,1,nenda mwaya nenda,1,New Zanzibar Modern Taarab na wapenzi big up,1,news,5,Ni bikini kwa kwenda mbele,1,Ni Dar mpaka Moro au.. tatu bila,1,ni furaha za muungano,1,Ni kazi ngumu yenye kuhifadhi utamaduni,1,Ni kuchakarika kuonyesha urafiki na biashara pia,1,ni mfumuko wa bei au mfumuko wa nchi,1,Ni muhimu kutazama afya yako,1,ni muziki kwa kwenda mbele,1,Ni muziki mpaka China,1,Ni raha tupu,1,Ni Serengeti Premium Lager,1,Ni Tigo na mawasiliano ya kisasa,1,Ni wakati wa kuujadili utamaduni,1,Ni zaidi ya jazz,1,Nitasubiri and welcome home,1,nje je?,1,NUKUU YA LEO,1,nyie mnasemaje kuhusu hili,1,Ona Kolelo na sindikizwa na Wazee wa Gwasuma,1,ona vya dunia,1,One step ahead,1,patna mwingine mjamzito,1,Pengine anamuogopa Jada Pinkett manake kwa wivu..,1,picha,494,Pole Jamila hayo ndiyo mashindano,1,poleni sana,1,poleni sana wanyalukolo,1,Powa sana,1,Profesa jamaa wanakumaindi,1,Roho za marehemu zipate pumziko la milele,1,Ruvuma,9,sakata dansi mpaka kwenye kilele cha dunia,1,sasa kumebakia ugonjwa mmoja polisi kuendesha mashtaka,1,sasa mifedha kila mahali hongereni,1,Sasa ni mavuno,1,Sasa ni wakati wa kutafuta upenyo ndani ya IDOLS,1,SAYANSI,9,SAYANSI ANGA,12,See Uluguru Montains,1,serikali inataka kujihami kwanini,1,Show of support Big Up Madame,1,Si kitu kidogo hata kidogo,1,si unajua tena namie naimwaga hivyo hivyo,1,Siasa,346,siasa habari,2,Sijui kama City wanajua Mbagala noma,1,Sijui tunaishi karne gani yailahi,1,Sinema,17,sio advencha....kaaa ...niko kibaruani,1,Sisi ndio tunaanza vitongoji,1,Sisi yetu macho na masikio,1,Slow slow jamani,1,sto,1,tabasamu kali la mwenge wa olimpiki,1,Tabora,1,Tazama Waziri Mkuu Pinda wasije wakapindisha maamuzi yako,1,TEKNOLOJIA,1,Thats big man game,1,This is crazy Africa,1,This is Mgeta,1,Tibet wamegeuza Olimpiki jukwaa la siasa,1,Titbits collection,1,Tubadili tamaduni,1,Tuchangie mambo yaive,1,tuendeleze sanaa,1,tuienzi na sisi mbona wizara haituambii,1,Tuipeleke kaskazini,1,Tuisaidie serikali shida ya Mererani,1,tujue namna ya kupumzika,1,Tulienda kustarehe au kufanya fujo,1,Tumsaidie mtototo huyu kurejea katika hali ya kawaida,1,tunahitaji haya,1,Tunajifunza kweli kutoka kwao,1,Tunapandisha chati tu,1,Tunasubiri,1,tunazidi kuhesabu siku,1,TUNAZISUBIRI ZA VINARA ADAR,1,Tuombe nafuu kwa wagonjwa,1,Tuombe rehema kwa mungu,1,Tuone yatufae,1,Tusingoje wengine watusemee,1,tutampa tafu kubwa Prof,1,tuuenzi utamaduni au vipi,1,Tuukuze na kuulinda,1,tuvipende,1,tuwalinde maalbino,1,Tuwe kweli wakweli,1,ubunifu siku zote hulipa,1,uchumi huzunguka kwa kuwawezesha wasukaji,1,udumu muungano,1,Ugonjwa huu wa sasa ni kitendawili,1,Ukiiona kolelo utaipenda,1,Ukirejea salama kila mtu anafurahi,1,Umelenga Mkuchika utamaduni unakufa,1,unaposaka uwakilishi wa dunia,1,urafiki,1,urembo,1,Usisahau wazee wa Ngwasuma,1,UTALII,1,UTAMADUNI,4,Video,2,Vionjo vipya ndani ya Gwasuma,1,Vita dhidi ya ufisadi,1,vitongoji Miss Tanzania navyo vimeanza,1,Vitu vikali vyazidi kuingia Dar,1,Vituko,77,Vituo vya polisi Tanga vyatelekezwa,1,VIVALO,1,Wacha tujifue,2,Wadau ilitolewa kiingereza,1,wakali wa ubunifu,1,wala usibabaike mwakwetu hii noma,1,wanadamu wanapotaka kujua zaidi,1,wanasema mpaka kieleweke,1,Wanataka kujua mali za JK na wengine,1,Wanawake wenye mvuto: Monroe,1,Wapo mabinti wa matawi ya juu,1,watu wanapofanya weli kwenye sanaa,1,waweza kurejea enzi ya Moro jazz na Cuban malimba,1,Wazee tupo kusindikiza,1,waziri,1,welcome dar baby,1,Wenzetu wameona sisi tunangoja nini kuangalia,1,wewe unasemaje,1,wigo mpana wa utamaduni,1,wilaya ya 'Mbagala' mlie tu,1,Yaaani sijui itawezekana,1,Yaani wakati mwingine hata huelewi prioty over priority,1,yeye mbele sisi nyuma,1,Yote maisha dada,1,ZA MOTOMOTO,1,Zanzibar,79,zawadi zinatakiwa ziende shule,1,ZILIZOTIA FORA,1,zitachangia kupunguza makali ya bei za umeme,1,
ltr
item
Lukwangule Entertainment: Taarifa ya Waziri Mkuu kuhusu Richmond aliyoitoa leo Bungeni
Taarifa ya Waziri Mkuu kuhusu Richmond aliyoitoa leo Bungeni
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhI84AAzXjYgxKt4llP6aLGpCnQgEVza_PIpESJMCg3yPyaE1dxJjk5tKpuU3I5p5_s6CARRMvczPju3WGSD2JHEFeoSqDwU2unwJnoZtE9JOtWEUbGkzGmoGXnF1BkiTJz-zz1LWP_rcep/s320/_MG_0002.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhI84AAzXjYgxKt4llP6aLGpCnQgEVza_PIpESJMCg3yPyaE1dxJjk5tKpuU3I5p5_s6CARRMvczPju3WGSD2JHEFeoSqDwU2unwJnoZtE9JOtWEUbGkzGmoGXnF1BkiTJz-zz1LWP_rcep/s72-c/_MG_0002.JPG
Lukwangule Entertainment
http://lukwangule.blogspot.com/2008/08/taarifa-ya-waziri-mkuu-kuhusu-richmond.html
http://lukwangule.blogspot.com/
http://lukwangule.blogspot.com/
http://lukwangule.blogspot.com/2008/08/taarifa-ya-waziri-mkuu-kuhusu-richmond.html
true
934549962738256429
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy