TANZANIA GENDER NETWORKING PROGRAMME P O BOX 8921, DAR ES SALAAM, TEL. +255 22 2443205;2443450;2443286 Mobile 255 754 784 050 Fax. 2443244,...
TANZANIA GENDER NETWORKING PROGRAMME
P O BOX 8921, DAR ES SALAAM, TEL. +255 22 2443205;2443450;2443286 Mobile 255 754 784 050 Fax. 2443244, Email info@tgnp.org, web www.tgnp.org
UZINDUZI WA MACHAPISHO: TATHMINI YA MIAKA 10 YA BEIJING: Mapendekezo kwa ajili ya Ushawishi, Utetezi na Mjadala wa Umma, NA HALI HALISI YA KIJINSIA TANZANIA:Kuimarisha Usawa wa Kijinsia,
TAARIFA KWA UMMA
Leo tunakutana katika mfululizo wa Semina za Kila Jumatano kuzindua rasmi chapisho la Hali Halisi na tathmini ya madai ya Miaka 10 ya Beijing.Huu ni uchambuzi mbadala wa hali ya mahusiano ya kijinsia Tanzania na mabadiliko muhimu yanayotakiwa katika kufanikisha ukombozi wa wanawake na usawa wa kijinsia.
Kwanini taarifa hii ni muhimu?
Watanzania wamekanganyikiwa sana juu ya taarifa tofauti kuhusu hali ya kiuchumi na hali ya maisha ya watu, nyingi ya taarifa hizi zimekuwa zikitolewa na serikali yenyewe, wafadhili vyama vya kiraia na watu binafsi..Ni hivi karibuni tu ambapo serikali imeelezea hali yake ilivyo kiuchumi, uchambuzi uliotolewa kupitia Bunge kuwafikia wananchi wa Tanzania. Taarifa hii ilidondoa vipengele vya mafanikoio kama vile kukua kwa uchumi katika eneo la uuzaji bidhaa nje ya nchi na kuongezeka kwa ajira. Kwa mujibu wa serikali na makundi yenye ushawishi mkubwa katika jamii yetu, kadhalika imeetaarifiwa kuwepo kwa hatua na mikakati madhubuti kuzingatia suala la jinsia katika sekta zote za serikali.
Hata hivyo tunaamini kwamba ni muhimu kwa wanaharakati wa masuala ya jinsia na ukombozi wa wanawake kufanya tathmini yao juu ya hali halisi katika ngazi zote kwa kutumia mtazamo wa wanawake na wasichana kadhalika na makundi mengine yaliyo pembezoni/yaliyosahaulika. Pamoja na kufanya tathmini hii pia ni muhimu wanaharakati kufuatilia jinsi serikali inavyotekeza mikakati na sera zake. Hatma ya maazimio na mapendekezo ya semina hii itasaidia katika tafakari ya vipaumbele ambavyo ni tofauti na vile vilivyopo vya sasa vya uzingatiaji wa masuala ya jinsia katika sera, utekelezaji na tathmini, kukosoa mfumo kiritimba uliopo, na kuweka mkakati wa kushinikiza hatua za utetezi na ushawishi.
Mnamo mwaka 2003, TGNP ilifanya uchambuzi wa tathmini ya utekelezaji wa mikakati ya maazimio ya kongamano la Dunia la Wanawake lililofanyika Beijing China mwaka 1995. Uchambuzi huu ulifanywa kwa niaba ya tume ya uchumi ya Umoja wa Mataifa ya Afrika na Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Tanzania. TGNP ilishirikisha pia wadau wengine miaka ya 2005 na 2006, na kupeleka madai na mapendekezo 15 madhubuti, ambayo yanazinduliwa leo hii a yakijulikana kama, Tathmini ya Miaka 10 ya Beijing: Mapendekezo kwa ajili ya Ushawishi, Utetezi na Mjadala wa umma. Madai haya yanagusia maeneo kama vile masuala ukombozi wa wanawake na usawa wa kijinsia, elimu, afya, uchumi, siasa na haki za wanawake.
Wakati huo huo, Mtandao wa Jinsia(TGNP) mnamo mwaka 2006 ilitoa chapisho la kiingereza lilijulikana kama Gender Profile of Tanzania 2006: Enhancing Gender Equity kwa msaada wa SIDA (Sweden), lililozinduliwa mwaka 2007 hapa katika semina hizi za jinsia na maendeleo (GDSS). Toleo la Kiswahili la Gender Profile sasa liko tayari, likiitwa, Hali Halisi Ya Kijinsia Tanzania:Kuimarisha Usawa wa Kijinsia. Chapisho hili linadondoa hitaji la kufanya mageuzi makubwa ya kiuchumi, katika suala zima la mahusiano ya jamii, masuala ya kisiasa na sheria kwa ujumla ili kufanikisha ukombozi wa wanawake na usawa na haki kijinsia. Katika chapisho hili chambuzi yakinifu umefanyika katika sera na mifumo ya uchumi mkuu; muundo wa mageuzi kiuchumi; ubinafsishaji; na mifumo ya soko huria; ajira, mila na utamaduni; sheria; siasa; vyombo vya habari; huduma za jamii na hatimae kuangalia hali ya mtoto wa kike. Taarifa hii inahitimishwa kwa muhtasari wa mafanikio, changamoto na fursa zilizopo ili kufikia lengo la ukombozi wa wanawake na usawa wa jinsia katika ngazi zote.
Leo tunakutana hapa kuzindua machapisho haya mawili, na la muhimu zaidi, kuungana pamoja katika kupanga jinsi gani tunavyoweza kufanikisha aina ya mabadiliko tunayodai-katika maisha yetu ya kila siku kadhalika katika mashirika yetu na jamii nzima kwa ujumla. Masuala yaliyoibuliwa na madai yaliyomo si mageni, mengi yao yalijadiliwa katika mijadala wa semina za jinsia na maendeleo (GDSS) kila wiki, na hususan ile iliyojadili matarijio ya Bajeti ya 2008/09 tarehe 14 mwezi Juni 2008 na ile iliyofanyika baada ya hotuba ya Bajeti tarehe 18 Juni 2008. Wanaharakati wa ukombozi wa wanawake na usawa wa jinsia wanatoa mwito na wanadai hatua za utekelezaji sasa!
Semina jinsia na maendeleo ya leo tarehe 27 Augusti 2008 itatoa fursa kwa wana GDSS, wanaFemAct, wadau wa mitandao na makundi yote, na wadau wengine kwa ujumla kupanga mikakati ya utekelezaji kwa pamoja kwa ajili ya kujenga uwezo na ushawishi, ili kuhakikisha kwamba madai na mapendekezo yaha yanazaa matunda.
Kila mshiriki atapata nakala ya chapisho na fomu ya mrejesho, na tunawakaribisha katika hatua ya baadae kutusadia na taarifa ya jinsi ambavyo chapisho hili limetumika na jinsi mnavyojiwekea mikakati ya ya kusonga mbele na katika harakati za ushawishi (na jinsi gani mtazitumia nakala za ziada za machapisho haya) Nakala za ziada zitapatikana baada ya kuwa tumepokea fomu za mrejesho kutoka kwenu.
Imetolewa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP)
………………………..
Usu Mallya
Mkurugenzi Mtendaji
Tarehe 27 Agusti 2008.

COMMENTS