Thursday, August 7, 2008

Waliovamia ubalozi waambiwa wameshalipwaaaa!!!

Wanafunzi waliovamia ubalozi wa Tanzania , Moscow, Urusi Agosti 5,2008 wakitaka kulipwa posho zao zote za Septemba na Oktoba mwaka 2007 wameula wa chuya .
Taarifa iliyotolewa na wizara ya mambo ya nchi za nje leo mjini dar es Salaam imesema kwamba wanafunzi hao kutoka Tanzania wlaiopo katika mwaka wa maandalizi wa lugha kwenye chuo cha Lumumba wameshalipwa posho zao zote wanazostahiki.
Wziara ya mambo ya nje wamesema kwamba kwa mujibu wa wizara ya elimu na mafunzo ya ufundi wanafunzi hao waliripoti chuoni Novemba 2007 na kulipwa posho zao kuanzia mwezi huo wa Novemba, 2007 hadi Septemba 2008.
Wizara hiyo ya mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa imesema kwamba bodi ya mikopo HESLB wamejulishwa kuwalipa posho zao za mwaka huu na mwakaniu kuanzia Oktoba 2008.

0 Comments:

Post a Comment

Subscribe to Post Comments [Atom]

Links to this post:

Create a Link

<< Home