Hali ya Athumani bado si nzuri, tumuombee kupona haraka
Leo mchana majira ya saa sita nilienda kumtembelea mpiganaji mahiri katika medani ya uandishi wa habari na upigaji picha Athumani Hamisi (picha) ambaye amelazwa hospitali ya Moi chumba I kwa matibabu baada ya kupata ajali ya gari huko Kibiti akielekea Kilwa Masoko kikazi. Sikuweza kupata nafasi ya kumuuliza daktari wake maendeleo yake. Lakini kundi kubwa la waandishi wa habari na wapiga picha walikuwepo kumjulia hali na alipata muda mdogo wa kusikiliza pole kutoka kwa watu mbalimbali.
Hali yake bado inaonekana ngumu kwani alikuwa akibubujikwa na machozi. Inataka moyo mkubwa kama wa Athumani Hamisi kuweza kuzungumza angalau neno kwa waliokuja kumjalia ari pale hospitalini.Inapasa kwa dini zetu kumkumbuka mpiganaji huyu mcheshi katika salam zetu kumtakia spidi katika kupona ili aweze kurejea tena katika libeneke na pia kutekeleza majukumu yake ya kifamilia.
Wakati anaingizwa hospitalini hapo alisikitika sana kuhusu watoto wake. Watoto hao ni pamoja na yatima ambao anawalea.Mungu amjalie kupona hima na kwa kupitia mikono ya madaktari aweze kupata tiba barabara itakayomnyua.


2 Comments:
Tunamwombea. Asante sana kwa update.
Msimbe mhesh Beda, Unajua tatizo letu la kupokea au kutumia pesa zetu bila maandalizi; Unakumbuka Waziri E. Lwassa alipopiga kelele za kujenaga shule bila Kelele za kutayarisha walimu Bora! Sasa la CT Scan ni tatitozx la kuleta vyombo bila kuandaa mafundi wake kuziangalia, na vile kwa kuwa ni moja hapao Muhimbili basi wakti mwingine ilikuwa inafanya kazi kupita kiwango chake, na pia wemekusanya pesa Lukuki lakini hawakuweza kuelekeza kwenye kuwekeza kwenye mashine Nyingine! TWAFAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAA
Post a Comment
Subscribe to Post Comments [Atom]
Links to this post:
Create a Link
<< Home