Monday, September 15, 2008

Inakuwaje huduma ya CT Scann inapokosekana nchi nzima?



What is happening? Sure usingelipenda kuamini hiki, mashine maalum ya CT scan ya pale Muhimbili ambayo ingeliweza kusema kila kitu kuhusu tatizo la Athumani Hamisi , mpiganaji aliyepata ajali ya gari siku nne zilizopita kuke Kibiti haifanyikazi na ile ya Aga Khan haifanyikazi na ile ya.... haifanyikazi... yaani sasa hilo hata siwezi namna ya kueleza kwani nasikia Muhimbili yaani Moi wao tatizo hawana zile dawa maalum zinazotumika katika mashine hiyo . Sasa hiyo kaaali kwelikweli....Niliuliza watu kazini kwake nini sasa kinaendelea wanasema wanafanya mpango wa kumuondoa kumpeleka jirani ili kupata kipimo hicho kwani bila kipimo hicho hakuna matibabu na ukizingatia lazima ijulikane maumivu yapo wapi ni muhimu kumvusha huko ili kupata vipimo kujua anatibiwa nini.Mungu na atusaidie tu kwani hakuna mabadiliko ya msingi katika maumivu yake.

Pichani ni mfano wa CT Scann na picha ndogo ni ya mpiga picha Athumani Hamisi

1 Comments:

At September 15, 2008 9:43 PM , Anonymous Tuplionyu said...

Wapunguze kununua magari ya fahari na wananunue mtambo wa CT Scan. na isiwe USED!

 

Post a Comment

Subscribe to Post Comments [Atom]

Links to this post:

Create a Link

<< Home