Liverpool yavunja mwiko
JINAMIZI la Liverpool kukosa ushindi wa ligi dhidi ya Manchester United kwa muda mrefu lilikwisha leo baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-1.
Alikuwa ni Ryan Babel aliyeingia akitokea benchi na kuandika bao la pili kwa Liverpool na hivyo kuwamaliza mabingwa hao wa Ulaya.
Carlos Tevez aliifungia United bao la kuongoza dakika tatu baada ya kuanza kwa mchezo huku Wes Brown akijifunga na kuisawazishia Liverpool kabla ya Babel kuandika bao la pili na kupata ushindi wa kwanza nyumbani dhidi ya United baada ya miaka saba.
“Tumekwenda mbali sasa, si tu kwa kupata pointi tatu, lakini pia tunajiamini,”alisema beki wa Liverpool, Jamie Carragher alipozungumza na Sky Sports News.
“Kwa muda mrefu sasa tumekuwa nje ya mstari, wanaotamba ni United na Chelsea. Inatupa nafasi ya kupumua upya”.
Liverpool imepoteza mechi tano na kutoka sare moja katika mechi sita za nyumbani za ligi dhidi ya majirani hao na nusura wapate kipigo kingine baada ya mpira uliotengezwa na mchezaji mpya Dimitar Berbatov aliyempasia Tevez na kuandika bao la kwanza katika dakika ya tatu tu ya mchezo.
Kipa Edwin Van der Sar aliizawadia Liverpool bao baada ya dakika 27 kwa kuruhusu shuti la Xabi Alonso kwenda moja kwa moja mguuni mwa Brown ambapo aliusukuma mpira golini mwake.


0 Comments:
Post a Comment
Subscribe to Post Comments [Atom]
Links to this post:
Create a Link
<< Home