RAIS Jakaya Kikwete amesema shule zinazojengwa katika maeneo ya Wahadzabe, watu wa jamii hiyo wasiachwe wasome peke yao, badala yake wachang...
RAIS Jakaya Kikwete amesema shule zinazojengwa katika maeneo ya Wahadzabe, watu wa jamii hiyo wasiachwe wasome peke yao, badala yake wachanganywe na wanafunzi kutoka maeneo mengine.
Alisema hatua hiyo itasaidia kuwafanya wanafunzi wa kabila hilo kujifunza tabia kutoka kwa makabila mengine ya wanafunzi ambao watapelekwa kusoma kwenye shule na pia kuzifanya shule zilizojengwa katika maeneo yao kuendelea kuwa na wanafunzi.
Rais pia aliagiza viongozi wa Wilaya ya Mbulu ambako kwa Mkoa wa Manyara ndiko wanakokaa kabila hilo ambalo wanaishi msituni huku wakitegemea chakula kinachotokana na matunda ya porini pamoja na mizizi, wajenge shule kubwa ambayo itasaidia kuchukua wanafunzi wengi.
“Ongezeni bidii, watu hawa ni lazima waondolewe porini na wasome, hatuwezi kuwaacha waendelee kuishi katika maeneo hayo,” alisema Kikwete wakati akipokea taarifa ya Mkuu wa Wilaya ya Mbulu, Elias Goloi.
Rais Kikwete pia aliagiza wanafunzi wa Kihadzabe ambao wanamaliza shule ya msingi wakifaulu, wapelekwe katika shule za sehemu nyingine ili waweze kuchanganyika na watu wengine.
“Hawa tukiwaacha waendelee kusoma wao peke yao hawawezi kujua kama kuna watu wengine humu duniani…mimi wakati nasoma pale Msoga kisha nikapelekwa Lugoba nilikuwa najua dunia hii ni ya Wakwere tu, lakini nilipoenda Kibaha Sekondari nikaona kumbe pia kuna watu wa kabila nyingine.
“Kwa hiyo na hawa wenzetu ni lazima tuwapeleke katika maeneo mengine, tusiwaache peke yao kwa vile tu ni Wahadzabe,” alisema na kuongeza bado jitihada zinahitajika kufanywa na uongozi ili kuwaletea maendeleo watu wa jamii ya Wahadzabe ili wafanane na watu wengine.
“Wasiwasi wangu shule hizo zinaweza kukosa wanafunzi hivyo ni lazima wachanganywe na wengine, wasisome peke yao,” alisema.
Naye Goloi katika taarifa yake, alisema Wilaya ya Mbulu ni miongoni mwa wilaya ambazo zina makundi maalumu ya jamii wakiwamo Wahadzabe ambalo linaendesha maisha yake kwa kuwinda, kuchuma na kuokota matunda, mizizi na kurina asali ya mwitu, huku wakihama hama katika bonde la Yaeda Chini.
Alisema wilaya imekuwa inachukua hatua mbalimbali kuhakikisha jamii hiyo inapata elimu kama jamii nyingine wilayani hapa, kwa kuwajengea Shule ya Msingi ya Yaeda Chini na kuifanya iwe ya bweni ili Wahadzabe wapate nafasi ya kuweka watoto. Kwa sasa ina wanafunzi wa msingi 60 wanaokaa shuleni.
Alisema wilaya pia inajenga shule mbili za msingi katika vitongoji vya Endajachi na Domanda vyote vya Wahadzabe kwa fedha za mpango wa MMEM ili kurahisishia kuwa na shule karibu na maeneo yao.
Alisema wilaya imeanzisha sekondari inayotarajiwa kuwa ya bweni ya Yaeda Chini na tayari imesajiliwa mwaka huu na imepokea wanafunzi wa kidato cha kwanza 18. Alisema hadi sasa shule hiyo iliyojengwa kwa nguvu za wananchi na msaada wa serikali imekamilisha madarasa manne na nyumba ya walimu.

Pichani rais Kikwete akitoka katika moja ya nyumba za wenyeji wake wilayani Mbulu, haya ndiyo maisha ambayo rais anataka watu kuondokana nayo.Picha na John Lukuwi wa Maelezo na Habari na Shdrack Sagati wa HabariLeo
COMMENTS