DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS UNITED REPUBLIC OF TANZANIA Telephone: 255-22-2114512, 2116898 E-mail: ikulumawasiliano@yahoo.com...
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
Telephone: 255-22-2114512, 2116898
E-mail: ikulumawasiliano@yahoo.com
press@ikulu.go.tz
Fax: 255-22-2113425
PRESIDENT’S OFFICE,
THE STATE HOUSE,
P.O. BOX 9120,
DAR ES SALAAM.
Tanzania.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Nchi za Afrika zimeonywa kuwa macho na uwezekano wa kugeuzwa soko kubwa la madawa ya kulevya kutoka Marekani Kusini, hasa baada ya Marekani kuwa imedhibiti soko lake.
Onyo hilo limetolewa leo (Jumanne, Oktoba 7, 2008) na Balozi mpya wa Colombia katika Tanzania, Mama Maria Victoria Suarez wakati alipokutana na Rais Jakaya Mrisho Kikwete Ikulu, Dar es Salaam.
Akizungumza na Rais Kikwete baada ya kuwa amewasilisha hati zake za utambulisho, Mama Suarez amesema kuwa upo uwezekano kuwa nchi za Afrika zikalengwa na wafanyabiashara wa biashara hiyo haramu ya madawa ya kulevya baada ya soko la Marekani kudhibitiwa.
“Kama unavyojua, Marekani iliyokuwa soko kuu la madawa ya kulewa sasa imedhibiti biashara hiyo kwa kiasi kikubwa, na hivyo inawezekana kuwa hawa wachuuzi wakaanza kutafuta soko jipya katika Afrika,” amesema mama huyo na kuongeza kuwa kwa sababu hiyo upo umuhimu mkubwa wa Afrika kushirikiana na Colombia katika udhibiti wa madawa ya kulevya.
“Utakuwa unajua Mheshimiwa Rais kuwa madawa ya kulevya yametusumbua sana katika Colombia, na hivyo tunao uzoefu kidogo ambao tunaweza kugawana na Afrika kwa jinsi Bara hili linavyoweza kupambana na madawa ya kulevya,” amesema mama huyo ambaye makazi yake yako Nairobi, Kenya.
Mama huyo amesema kuwa kwa sasa inaonekana kuwa sehemu ya Afrika iliyoathirika zaidi ni Afrika Magharibi, na kuwa bado eneo la Mashariki halijaguswa sana na biashara hiyo haramu.
Lakini Rais Kikwete amemwambia mama huyo kuwa hata Afrika Mashariki imeanza kuwa soko kubwa la madawa ya kulevya. “Hapa sisi tunalo tatizo kubwa. Hapa mjini, kwa mfano, vijana wengi wameharibiwa sana na madawa haya. Tunahitaji uzoefu na ushirikiano wa Colombia katika jambo hili.”
Rais pia amepokea hati za utambulisho kutoka kwa Balozi mpya wa Jamhuri ya Shirikisho la Ujerumani, Dk. Guido Cornelius Herz.
Katika mazungumzo kati yake na Rais Kikwete baada ya kuwa amewasilisha hati zake, Dk. Herz amemhakikishia Rais Kikwete kuwa Ujerumani haitapunguza misaada yake kwa Tanzania ama nchi nyingine za Afrika kutokana na misukosuko mikubwa inayoukumba mfumo wa fedha duniani.
“Napenda kukuhakishia Mheshimiwa Rais kuwa pamoja na misukosuko mikubwa inayoukumba mfumo wa fedha duniani, hasa katika nchi ya Marekani na Bara la Ulaya, bado Ujerumani itaendelea kuheshimu ahadi zake kwa wabia wake wa maendeleo, kama Tanzania na nchi nyingine za Afrika,” amesema Balozi huyo.
Dk. Herz ametoa uhakikisho huo baada ya Rais Kikwete kuwa amesema kuwa ingawa kwa sasa Tanzania haijakumbwa na athari za misukosuko hiyo ya mfumo wa fedha duniani, wasiwasi ulioko ni kwamba nchi tajiri zinazokumbwa na hali hiyo zinaweza kuamua kupunguza misaada yake kwa wabia wake wa maendeleo katika Afrika.
Rais pia amepokea hati za utambulisho kutoka kwa mabalozi wapya wa Austria na Thailand. Mabalozi hayo, Apichit Asatthawasi wa Ufalme wa Thailand na Roland Hauser wa Austria wana makazi yao Nairobi, Kenya.
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
07 Oktoba, 2008

COMMENTS